Mwafaka wa Umeya wa Arusha wapatikana

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Hatimae ule utata wa meya ulio sababisha watu watatu kupteza maisha umepatiwa ufumbuzi baada ya mazungumzo yaliyokuwa yakifanywa na Waziri mkuu na Freeman Mbowe, kufikia mwafaka kuwa madiwa wakae wakubaliane ndipo leo walipo kaa madiwa wakafikia wamfaka kama ifatavyo...

Meya Gaundence Lyimo CCM
Naibu Meya Mallah CDM alipata kura 22 kati ya 25...2 zilisema hapana na 1 iliharibika
Kamati ya Uchumi na Elimu Bayo CDM
================
Peter Saramba na Moses Mashalla, Arusha
HATIMAYE mgogoro wa uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Arusha umepata ufumbuzi baada ya pande zinazohusika kufikia muafaka wa kupokezana madaraka.

Katika muafaka huo uliofikiwa baada ya majadiliano yaliyodumu kwa zaidi ya miezi miwili CCM kitaendelea kushikilia nafasi ya umeya huku Chadema kikipewa unaibu kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.

TLP kitachukua nafasi ya unaibu meya kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya ile minne ya Chadema kukamilika

Makubaliano mengine ni Chadema na CCM kuongoza kwa kupokezana kamati mbili za kudumu za uchumi, elimu na afya na ile ya mipango miji, mazingira na ujenzi ambapo kikao cha jana kiliwachagua John Bayo (Chadema) na Ismail Katamboi (CCM) kuongoza kamati hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani wa Manispaa kilichomchagua diwani wa Kimandolu, Estomi Mallah kuwa naibu meya, mwenyekiti wa kamati ya muafaka, Michael Kivuyo alisema uamuzi huo umejali maslahi ya umma na kuweka pembeni itikadi na maslahi ya vyama.

"Tumekubaliana kusahau yote yaliyotokea nyuma, tumeanza ukurasa mpya kwa maslahi ya wananchi ambao wanahitaji kuunganishwa na viongozi wao katika harakati za maendeleo ambayo hayajali itikadi," alisema Kivuyo.

Kwa upande wake, Meya liyekuwa akipingwa uchaguzi wake, Gaudance Lyimo alisema "Nimeufurahia muafaka huu. Kimsingi tungeweza kuendelea na shughuli zote, lakini ingekuwa ngumu kutekeleza majukumu yetu katika hali iliyokuwepo,"

Alisema ni afya kwa maendeleo ya Manispaa ya Arusha kufanya kazi pamoja na madiwani wa vyama vyote, hasa Chadema yenye idadi kubwa kwa maendeleo ya umma uliowaamini na kuwachagua.

Meya Lyimo ambaye ni diwani wa Kata ya Olorieni aliwagiza watendaji wote wa Manispaa kuwapa ushirikiano unaostahili madiwani wote katika utekelezaji wa majukumu yao bila kubagua wala kuangalia itikadi za vyama vyao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha aliyekuwa mmoja wa wajumbe walioshiriki vikao vya kutafuta muafaka huo alisema tatizo la uchaguzi wa meya na mauaji yaliyotokea yalikuwa ni jambo la kusikitisha ambalo katika muafaka huo wamezingatia makubaliano yatakayohakikisha hayatajirudii siku zijazo.

"Natoa wito sasa kwa madiwani wote kutekeleza wajibu wao kuwakilisha na kutetea maslahi ya wananchi bila kujali itikadi za vyama vyao kwai kiongozi akishachaguliwa anawakilisha watu wote wenye itikadi tofauti na hata wasiokuwa na vyama," alisema Mushi.

Naibu Meya mpya kwa upande wake, aliahidi ushirikiano wa dhati kwa Meya na madiwani wote ili kuharakisha na kufanikisha maendeleo ya Manispaa ya Arusha yaliyokwama kwa kipindi kirefu kutoka na mgogoro uliokuwepo.

"Naamini sasa mstahiki Meya atapata usingizi baada ya muafaka huu kwani alikuwa akiwiwa vigumu kutekeleza majukumu yake. Wananchi wa Arusha sasa watarajie kuona na kupata maendeleo yaliyokusudiwa," alisema Mallah.

Zaidi ya Mkuu wa Wilaya na mwenyekiti wao, Kivuyo, kamati ya kutafuta muafaka wa mgogoro huo uliosababisha vifo vya watu watatu Januari 5, mwaka huu, iliundwa na wajumbe 10, watano kutoka CCM na wengine Chadema.

Kutoka Chadema wajumbe walikuwa wa kamati hiyo iliyoanza vikao vyake tangu Aprili mwaka huu walikuwa John Bayo, Samson Mwigamba, Efatha Nanyaro na Amani Golugwa wakati CCM iliwakilishwa na Abdulrasul Tojo, Ismail Katamboi, Lilian Mmasi, Karim Moshi, Musa Sunja na Meya Lyimo.

Baada ya kikao cha muafaka na uchaguzi wa naibu meya na wenyeviti wa kamati mbili za kudumu, madiwani wote walisimama, kushikana mikono na kuimba wimbo maarufu wa kuhimiza mshikamano maarufu kwa jina la ‘solidarity forever'.

Wimbo huo uliashiria mwisho wa mgogoro na mwanzo wa ushirikiano.

Maswali ambayo CHADEMA WASIPO yafanyia kazi yatawagarimu

1. Ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya polisi waliouwa raia wasiokuwa na hatia? Je, serikali itafanya nini kwa ajili ya familia za waliouwawa tar.5 jan??

2. Je Mary chatanda bado ataendlea kuwa mjumbe halali wa halmashauri ya manispaa ya Arusha??.
 
sasa hapo kulikua na haja ya kupigwa raia risasi?kumbe jambo lenyewe linazungumzika.na walioua watachukuliwa hatua gani?
 
Hatimae ule utata wa meya ulio sababisha watu watatu kupteza maisha umepatiwa ufumbuzi baada ya mazungumzo yaliyokuwa yakifanywa na Waziri mkuu na Freeman Mbowe, kufikia mwafaka kuwa meya ataendelea kubaki yule yule wa CCM na naibu meya atakuwa mallah na mwenyekiti wa kamati zote atakuwa John Bayo...nitaendelea kuwajuza zaidi
Tujuze mkuu; Mallah anatoka chama gani na pia John Bayo
 
Tujuze mkuu; Mallah anatoka chama gani na pia John Bayo

Estomih Malla ni Diwani wa CHADEMA kata ya Kimandolu na Bayo pia anatoka CDM. Malla ndiye aliyetakiwa awe Meya wakamweka mamluki wao Lyimo.
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Hakuna demokrasia isiyo na gharama. Viva Chadema. Hawa Magamba bila kujitoa mhanga wangefika mahali wangekuja kutupora mpaka wake zetu kama walivyokuwa wanafanya Machifu wa zamani maana walishataka kujiona ni Miungu watu.

Vipi ule utetezi wa Lema bungeni, au Spika kaupotezea!

Je katika mazungumzo hayo Waziri mkuu (Mzee wa Wapiga mizinga Bungeni) ameomba msamaha kwa kulidanganya Bunge!
 
Hatimae ule utata wa meya ulio sababisha watu watatu kupteza maisha umepatiwa ufumbuzi baada ya mazungumzo yaliyokuwa yakifanywa na Waziri mkuu na Freeman Mbowe, kufikia mwafaka kuwa meya ataendelea kubaki yule yule wa CCM na naibu meya atakuwa mallah na mwenyekiti wa kamati zote atakuwa John Bayo...nitaendelea kuwajuza zaidi

Kijana Crashwise nakupongeza mkuu;haya mazungumzo yamefanyika lini na wapi mbona nimemwona Mbowe bungeni leo au walifanya over the weekend?
 
Hatimae ule utata wa meya ulio sababisha watu watatu kupteza maisha umepatiwa ufumbuzi baada ya mazungumzo yaliyokuwa yakifanywa na Waziri mkuu na Freeman Mbowe, kufikia mwafaka kuwa kama ifatavyo

Meya Lyimo CCM
Naibu Meya Mallah CDM
Kamati ya Uchumi na Elimu Bayo CDM
Kamati ya Fedha Lyimo TLP

Mkuu hii ni habari njema sana
Hongera kwa kutujuza
Hebu tupe mazungumzo kamili yalikuwaje maana tumechoka kila siku Arusha kusikia habari za meya
 
Kijana Crashwise nakupongeza mkuu;haya mazungumzo yamefanyika lini na wapi mbona nimemwona Mbowe bungeni leo au walifanya over the weekend?
Haya mazungumzo yalikuwa yakiendelea tangu CHADEMA TAIFA walipo toa siku 21, ndipo kabla ya siku 21 kuisha serikali kupitia waziri mkuu wakaanza mazungumzo hata yule raisi msitaafu wa ujerumani aliekuja juzi alikuja kwa mazungumzo hayo hayo..
 
So tatizo ilikua ni kupata nafasi za uongozi tu
na sio mchakato wa uchaguzi kubakwa?

shame on mbowe,you can't stand for what is right!
Yaani hii itatumika kisiasa dhidi yenu kwamba "mna uchu wa madaraka"
hadi mjute,

Am watching
 
Mkuu hii ni habari njema sana
Hongera kwa kutujuza
Hebu tupe mazungumzo kamili yalikuwaje maana tumechoka kila siku Arusha kusikia habari za meya
Hizo ni taarifa juu ya mwafaka kuhusiana na mwenendo mzima wa mazungumzo sijui naamini kuna viongozi wa CDM humu watakuja kuyaweka wazi...
 
Hizo ni taarifa juu ya mwafaka kuhusiana na mwenendo mzima wa mazungumzo sijui naamini kuna viongozi wa CDM humu watakuja kuyaweka wazi...

Asante sana mkuu kwa taarifa
tutasubiri watufafanulie watakapokuja humu jamvini
ila ni jambo bora sana kufikia mwafaka wa jambo hilo
 
So tatizo ilikua ni kupata nafasi za uongozi tu
na sio mchakato wa uchaguzi kubakwa?

shame on mbowe, you can't stand for what is right!
Yaani hii itatumika kisiasa dhidi yenu kwamba "mna uchu wa madaraka"
hadi mjute,

Am watching
naamini watalitolea ufafanuzi...
 
Sasa huo uchaguzi umefanyika lini? bado ni uvunywaji wa sheria na kanuni maana wanahitajika kuitisha full council na kufanya uchaguzi wa Meya baada ya idadi ya wajumbe wanaohitajika kufika. Hapo bado sheria imekiukwa!!
 
So tatizo ilikua ni kupata nafasi za uongozi tu
na sio mchakato wa uchaguzi kubakwa?

shame on mbowe,you can't stand for what is right!
Yaani hii itatumika kisiasa dhidi yenu kwamba "mna uchu wa madaraka"
hadi mjute,

Am watching
Ni bora kuliko kuendeleza uhasama na watu wakaendelea kufa. Wamefikiria maisha ya watu kwanza, kwa sababu wangeendelea kukomaa na uchaguzi, uchaguzi usingefanyika na matokeo yake ni fujo na mauaji tena. Hongera Mbowe kwa muafaka huu. Mr Speaker continue watching.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom