Mwachieni Gire, nunueni mitambo ya Dowans!

Jamaa wa Richmond wameshaoiga mkwala kuwa mitambo yao lazima inunuliwe otherwise watamwaga Mtama kwenye kuku wengi kitu kinachohatalisha utawala wa CCM.

Hizi mbio zote ni kutetea utawala wa CCM otherwise hakuna kitu cha maana wanachojairibu kufanya. kwanini tununue mitumba wakati tunaweza kununua vipya, kila kitu mitumba ndege ya rais, rada, na vingine alivyotaja mdau huko juu, hii haingii akilini kwanini hatupendi kununua vitu vipya hata kama ni ghari, kama haiwezekani kununua si bora tuache tu.

Mimi nilikuwa nawashauri CCM kama wananweza kutangaza kuwa CCM ilitumia pesa za wananchi kwenye uchaguzi halafu wakajiudhuru wote ukaitishwa uchaguzi mpya, najua watapata credit zaidi na watarudi madarakani kuliko hii mipira yao ya paka na panya kila siku.
 
Waziri (kijana) wa mambo ya ndani kukiuka sheria za dhabuni na kuingilia mchakato wa Vitambulisho - Tunamhukumu/tunalaumu
Wabunge kutetea kukiuka sheria za manunuzi ili kununua mitambo mitumba ya dowans- Tunaunga mkono/tunapongeza

Watanzani huu utamaduni wa kufuata taratibu tulizojiwekea bado ni mchanga hatufai kuuchezea kwa gharama zozote, inabidi tufate taratibu zetu tulizojiwekea wenyewe!

Siku moja hili linaweza tumika kutuhukumu kama Ngeleja anavyosema kua ni sahihi kununua mitambo mitumba kwakua ATCL nao wamefanya vinyohivyo! kitakachofuata atakuja tokea rais aseme wananchi wananipenda nitaongeza awamu ya tatu na ya nne ya uongozi wangu hivyo tukiuke katiba kidoogo kwasasa! tuwe makini!
 
Mtanzania,

Una-determine vipi value for money na hasa ukizingatia kwamba serikali yetu iliyo madarakani imejaa mafisadi na usanii wa kila aina? Kila kitu kinaendeshwa kienyeji na malengo ya kuendesha kienyeji ni kuondoa legal implications just in case mambo yakienda kombo.

Huyo mjerumani aliyekuja kutathimini hiyo mitambo alikuwa na mkataba wa kufanya hiyo kazi? Kama hakuna mkataba ama any legal agreement ya kufanya kazi hiyo na ikatokea kwamba mitambo ikaja kuwa bomu after 2 yrs, mtamshitaki nani kwamba aliwaingiza mkenge? Kwenye business kampuni ikipewa ushauri wa ku-invest sehemu fulani na pesa ikaja ikaenda na maji, mwenye kampuni ana haki ya ku-sue aliyemshauri kwa kusababisha hasara. Tukifanya hivyo hapo nitaamini kwamba tunaangalia value for money ya hiyo mitambo. Lakini mpaka dakika hii naona mambo yanapelekwa kienyeji na yakija kuharibika mbele ya safari hakuna ambaye atawajibika wala kuwajibishwa.

Tatizo jingine ni kwamba CEO wa TANESCO (Dr. Rashid) ni business partner wa mmiliki wa Dowans (Rostam). Kwanini watu wasione hapa kuna harufu? Mangapi machafu yamesemwa kuhusu Rostam na hasa anapokuwa na access na mahali fulani halafu awe na shida yake, hawezi kugonga mwamba hata siku moja. Hilo ndiyo ambalo wengi linawatia mashaka sana na kuona kwamba kuna harufu ya deal/ufisadi.

Kama mambo yakipelekwa kitaalam na kisheria, sina tatizo na ununuzi wa hiyo mitambo, ili mradi tuweke ground nzuri ya kuhakikisha kwamba mitambo hiyo ikiwa bomu basi iwepo namna ya ku-address hilo tatizo kwa mtu/watu kuwajibika ama kulipa hasara ambayo tutakuwa tumepata.

Kwa upande wa fedha, sidhani kama ni tatizo. Usishangae ukisikia kwamba bei ya mitambo hiyo ni karibu sawa na bei ya mitambo mipya. Katika hoja za TANESCO kutetea ununuzi wa mitambo ya Dowans hawajagusia swala la ukosefu wa hela ama unafuu wa bei, hoja yao kubwa ni kwamba kununua mitambo mipya mchakato wake utachukua muda mrefu na hivyo ama tununue mitambo ya Dowans au tuingie gizani.

Swali la mwisho dogo tu, kuna mahali nimesoma wanasema kwamba mitambo imetumika kwa masaa 800 (labda kama nilikosea kusoma). Masaa 800 ni sawa na mwezi mmoja iwapo mtambo unafanyakazi kwa masaa 24. Hivi kweli inawezekana mitambo hiyo ikawa imetumika kwa mwezi mmoja tu? Kuna taarifa zinasema kwamba baadhi ya mitambo ilikuja ikiwa imeishatumika kutoka huko ilikotoka, je ukijumlisha matumizi ya wakati wa mkataba kuanzia mwanzoni mwa 2007 mpaka August 2008, ina maana imetumika kwa masaa hayo tu? Hata kama ni masaa 8000 bado inakuwa ngumu kuamini kwa kiasi fulani.
 
Sipo pamoja na Zito katika hili! Anakosea mno. Hatuwezi kuhalalisha uhuni kwa kisingizo cha dharura. Tunajenga msingi mbaya wa kutofuata taratibu kwa kisingizio cha maslahi ya taifa na unafuu!

Huu unafuu unazungumziwa sasa ni baada ya kulinganisha na mitambo ipi, gharama zipi? Sula la muda(umri) wa mitambo limeangaliwa katika hoja za unafuu? Isije ikadumu kwa miaka miwili badae tukaanza kutafutana.

Ni aibu kama taifa kung'an'gania kitu haramu. Haiwezekani kila kitu kinachohusu richmond/Dowans kifanyike kwa kukiuka taratibu. Lowasa na wenzake waliyafanya walioyafanya kwa singizio cha dharura!

Tutatengeneza njia mpya ya uwizi kwa watu kuchelewa kufanya maamuzi kwa makusudi ili "dharura" ifike, tuwape "kibali" cha kukiuka taratibu na hatimae kutuibia! Ni aibu ya mwaka kwa wabunge(watunga sheria) kutetea ukiukwaji wa taratibu, ni dhihaka kubwa kwa utawala bora.

Ni kwanini serekali inataka baraka za bunge kufanya maamuzi? Hasa kwa hili! Dowans ni haramu. Hakuna maelezo yoyote yatakayosafisha haramu ile. Nakubaliana na mwakayembe kwamba nafasi ya bunge hapa ni kushauri sijui kwanini Zito anataka bunge liamue! Serekali nayo imejikausha! Mtego wa kitoto!

Ikiwa TANESCO itashindwa kututoa katika "dharura" hiyo, utakuwa ni uzembe wao, haiwezekani wakawa na suluhisho moja tu la kihuni. Ni uvivu,uzembe, uhuni na ufisadi!
 
Hivi vitu vinajulikana (Production ya umeme its not a guess work) i.e. what and when tutahitaji kuongeza nguvu ktk grid ya taifa.........Kama utaalamu wenyewe ndio huo wa kuzima moto.........basi bana

watu wamesahau kuwa this was a planned deal ya mafisadi,

Mtanzania unasahau kuwa wanasiasa hao hao ndio wametufikisha hapa tulipo, wametukimbiza na IPTL na sasa RDC/Dowans.........sasa wanakuja eti dharula....halafu unasema tunaingiza siasa kwenye mambo muhimu......ok nyie endeleeni ku-cover hizo prejudices........

usikute tunahangaika kununua mitambo michakavu wakati miradi ya umeme tuliyonayo ina uwezo wa kuzalisha beyond our need......and simply because we don't want to spend money huko kwa kuwa hakuna value for our money.......those projects are doomed White elephants.........
 
Mkuu Ogah,

Labda kama huelewi maana ya value for money. Toka lini value for money ika overide standards zilizopo?

Mnaingiza siasa kwenye kila kitu na ndio matatizo ya Tanzania.

Value for money inaendana na quality, inaendana na return ambayo inaweza kupatikana kutokana na investment fulani.

Watanzania wengi sasa wamekuwa wafuata upepo. Eti Zitto katetea ununuzi wa mitambo tayari kasaliti Watanzania, kapewa pesa na mafisadi, nonesense!

Ningelikuwa mimi mhusika ningependekeza kununuliwa baada ya kuangalia sheria zilizopo na kisha ningekuwa tayari kuwajibika kama hasara ingetokea kutokana na ununuzi huo.

Kwenye hili suala watu mmegubikwa na chuki binafsi kuliko reasoning, sawa wengi hatumpendi Rostam, lakini je ndio tuathiri nchi nzima kwa ajili ya kumkomoa Rostam?

Hizi siasa za personalities ndio mwanzo wa matatizo makubwa kwa Afrika. Kama Rostam ana makosa, mpelekeni jela lakini sio kwamba hata jambo la maana kwasababu tu Rostam anahusika basi ni kupinga tu.

Leo hii wanasiasa eti wanajua wapi kwa kununua mitambo kwa bei rahisi. Ununuzi wa mitambo ni sehemu ndogo tu, matatizo makubwa yako kwenye operational cost.

Tutapoteza miezi kujadili jambo moja huku wananchi Tanzania hawana umeme na hakuna kinachofanyika.

Sawa endeleeni na siasa zenu za do nothing! Kama Tanesco wanapesa, sasa wanasubiri nini? Si wakanunue hiyo mitambo mipya na nchi iache kuhangaika na matatizo ya umeme?

Ni rahisi sana kwa mimi hapa Mtanzania nikiwa London kupiga siasa, kwasababu sipati hasara ambazo wananchi na wafanyabiashara walioko Tanzania wanapata shauri ya matatizo ya umeme.

Mtanzania,
Nimeshindwa kukuelewa hapa! Kwa nini tununue zile mashine mitumba wakati kuna mashine nyingi na nzuri kuliko zile ambazo zitagharimu kidogo, na procurement process itakuwa simpler? Kila mtu including TANESCO wanajua mashine kama hizi zimetapakaa duniani. Ok tuwaachie hawa jamaa hizo machine zao tukanunue mashine zenye ubora. Kwa nini tununue mashine zenye dispute wakati kuna machine ambazo hazina dispute? Kwani zile machine zimetoka mars! please I do not see what kind of returns and value of money you are trying to direct us to!
 
Mtanzania,
Mkuu, huo mtazamo wa Value of money upo kwa hao wauzaji Dorwans na ndio maana wanataka kwa kila hali mitambo ile inunuliwe..Those generators worth something today in the hands of the government..kwetu sisi hazina value yoyote zaidi ya service inayotolewa..
Swala la Obama na China nadhani watu kama wewe mnashindwa kulifahamu vizuri.. Haki za binadamu zinavunjwa na Marekani yenyewe, China na Marekani ni nchi ambazo zinatumia siasa zao kuwapumbaza watu kama nyie..Nenda ktk list ya Amnesty International uone ni nchi ngapi zinakabiriwa na mashtaka ya aina hii..

Mkuu sisi na Dorwans hatuna biashara hilo kwanza..sisi na Rostam hatuna biashara isipokuwa ni wezi au mdudu ndani ya system yetu wakati Marekani na China ni nchi zilizokubaliana kufanya biashara... ndani ya biashara hiyo kama kuna watu kama Dorwans au Rostam watawawajibisha bila kujali value of money ambayo inaleta madhara kwa wananchi wake.. nadhani unakumbuka toys na maziwa ya China yaliyokuwa pulled out of sheves Marekani na China wenyewe kisha basi wahusika wake wamehukumiwa KIFO!..Now, that's what I call value of money.. wajinga kama hawa wasiojua tahamani ya maisha na fedha hawatakiwi kuishi na binadamu wengine.. Jela au kifo tu!
Unachoshindwa kuelewa ni kwamba mitambo hii ni ya UZALISHAJI sio matunda ya uzalishaji wenyewe..hivyo hao weusi unaowasema wako well equiped ktk kazi zao, wana vifaa vya kisasa na vipya sio mitumba..ONLY in TANZANIA, mitumba ndio inapewa kipaumbele..
 
Mkandara, Ogah, et. all,

Labda hamjasoma nilichoandika, nilichosema mimi ni kwamba ningeangalia value for money. Kama kuagiza mtambo mpya ni more value for money ningeshauri tuagize mitambo mipya lakini kama kununua hiyo iliyopo ambayo tayari tulikuwa tunaitumia ni more value for money basi kuna haja ya kufanya hivyo.

I am not ruling anything in or out. Uamuzi ungetokana baada ya kusikiliza ushauri wa wataalamu mbalimbali. Concept ambayo ningetumia kuamua ni hiyo value for money.

Kama kuna mtu anasema kuna mtambo kama huo huo sehemu na unauzwa kwa bei ndogo au sawa na huu, hiyo ni obvious nitachagua mtambo mpya.

Kinachonikisitisha mimi kwenye huu mjadala ni ile hasira ya ku rule out kabisa huo mtambo kwasababu za kisiasa. Sio kwasababu ununuzi kama huo hautakuwa value for money kwa mlipa kodi wa Tanzania bali kwasababu hatutaki mbaya wetu Rostam afaidike. Mimi naangalia upande mwingine wa shilingi, kama taifa litafaidika, i don't care tutanua wapi huo mtambo. Hapo ndipo tofauti kubwa kati yenu na sisi wengine.

Pia lazima ifike mahali muanze kukubali kwamba binadamu tunatofautiana kimawazo na kiakili. Haiwezekani muda wote mawazo yetu yafanane, kuanza kuwaandama watu kama akina Zitto kwasababu safari hii ana mawazo tofauti na ya kwenu naaona huko kunabomoa kuliko kujenga.Mnaweza kupingana naye kwa hoja lakini sio kuanza ku question uzalendo wake hata pale ambapo hamna ushahidi wowote.

Msipoangalia mtajenga taifa la akina Kawawa, watu ambao wanaangalia upepo kabla ya kuamua kuchukua hatua fulani. Viongozi kama hao ni hatari kubwa kwa nchi.

Mimi nitaona mna hoja kama mtamwambia waziri kwamba bei ya mtambo kama huo hii hapa na hawa wanaweza kuufikisha mpaka TZ kwa pesa hizi. Kama bei yake itakuwa nafuu, nitashangaa kwanini waziri akatae? Kwanini Idrisa akatae?
 
Hivi vitu vinajulikana (Production ya umeme its not a guess work) i.e. what and when tutahitaji kuongeza nguvu ktk grid ya taifa.........Kama utaalamu wenyewe ndio huo wa kuzima moto.........basi bana

watu wamesahau kuwa this was a planned deal ya mafisadi,

Mtanzania unasahau kuwa wanasiasa hao hao ndio wametufikisha hapa tulipo, wametukimbiza na IPTL na sasa RDC/Dowans.........sasa wanakuja eti dharula....halafu unasema tunaingiza siasa kwenye mambo muhimu......ok nyie endeleeni ku-cover hizo prejudices........

usikute tunahangaika kununua mitambo michakavu wakati miradi ya umeme tuliyonayo ina uwezo wa kuzalisha beyond our need......and simply because we don't want to spend money huko kwa kuwa hakuna value for our money.......those projects are doomed White elephants.........

aaaaggghhhhh...umeanza tena na wewe....
 
Kama hiyo mitambo ya Dowans ina thamani basi akaiuze kwenye soko la dunia. Au awauzie Waganda au Wakenya, kwani wao hawataki umeme? Kwa nini Tanzania peke yake ndiyo ishinikizwe kwa kisingizio kuwa tutaingia gizani kama haitanunuliwa? Richmond wameiingiza mitambo hiyo Tanzani kinyemela. Tukawakataa. Kabla hatujapumua Rostam akasema niachieni mimi nitawauzia Wadangayika. Akamlipa Richmond na sasa anatudai. Richmond hakuondoka mkono mtupu kama alivyotudanganya rais. Na Rostum anataka kurudisha hela yake, tena maradufu, kama siyo mara tatu ya mgao aliowapa Richmond. Tuikatae. Hela yetu ina thamani. Tununue mingine mipya mara moja.
 
Mtanzania,
Nimeshindwa kukuelewa hapa! Kwa nini tununue zile mashine mitumba wakati kuna mashine nyingi na nzuri kuliko zile ambazo zitagharimu kidogo, na procurement process itakuwa simpler? Kila mtu including TANESCO wanajua mashine kama hizi zimetapakaa duniani. Ok tuwaachie hawa jamaa hizo machine zao tukanunue mashine zenye ubora. Kwa nini tununue mashine zenye dispute wakati kuna machine ambazo hazina dispute? Kwani zile machine zimetoka mars! please I do not see what kind of returns and value of money you are trying to direct us to!

Mkuu IO,

Wapi kwenye maandishi yangu nilikoshauri tununue hii mibovu na kuacha mipya?

Ninachosema mimi ni kwamba tuangalie value for money, kama mitambo kama hiyo hiyo inauzwa sehemu kwa bei nzuri, kwanini tunapoteza muda? kwanini tusinunue?

Ila kama hiyo mitambo iliyopo tayari TZ ni value for money, ningelikuwa mimi ningenunua na kuwajibika kama baadaye ingeonekana nimeliingizia hasara taifa. Uongozi ni kuchukua maamuzi magumu magumu na wala sio kusubiri upepo unavuma kuelekea wapi.

Siwezi kukataa kununua kitu ambacho washauri wote watasema kinafaa kwa kazi husika kwasababu tu eti mbaya wangu atafaidika na deal. Kwa mimi kigezo kikubwa lazima kiwe kufaidika kwa nchi.

Kama kuna machine mnazozisema si waonyesheni Tanesco? Si mwonyesheni Ngeleja? Hii ya kusema juu juu tu bila kuja na data kamili kwamba mheshimiwa huu mtambo unaotaka kununua una miaka mitatu, unafanana na huu mpya ambao mpaka kufika TZ bei itakuwa katribu tu, huyo waziri akikataa ni either kichaa au fisadi mkubwa. Siamini kwenye hili suala ni ufisadi.

Mjadala wa namna hiyo ndio utakuwa na tija lakini sio hizi sera za personalities, hatuwezi kununua kwasababu tutamtajirisha Rostam. Yaani hata kama kutakuwa na faida kwa nchi, uko tayari hiyo faida ipotee kwasababu tu hutaki Rostam afaidike?
 
Mtanzania,

Una-determine vipi value for money na hasa ukizingatia kwamba serikali yetu iliyo madarakani imejaa mafisadi na usanii wa kila aina? Kila kitu kinaendeshwa kienyeji na malengo ya kuendesha kienyeji ni kuondoa legal implications just in case mambo yakienda kombo.

Huyo mjerumani aliyekuja kutathimini hiyo mitambo alikuwa na mkataba wa kufanya hiyo kazi? Kama hakuna mkataba ama any legal agreement ya kufanya kazi hiyo na ikatokea kwamba mitambo ikaja kuwa bomu after 2 yrs, mtamshitaki nani kwamba aliwaingiza mkenge? Kwenye business kampuni ikipewa ushauri wa ku-invest sehemu fulani na pesa ikaja ikaenda na maji, mwenye kampuni ana haki ya ku-sue aliyemshauri kwa kusababisha hasara. Tukifanya hivyo hapo nitaamini kwamba tunaangalia value for money ya hiyo mitambo. Lakini mpaka dakika hii naona mambo yanapelekwa kienyeji na yakija kuharibika mbele ya safari hakuna ambaye atawajibika wala kuwajibishwa.

Tatizo jingine ni kwamba CEO wa TANESCO (Dr. Rashid) ni business partner wa mmiliki wa Dowans (Rostam). Kwanini watu wasione hapa kuna harufu? Mangapi machafu yamesemwa kuhusu Rostam na hasa anapokuwa na access na mahali fulani halafu awe na shida yake, hawezi kugonga mwamba hata siku moja. Hilo ndiyo ambalo wengi linawatia mashaka sana na kuona kwamba kuna harufu ya deal/ufisadi.

Kama mambo yakipelekwa kitaalam na kisheria, sina tatizo na ununuzi wa hiyo mitambo, ili mradi tuweke ground nzuri ya kuhakikisha kwamba mitambo hiyo ikiwa bomu basi iwepo namna ya ku-address hilo tatizo kwa mtu/watu kuwajibika ama kulipa hasara ambayo tutakuwa tumepata.

Kwa upande wa fedha, sidhani kama ni tatizo. Usishangae ukisikia kwamba bei ya mitambo hiyo ni karibu sawa na bei ya mitambo mipya. Katika hoja za TANESCO kutetea ununuzi wa mitambo ya Dowans hawajagusia swala la ukosefu wa hela ama unafuu wa bei, hoja yao kubwa ni kwamba kununua mitambo mipya mchakato wake utachukua muda mrefu na hivyo ama tununue mitambo ya Dowans au tuingie gizani.

Swali la mwisho dogo tu, kuna mahali nimesoma wanasema kwamba mitambo imetumika kwa masaa 800 (labda kama nilikosea kusoma). Masaa 800 ni sawa na mwezi mmoja iwapo mtambo unafanyakazi kwa masaa 24. Hivi kweli inawezekana mitambo hiyo ikawa imetumika kwa mwezi mmoja tu? Kuna taarifa zinasema kwamba baadhi ya mitambo ilikuja ikiwa imeishatumika kutoka huko ilikotoka, je ukijumlisha matumizi ya wakati wa mkataba kuanzia mwanzoni mwa 2007 mpaka August 2008, ina maana imetumika kwa masaa hayo tu? Hata kama ni masaa 8000 bado inakuwa ngumu kuamini kwa kiasi fulani.

Keil,

Umeongea hoja mbalimbali, huu ndio mjadala unaotakiwa. hayo ndio mambo yanayotakiwa kupatiwa majibu na wala sio hiyo mijadala ya personalities.

Kiongozi yeyote makini na asiye fisadi atataka kupata majibu ya maswali yako kabla ya kununua hiyo mitambo.

Kama nilivyoandika huko nyuma mimi si rule out au rule in kitu chochote. Nilichoandika tu ni kwamba ningetumia value for money kuamua kama tununue hiyo mitambo au la.

Kama kuna mtambo mpya wenye specifications karibu sawa na mtambo wa zamani na bei karibu sawa, bila wasiwasi wowote mtambo mpya utakuwa na value for money kubwa kuliko mtambo mbovu.

Tunatakiwa tujadili mambo kama haya, je kama kuna mitambo mipya sehemu ni wapi, ina uwezo gani, bei zake zikoje nk.

Tukiendeleza mijadala kwa kufuata wanachosema wanasiasa, ambao hata ukiwauliza lete data hawana, tunaumiza vichwa bure. Kama kuna mitambo rahisi mahali na mipya basi tukanunue hiyo.

Hoja yangu ni ile ile sio wakati wote kitu kipya ni value for money, ndio maana nikatoa na mfano wa magari.
 
Jibu rahisi ni NDIYO!

Mkuu Jasusi,

Hapo ndio tunapotaofautiana. Hapo ndipo wenzetu walipotuzidi, inapokuja suala la maslahi, wanangalia maslahi yao kabla ya kuangalia ya mwingine.

Ndio maana wale Wamarekani hawakuangalia Gaddafi atafidi vipi, waliangalia watapata compensation ya madola mangapi. Yule mzee mmoja tu akasema NO, ni bloody money, wengine wote wakakunja pochi zao na kutokemea.
 
Mkuu IO,

Wapi kwenye maandishi yangu nilikoshauri tununue hii mibovu na kuacha mipya?

Ninachosema mimi ni kwamba tuangalie value for money, kama mitambo kama hiyo hiyo inauzwa sehemu kwa bei nzuri, kwanini tunapoteza muda? kwanini tusinunue?

Ila kama hiyo mitambo iliyopo tayari TZ ni value for money, ningelikuwa mimi ningenunua na kuwajibika kama baadaye ingeonekana nimeliingizia hasara taifa. Uongozi ni kuchukua maamuzi magumu magumu na wala sio kusubiri upepo unavuma kuelekea wapi.

Siwezi kukataa kununua kitu ambacho washauri wote watasema kinafaa kwa kazi husika kwasababu tu eti mbaya wangu atafaidika na deal. Kwa mimi kigezo kikubwa lazima kiwe kufaidika kwa nchi.

Kama kuna machine mnazozisema si waonyesheni Tanesco? Si mwonyesheni Ngeleja? Hii ya kusema juu juu tu bila kuja na data kamili kwamba mheshimiwa huu mtambo unaotaka kununua una miaka mitatu, unafanana na huu mpya ambao mpaka kufika TZ bei itakuwa katribu tu, huyo waziri akikataa ni either kichaa au fisadi mkubwa. Siamini kwenye hili suala ni ufisadi.

Mjadala wa namna hiyo ndio utakuwa na tija lakini sio hizi sera za personalities, hatuwezi kununua kwasababu tutamtajirisha Rostam. Yaani hata kama kutakuwa na faida kwa nchi, uko tayari hiyo faida ipotee kwasababu tu hutaki Rostam afaidike?

Hivi utata uliokuwa umeigubika kampuni ya Dowans umemalizika na wamiliki wake kujitokeza wazi wazi kutaka kufanya biashara na serikali ? Je serikali inaweza kuingia kwenye mazungumzo na kampuni ambayo inaonekana wazi kuwa ni ya kitapeli ? Yaani wezi walioitapeli serikali ndio sasa hao hao wanataka kuinusuru serikali kwa kuiuzia mitambo iliyopatikana kitapeli ? Na zaidi itawezekana vipi serikali ishiriki katika mipango ya kitapeli. Hebu tujikumbushe aliyosema Dr. Idris Rashidi akivunja mkataba na Richmond mwaka jana.

Dr Rashidi noted that a review of the contract by the legal expert had established that it violated the Public Procurement Act No.21 of 2004. ''Because of that violation the contract between Tanesco and Richmond Development Company LLC was not legal and is not legally enforceable,'' said Dr Rashidi.

The Tanesco MD further said the re-assignment of the Richmond contact to Dowans Holdings of South Africa and later Dowans Tanzania Limited did not follow the proper contractual procedures as signed. He said the re-assignment was illegal because Tanesco had entered agreement with Richmond Development Company LLC and not RDEVCO as indicated in the later stages of re-assigning the contract to Dowans.

Sasa leo Dr Idris Rashidi anapendekeza serikali inunue mitambo hiyo ya Dowans. Hapa bado tuna"deal" na Richmond ile ile iliyobatizwa Dowans na kuendeleza utapeli ule ule kama kazi. Sasa nikisema - Serikali ya Jamhuri ya Tanzania inashiriki kwenye utapeli wa wananchi wake kwa sababu na yenyewe imeingia madarakani kitapeli - Je nitakuwa nimekosea ?
 
Sasa nikisema - Serikali ya Jamhuri ya Tanzania inashiriki kwenye utapeli wa wananchi wake kwa sababu na yenyewe imeingia madarakani kitapeli - Je nitakuwa nimekosea ?
Yes, utakuwa umekosea sana, tena sana tu!
 
Tukiendeleza mijadala kwa kufuata wanachosema wanasiasa, ambao hata ukiwauliza lete data hawana, tunaumiza vichwa bure. Kama kuna mitambo rahisi mahali na mipya basi tukanunue hiyo.

Nadhani umesahau kwamba wanasiasa hao hao ndiyo "watalaam" wetu na ndiyo wanafanya maamuzi ya mwisho hata pale yanapopingana na wataalam walioajiriwa kwa ajili ya kutoa utalaam wao.

Naomba nikurudishe kwenye sakata la Richmond. Net Group Solution waligoma kuingia mkataba na Richmond kwa sababu za kitaalam. Baada ya hapo, ngoma yote ilibebwa nzima nzima ikapelekwa wizarani ambako ndiko mkataba uliandaliwa. Baada ya kumaliza kuandaa mkataba management ya TANESCO iliitwa kwenda kusaini huo mkataba. Sasa kwenye mazingira kama hayo unategemea upate value for money? Kwenye sakata la Richmond serikali hii hii ilitupilia mbali ushauri wa PPRA ambao ni wataalam wa manunuzi. Leo ndiyo tutaamini maneno ya Ngeleja na Idrisa ambao ni mabesti wa Rostam na wamefanyakazi/biashara pamoja tangu wakiwa Vodacom?

Kinachoendelea sasa hivi ni kujenga mazingira ya kukwepa kuwajibika mbele ya safari. Lini ulisikia serikali inaomba ridhaa ya Bunge ili inunue kitu chochote? Haya yanatokea kwa kuwa wamegundua ile mianya ya kupeleka mambo kienyeji enyeji haipo upande wao na ndiyo maana wanazunguka kila kona ili kuomba support. Keshokutwa mitambo ikifa watakuja kusema walipata ridhaa ya Bunge. Hivi Bunge lina watalaam wa kutoa ushauri wa kitaalam kwenye ununuzi wa mitambo ya kufua umeme?

Value for money haiwi determined na Bunge wala na kamati za Bunge bali inakuwa determined na watalaam wa fani hiyo ambao wapo lakini ama hawatumiki kwa kuwa na misimamo fulani au wanaotumika wamekubaliana na mafisadi. Wengi wa hao watalaam wameishia kuwa frustrated na ndiyo maana kila kukicha tunaona vitu vinachomolewa kwenye files na kumwagwa hadharani. Kwanini wahusika wa kutuingiza kwenye mkenge wa Richmond mpaka leo hii bado wako kwenye ofisi zao na sasa ni karibu mwaka mzima tangu Bunge lipendekeze? Kwa kifupi ni kwamba watalaam hao walikuwa wanaagizwa na wanasiasa wetu na ndiyo maana serikali imeshindwa kuwafuta kazi kama jinsi Bunge lilivyopendekeza.

Kutokana na hali hiyo ndiyo maana kila kinachofanywa na serikali watu wanakiangalia kwa makini na wakati mwingine tunaweza kujikuta tuna-doubt hata vitu ambavyo ni genuine, ni kwa kuwa wao ndiyo wametufikisha hapa. Wewe ukiwa na mwanao na kila kukicha unamwahidi kumfanyia mambo mazuri na mwisho wa siku humtimizii, baadaye atakuona ni tapeli tu na hawezi kukuamini hata siku ukiwa na ahadi ya kikweli.
 
Naomba niulize kuwa hivi hawa Dowans walitangaza lini kuuza mitambo yao?Na ni lini walifungua kesi Paris?Lini TANESCO/serikali waliizuia hii mitambo ili ikitokea wameshinda kesi basi waichukue.
Maana sidhani kama inawezekana wakatangaza kuiuza huku wakijua imezuiliwa,au walispecify kuwa mnunuzi ataichukua mara kesi itakapoisha na wao wakawa washindi kwenye kesi hiyo!!Cha kushangaza zaidi ni pale aliyeizuia mitambo hiyo ndo anayetaka kuinunua....
 
Ni hatua nzuri kwa JF kutambulika na vyombo mbalimbali. Hongera kwa wote walioifikisha hapa JF na tuendelee na kazi.

Mheshimiwa Zitto salama?

Mkuu samahani, mpaka sasa hivi nimeshindwa kuwa na msimamo kwenye swala la Dowans. NAAMBIWA KAMATI YAKO INASEMA tununue ile mitambo. Well I have had reservations kwa sababu nilijua from the beggining serikali haina nia ya kulishughulikia hili swala zaid ya kutafuta hela za kampeni mwakani. Na nikajiuliza kwani tangu tupate matatizo ya umeme..tumeshindwa kuwa na contigency plans kulikabili hili swala la umeme? Mpaka tukurupuke sasa hivi?

Sasa mkuu kama Mbunge na mwakilishi wetu naomba MSIMAMO wako. Maana mpaka sasa hivi nimeshindwa kukuhukumu au kuku-associate na kauli za magazeti wakati sijakusikia wewe mwenyewe. MAANA ni rahisi ukawa quoted out of context. What exactly did you say?

Please if you wont mind, naomba unipe stand yako. NA KAMA umeshaelezea humu jamvini basi nipe link.

Shukrani sana Zitto

Masanja,
 
Back
Top Bottom