Mwakyembe: Marufuku abiria Kuchimba dawa njiani

Mwakyembe: Marufuku abiria Kuchimba dawa njiani

mh. dr. harison mwakyembe ametoa tamko kuwa sasa hivi gari lolote la abiria litakalo onekana limesimama njiani kwa ajili ya abilia wake kuchimba dawa (kujisadia) litachukuliwa hatua za kisheria.
Kama kweli kasema kachemsha ajenge vyoo vya abiria na parking ya magari humo njiani aone kama kuna mtu atakwenda porini, hajui kujisaidia porini watu wanarisk sana kuumwa na nyoka au wadudu wengine wakali. Huyu naye nadhani anatafuta sabubu ya kusema tumesema Mmalawi. Barabara ya Makuyuni to Ngorongoro ina vyoo akaone kama kuna kuchimba dawa porini.
 
Mi nahisi ile sum haikumwathiri tu ngozi, bali ubongo pia. Tangu ameugua Mwakyembe anaongea vitu vya ajabu ajabu!
 
angekua mzaliwa wa dar nisingemshangaa, sababu mtu mwenyewe mzaliwa wa mbeya ngoja nimwone kituko.!

mkuu wangu,huyu jamaa hajapona vizuri. bado kichwa chake kina matatizo. tumbo linapochafuka halibishi hodi. pengine tuwe tunasafiri na pampas!
 
Huyu waziri Mwakyembe ameishiwa sera, hivyo akaamua kuwa mpayukaji! Anatakiwa apelekwe shule na Mheshimiwa Mengi (wa IPP) kujifunza kwamba ili kutunza mazingira ni lazima kujenga mazingira. Mheshimiwa waziri, kama wachangiaje wengi walivyonena, kwa mshahara unaolipwa kama waziri, badala ya kupayukapayuka kwa kuwa Spika kakupatia fursa, lieleze bunge letu tukufu ni vyoo vingapi wizara yako imejenga kwenye hizo barabara kuu, na kwamba kwa sababu vyoo vipo - sasa ni marufuku kuchimba hiyo miti. Kinyuma cha hapo - kaa kimya kabisa! Mimi nimewahi kutembea kwa wenzetu Marekani, na ninaamini fika kwamba wengi wenu ninyi vigogo mmeshawahi kufika huko, au kwa matembezi au kimasomo. Mnajua fika kwamba kila baada ya maili 60 kwenye barabara zote kuu, kuna sehemu ya kupumzika, ikiwa ni pamoja na vyoo vinavyosafishwa kila baada ya mtu kukitumia - yaani ameajiriwa na serikali. Badala ya kupayukapayuka hovyo, unapaswa kuagiza wizara yako kuhakikisha kwamba kuna choo kila baada ya Maili 60 (Km 110). Ukifanya hivyo, huna haja ya kupiga marufuku ukataji miti unaofanywa na abiria. Kwanza acha kututukana watanzania eti kwamba sisi si wastaarabu! Acha nikujulishe kwamba hata nguruwe akijengewa vizuri, kamwe hajichafui au hakanyagi mahali anapolala! Ukimwona nguruwe mchafu, ni kwa sababu Bwana mmiliki wake kamjengea mazingira ya kujichafua. Ukiona Mtanzania akichimba hiyo miti, si kupenda kwake wala kwa dereva anayesimamisha gari - shida zinazosababishwa na ninyi vigogo zimetufika shingoni. Tangu ile vita ya Kagera, Mtanzania amekuwa anahadaiwa na huto tuvigogo - Oooo jifunge mkanda, tafuta mshipi, jikaze kdogo, vumiliavumilia kidogo - na sasa wewe Mwakyembe unathubutu kuwaagiza watanzania kwa kupitia bunge kwamba yabidi kuvumilia na kujikaza hata kwenye mwito wa kimaumbile! Jamaaaaaani! Mimi nafikiri yakubidi uombe msamaha kwa hilo, au kama wabunge wanajua kazi yao, inabidi wakusihi na wakutake uanze kazi ya kujenga sehemu za kupumzika pamoja na vyoo kwenye hizo barabara kuu. Kwani hawaoni kwamba umechokoza nyuki na inakubidi kuhakikisha kwamba wamerudi kwenye mzinga wao? Eboooooooooo!
 
Duh sasa uhuru binafsi unaanza kuingiliwa......lakini kama shida yake ni kuvunjwa kwa heshima ya watu wazima basi wenye vyombo vya usafiri wanaweza kulidhibiti hilo kwa kuwachimbisha dawa abiria kwa vituo kwa kufuata umri/jinsia.....kuliko kupiga marufuku......au anataka tusafiri na mifuko ya rambo????
 
Akihitimisha hoja yake ya Mawasiliano na Uchukuzi amesema hakuna kujisaidia njiani hata kama unaharisha humo humo kwenye basi au chombo cha usafiri unachotumia
Basi wekeni sheria ya wenye mabasi au vyombo vya usafiri waweke vyoo kwa ajili ya abiria kujisaidia maana kuna umuhimu gani wa kupiga marafuku abiria kutochimba dawa njiani huku kuna wakati watu unakuta wengine wamekula matoke na vichuri sasa kwenye vyombo vya usafiri visiposimama ili kutoa fursa kwa yule anaehitaji kuchimba dawa afanye hivyo c wanataka watu/abiria kujisaidia kwenye vyombo hivyo

Hii ni hatari sasa!! Kama inaanza kutekelezwa MARA MOJA; ina maana tutalazimika kusafiri tumevaa PAMPERS???

Na beer za safarini zinavyoleta mkojo hovyohovyo........
 
Nadhani tunaangalia hii hoja vibaya. Yes, kuchimba dawa ni sawa, lakini kwa karne hii watu kuendelea kujisadia maporini ni fedheda! We cannot claim to be a modern nation yet, tunajisaidia maporini! Kuna njia mbali za kuondokana na hii aibu, moja ni kwa mabasi yanayokwenda mikoani kuwa na vyoo, au kujenga public toilets kila baada ya kilometer kadhaa. Ni hili la pili linawezekana kabisa kwa kuagizia kila mkoa ambao uko kwenye Highway kujenga decent public toiletS. Lakini hatuwezi kufumbia macho hali ya sasa maana inatoa taswira mbaya kwa kwa watanzania kama jamii.

Tukubali ukweli.
Hivi kumbe na sisi tunajiita modern nation! Nilidhani bado tuko karne ya 18! Kwanza vyoo vyenyewe sina hakika kama tunajua kuvitumia, oops sorry...kumbe vyoo vya shimo! Modern nation indeed!
 
good move kulinda mazingira na kujenga jamii iliyostaarabika na kujiheshimu....

shaka yangu ni ikiwa system iko tayari kwa implementation...naandika kwa kuzingatia historia ya matendo yetu, sisi ni wepesi sana wa kutoa maagizo pasi na kuwa na miundo msingi ya kufatilia na kutekeleza maagizo hayo. Mifano ya karibuni kabisa ni katazo la kutokuvuta sigara hadharani n.k.


Katika hili la mwakyembe mathalani, kuna maandalizi gani ya kuwasaidia binadamu hawa ambao wako safarini ili kupata haki yao ya kibinadamu ya kujisaidia???? Mfano mi naishi Tabora, safari ya tabora kwenda Dsm huanza saa 12 asubuhi. kutoka Tbr mpaka Itigi ni kama 200kms za rough road....safari hiyo huchukua saa 4 hivi. hapo katikati hakuna sehemu yoyote ya maana ambapo basi litaweka kituo ili watu wajisaidie..kweli unategemea basi litakwenda for 7hrs mpaka Dom pasi na kusimama pahala watu wakajisaidia???

Kimsingi, tunakubaliana na wazo la Mwakyembe..swali ni tutamudu??? tumejiandaa kumudu au ni abrakadabra za akina Panglos????!!!
 
Kwa vile Mwakyembe ameamua kuchimba dawa iwe marufuku, tujaribu kumsaidia na Economics za such a scheme. Yafuatayo ni mawazo yangu tu, they are open to criticisms; nia yangu ni kuja na kitu cha kuanzisha mjadala towards hii solution. Nitatumia route ya Arusha – Dar-es-salaam. Tuanze na assumptions kuu kama ifuatavyo:

1. Moja, kwa wastani, binadamu huenda chooni kati ya mara tano na saba kwa siku. Ili kupata namba iliyokamilika, tutumie namba 6 (sita) kama idadi ya trips za mtu kwenda chooni in a day.

2. Mbili, umbali wa Arusha to DSM ni kama kilometa 600.

3. Tatu, safari ya Arusha – DSM kwa wastani huchukua masaa (10) kumi.

4. Nne, idadi ya mabasi kwa siku (kwenda na kutoka Dar/Arusha) sio chini ya mabasi 50. Kila basi linabeba wastani wa abiria 55. Hii ina maana kwa siku, njia ya DSM – Arusha inatumiwa na abiria at least 2,700 (elf mbili na mia saba).

5. Tano, iwapo safari ya Arusha – DSM inachukua wastani wa masaa kumi na iwapo kwa wastani mtu anajisaidia mara sita kwa siku, then katika masaa kumi ya safari ya Dar-Arusha/Arusha-Dar, mtu atahitaji kujisaidia 1.6 times. Lakini ili tupate namba rahisi kuitumia, lets round it up iwe mbili (2) na ku assume kwamba katika muda wa masaa kumi, wastaniwa idadi ya matumizi ya choo kwa mtu ni mara mbili (2).

6. Sita, katika mazingira ya safari, haja ndogo huchukua wastani wa dakika mbili (2), na haja kubwa wastani wa dakika tano (5). Hivyo wastani wa mahitaji ya abiria kujisaidia katika kila kituo ni dakika 3.5 (average ya haja kumba na ndogo). Tutumie dakika tatu (3) for simplicity reasons.

Tumeona kwamba kuna jumla ya mabasi 50 yanayosafiri dar- Arusha na Arusha – dar kwa siku, hivyo kwa wastani, kila route ina mabasi 25 kwa wastani. Mabasi haya huondoka kwa awamu nne kama ifuatavyo: 6AM, 7AM, 8AM, na 9AM. Tukigawanya awamu hizi nne kwenye jumla ya mabasi 25, tunapata idadi ya mabasi 6; na haya mabasi sita yatakuwa yanafika after every hour kwenye kituo cha kwanza kwa kujisitiri. Kila basi lina abiria 50 kwa wastani, Kwahiyo kila baada ya ONE HOUR, kutakuwa na jumla ya mabasi 6 yenye jumla ya abiria 300 katika vituo hivi vipya. Sasa ili kila abiria apate dakika tatu za kujisaidia, kama kuna choo kimoja (one passanger at a time), ina maana muda utakaotumika kuhudumia mabasi haya sita yenye abiria 300 ni dakika 900 (sawa na masaa 15) iwapo kutakuwa na choo kimoja. Sasa ili ili tuweze ku spare only ONE HOUR kwenye kituo, ina maana serikali inatakiwa kujenga jumla ya vyoo kumi na tano (15) ili abiria 300 wanaoshushwa na mabasi sita kila baada ya saa (jumla ya abiria 300 per hour) wasikae zaidi ya ONE HOUR katika kituo cha kwanza cha kujisaidia kwa kujisitiri.

Tukumbuke kwamba hii ni kwa mabasi 25 ya route ya DSM – ARUSHA, Kwahiyo kwa mabasi ya route ya ARUSHA – DSM, serikali pia itabidi kujenga vyoo vingine kumi na tano (15) to serve abiria wa upande ule mwingine ambao pia watakuwa abiria 300 after every one hour.

But this is where it gets trickier:

Tumeona kwamba abiria atahitaji kutumia choo mara mbili ndani ya muda wa safari ya masaa kumi yenye umbali wa kilomita 600 KM. Hii ina maana kwamba inabidi serikali ijenge vyoo kumi na tano Kilometa 180-200 kutokea DSM kwenda Arusha (kabla ya kufika njia panda ambako kuna vyoo tayari kwenye ile sehemu ya mapumziko na vyakula inayomilikiwa na mwenye mabasi ya Dar Express) ili abiria wa DSM – ARUSHA waweze kutumia vyoo kwa mara ya kwanza tangia waanze safari ya Dar – Arusha, halafu matumizi ya pili ya choo ndio yawe pale kwenye vyoo vya njia panda vya Dar Express. Baada ya ya hapa, abiria wa DSM – Arusha hawatakuwa na fursa nyingine tena ya kujisaidia mpaka mwisho wa safari – yani Arusha. Same principle will also apply kwa abiria wanaotokea Arusha kwenda ambapo pia kutahitajika ujenzi wa vyoo vingine kumi na tano (15) kilometa kati ya 180 – 200 kutokea Arusha kwenda Dar, halafu hawa pia watapata fursa ya kutumia choo kwa mara ya pili pale kwenye vyoo na restaurant ya dar express, na na baada ya hapo hapatakuwa na fursa tena ya kutumia choo mpaka mwisho wa safari – yani Dar-es-sa;aam (ubungo).

I have not taken into account ya gharama za ujenzi wa vyoo hivi jumla ya at least 30, pia gharama za usafi, ulinzi ili watu wasiibe vitu kama mbao na mabati, na pia gharama za maintenance (mfano repairs za hapa na pale, kukata nyasi nyoka wasiingie n.k). Nadhani vyoo vya shimo would be more suitable. Vile vile masuala ya tissues na maji ya kunawa, my assumption ni kwamba abiria watajihudumia wenyewe katika haya.

Haya ni mawazo yangu tu ya haraka haraka ambayo kuna uwezekano nikawa way off, lakini angalau tupate sehemu ya kuanzia na mjadala, hasa kubadilishana mawazo kuhusu the best way forward.
 
Mi ningemuelewa kama angesema ni uchafuzi wa mazingira kwa hicho anachopiga marufuku bado hatujafikia kiwango cha kuwa na umbali mfupi kati ya mji na mji. isitoshe anataka kuleta mambo ya ulaya wenetu Mabasi yao yana Vyoo sisi huku hakuna, pia viongozi wa nchi hii mara nyingi wanapopata wanasahau walikotoka yeye anatembea kwenye V8 full kiyoyozi anapanga sheria kwetu walala hoi, hilo ni tamko lakini halitekelezeki amejifurahisha tu kuongea.
 
Dah nilikuwa cjackia nilikuwa porini ka mnyama,
Sasa hii ni dili ngoja niichangamkie kujenga vyoo kila mahali kama petrol station,hakishindikani kitu chini ya jua.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kachanganyikiwa huyu babu sio mzima, hivi yeye anaweza kusafiri safari ndefu bila kukojoa njiani??pointless
 
Akihitimisha hoja yake ya Mawasiliano na Uchukuzi amesema hakuna kujisaidia njiani hata kama unaharisha humo humo kwenye basi au chombo cha usafiri unachotumia
Basi wekeni sheria ya wenye mabasi au vyombo vya usafiri waweke vyoo kwa ajili ya abiria kujisaidia maana kuna umuhimu gani wa kupiga marafuku abiria kutochimba dawa njiani huku kuna wakati watu unakuta wengine wamekula matoke na vichuri sasa kwenye vyombo vya usafiri visiposimama ili kutoa fursa kwa yule anaehitaji kuchimba dawa afanye hivyo c wanataka watu/abiria kujisaidia kwenye vyombo hivyo

Hivi ukibanwa na haja ukiwa kwnye ndege toka TZ kwenda USA unajisaidiaje huko angani?. TUJUZENI, MAANA WENGI WETU HATUJAPANDA NDEGE.
 
dili hilo hayo maeneo yanayotumika kuchimba dawa huwa sehemu kubwa ni misitu je ni mali ya serikali kama inawezekana watoe maeneo wajasiriamali wajenge vyoo vya kulipia

Ni sawa Kabisa, na sio hivyo tu, bali pia, wajenge recreation points huko njiani!
 
''ABIRIA NI MARUFUKU KUCHIMBA DAWA NJIANI'', Mwakyembe alipuka bungeni.
Waziri wa uchukuzi ametoa agizo bungeni jioni hii kwamba kuanzia tarehe 1 sept 2012,Ni Marufuku kwa mabasi kusimama njiani kwenye vichaka ili abiria wakachimbe dawa,akidai inavunja heshima na utu wa Mtanzania kwa Mama mtu mzima kuchuchumaa hapa akichimba dawa na kijana mdogo naye hapa akichimba dawa.

Kwa hiyo baada ya kupiga marufuku ametoa alternative gani ya abiria kujisaidia safarini? Au atajenga vyoo kila baada ya kilometa kadhaa? Simuelewi, maana suala la wasafiri kuchimba dawa limekuwepo tangu enzi na enzi, ni sehemu ya utamaduni wetu watz wasafiri ndani ya mabasi kila siku.
 
Ukiichukua akili ya Dr. Mwakyembe pamoja mkuu wa kaya na wengineowote wanaowafanania inaonekana kabisa wanafikiria na kutoa maamuzi kwa mambo ya msingi kwa kutumia ubongo ulioathiriwa na sumu ya poloseum waliyompa huyo Dr mropokaji.Poor Dr.Mwakyembe ,pooor CCM gvt.
 
naona tangu augue amekua hakojoi wala hanyi wala kuharisha

hongera zake, yeye andhani yanayosimama ni mabasi amesahahu wanaosimamisha ni raia wema kama yeye

nimeshawahi kumshuhudia akikojoa njiani safarini wakati akiwa afirka mashariki

he thinks he is now GOD
 
Back
Top Bottom