Mwakyembe: Marufuku abiria Kuchimba dawa njiani

kupiga marufuku bila kuweka njia mbadala haisaidii, nchi za wenzetu kuna facilities muhimu kwa "kuchimba dawa", kupumzika kwa muda na kupata mlo ktk njia kuu karibu kila 50km, hivyo huna sababu za kugongwa na nyoka machakani.

Mh Mwakyembe kama kweli umemaanisha (maana mara nyingi uwa ni siasa tu), jenga kwanza hizo facilities huko njiani ndo ije kauli ya "marufuku kuchimba dawa", kinyume cha hapo ni ngumu kumesa.
 
Anatengeneza mazingira ya kuchukua chake mapema au kitu gani hapo kinacho andaliwa
 
Kwa kweli huu huwa ni msaada tu wa madereva wa mabasi kwani ukiangalia economics zake, hauna faida yoyote kwa mwenye basi kwani muda hupotea; kwahiyo ni vyema tusiwaangalie madereva wa mabasi kama vile hawajali utamaduni wa watanzania; hili suala ni demand-driven na ni abiria ndio uendekeza, vinginevyo sheria mpya itafaidisha zaidi wenye mabasi kuliko inavyodhaniwa.
 
huu ni utan sasa, kitu kama hiki hakiwezekan hata kidogo, kuchimba dawa ni haki yetu na dawa tutachimba popote pale, hata hao trafick mbona wanachimba dawa mara kibao tu.
 
Kutamka sawa, lakini je ktk ku-enforce hicho alichotamka itawezekana????. Ni sawa na alipoamua kupanda daladala eti kuchunguza kero ktk public transport. Sensationalism tupu!! --Kama ni soka, anacheza na jukwaa.Tatizo la Tz si uwepo wa sheria au kukosekana matamko kama hayo; Tatizo ni usimamizi wa sheria.
 
I have been impressed by high level of intellectual capacity you have bravely shown when answering the questions from MPs on various matters raised particularly that regarding the call for you to resign because of the ill fated Mv Skagit. Hapa ndio unaona pride ya kusoma. Hongera sana Mwakyembe. Pamoja na kuwa siipend CCM, lakini on individual basis I congratulate you!
 
Sasa hivi watatengeneza vyoo na kulazimisha mabasi kuvitumia, kwa fee ya Tsh 200 kwa kichwa.

Halafu vitakuwa vinanukaa kuliko kile cha Mnazi Mmoja.

I can see this being a cashcow for them, maumivu ya kichwa huanza pooolepoole.
 
Huyu jamaa naona ameiga mambo ya Magufuli, anayeanza kutaja kilomita za mabarabara hata kama swali aliloulizwa alihitaji kutaja kilomita. Magufuli kama uko makini kumsikiliza huwa anachomekea vitu irelevant sana anapoongea au kujibu maswali.
Nimeanza kuona na huyu jamaa naye ameiga ujinga huu wa kutaka sifa tu kwa kufuatilia vitu vidogovidogo. Nakumbuka wakati wa mkutano wa magamba pale jangwani aliongelea habari za daladala kukatisha route eti atapambana nao wakati mapaka leo sijaona akipambana nao. Wizara ina matatizo makubwa halafu waziri anaongelea kuchimba dawa bungeni kweli au kukatisha route za daladala? ishu ndogo kama hizi hata huna haja ya kuziongelea ni utekelezaji tu! Badala ya kukaa akaumiza kichwa ni namna gani ATCL/TRL/TAZARA/ zitafufuka!
 
Nadhani tunaangalia hii hoja vibaya. Yes, kuchimba dawa ni sawa, lakini kwa karne hii watu kuendelea kujisadia maporini ni fedheda! We cannot claim to be a modern nation yet, tunajisaidia maporini! Kuna njia mbali za kuondokana na hii aibu, moja ni kwa mabasi yanayokwenda mikoani kuwa na vyoo, au kujenga public toilets kila baada ya kilometer kadhaa. Ni hili la pili linawezekana kabisa kwa kuagizia kila mkoa ambao uko kwenye Highway kujenga decent public toiletS. Lakini hatuwezi kufumbia macho hali ya sasa maana inatoa taswira mbaya kwa kwa watanzania kama jamii.

Tukubali ukweli.
 
sometime hebu hawa jamaa wafanye tathimini kabla ya kutoa hitimisho, wasije wakaongea tu kusikika wapo. Hapo kakurupuka kusema kweli.
 
madaraka hulevywa vibaya!! wangeanza kwanza kujenga vyoo ndo waje na maagizo km haya, anadhani hata wasafiri wanapenda kuchimba dawa vichakani? wangeanza kwa kuamuru wanapojenga barabara lazima na vyoo vijengwe (kwenye mikataba ya ujenzi wa barabara kuwe na kipengele cha ujenzi wa vyoo)
 
Msihofu. Kwani hamuwajui viongozi wetu Tz? Makalio ya mwanamke yanayoanikwa kila leo kwenye tv zetu hawasemi! Amri hii itajifia km ilivyokuwa ya kuzuia vidumu kununua mafuta 'sheli'. Haiendani na hali halisi.
 
Kuzuia ni wazo zuri, je kuna vyoo vya kulipia humo njiani ambapo abiria wanaweza kwenda kuchimba dawa? Au amezuia tu ili apate umaarufu kwenye vyombo vya habari?
 
Anajua kwamba wadeni wake wa ATCL wamefuata hela yao na tayari wamezuia ndege yao isiruke leo?
 
''abiria ni marufuku kuchimba dawa njiani'', mwakyembe alipuka bungeni.
Waziri wa uchukuzi ametoa agizo bungeni jioni hii kwamba kuanzia tarehe 1 sept 2012,ni marufuku kwa mabasi kusimama njiani kwenye vichaka ili abiria wakachimbe dawa,akidai inavunja heshima na utu wa mtanzania kwa mama mtu mzima kuchuchumaa hapa akichimba dawa na kijana mdogo naye hapa akichimba dawa.

hapa nafikiri anapaswa kutumia busara na kuhamasisha wanavijiji kujenga vyoo kandokando ya barabara kuuu ili kutoa huduma hiyo kwani atakuwa hawatendei haki abiria wa mabasi kwa sababu kuna mabasi mengi hutembea mwendo mrefu bila kupiti kwenye sehemu ya huduma na wakati mwingine kuna dharula.
 
Back
Top Bottom