Mwafaka wa Umeya wa Arusha wapatikana

Mwafaka wa Umeya wa Arusha wapatikana

huku kugawana madaraka kutaligharimu taifa hili....siku hizi ndo mchezo huo africa nzima
 
huku kugawana madaraka kutaligharimu taifa hili....siku hizi ndo mchezo huo africa nzima

Inakera sana, watu wanajitoa mhanga kwa ajili ya demokrasia ya kweli, halafu leo wanaleta mzaha. Heri wangerudia huo uchaguzi ashinde huyo mwizi. Sasa kama kulikua kunauwezekanao wa kugawana madaraka mezani, kwanini tuliaminishwa vinginevyo. Afrika kweli ni bara la giza. Ndio maana hatuendelei kila kitu tunafanya mzaha.

Kesho watatuibia fedha za kodi zetu mwishowe watakuja na majibu marahisi kama ya JK rudisha yaishe. Mkirembulia uwajibikaji wa sheria mnajenga shimo ambalo hakuna atakayeweza kufukia. Lazima sheria zifuate mkondo na gharama zake, ndio chimbuko la utawala wa haki na usawa. Hakuna njia za mkato. Tunapigia kelele haki za mezani ndizo zinazotufanya wanyonge na masikini. Je ni wangapi wanaporwa haki na hakuna swala la muafuaka mezani? Je Ndigu wa marehemu waliokuwa wanapigania haki, kweli wanahadhi ya haya yanayotokea. Je kesho CCM wakiiba kura na kujitangazia ushindi tuamini tena kutetea ushindi wa mezani ?

Afrika inasikitisha sana. Tanzania inakera sana. Ndio maana kila kitu shaghala baghala.
 
Tunaomba viongozi wa cdm waje hapa ukumbini watupe tamko la chama ili iwe taarifa ya hakika.mweshimiwa Regia njoo ututolee huu utata.
 
mkuu ila kilichofanyika sicho kwakuwa CDM walikuwa wanapigania mfumo mbovu uliyotumika kumpata meya, CDM walipinga sana na kutaka uchaguzi urudiwe ishinde au isishinde ila taratibu na kanuni zifuatwe nasikugawana madaraka kama ilivyotokea.vile vile CDM walipinga mifumo kama hiyo iliyotokea sehemu mbalimbali kama kenya, ivory cost na kungineko kule kulikotokea mkanganyiko wakupindisha sheria kwa uchu wa madaraka.kwa hili CDM wakubali yakuwa wamechemsha au nisema kwa msisitizo tumechemsha kukubali kuruhusu mianya kama hii ya kupindisha sheria na kujenga mazoea ya kufanya mazungumzo mbeleni huko.CDM hapa hatujamaliza tatizo bali tumeongeza tatizo tena kubwa sana, na mjue yakuwa mmemuweka LEMA kwenye wakati mgumu sana kwakuwa siku zoe amekuwa akipigania ukweli sasa nyie kwakuwa ni wengi mmeupindisha ukweli, na kura iliyo haribika ilikuwa ni yadiwani wa kata ya revyolosi mh NANYARO ambaye alipinga sana uchanguzi huwo ambao umewasaliti wananchi.JF tuache kushabikia ujinga CDM ikikosea lazima tuikosoe kwakuwa ndicho chama cha matumaini ya watanzania na ni chama kinachoenda ikulu, utaratibu kama huu ni wakupinga sana ili siku nyingine usijirudie tena.haya ni mawazo yangu binafsi kama wengine jinsi walivyotoa mawazo yao
Naunga mkono mkuu na hii hali ikendelea kuachiwa itatufikisha hapo cuf ilipo sasa lazima tumaanishe na kupigania kile tunachokiamini siku zote, ikiwa tulipinga utaratibu wa kumpata meya then leo mnakuja na muafaka ambao hakuna kiongozi yeyote wa chama aliwahi sema kuna mazungumzo yanaendelea huku damu za watu zilishamwagika kumbe mngeweza epusha hili mapema binafsi nasikitika sana . Tunaomba chama watoe tamko juu ya huo muafaka pia mikakati gani watafanya kuhakikisha kanuni zememushikeri zinabadilishwa ili lisijirudie tena au baada ya kupata uongozi imekuwa basi!
 
Bora malumbano yameisha. Sasa wananchi wanataka kazi ionekane sio majigambo.
 
Chadema wamefunga ndoa na CCM, ya kuitawala Arusha, inachekesha sana nyie Pro-Chadema-JF, leo mmepongeza Muafaka wenu na CCM wakati Muafaka wa CCM na CUF, Zanzibar Mlikuwa kila siku mnaukejeli ikafikia mpaka viongozi wenu wakasema awawezi kuungana na CUF, sababu wameungana na CCM, leo Chadema wamefanya nini kama sio na wao wamefunga Ndoa na CCM. Mahakama kuu ya Arusha wanajiandaa kuwafutia Kesi viongozi wa Chadema ili kubariki ndoa, sasa sijui Lema na wenzake watafanyia wapi maandamano yao saizi wao wameolewa na CCM
 
Hongera, Chadema kwa kuweka maslahi ya wana Arusha mbele. Pia hongera CCM kwa kugundua kwamba umbumbu wa Makamba hauwafai kwa sasa
 
Naunga mkono mkuu na hii hali ikendelea kuachiwa itatufikisha hapo cuf ilipo sasa lazima tumaanishe na kupigania kile tunachokiamini siku zote, ikiwa tulipinga utaratibu wa kumpata meya then leo mnakuja na muafaka ambao hakuna kiongozi yeyote wa chama aliwahi sema kuna mazungumzo yanaendelea huku damu za watu zilishamwagika kumbe mngeweza epusha hili mapema binafsi nasikitika sana . Tunaomba chama watoe tamko juu ya huo muafaka pia mikakati gani watafanya kuhakikisha kanuni zememushikeri zinabadilishwa ili lisijirudie tena au baada ya kupata uongozi imekuwa basi!
Kama wewe si mfuatiliaji wa mambo tutakusaidiaje sasa.
 
Chadema wamefunga ndoa na CCM, ya kuitawala Arusha, inachekesha sana nyie Pro-Chadema-JF, leo mmepongeza Muafaka wenu na CCM wakati Muafaka wa CCM na CUF, Zanzibar Mlikuwa kila siku mnaukejeli ikafikia mpaka viongozi wenu wakasema awawezi kuungana na CUF, sababu wameungana na CCM, leo Chadema wamefanya nini kama sio na wao wamefunga Ndoa na CCM. Mahakama kuu ya Arusha wanajiandaa kuwafutia Kesi viongozi wa Chadema ili kubariki ndoa, sasa sijui Lema na wenzake watafanyia wapi maandamano yao saizi wao wameolewa na CCM

Wewe inaonekana mtoto wa juzi kwani Kigoma mbona Chadema waliwahi kuongoza halmashauri kwa kupokezana umeya? Nani kakwambia kushirikiana na mtu ni kufunga naye ndoa? Of course siungi mkono msimamo wa Chadema kuhusu CUF na serikali ya umoja wa kitaifa
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Wewe inaonekana mtoto wa juzi kwani Kigoma mbona Chadema waliwahi kuongoza halmashauri kwa kupokezana umeya na CCM? Nani kakwambia kushirikiana na mtu ni kufunga naye ndoa? Of course siungi mkono msimamo wa Chadema kuhusu CUF na serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar ya ya
 
uliza kigoma ilikuwaje?

huna hoja ,umejaa ubishi ubishi tuu
 
Wewe inaonekana mtoto wa juzi kwani Kigoma mbona Chadema waliwahi kuongoza halmashauri kwa kupokezana umeya na CCM? Nani kakwambia kushirikiana na mtu ni kufunga naye ndoa? Of course siungi mkono msimamo wa Chadema kuhusu CUF na serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar ya ya
muafaka wa CCM na CUF Zanzibar tunaweza kufananisha? na wa Arusha kati ya CCM na CDM...
 
Chadema wamefunga ndoa na CCM, ya kuitawala Arusha, inachekesha sana nyie Pro-Chadema-JF, leo mmepongeza Muafaka wenu na CCM wakati Muafaka wa CCM na CUF, Zanzibar Mlikuwa kila siku mnaukejeli ikafikia mpaka viongozi wenu wakasema awawezi kuungana na CUF, sababu wameungana na CCM, leo Chadema wamefanya nini kama sio na wao wamefunga Ndoa na CCM. Mahakama kuu ya Arusha wanajiandaa kuwafutia Kesi viongozi wa Chadema ili kubariki ndoa, sasa sijui Lema na wenzake watafanyia wapi maandamano yao saizi wao wameolewa na CCM
Huna lolote wewe kawashauri kwanza magamba wamalize mgogoro wao wa Chatanda na UVCCM Arusha Chadema ina mambo mengi ya kufanya si kukalia migogoro isiyoisha.
 
Wewe inaonekana mtoto wa juzi kwani Kigoma mbona Chadema waliwahi kuongoza halmashauri kwa kupokezana umeya? Nani kakwambia kushirikiana na mtu ni kufunga naye ndoa? Of course siungi mkono msimamo wa Chadema kuhusu CUF na serikali ya umoja wa kitaifa
Hii kesi tofauti na ya Kigoma, kama umeamua kuifananisha sawa lakini ujue tatizo la Arusha uchaguzi wa meya ulikuwa na kasoro kwa mujibu wa Chadema
 
uliza kigoma ilikuwaje? huna hoja ,umejaa ubishi ubishi tuu
Hivi tatizo la Kigoma ndio likuwa kama tatizo la Arusha? unaniona mbishi lakini ata Chadema wenzako sidhani kama wamefurahia ili jambo la kugawana madaraka mezani
 
mkuu ila kilichofanyika sicho kwakuwa CDM walikuwa wanapigania mfumo mbovu uliyotumika kumpata meya, CDM walipinga sana na kutaka uchaguzi urudiwe ishinde au isishinde ila taratibu na kanuni zifuatwe nasikugawana madaraka kama ilivyotokea.

vile vile CDM walipinga mifumo kama hiyo iliyotokea sehemu mbalimbali kama kenya, ivory cost na kungineko kule kulikotokea mkanganyiko wakupindisha sheria kwa uchu wa madaraka.

kwa hili CDM wakubali yakuwa wamechemsha au nisema kwa msisitizo tumechemsha kukubali kuruhusu mianya kama hii ya kupindisha sheria na kujenga mazoea ya kufanya mazungumzo mbeleni huko.

CDM hapa hatujamaliza tatizo bali tumeongeza tatizo tena kubwa sana, na mjue yakuwa mmemuweka LEMA kwenye wakati mgumu sana kwakuwa siku zoe amekuwa akipigania ukweli sasa nyie kwakuwa ni wengi mmeupindisha ukweli, na kura iliyo haribika ilikuwa ni yadiwani wa kata ya revyolosi mh NANYARO ambaye alipinga sana uchanguzi huwo ambao umewasaliti wananchi.

JF tuache kushabikia ujinga CDM ikikosea lazima tuikosoe kwakuwa ndicho chama cha matumaini ya watanzania na ni chama kinachoenda ikulu, utaratibu kama huu ni wakupinga sana ili siku nyingine usijirudie tena.

haya ni mawazo yangu binafsi kama wengine jinsi walivyotoa mawazo yao
Kwa kweli kuna wakati nakuwa na mawazo kama yako lakini inafika sehemu najiuliza hivi kama mwafaka huu usingefanyika tulikuwa tayari kwenda msituni maana ndicho kilicho kuwa kimebaki au kulikuwa na njia gani nyingine mubadala...wakati huu maendeleo tusinge yapata achiliambali hatujayapata kwa karibu miaka 50 sasa...je wananchi wangeendelea kutuunga mkono kwa kwa miaka yote mitano, je wasinge gawanyika ingawa najua hata baaada ya mwafaka huu kuna wano pinga kabisa hasa vijana lakini watu wazima wengi wanaipongeza CDM lakini tujiulize tunaopiga mwafaka huu kipi kina manufaa kwa wananchi ukiweka kando manufaa ya chama....nina uhakika kuna vijana walikuwa tayari kuiunga mkono chadema kwa vyovyote..
 
Huna lolote wewe kawashauri kwanza magamba wamalize mgogoro wao wa Chatanda na UVCCM Arusha Chadema ina mambo mengi ya kufanya si kukalia migogoro isiyoisha.
Kwa hiyo ndoa ya Chadema na CCM, umeikubali?
 
muafaka wa CCM na CUF Zanzibar tunaweza kufananisha? na wa Arusha kati ya CCM na CDM...
Hatuwezi kufananisha kwani Zanzibar sio Manispaa. Pili, Hakuna siku Maalim Seif atabadilishana madaraka na Rais Shein. Tatu, KATIBA ya JMT wala haitambui uwepo wa Maalim Seif.
 
Inanisikitisha, Inanikera na Inaniudhi hasa ninapowakumbuka viongozi wa Cdm walipokuwa wakihamasisha watu wajitokeze kwenye maandamano bila kujali Itakadi za vyama vyao, Dini zao, Kabila zao, Rangi zao na Jinsia zao....kupinga matokeo ya Uchaguzi wa meya wa Arusha. Maskini Wakazi wa Arusha walioacha Shughuli zao na kuitikia mwito huo ambao ulipelekea kupoteza maisha ya watu 3 na wengine kupoteza viungo vyao vya mwili. Leo hii tunashuhudia makubaliano ya kugawana madaraka ya jiji la Arusha yasiyoshirikisha
 
Back
Top Bottom