Mwakyembe: Marufuku abiria Kuchimba dawa njiani

Mwakyembe: Marufuku abiria Kuchimba dawa njiani

Duh kaka yangu mwakyembe heshima yake inazidi kuporomoka,ameshauriana na wenzake adhari za hili au karopoka tu? Kwa mazingira gani ya porini mtu asijisaidie! Tabu hawa watu wa mashangingi wanajisahau sana maana wao umbali mrefu wanakwea pipa wanasahau sisi tunatoka Dar hadi Karagwe kwa basi!

daaaah nimeamini sumu aliyopewa mwakwembe ni mbaya sana!
 
Mwakyembe na kwenye mradi wako wa treni kutoka Station mpaka Ubungo hizo treni zitakuwa na vyoo.
 
Serikali itengeneze sehemu maalum kwa ajili ya wasafiri kujisadia.
Siyo kikataza kuchimba dawa wakati hakuna vyoo kwenye barabara kuu.
Hapo ndo ninapomshangaa na mimi mwakyembe,sijui keshaanza kulewa sifa na ndio sababu anaanza kuja na maamuzi ya kukurupuka,mi najiuliza keshaandaa choo ngapi barabarani,au hajui kuharisha inakuwaje?pengine bado hajapona vizuri.
 
Dar, toka Tunduma hadi Dar, chakula Ilula au Kitonga au Ruaha mbuyuni bila kuchimba dawa hapo, mmm, sijui, then toka Arusha hadi Dar, chakula Mombo then hadi Dar, sijamaliza, safaro kutoka Mwanza hadi Dar, chakula cha mchana Singida, then baada ya hapo Dar, aaaah, sipati picha hakika, anyway, mwongozo hapo kwa Riz1, hii umepinga kama sisi au kwasababu mtoa hoja sio chaguo la mzee?
 
Pumbav angetoa tamko hili akiwa ameruhusu watu kuchimba vyoo vya kulipia polini ili kuwastili abiria.
 
mh. dr. harison mwakyembe ametoa tamko kuwa sasa hivi gari lolote la abiria litakalo onekana limesimama njiani kwa ajili ya abilia wake kuchimba dawa (kujisadia) litachukuliwa hatua za kisheria.

Kama hili ni la kweli atakuwa ameanza kulewa sifa. Kabla ya kutoa agizo hilo angehakikisha kuwa ameweka vituo vyenye public toilets za kutosha kwenye maeneo hayo.
 
Mtu mwenye afya ambaye haumwi, kunya au kukojoa porini sio kuchafua mazingira kwani Kinyesi cha mtu mwenye afya ni mbolea.

Na hivi ni watu wangapi huko vijijini wasiokuwa na vyoo wanaokunya huko porini? Mazingira barabarani yanachafuliwa na utupaji wa taka dirishani kutoka kwenye magari.

Ukisafiri barabara zetu kuu utaona mita tano kando kando ya barabara zimejaa makopo, chupa za plastiki, mifuko ya rambo na takataka nyingi sana zisizooza.

Tukiendelea kwa mwendo huu kwa kulifumbia macho tatizo hili litakuja kuwa janga la taifa huko mbeleni. Hichi ndicho Mwakyembe angefaa akivalie njuga.
 
mh. dr. harison mwakyembe
ametoa tamko kuwa sasa hivi gari lolote la abiria litakalo onekana
limesimama njiani kwa ajili ya abilia wake kuchimba dawa (kujisadia)
litachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa sheria namba ngapi ya mwaka gani? Hajatulia huyo!
 
watanzania tutabadilika lini? Huu ni uchafuzi wa mazingira na pia unachangia sana ajali kwa mabasi na malori kusimama sehemu zisizostahili, viongozi wamechelewa sana kutoa hili agizo! Lakini kama kawaida ya wanachadema watapinga tu hata kama ni kwa usalama wa watanzania.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Wagonjwa wa kisukari hawatasafiri?.........inabidi serikali ijenge vyoo njia nzima au wenye mabasi waweke vyoo ndani ya mabasi
 
huyu jamaa naanza kuamini ugonjwa umempeleka kumbaya hajapona sawasawa utasema hakuna kuchimba dawa huku hauna vyoo njiani. hili nalo linahitaji elimu?
 
Sasa nimeamini Viongozi wetu hawajui maisha yetu sisi wananchi. Dr. Mwakyembe anasema watu wasikojoe njiani wakati wa safari kwamba wanadhalilishwa. Hivi ashawahi kubanwa na mkojo akiwa kwenye haya mabasi yetu (hayana vyoo) halafu eti asubiri hadi basi likasimame mahali kwenye choo (sijui kilomita ngapi mbele) ndio akojoe? Na kuna watoto wadogo wasioweza kuvumilia mkojo muda mrefu, kuna wagonjwa wa kisukari, wagonjwa wa tumbo n.k.

Najua hawa viongozi wetu wakisafiri safari fupifupi wanakuwa na magari yao ya kifahari tena ya Serikali na wanaweza kusimama mahali popote hata kwenye duka wakaomba choo. (watu 40 kwenye basi wanaweza kuomba choo mahali popote? Najua pia wakisafiri safari ndefu wanatumia ndege, sasa maisha yetu watayajuaje?

Ndugu zangu kuchimba dawa njiani sio hiari ya dereva ambaye mwakyembe amesema wakisimama njiani atawaadhibu, bali ni abiria wanapobanwa na haja wanahitaji kuchimba dawa. Sasa mbona gari linaposimama hakuna anayeacha kushuka asubiri gari lifike mahali penye choo?

Maelezo/uamuzi wa Dr. Mwakyembe sio sawa kwetu sisi wananchi.
 
Dr mwakyemba siasa sasa zinakupeleka kubaya. Hivi wale ndugu zako wa kyela wanaweza kusafili umbali mrefu bila kwenda haja?

Kwa ushauri wangu mdogo ni hv ungetafuta njia mbadala ya watu kujisaidi pindi wawapo safarini kisha ndio upige marufuku watu kuchimba dawa, nafikili utafarahi sana kusikia kuwa watu wamejinyea kwenye magari. Fikiri kabla ya kutamka.
 
mi naona kama kachemka flani hapo, hivi safari ya mwanza-dar au dar-mbeya , bila kucimba dawa itafika? au kwa sbabu wao wanapanda ndege? kweli aliyeshiba hamkumbi mwenye njaa...
 
This dude mwakyembe mara ya mwisho ulipanda bus lini la kwenda mkoa? Unatoa mawazo kama unafikiria kwa kutumia masaburi! Get real! Fanya mambo ya msingi dont talk ili usikike kwamba umesema, ni bora ungekaa kimya, and some people are thinking u are presidential material what a joke! Mkishapata uongozi mnasahau kabisa mlikotoka. Hivi nyinyi viongozi mna matatizo ya kufikiri eennh, mf natoka mbeya naenda mpanda unataka nijisaidie wapi?
Au abiria anayetoka mbeya anaenda tabora kupitia chunya akajisaidie wapi? Kwanza lami hakuna! Kweli uko vizuri kichwani wewe? Umenikera sana, umeacha kuongea mambo ya maana unaleta ujinga hapa! Weka lami nchi nzima weka public toilets then ndo uje uongee hayo!
 
sure yeye anatumia vx akifika mahali atasimama, saa kwa wale wanaotoka dar kwenda arusha first break ni pale korogwe je watoto watavumilia?
hii haingii akilini.
kuna sehemu wami wamejenga choo njiani na mabasi husimama pale lakini choo kimoja kwa abiria 70 mda gani utapotea hapo? mwakyembe kwa hili kachemka tena sana.ahimimze ujenzi wa vyoo basi kila kijiji kilichokaribu na barabara wajenge na watoze abiria sh 50 labda kwaajili ya kuviboresha.
 
Serikali itengeneze sehemu maalum kwa ajili ya wasafiri kujisadia.
Siyo kikataza kuchimba dawa wakati hakuna vyoo kwenye barabara kuu.

Sio sahihi kwa waziri kutoa amri ambayo haitekelezeki. Yeye anapokwenda kwao Kyela anakuwa na gari lake na ana uhuru wa kuchimba dawa mahala popote pale njiani na hakuna wa kumthibiti, lakini kwa sie walala hoi ambao ndio wapiga kura wake safari ya Kwenda Kyela toka Dar kwa mafano ni mbali sana na hakuna sehemu maalum humo njiani designated kwa wasafiri kujisaidia!! Amri hii ingekuwa na maana pale tu kama huduma hiyo ya vyoo ingekuwa inapatikana humo njiani nchi nzima halafu wenye mabasi wanaivunja; hata hivyo sijui kama kuna capacity ya kuisimamia amri hiyo tata!! Kuna umuhimu wa umoja wa wenye mabasi yaendayo mikoani kulitolea TAMKO agizo hilo la waziri.
 
Du,hii sasa kali;basi mabasi yawe na vyoo maana vinginevyo itakuwa balaa!!!
 
Ni jambo la kuchekesha kidogo na kushangaza ingawa ndiyo kiongozi amesema..Hofu yangu ni kwamba hivi hili agizo limeandaliwa mazingira gani..?!Maana watu wanamatatizo mbalimbali na binadamu hatulingani wakati tunapokuwa safarini..kuna wengine wanamatatizo ya kisukari hivyo kubanwa haja ndogo mara kwa mara ni kitu cha kawaida ..watoto sasa hawa wanaposubiri vituo vikubwa humo ndani kumeandaliwa utaratibu gani wa kuwasaidia..! Au wanajisahau kuwa wanachotumia abiria ni bus na si shangingi..jamani viongozi wetu tufikirie wakati mwingine. Ni kweli wanawake hudhalilika lakini watz wamekuwa wastaarabu hata sehemu zinaposimama hizo bus..wanaume hujitenga.. na wanawake wengi husafiri na khanga kwaajili ya kujisitiri..agizo ni zuri ila maandalizi hakuna na halitasaidia bali litaumizaaa wengi.Ni maoni TU!
 
Back
Top Bottom