Mwakyembe: Marufuku abiria Kuchimba dawa njiani

Mwakyembe: Marufuku abiria Kuchimba dawa njiani

Vijengwe vyoo kila baada ya kilomita kadhaa au kila miji iliyopo katika barabara kuu.

Kweli hili ni jambo mtambuka,,nani atakuwa anavihudumia sasa hivyo vyoo,,maana hivi tu vilivyopo baadhi ya stand, vya halmashauri nadhani ambavyo wanachaji hela kujisaidia haja ndogo ama kubwa vinatisha kwa uchafu
 
Nadhani tunaangalia hii hoja vibaya. Yes, kuchimba dawa ni sawa, lakini kwa karne hii watu kuendelea kujisadia maporini ni fedheda! We cannot claim to be a modern nation yet, tunajisaidia maporini! Kuna njia mbali za kuondokana na hii aibu, moja ni kwa mabasi yanayokwenda mikoani kuwa na vyoo, au kujenga public toilets kila baada ya kilometer kadhaa. Ni hili la pili linawezekana kabisa kwa kuagizia kila mkoa ambao uko kwenye Highway kujenga decent public toiletS. Lakini hatuwezi kufumbia macho hali ya sasa maana inatoa taswira mbaya kwa kwa watanzania kama jamii.

Tukubali ukweli.

Kimsingi upo sahihi kabisa, ni muhimu tukahamishia mjadala katika economics zake kama nia kweli ni kutatua tatizo. Hapa tunafanyeje? route kwa mfano ya Dar - Arusha kwa siku kuna mabasi sio chini ya 50 yanayokwenda both ways, on average, basi lina abiria 55, which means kwa siku kuna abiria zaidi ya 2,500 wanahohitaji kujisaidia huko njiani kwenye umbali wa karibia kilometa 600;

Tunafanyeje in terms of vyoo vingapi, nani ata manage, na what's the equilibrium point ambayo itaondoa/punguza cost in terms of time kwa wenye mabasi na abiria? Mawazo na maswali yangu hayapo as structured but nia yangu kujaribu kuendeleza mjadala towards utafutaji wa solution.
 
Mwakyembe hapa kakosea sana, kwani kuna mtu anapenda kujisaidia njiani/ kichakani akiwa safarini?
Kwa hili abiria wa mabasi waendelee kusimama na abiria kujisaidia kama kawa, basi aongee na Mungu kwanini aliweka mavi/mkojo au yy hajisaidii...????? au atengeneze vyoo kila 50 km hivi, for this ur score is 00%

Shame on you Mwakyembe hili ur wrong....
 
Huyu jamaa naona ameiga mambo ya Magufuli, anayeanza kutaja kilomita za mabarabara hata kama swali aliloulizwa alihitaji kutaja kilomita. Magufuli kama uko makini kumsikiliza huwa anachomekea vitu irelevant sana anapoongea au kujibu maswali.
Nimeanza kuona na huyu jamaa naye ameiga ujinga huu wa kutaka sifa tu kwa kufuatilia vitu vidogovidogo. Nakumbuka wakati wa mkutano wa magamba pale jangwani aliongelea habari za daladala kukatisha route eti atapambana nao wakati mapaka leo sijaona akipambana nao. Wizara ina matatizo makubwa halafu waziri anaongelea kuchimba dawa bungeni kweli au kukatisha route za daladala? ishu ndogo kama hizi hata huna haja ya kuziongelea ni utekelezaji tu! Badala ya kukaa akaumiza kichwa ni namna gani ATCL/TRL/TAZARA/ zitafufuka!

Mazee unajua hata na mimi nimelifikiria hili.

Hivi katika mambo yooote yaliyo matatizo katika Wizara yake, hili ndio kaona la kipaumbele?

Au ilikuwa vipi mpaka hili likaibuka?
 
mh. dr. harison mwakyembe ametoa tamko kuwa sasa hivi gari lolote la abiria litakalo onekana limesimama njiani kwa ajili ya abilia wake kuchimba dawa (kujisadia) litachukuliwa hatua za kisheria.

Hivi jamani kwa nini viongozi wa TZ wanashindwa kushughulikia major issues na badala yake wanatumia nguvu nyingi kupambana na minor issues.

Hili suala ni la bwana afya na wala waziri mzima atakuwa hana kazi kama anathubutu kusimama na kutangaza eti abiria hawaruhusiwi kujisaidia haja ndogo njiani. Kitanda usicholala hujui kunguni wake na ndivyo ilivyo kwake kwani angesafiri kwa basi abanwe na haja angetia akili .
 
kweli akili zikiwa nyingi sana mwishowe unakuwa chizi,naanza kuuamini huu msemo,ningekuwa na mshkaji wng fln hv angesema anagongwa huyu
 
nakupa 'like' mvumbuzi,ni ukweli mtupu uliouainisha!
 
Wana siasa always wanaleta mambo ya ajabu ajabu tuu, hapa Mwakyembe kachemka
 
Big up Dr kwa uamuzi wako. Ni aibu sana na ni ufinyu wa mawazo baada ya miaka 50 ya Uhuru tunawaza mawazo ya kizamani. Kuna shida gani kila Halmashauri kujenga "rest areas" katika maeneo yao? Hebu tubadilike kifkra. Yeyote anayempinga Dr anadhihirisha uzamani. Kumbukeni sisi siyo mbwa ni wanadamu....... Big up again Dr. Kanyagia hapo hapo mpaka kieleweke.....

Sidhani kama wadau waliotoa maoni yao wanapinga hilo wazo, bali wanashangaa kutoa amri wakati hujaandaa mipango ya kui-enforce kikamilifu hiyo amri.

Mipango mizuri ni kama hiyo unayopendekeza ya kuiitaka ama kuiwezesha kila almashauri au kila mkoa kujenga 'rest area' moja ambapo barabara kuu zinapita!

Kansa ya kiutendaji inayotusumbua bongo ni kuwa REACTIVE badala ya kuwa PROACTIVE katika utoaji huduma za kijamii. Tunasubiri hadi majanga yatokee (kama hayo ya UCHIMBAJI DAWA) ndio tukurupuke na utoaji amri.
 
sijui kwa nini ukiingizwa serikalini uwezo wa kufikiri unaisha.
Nahisi kuna dawa wanapewa wakati wanaapishwa.
 
Nilisikia kapanda treni majuzi, Namshauri apande Saibaba Arusha to Dar, na awe amejikoki breakfast kama kawa, alafu atoboe mpaka mombo bila kuchimba dawa. Ili a testi zari kabla. Mi nadhani wangeweka pit stops zenge vyoo angalau every 250km. Ndipo sheria ifuate.
 
Ukishasikia hivyo tu ujue dili la wachache linakuja,apo utasikia serikali imetangaza zabuni za kutengeneza vizibo vya kuzuia haja kubwa na ndogo.
 
mh. dr. harison mwakyembe ametoa tamko kuwa sasa hivi gari lolote la abiria litakalo onekana limesimama njiani kwa ajili ya abilia wake kuchimba dawa (kujisadia) litachukuliwa hatua za kisheria.


akimaliza hili, atusaidie kwenye " ABIRIA KULA NA KUCHIMBA DAWA DK 5" INAUDHI SN. TUPEWE WALAU NUSU SAA! NA WENYE VYOMBO VYA USAFIRI WASHINIKIZWE KUTII HILO! PIA HATA BEI ZA SEHEMU WANAZOTULAZIMISHA KULA ZIANGALIWE.NI KUBWA
 
Kauli hiyo ya Mwakiembe ingendana na kujenga vituo vya kupumzika kando ya barabara kuu kila baada ya KM kadhaa, la sivyo watu hawawezi kutembea bila kujisaidia toka Dar hadi Mwanza, Arusha, Moshi, Songea, Mbeya, Sumbawanga n.k
 
Hii meli iliozama July haikuzamia maji ya Znz bali ilizama ikiwa maji ya Tz bara na ilianzia safari Dar. Yeye Mh Mwakyembe na timu ya watu wake ndio walitakiwa kufuatilizia. Sababu meli origin yake ni Znz wakawaachilia wazanzibari wahangaike kuokoa majeruhi na kuopoa waliokufa. Hii ni aibu basi tu lakini uhakika unaeleweka maana hata Spika hakuona umuhimu wa kuahirisha Bunge siku ya tukio.
 
Namshauri apande Saibaba Arusha to Dar, na awe amejikoki breakfast kama kawa, alafu atoboe mpaka mombo bila kuchimba dawa. Ili atesti zari kabla. Mi nadhani wangeweka pit stops zenge vyoo angalau every 250km. Ndipo sheria ifuate.

Si bora Sai Baba, apande kitu kinaitwa CHAKITO Long Way aisome namba.

TUMBIRI (Tunduru, Ruvuma - Tanzania),
tumbiri@jamiiforums.com
 
sasa barabara nyingi hazina hata vyoo vya abiria njiani....makandarasi wengine huweka vyoo njiani mfano barabara ya karatu -makuyuni arusha kuna vyoo safi njiani lakini njia zingine hakuna...
atambue hili kwanza ili achukue hatua......
 
Ameandaa mazingira? Ndo maana ahadi nyingi za kibongo hazitekelezeki. Wapi kuna stop points barabara yote ya Mz- Dar? Nchi hii bwana, anataka wachimbe dawa kwenye chupa za maji?
 
huyo hajui alisemalo kuchimba dawa muhimu kwa hyo ujiharishie ndani ya gar?
 
Yeye anaona wanawake wanadhalilika kwani yeye ni waziri wa wanawake jinsia na watoto mpaka awasemee!
Alafu "Mgema akisifiwa tembo ulitia maji" ndo huyu Mwakyembelembele kila kitu anajifanya kujua
Kupanda garimoshi na daladala sio ndio umeshajua kero za watanzania
 
Back
Top Bottom