Mwafaka wa Umeya wa Arusha wapatikana

hakika mhe mbowe una kesi ya kujibu...tena majibu ya msingi yatakayoturidhisha wananchi wa arusha na wapenzi wa chadema.
Tumesikia muafaka umepatikana khs meya wa arusha tunafurai ni jambo jema kwetu lkn pia tumesikia kulikuwa na majadiliano ya siri yakiendelea kati ya mbowe na pinda na hatimaye kufikia muafaka huo wa arusha hapa sasa ndipo shaka ilipo. Wakati bavicha-arusha wakifanya maandalizi ya maandamano mengine kupinga uchaguzi wa meya huyo, kwa bahati nzuri tukasikia maandamano hayatakuwepo


ulitaka mazungumuzo yafanyikie kwenye uwanja wa shekh amri abeid? Umetumwa na n.e.p.i wewe.
 
Hakika ni vigumu kuwaelimisha waliojiandaa kutokuelemika.
Nyerere aliwai kusema ni lazima Walimu wawafundishe wanafunzi kuwa wadadisi wasiwe wanakubali tu kwa urahisi. Cdm ni chama cha watu makini wenye uwezo wa kupembua na kudadisi.
 
Mwanaharakati unatumia ngucvu nyingi sana kujaribu kuibua mgogoro kuhusu muafaka huo. Kwanza ujue watanzania wanakitazama CDM kwa macho mawili kutokana na propaganda chafu za CCM kuwa ni chama cha fujo. Hivyo kitendo cha kukubali kuingia katik amuafaka kuhusu jambo hilo ni ushindi mkubwa sana kwa CDM na wote wanaokitika mema. Watanzania nchi nzima wangeliishangaa sana CDM kukataa kufanya muafaka kuhusu suala la Meya, cheo ambacho kisipojazwa Halmashauri ya Arusha inaweza kuendelea kuwepo na kuwapatia wananchi wa Arusha huduma kama kawaida.Watanzania hivi sasa wanaitegemea sana CDM kwa ajili ya kudai hgaki zao mbali mbali hivyo isingekuwa busara kungangania jambo moja wakati wote, ili mradi haki ya wanaarsha imeshapatikana japo ni katika mufaka. Ni lazima katika siasa tujue kuwa upo wakati itabidi ufanya "Give and Take"
Nadhan kitu cha msìngi ni kuangalia maridhiano kati yao kama yana kidhi haja ya wadhirika (Watanzania) wala si usiri wao, tufahamu kwamba there are things to succeed nids secrecy bt shld adhere atleast prìncplfs of transparency !! BUT ARUSHA- BAVICHA walisema NO mandamano coz kulikuw na source from Mr F.M -Kijana Jenga hoja kufuata Facts na sio Hisia
 
Wakuu,
Kwa miezi kadhaa Mkoa wa Arusha umekuwa katika mgogoro uliosababishwa na uchaguzi wa Meya na naibu meya kupingwa kwa kuwa inasemekana ulikiuka kanuni za uchaguzi. Jambo hili lilipelekea umwagaji wa damu na hata kufunguliwa kwa kesi kwa baadhi ya makamanda wa chadema.

Hivi majuzi hatimaye suluhisho la mgogoro huo lilipatikana kwa kufikia makubadiano ya kugawana madaraka. Je, hii yaweza kuwa janja ya ccm kupunguza kasi ya chadema Arusha kama ilivyofanya kwa Cuf Zanzibar?
 
Thats exactly what I thought. Nilianzisha a similar thread on this. Kwahiyo matokeo ya uchaguzi 2015 inaweza kuwa serikali ya mseto?
 
Wakuu,
Kwa miezi kadhaa Mkoa wa Arusha umekuwa katika mgogoro uliosababishwa na uchaguzi wa Meya na naibu meya kupingwa kwa kuwa inasemekana ulikiuka kanuni za uchaguzi. Jambo hili lilipelekea umwagaji wa damu na hata kufunguliwa kwa kesi kwa baadhi ya makamanda wa chadema.

Hivi majuzi hatimaye suluhisho la mgogoro huo lilipatikana kwa kufikia makubadiano ya kugawana madaraka. Je, hii yaweza kuwa janja ya ccm kupunguza kasi ya chadema Arusha kama ilivyofanya kwa Cuf Zanzibar?

Mimi nafikiri sio jambo baya kufikia muafaka kama huo wa Arusha. kilichotakiwa tu ni kwamba inatakiwa maelezo ya kina yatolewe juu ya mazingira ya muafaka huo. kwa kuwa serikali imetumia gharama nyingi kupotosha umma kuhusu matukio hayo ya Arusha, ndio maana imejificha katika muafaka huo, kukwepa kujibu maswali magumu, kama ambavyo mpaka sasa hivi Spika Makinda amekuwa bubu kuhusiana na lile sakata la PM Pinda kusema uwongo bungeni. serikali haitakiwi kujifunika shuka kwa mambo ya Arusha. shuka iondolewe na wenye wajibu wa kufanya hayo yote ni CHADEMA
 
Ndugu wanawema wenzangu nimelazimika kuzungumzia swala la Arusha kwani nimeshangazwa sana na aina ya makubaliano yaliyofanyika na kufikiwa na kuitwa muafaka hapa napata swali gumu sana kwani tatizo la mgogoro wa Arusha lilikuwa ni nini? Chadema kukosa madaraka ya umeya au Uchaguzi batili wa kuchagua meya? kwenye suluhisho eti Chadema wamepewa unaibu meya tena kwa miaka minne kwa kupokezana na TLP jamani haya ni maajabu ya mwaka kwakweli nimeshangaa sana na kwa suluhisho hili ni kwamba tatizo kumbe si haki ni madaraka! kwa maana kwamba suluhisho sasahihi ilikuwa lazima kurejea kwenye hoja ya msingi ambayo ni kuwa UCHAGUZI WA MEYA WA ARUSHA HAUKUWA HALALI kwani ulikiuka sheria za uchaguzi hivyo basi SULUHISHO HALALI LILIKUWA NI KURUDIA UCHAGUZI HUO ATAKAYESHINDA YEYOTE AONGOZE hapo ndio suluhisho sahihi. Mtazamo wangu mimi suluhisho lolote nje na hili ni BATILI hoja ya kugawana nafasi ya unaibu meya kwakweli haikuwa hoja ya msingi kwani sheria inapopindishwa suluhisho ni kufuata Sheria na sikuendelea kuipindisha.Chadema wafanye Uchunguzi namna muafaka huu ulivyofikiwa ninauhakika lazima kuna namana iliyofanyika huyo naibu meya achunguzwe na vyombo halali vya chama
 
Kaka Mgheni nilishasema sana hapa jamvini juu ya huo muafaka lkn kwa sababu wanajamvi wengi wametekwa na fikra za mtu mmoja mmoja ndani ya Chadema basi kuelewa imekuwa ngumu sana. Ni vyema tukahoji muafaka huu umefanyika kwa maslahi ya wananchi au chama? na kwanini kulikuwa na siri nzito juu ya majadiliano ya muafaka huu kati ya Pinda na Mbowe? Tunataka kuijenga Cdm bora na Si bora Cdm kama ilivyo Cuf, Tlp, Nccr. Cdm kila mwanachama ana haki ya kuhoji tusilewe na sifa mtu mmoja. viva Cdm, viva Tz.
 
Hapa chadema waliona ccm hawawezi kuachia hicho kiti hata kwa rungu au mtutu ndio maana hata Kama sheria zilivunjwa wakalainika kusema kweli hata mi nilihoji sana humu jamvini ila hatuna namna walishakubaliana imeshatoka.
 
Mara baada ya ubabe na ukiukaji wa waziwazi wa uchaguzi wa Meya mjini Arusha Desemba 2010,Chadema na wakazi wa Arusha waliamua kuionyesha dunia kuwa wanaweza kudai haki hata kwa gharama yoyote.CCM kwakutoamini nguvu ya umma wakapambana na raia na kuwauwa watu watatu na kudhihirisha nguvu ya umma haizuiliki siku ya mazishi serikali yote ikaenda likizo kwa hofu ya maelfu ya watu walioandamana na kufanya maziko kwa amani.

Viongozi wa Chadema na wananchi walipigwa,kudhalilishwa na kujeruhiwa na wengine wana vilema vya maisha achilia mbali wale waliouwawa.Hamasa yote ilitokana na viongozi wa kitaifa na mkoa wa CDM kuwatia moyo wananchi kudai haki zao nakuonyesha wako pamoja nao kwa matangazo ya redio,magari barabarani,mabango n.k.Leo hii bila taarifa yoyote kwa wananchi wa Arusha tunaambiwa CDM wamemkubali Meya FEKI na CDM watachukua unaibu meya na TLP(wenye diwani mmoja).Hakika wanasiasa ni wapuuzi wa hali ya juu kabisa hapa duniani wao wanachowaza ni madaraka tu na wananchi tunafanya daraja lao.CHADEMA MNAWACHEKA NA KUWATUKANA CUF KWA KUFUNGA NDOA HALALI (KWA KATIBA YA ZNZ) HUKU NYIE MKIFUNGA NDOA YA MKEKA WA WEZI WA MCHANA.SHAME ON YOU SIMPLE MINDED LEADEARS OF CDM ESPECIALLY LEMA,ambaye nakuhesabu kama mcheza komedi fulani NA MAPOLISI WA aRUSHA.

Hakuna asiyetaka maelewano na amani na mwenzake lakini kwanini wadau hatujashirikishwa na kupewa taarifa kama wakati wa sekeseke na mnaendelea kukaa kimya mkijidai mko busy bungeni kumbe ni matumbo yenu tu.

Arusha huwa hatuangalii chama tunaamua kwa kuangalia watendaji na misimamo yao hivyo CDM msidhani mmepata mnaweza poteza kila kitu hapa kwa unafiki wenu.Au mmesahau Arusha ilikuwa ya NCCR na baadaye TLP na nyie hamkuwa na hata diwani?

PEOPLES POWER HAICHAGUI CHAMA!!!!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom