Mwakyembe: Marufuku abiria Kuchimba dawa njiani

hendeboy

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
218
21
Mh. Dr. Harison Mwakyembe ametoa tamko kuwa sasa hivi gari lolote la abiria litakalo onekana limesimama njiani kwa ajili ya abilia wake kuchimba dawa (kujisadia) litachukuliwa hatua za kisheria.
 
Akihitimisha hoja yake ya Mawasiliano na Uchukuzi amesema hakuna kujisaidia njiani hata kama unaharisha humo humo kwenye basi au chombo cha usafiri unachotumia
Basi wekeni sheria ya wenye mabasi au vyombo vya usafiri waweke vyoo kwa ajili ya abiria kujisaidia maana kuna umuhimu gani wa kupiga marafuku abiria kutochimba dawa njiani huku kuna wakati watu unakuta wengine wamekula matoke na vichuri sasa kwenye vyombo vya usafiri visiposimama ili kutoa fursa kwa yule anaehitaji kuchimba dawa afanye hivyo c wanataka watu/abiria kujisaidia kwenye vyombo hivyo
 
''ABIRIA NI MARUFUKU KUCHIMBA DAWA NJIANI'', Mwakyembe alipuka bungeni.
Waziri wa uchukuzi ametoa agizo bungeni jioni hii kwamba kuanzia tarehe 1 sept 2012,Ni Marufuku kwa mabasi kusimama njiani kwenye vichaka ili abiria wakachimbe dawa,akidai inavunja heshima na utu wa Mtanzania kwa Mama mtu mzima kuchuchumaa hapa akichimba dawa na kijana mdogo naye hapa akichimba dawa.
 
angekua mzaliwa wa dar nisingemshangaa, sababu mtu mwenyewe mzaliwa wa mbeya ngoja nimwone kituko.!
 
Hahahahahaaa! Anasema mipaka yake ya uwaziri inaishia CHUMBE... hata hizo meli za Iran zilizosajiliwa Zanzibar hana taarifa nazo naye amesikia tu. Anasema waziri aliejiuzulu Zanzibar alitakiwa ajiuzulu tangu ajali ya spice islander.
 
dili hilo hayo maeneo yanayotumika kuchimba dawa huwa sehemu kubwa ni misitu je ni mali ya serikali kama inawezekana watoe maeneo wajasiriamali wajenge vyoo vya kulipia
 
ameeleza kuwa hato jiuzulu .. Kwa ajali za majini zilizo jitokeza.. Na amesema kwa uwaz jinsi gani. Hausiki.. Ametoa.. Na kuwa sheria ziko waz amewapa wabunge shule ya kutosha..
 
Asiyejiuzulu hasemi "Sijiuzulu".

Ukishasema "Sijiuzulu" ushapiga hatua moja kuelekea kujiuzulu.
 
Ni kweli kwa sababu zanzibar ni nchi kwa mujibu wa katiba yao ambayo muungano haujaikataa kwa hiyo mwakyembe yuko sahihi kabisa
 
Ok, basi wahakikishe kuwa mabasi yote yanayoenda mbali, eg Mikoani, nje ya Dar, yana vyoo, anafikiri watu wanapenda kukojoa vichakani?!, wanakuwa wamebanwa na haja vya kutosha
''ABIRIA NI MARUFUKU KUCHIMBA DAWA NJIANI'', Mwakyembe alipuka bungeni.
Waziri wa uchukuzi ametoa agizo bungeni jioni hii kwamba kuanzia tarehe 1 sept 2012,Ni Marufuku kwa mabasi kusimama njiani kwenye vichaka ili abiria wakachimbe dawa,akidai inavunja heshima na utu wa Mtanzania kwa Mama mtu mzima kuchuchumaa hapa akichimba dawa na kijana mdogo naye hapa akichimba dawa.
 
tundu lisu.. Ameanza kwa fungu 1001, mshahara wa waziri.. Na swali.. Anataka kujua kuhusu meli za ajali kama zilifanyiwa ukaguz? Na lin? Na matokeo yake? Masuala ya uchukuz sio ya muungano mpaka chumbe.! Amesema mwakyembe hawez kukwepa kujiuzulu
 
Wkuu, sasa hivi waziri wa Uchukuzi, Dr. H. Mwakyembe ametangaza kuwa kujisaidia kwa wasafiri wa mabasi maarufu kwa "kuchimba dawa" mwisho ni tarehe 1 Septemba 2012!!!
Akitangaza uamuzi huo wa serikali, Dr Mwakyembe amesema ni kinyume na utamaduni wa Mtanzania kwa watoto na wakubwa kuchanganyika kisha kujisaidia kwa pamoja. Akiendelea kufafanua alisema kwa kutolea mfano, kwamba utakuta mzazi wa kike akisema kumwambia mwanae "nitakuvulia nguo....." Akatolea mfano kuwa hata katika kuogelea si rahisi watu kuogelea kwa kuchanganyika na watoto wao.
Sasa anashangaa kwa watu kuchanganyikana wakati wa "kuchimba dawa". Kwa hiyo amepiga marufuku kujisaidia kwa mtindo wa kusimamisha gari porini ili watu wajisaidie.
Nawasilisha wakuu.
 
..ni bajeti ya "kufufua" sekta ya mawasiliano na uchukuzi.

..ina maana sekta hizo ziliachwa zikafa au ziliuawawa.

..sasa jiulize ni chama gani kilihusika na uzembe huo.

..ukipata jibu, usikupigie tena kura chama hicho.
 
Serikali itengeneze sehemu maalum kwa ajili ya wasafiri kujisadia.
Siyo kikataza kuchimba dawa wakati hakuna vyoo kwenye barabara kuu.
 
Back
Top Bottom