Mwafaka wa Umeya wa Arusha wapatikana

Mwafaka wa Umeya wa Arusha wapatikana

Sasa unamdanganya nani? au umeamua kujifariji na kujiliwaza na msogo wa mawazo ya ndoa ya CCM na Chadema, yani kupokezana hizo kamati na kupokezana unaibu meya Chadema na TLP, nyie kwenu ndio ushindi?
hili la kupokezana kuhusu kugawana madaraka si ata uko kigoma walishafanya hivyo? Lakini cha msingi hapa ni chadema kuwa makini akuna jinsi wawatekeleze wananchi kile wanachotaka na wajitahidi kufanya mambo kwa cgance waliyopewa
 
ivi ni nani aliyeua ni chadema au polisi.sijui
 
uliza kigoma ilikuwaje?

huna hoja ,umejaa ubishi ubishi tuu

Kigoma CCM na CHADEMA waligawana madaraka baada ya kila chama kuwa na madiwani sawa;hata uchaguzi ulipofanyika hakuna diwani wa chama kimojawapo aliye defect kwenda kwingine;nakumbuka Mheshimiwa Zitto Kabwe kwa niaba ya CHADEMA alishinda ukumbini siku nzima kulinda kura za CHADEMA;Kigoma ilikuwa ni demokrasia iliyochukua mkondo wake na wala hakukuwa na ukiukwaji wa wazi wa sheria za kupiga kura kumpata meya wa mji huo kama ilivyokuwa Arusha

Hii ni tofauti kabisa na CHADEMA-Arusha;ugomvi wa wana mapinduzi pale Arusha ilikuwa ni kukiukwa kwa sheria za chaguzi za serikali za Mitaa kwa kuletwa mpiga kura toka Tanga;watu 3 waliokufa Arusha walipoteza maisha yao kwa sababu ya kutetea demokrasia na wala sio kwa kutetea kugawana madaraka!

Maamuzi ya CHADEMA kuhusu kugawana madaraka-Arusha ni ya"hovyo hovyo;hawajasimamia kile wlaichokuwa wanatuambia;ni maamuzi rahisi kwa ndugu za wahanga waliopoteza ndugu zao na kikubwa zaidi ni maamuzi yanayokera"; Walichofanya CHADEMA ni kitanzi chao cha kisiasa na watu makini wanaweza wakaanza sasa kuwaona kama ni waroho wa madaraka tu;wangesisitiza uchaguzi urudiwe upya na Mary Chitanda asipige kura na hata kama CCM watashinda kwa uwingi wao na iwe hivyo lkn sheria zifuatwe!

Kama namuona tu Nape Nnauye anavyocheka hapo alipo,na akija na dongo la uroho wa madaraka wa CHADEMA atakuwa na points nyingi tu za kutetea hoja yake;kwa mara ya kwanza toka awe kiongozi wa kitaifa CCM Nape ata make sense!
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Tunaomba tu wasije wakafunga ndoa na hawa ccm kama ilivyowakuta wenzao cuf huko zanzibar. Nakumbuka wakati maalim seif anatangaza maridhiano na ccm, baadhi ya wanacuf walionekana wakilia kwa hasira kwenye televisheni.
Mabagala,Hupo wapi wewe unataka ndoa gani tena? Kwa kwakuakikishia hii ni ndoa safi, Lema, saizi akiitisha maandamano Arusha, naibu meya Estomi Mallah, kutoka CDM atamkataza mara moja sasa utajiuliza kwa nini amkataze. Zinduka kaka Arusha saizi inatawaliwa na CDM na CCM
 
Hivi maandamano yale yote yalilenga kugawana madaraka kati ya CDM na CCM??!! na sio kurudia Uchaguzi wa meya. Basi kama ndo hivyo we hv a long journey to approach a radical change.
Huu haukuwa msimamo wa CHADEMA yaani kugawana m,adaraka walitaka uchaguzi urudiwe bila kujari kama CCM watashinda au CDM watashinda...hii ya kugawana imekuja baada ya majadilianao na fikiri na ushauri wa viongozi mbalimbali tukumbuke raisi msitafu wa ujerumani hivi majuzi alikuja hapa Arusha kujadilia kuhusiana na swala hili...
 
Tunaomba tu wasije wakafunga ndoa na hawa ccm kama ilivyowakuta wenzao cuf huko zanzibar. Nakumbuka wakati maalim seif anatangaza maridhiano na ccm, baadhi ya wanacuf walionekana wakilia kwa hasira kwenye televisheni.
hakika hata hapa Arusha leo hii ukipita mitaani kukusanya maoni watu wamegawanyika sana vijana wengi hawaungi mkono tofauti na watu wazima wengi wanaunga mkono...
 
So tatizo ilikua ni kupata nafasi za uongozi tu
na sio mchakato wa uchaguzi kubakwa?

shame on mbowe,you can't stand for what is right!
Yaani hii itatumika kisiasa dhidi yenu kwamba "mna uchu wa madaraka"
hadi mjute,

Am watching

Ahsante mkuu, sasa hii nayo inatofauti gani kati ya ndoa ya CUF na CCM kule Zenji? Yaani duh! kumbe CDM wanapenda sana uke wenza...nataka sitaki kumbe ndio ilipowafikisha hapa. Poleni sana..lakini ndio hivyo tena mmeshaolewa na CCM.
 
Kwenye hili jambo la Arusha. CDM wamepoteza Status yao!! ni ngumu sana tena kuwajenga watu hasa vijana kujitolea kwenye mapambano kama mwisho wake ni kukaa mezani na kugawana madaraka
 
Hii ina maana gani? mie nachanganyikiwa na sielewi, nahitaji ufafanuzi zaidi wanajamvi.
Ni majuzi tu CHADEMA walizunguka nchi nzima wakisema CUF ni CCM B kwa sababu imeunda serikali na CCM zanzibar.
Leo CHADEMA nao wamekubali kuunda serikali ndogo Arusha kwa kushirikiana na CCM, natizama suala hili kwa umakini mkubwa mno, naanza kupata mashaka makubwa sana na CDM.
Ina maana CUF kuunda serikali moja na CCM ni dhambi kubwa mno lakini CHADEMA kuunda serikali moja na CCM siyo dhambi?
Naomba kila mwenye akili atumie akili zake hapa, tuweke ushabiki wa vyama pembeni.
CUF + CCM - ZANZIBAR = CUF ni mke wa CCM, CUF ni CCM B, CUF ni kibaraka wa CCM, CUF siyo chama cha upinzani.
CDM + CCM - ARUSHA = CHADEMA ....................................????????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Nisaidieni.
 
Lazima Chadema watueleze wazi kitu gani kiliwafanya wafikie hatua hii,wakati msimamo ulikuwa mwingine,vinginevyo tuache kuwaunga mkono kabisa hawawezi kula matapishi yao ,maelezo inaonyesha uchaguzi ulifanyika kwa baadhi ya nafasi na nafasi nyingine hazikuguswa hii ni uamuzi wa hovyo sana kisiasa
 
Huu haukuwa msimamo wa CHADEMA yaani kugawana m,adaraka walitaka uchaguzi urudiwe bila kujari kama CCM watashinda au CDM watashinda...hii ya kugawana imekuja baada ya majadilianao na fikiri na ushauri wa viongozi mbalimbali tukumbuke raisi msitafu wa ujerumani hivi majuzi alikuja hapa Arusha kujadilia kuhusiana na swala hili...

Hapo sasa ndio panapoudhi kwani wao wanaweza kubadilisha ajenda kwa sababu ya mtu fulani,wasipolijibu vizuri hili litawagharimu,lazima tuelezwe kwa uwazi kabisa kitu gani kimepelekea uamuzi wa ajabu ajabu huu
 
sasa nimeamini kuwa kila mara ccm wanacheza ngoma ya chadema ambayo inawatesa sana na hasa mzimu wa dr slaa, nadhani ndio kazi ya siasa hiyo si mchezo......... makamba analo na kauli zake za kutofanya muafaka wa pamoja, lowasa aliwaambia mapema kabla hawajamua kumvua gamba.
What a wonderful politics!
 
Mimi nadhani Chadema si wagomvi .Ila CCM wamejifunza kutokana na hili matumizi ya madaraka vibaya hayatakiwi .Hongereni Chadema jipangeni tena uchaguzi ujao .
 
Huu haukuwa msimamo wa CHADEMA yaani kugawana m,adaraka walitaka uchaguzi urudiwe bila kujari kama CCM watashinda au CDM watashinda...hii ya kugawana imekuja baada ya majadilianao na fikiri na ushauri wa viongozi mbalimbali tukumbuke raisi msitafu wa ujerumani hivi majuzi alikuja hapa Arusha kujadilia kuhusiana na swala hili...
Mkuu, kwa hiyo huu Mwafaka ni wa Rais wa zamani wa Ujerumani, tunashukuru kwa taarifa zako, Pro-Chadema msiwe na wasiwasi huu sio msimamo wa CDM
 
Mzee MAKAMBA ashitakiwe kwa kukaidi mawazo ya busara aliyoyatoa LOWASA!Laiti ccm ingekubali kukaa chini kwa mazungumzo kama walivyofanya sasa mauaji yasingetokea!
 
Arusha imetutia aibu wana CDM. Sikutegemea muafaka kama ule. Kwani kura zingefanya nini kurudiwa zote. Wanaleta demokrasia ya namna gani? Sheria zilivunjwa, wananchi wakalia, wakafa ili haki itendeke. Viongozi wote wana kesi. Kilio chetu tunataka uchaguzi huru na wa haki. Hivi kweli tutafika kwa hatua hizi. Ngoja 2015 utaona, CCM watatupiga katafunua wakijua tukipewa umakamu meno kama kenge. Doesnt look good. Hata kama alikuja nani, swala lilikuwa lazima sheria zifuatwe ili kuwa fundisho la kuvunja sheria na kuleta mamluki.

Halafu kichefu chefu kingeni nimesoma kwenye magazeti, eti Meya alichaguliwa kihalali. Come on my leaders naomba mmoja aje hapa atoe maelezo nini mmekifanya Arusha. Na hili si swala la madiwani, majibu ya kisanii hayatakubaliwa. Najua Chama ndicho kimeamua kupokea huo muafaka. Maelezo kabla mizuka haijutupanda. Huku sio kwa Magamba, wanaambiwa magamba ni watu wote wanakenua.
 
Ingawa washabiki wa pande zote tupo wengi lakini inafaa tuwapongeze wote wawili, CCM na CDM kwa kufikia muafaka. Kuna siku mtu alisema humu JF, sikumbuki ni nani, aliwaasa CDM wajifunze kutoka kwa CUF.

Siasa maana yake ni Siasa, it should be give and tack on our leaders for the benefit of us, Raia.

Hongera CCM
Hongera CHADEMA.

Haya mods, fungeni huu mjadala tukabishane mengine hukoooo.

Kumbe, wewe huwa unabishana lo, sikujua hilo nilifikiri huwa unamaanisha unachosema.
 
Mkuu, kwa hiyo huu Mwafaka ni wa Rais wa zamani wa Ujerumani, tunashukuru kwa taarifa zako, Pro-Chadema msiwe na wasiwasi huu sio msimamo wa CDM
Aliekutangulia akikushauri ni vema ukamsikiliza ukifanya kinyume utaitwa ushauriki kama alivyo Kikwete, cha msingi ni kuchuja ukiona yana maslahi kwa wananchi basi huna budi kufanya hivyo lakini uking'ang'ania maslahi ya chama kama CCM navyofanya basi tungepotea wengi maandamano amabyo yangefanyika sasa hivi kupiga meya fake....
 
Ni kwa bahati mbaya mgogoro huo umeisha baada ya watu kupoteza maisha. Kama sio ubabe wa mwanamagamba Yusufu Makamba haya yote yasingetokea. Kumbe walikuwa na uwezo wa kukaa chini na kuzungumza. CCM waache kuwatumia Polisi kwa mambo ambayo yangeweza kutatuliwa kirahisi.
 
Walio uwawa? waliojeruhiwa? wliosota rumande? walio na kesi mahakamani? walioingia gharama? ....... yaani wasifanye maksihara kabsaaa hii ni vitaa No Retreat, No Surrender.
 
Back
Top Bottom