Mwachieni Gire, nunueni mitambo ya Dowans!

Mwachieni Gire, nunueni mitambo ya Dowans!

"MATATIZO YETU YAKO KWENYE DNA. SI BURE! MAANA HATA KUNGEKUWA NA MCHAWI..ASINGETUROGA WOTE KIASI HIKI"!-Masanja JF

hivi mafisadi wao hawajarogwa???? wana akili kuliko wananchi au?
 
Kununua mitambo iliyotumika kututapeli ni kuidhinisha utapeli huo,sijui masikini Zito kalishwa nini sasa anatetea mitambo ya kifisadi sasa chama chake kitaaminika vipi kama ameanza mapema hivi,Mungu endelea kutuonyesha wanafiki ili tutafute Viongozi wenye nia nzuri na Nchi hii.Mitambo hiyo ingetaifishwa na serikali kwani ilitumika kutapeli na si kuyanunua.Wapinzani wenye nia njema mpo?Zito naona anaelekea kubaya inabidi kutafakari nyendo zake.

Kweli Mkuu, kama sitasikia kauli ya Zito kwenye hili suala basi nitapoteza imani naye! Amelishwa nini hadi aanze kutugeuka mapema hivi? Hivi kweli huyu bado ni Obama wa Tz? Anatakiwa aje haraka sana iwezekanavyo ili atueleze. Vinginevyo tuamini ana % zake katika hili dili. Hakuna mtu mwenye akili timamu na ambaye hana ajenda ya kifisadi anaweza kutetea ununuzi wa mitambo chakavu kutoka kampuni chakavu (i.e ya kitapeli!!
 
"MATATIZO YETU YAKO KWENYE DNA. SI BURE! MAANA HATA KUNGEKUWA NA MCHAWI..ASINGETUROGA WOTE KIASI HIKI"!-Masanja JF

hivi mafisadi wao hawajarogwa???? wana akili kuliko wananchi au?

Wote tumerogwa. Mafisadi wamerogwa ili waibe hata pale ambapo hakuna kitu cha kufisadi! Wako tayari kuuza hata maji ya bahari endapo rasilimali za kufisadi zitaisha!! Na sisi wengine tumerogwa kwa kupewa dawa ya usingizi. Tumepigwa nyamrunda (anaesthesia) kiasi kwamba tunaendelea kutesa njonzini kama mtu aliyebwia cocaine!!!

Hata hivyo nadhani mchawi wetu aliingiza uchawi wake kwenye DNA.
 
dk idrisa + ngeleja+ ccm = rostam.

naomba mitambo inunuliwe tuache chuki za kibinafsi kwenye mambo ya kitaifa!!!

hivi tatizo ni mitambo au dowans kuwa na uhusiano usiothibitishwa na ROSTAM??

TUSONGE MBELE KAMA TAIFA, MAJUNGU NA MALALAMIKO YASIYOJENGA HAYAFAI.

Game bado bichiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.....mtandao +magazeti kampeni + kikundi pigia kelele ufisadiiiiiii (wabunge, wafanyabiashara, wanasiasa, wanaharakati walioombwaaa)
 
Kweli Mkuu, kama sitasikia kauli ya Zito kwenye hili suala basi nitapoteza imani naye! Amelishwa nini hadi aanze kutugeuka mapema hivi? Hivi kweli huyu bado ni Obama wa Tz? Anatakiwa aje haraka sana iwezekanavyo ili atueleze. Vinginevyo tuamini ana % zake katika hili dili. Hakuna mtu mwenye akili timamu na ambaye hana ajenda ya kifisadi anaweza kutetea ununuzi wa mitambo chakavu kutoka kampuni chakavu (i.e ya kitapeli!!

Hiyo ni rangi moja tu ya Zitto, stay tuned mbeleni atatoa nyingine,
 
Watanzania ni "wazoefu" vitu "USED". kuanzia kuoa/kuolewa mke/mme used, magari used, nyumba used, ndege used, mitambo ya Richmond used, vyeo na madaraka tunawapa viongozi ambao ni used,.....Chama kinacho tutawala ni kilekile used!

Wildcard,

Mimi napenda mitumba, kwanini ninunue gari jipya kwa dola 30,000 wakati gari hilo hilo naweza kulinunua baada mwaka kwa dola 15,000? Kwanini nichukue toto bichi bichi ambaye atanisumbua na hajui kitu wakati nikichukua used anajua mambo yote?

Lazima utofautishe kati ya kununua kitu kilichotumika na ufisadi. Tatizo la Tanzania sio ununuzi wa vitu vilivyotumika bali ni ufisadi na ujambazi.

Kung'ang'ania kwamba eti lazima kununua kitu kipya naona sio busara kabisa. Wengine tunaangalia kitu kinaitwa value for money. Hata kama kitu ni used lakini ununuzi wake unaweza kuwa na value for money kubwa kuliko kutupa mabilioni kununua kitu kipya kwa faida ndogo sana.

Mimi naona maskini ambao wanakimbilia kununua magari mapya ni wapumbavu kabisa (wakiwemo Wabunge), nikiwapendelea nitawaita wajinga.

Sasa tuje kwenye mitambo ya Dowans, labda kikwazo ni hiyo sheria ambayo mimi naamini imepitwa na wakati ya kung'ang'ania ununuzi wa vitu vipya tu. Hiyo mitambo iko hapo tayari, wenye nayo hawana kwa kuipeleka, naamini tukiwa makini tunaweza kuipata kwa bei ambayo ni karibu na ya kutupa. Kama wataalam watathibitisha inafaa na itakuwa na value for money kubwa, hata mimi ningekuwa waziri ningeshauri tuinunue.

Tatizo la Tanzania ya leo kila mtu anajifanya anajua, kila mtu ni mwanasiasa kiasi kwamba wale watu ambao wangekuwa tayari kuchukua maamuzi makubwa na magumu kwa faida ya nchi wanaanza kuwa waoga kwasababu ya kuogopa kuambiwa ni mafisadi.
Kila mtu akitoa mawazo yake huru, mnaanza kusema ana uhusiano na mafisadi. Hii nchi kweli itaongozeka vipi?
 
Mtanzania,
Mkuu mawazo yako murwaa kabisa ikiwa ununuzi wa gari jipya unafanywa na wewe au mtu kama wewe na kwa sababu kama zako!..Sio mimi na kwa sababu zangu siwezi kabisa kununua au hata kufikiria kununua mtumba..
Mkuu tunazungumzia miundombinu hapa, chombo cha kuendesha uchumi wa nchi na sio gari la kutembelea kutoka magomeni kwenda mjini kazini!..Fikra za mitumba ni fikra zilizopitwa na wakati sawa na nguo za mitumba kwani hata mvaa nguo za mitumba anaweza kusema ni ujinga kununua nguo mpya wakati mwaka mmoja tu wa matumizi yake nguo hiyo haina thamani tena..
Na kama nilivyosema inategemea na sababu kwani nguo ya Harusi ni nguo ya siku moja hivyo huwezi kusema ni upumbavu kununua nguo hiyo kwa matumizi ya siku moja!..

Nirudi ktk mada husika, mkuu wangu generator ya Umeme hata kama ipo nchini iina utata mkubwa na wahusika wake.. Kama nilivyokwisha sema sintanunua kitu toka kwa Mwizi ikiwa kitu hicho kipo dukani...Ni sawa na mama anayekataa fedha za mwanae kwa sababu zinatokana na drugs hata kama fedha hizo zitaweza kumwondolea matatizo ya nyumbani.. Ni Principal ambayo haina muda wala kupitwa na wakati..

Laukama sababu kubwa ya sisi kununua mitambo hiyo ingetokana na uwezo wetu mdogo, na pili labda kwa ajili ya jengo fulani la serikali labda hapo ningefikiria sana lakini sivyo! mitambo hiyo ililetwa nchini kutumika kwa muda mfupi tu, iweje leo mkataba uliopikwa ugeuzwe kuwa long term strategy tukitumia sababu zile zile ambazo zilitulazimu kuwachukua Richmond!.. Kumbuka mkuu wangu wakati wa Richmond tuliambiwa hivyo hivyo na wakacheza mchezo hawa jamaa kutofanya ukarabati ktk dams yetu ya Mtera na tukaambiwa sababu kubwa ya ukosekanaji wa Umeme ilikuwa mvua..wakakata umeme huku nahuko kuonyesha umuhimu wa Richmond!..mara tukaahidia mvua za kisayansi na kadhalika..ili mradi walicheza na akili zetu. Kwa miaka zaidi ya 8 tulikuwa na shida ya umeme Dar na tukajivuta hivyo hivyo..
Na hata kabla Richomond hawajafika na mitambo yao mvua zilianza kunyesha tukaambiwa hakuna tena tatizo la umeme, watu wakaanza ku suggest hakuna haja ya Richmond isifungwe wala kuunganishwa ktk grid ya Taifa.. lakini kwa sababu tulikuwa tayari ndani ya Mkataba Richmond waliendelea na shughuli za ufungaji ndipo bomu liliporipuka Kitaifa..
Kwa hiyo leo hii tunapoambiwa kwamba bila mitambo ya Dorwans nchi itakuwa kizani nashindwa kuelewa wakati hawa jamaa wanatupa only 100 kwts!..na Mtera hadi sasa hivi haifanyi kazi 100% hata kama tumeanza kutumia gas zaidi ktk uzalishaji wa Umeme..Hivyo mkuu wangu hatuna sababu kabisa isipokuwa ni zile akili za MITUMBA... Mwinyi aliruihusu mitumba kama ni suluhisho la Muda (short term) leo tunakata miaka 20 na mitumba ina soko kubwa kuliko biashara ya mali inayotengenezwa viwandani..Sasa huu uchumi wetu utakuwa vipi ikiwa mitumba ndio inazungusha uchumi wa nchi?..
Noo mkuu wangu, hawa kina Lowassa hawan mahala pa kuipelekea hiyo mitumba yao na mkataba wetu ulikuwa wa muda hivyo hakuna haja kabisa ya kuendelea kutumia mtu wa kati wakati Tanesco wanaweza kabisa kujiendesha wao kama shirika bila kuingiliwa na wanasiasa.. Mtambo wowote wa kuzalisha umeme kwa nchi ni lazima uwe MPYA.. huwezi ku risk kununua mtumba ktk mradi mkubwa kama huu, kwa kutumia biashara ya daladala...Huu ni urithi mkubwa wa fikra za biashara ya nguo za mitumba, tumeupeleka kwenye daladala, mabus, malori na hata ndege zetu. Kila siku hayakosi kusimama kazi na yanaua watu tunashindwa kuelewa sababu isipokuwa kutafuta mchawi hao - madereva..
 
Mkandara,

Kama nilivyoandika mwanzoni, kwa mimi muhimu kwenye hili ni value for money.

Binafsi kama mhandisi mwenye ujuzi wa mambo ya biashara pia sitajali kufanya biashara na mtu ambaye kwenye maisha ya kawaida siwezi kwenda naye kitandani.

Wote tumeona Obama anamtuma mama Clinton kwa Wachina na kumwambia mambo ya human rights weka pembeni. Najua wazi Obama hafurahii mambo hayo ya Wachina lakini
kwenye dunia ya leo unaangalia maslahi yako, maslahi ya nchi na sio kujali kama huyo mbaya wako atafaidika au la.

Kama wataalamu wetu wanasema kununua mitambo ya Dowans ni better option, mimi ningeenda na hilo bila kujali wabaya wetu akina Rostam watafaidika au la. Muhimu ni kuhakikisha nchi inafaidika katika hiyo transaction.

Hapa tunatofautiana mawazo, ila ninachopinga ni kuanza kufikiri kila anayeona kuna haja ya kununua hiyo mitambo basi ana uhusiano na ufisadi au mafisadi. Binafsi baada ya kusoma maelezo ya Tanesco, naamini ningeunda independent team kuchunguza kama ununuzi kama huo unaweza kuwa na faida kwa taifa na kisha kuangalia sheria zetu zinasema nini.

Kama nilivyoandika mwanzoni kukimbilia kununua kitu kipya kwasababu tu ni kipya hata kama value for money yake ni mbaya kuliko kitu kilichotumika mimi nitaita ni ujinga mkubwa. Ndio matatizo hayo hayo tunayaona hata huku nje ya Black man's car (Benz au BMW). Mtu mweusi yuko tayari hata familia yake isote lakini lazima aendeshe BMW hata kama gari lina miaka 10. Wakati magari mengine mengi ambayo si brand yanatumia parts karibu nyingi ambazo zimetengenezwa na manufacrurers wale wale wanaotengeza parts za BMW na karibu kila kitu ni sawa isipokuwa bei na mambo mengine machache.

Ndio maana Afrika tunaletewa vitu vya zamani vilivyopakwa rangi na kudanganywa ni vipya. Tuna matatizo makubwa sana!
 
Mtanzania,
Ndio maana Afrika tunaletewa vitu vya zamani vilivyopakwa rangi na kudanganywa ni vipya. Tuna matatizo makubwa sana!
Mkuu hiki ndicho nachozungumzia..hadithi nyingine unaziongeza tu kuweka radha ya mjadala..
Mama Clintyon yuklo China kufanya biashara anafunga ma deal sio sisi na Dorwans hatuna biashara isipokuwa tunaibiwa!.. kuna tofauti kubwa sana kisha kumbuka stimulus ya Obama inategemea zaidi mikopo toka China ambao ndiye wadeni wao wakubwa..
Na kuhusu watu weusi kununua magari ya fahari, mkuu hivi unawajua wazungu au unazungumzia asilimia ndogo sana na Weusi waliofanikiwa?.. Ktk nyumba 100 za fahari Hollywood utakuta waswahili ni chini ya 10 tena basi hata kupata nyumba ni shida pamoja na fedha zako..
Kifupi ni hivi huo mfanoi wa weusi wanaonunua vitu vya fahari ni exactly nachozungumzia hapa.. Hawa viongozi wetu wapo radhi kununua magari ya fahari, majumba ya fahari na kila starehe zao wenyewe wakati wanatuacha sisi familia yao yaani wananchi na mtumba wa generator ya Dorwans..
 
Na kuhusu watu weusi kununua magari ya fahari, mkuu hivi unawajua wazungu au unazungumzia asilimia ndogo sana na Weusi waliofanikiwa?.. Ktk nyumba 100 za fahari Hollywood utakuta waswahili ni chini ya 10 tena basi hata kupata nyumba ni shida pamoja na fedha zako..mzungu havai mtumba ila kwa homeless na kupelekwa Afrika...
Kifupi ni hivi huo mfanoi wa weusi wanaonunua vitu vya fahari ni exactly nachozungumzia hapa.. Hawa viongozi wetu wapo radhi kununua magari ya fahari, majumba ya fahari na kila starehe zao wenyewe wakati wanatuacha sisi familia yao yaani wananchi na mtumba wa generator ya Dorwans..
 
Mtanzania,

Mkuu hiki ndicho nachozungumzia..hadithi nyingine unaziongeza tu kuweka radha ya mjadala..
Mama Clintyon yuklo China kufanya biashara anafunga ma deal sio sisi na Dorwans hatuna biashara isipokuwa tunaibiwa!.. kuna tofauti kubwa sana kisha kumbuka stimulus ya Obama inategemea zaidi mikopo toka China ambao ndiye wadeni wao wakubwa..
Na kuhusu watu weusi kununua magari ya fahari, mkuu hivi unawajua wazungu au unazungumzia asilimia ndogo sana na Weusi waliofanikiwa?.. Ktk nyumba 100 za fahari Hollywood utakuta waswahili ni chini ya 10 tena basi hata kupata nyumba ni shida pamoja na fedha zako..
Kifupi ni hivi huo mfanoi wa weusi wanaonunua vitu vya fahari ni exactly nachozungumzia hapa.. Hawa viongozi wetu wapo radhi kununua magari ya fahari, majumba ya fahari na kila starehe zao wenyewe wakati wanatuacha sisi familia yao yaani wananchi na mtumba wa generator ya Dorwans..

Mkandara,

Siongelei mamilionea ambao wana pesa zao hata wakitumia ovyo hakuharibiki kitu. Naongelea watu wa kawaida ambao kwenye hii dunia yetu ndio wengi.

Mfano wa Obama ni mfano halisi kwenye hii case. Yuko tayari kufanya biashara na Wachina hata kama hakubaliana nao kwenye mambo mengi. Sisi tunajifanya kukataa kununua mtambo kwasababu tu eti Rostam atafaidika. Tukatae kwasababu is not value for money lakini sio hizo sababu mnazotoa.

Unasema mzungu havai mitumba? Basi angalia mama Beckham anakonunua baadhi ya nguo zake. Posh's charity shop visit sparks huge surge in takings | Mail Online

Hapo Mtanzania atasema haiwezekani.
 
1. wanasema baadhi ya policy za manunuzi ya mitambo/products imepitwa na wakati!

2. na kwamba value of our money iwe ndio kigezo cha ku-overide standards zilizopo....dah

3. na kwamba eti hatuna option nyingine, bali ni kununua hiyo mitambo michakavu otherwise tuende gizani!

4. na kwamba mbona tunanunua mitambo ya IPTL ambayo ni ya zamani zaidi ya hii ya Dowans

5. na kwamba mtaalamu aliletwa kutathmini ili kuona kama mitambo michakavu ni value for our money or not......DAMN!

NB:
Hivi tulinunua/tulikodisha ile Ndege (sijui Boeing sijui AirBus) for value of our money.....kwa sababu pia tulitumia wataalamu kutathmini ile ndege Vs value of our money.....eehh

.......I mean mimi sio mhandisi, lakini i don't know what kind of a nation we are trying to build here........
 
Kumekuwa na Tetesi na hofu miongoni miongoni mwa wananchi wapenda mageuzi kuwa watu waliowapenda na kuwaamini wamewageuka na kuwasaliti kama walivyowahi kusalitiwa na Dr Lamwai na Dr Kaburou.

Hofu yao imetokana na misimamo yao isiyoendana na maadili inayolazisha ununuzi wa mitambo chakavu ya kufua umeme ya kampuni tata ya Downs(Mjukuu wa Richmond) kwa kisingizio cha kuwaepusha watanzania na Giza endapo mitambo hiyo chakavu haitanunuliwa.

Imefikia hatua ya waheshimiwa hawa kutaka sheria ya manunuzi ibadilishwe ili mitambo hii chakavu inunuliwe. Wanasema eti hiyo sheria ya manunuzi siyo msahafu hivyo lazima ibadilishwe ili mitambo inunuliwe.

Wapenda mageuzi wamekumbushwa majonzi yaliyowapata baada ya kile walichofanyiwa na Dr Masumbuko Lamwai miaka ya 90.

Usaliti huu wa hawa jamaa kujiunga na kundi la mafisadi wapora nchi kwa kisingizo cha kuliokoa taifa umeelezwa kuwa utakuwa na pande nyingi za maumivu lakini kubwa mbili

1. Wizi wa mchana kweupe wa mali ya watanzania.

2. Wapenda mageuzi na watanzania kwa ujumla kukatishwa tamaa kwa mara nyingine tena hivyo kuifanya safari ya mageuzi kuwa mbali sana kwa watanzania. Hii inatokana na ukweli kwamba Roho za watu zimetumbukia nyongo na itawachukua mda mrefu sana kujenga uaminifu kwa watu wengine kama uaminifu na support kubwa waliyokuwa wameonyesha kwa wasaliti hawa.
 
Siku zote Wananchi tunatakiwa kuangalia ukweli na si watu, manake Zito na Dr. Slaa ni binadamu kama sisi na si Malaika. Hivyo dhamira yetu wananchi tunapopigania haki tunatakiwa tujue nani yuko nasi kwa muda huo, lakini hatuangalii jina na aliwahi fanya nini nyuma.
 
Unachokisema ni kweli au isiwe kweli.

Binafisi Lamwai aliniathiri sana kipindi kile mpaka kuja kutengamaa kama nilivyo sasa ilinichukua mda mrefu kwa kweli.

Lakini bila shaka unafahamu nini athari za wasaliti hawa kwenye mageuzi. Athari ni kubwa kulikounavyofikilia.
 
1. wanasema baadhi ya policy za manunuzi ya mitambo/products imepitwa na wakati!

2. na kwamba value of our money iwe ndio kigezo cha ku-overide standards zilizopo....dah

3. na kwamba eti hatuna option nyingine, bali ni kununua hiyo mitambo michakavu otherwise tuende gizani!

4. na kwamba mbona tunanunua mitambo ya IPTL ambayo ni ya zamani zaidi ya hii ya Dowans

5. na kwamba mtaalamu aliletwa kutathmini ili kuona kama mitambo michakavu ni value for our money or not......DAMN!

NB:
Hivi tulinunua/tulikodisha ile Ndege (sijui Boeing sijui AirBus) for value of our money.....kwa sababu pia tulitumia wataalamu kutathmini ile ndege Vs value of our money.....eehh

.......I mean mimi sio mhandisi, lakini i don't know what kind of a nation we are trying to build here........

Mkuu Ogah,

Labda kama huelewi maana ya value for money. Toka lini value for money ika overide standards zilizopo?

Mnaingiza siasa kwenye kila kitu na ndio matatizo ya Tanzania.

Value for money inaendana na quality, inaendana na return ambayo inaweza kupatikana kutokana na investment fulani.

Watanzania wengi sasa wamekuwa wafuata upepo. Eti Zitto katetea ununuzi wa mitambo tayari kasaliti Watanzania, kapewa pesa na mafisadi, nonesense!

Ningelikuwa mimi mhusika ningependekeza kununuliwa baada ya kuangalia sheria zilizopo na kisha ningekuwa tayari kuwajibika kama hasara ingetokea kutokana na ununuzi huo.

Kwenye hili suala watu mmegubikwa na chuki binafsi kuliko reasoning, sawa wengi hatumpendi Rostam, lakini je ndio tuathiri nchi nzima kwa ajili ya kumkomoa Rostam?

Hizi siasa za personalities ndio mwanzo wa matatizo makubwa kwa Afrika. Kama Rostam ana makosa, mpelekeni jela lakini sio kwamba hata jambo la maana kwasababu tu Rostam anahusika basi ni kupinga tu.

Leo hii wanasiasa eti wanajua wapi kwa kununua mitambo kwa bei rahisi. Ununuzi wa mitambo ni sehemu ndogo tu, matatizo makubwa yako kwenye operational cost.

Tutapoteza miezi kujadili jambo moja huku wananchi Tanzania hawana umeme na hakuna kinachofanyika.

Sawa endeleeni na siasa zenu za do nothing! Kama Tanesco wanapesa, sasa wanasubiri nini? Si wakanunue hiyo mitambo mipya na nchi iache kuhangaika na matatizo ya umeme?

Ni rahisi sana kwa mimi hapa Mtanzania nikiwa London kupiga siasa, kwasababu sipati hasara ambazo wananchi na wafanyabiashara walioko Tanzania wanapata shauri ya matatizo ya umeme.
 
Akizungumzia taarifa zinazodai kuwa mitambo ya Dowans ilishanunuliwa na serikali muda mrefu na kinachofanyika sasa ni taratibu tu za kubariki kitendo hicho, Shelukindo alisema hana hakika na taarifa hizo

Hahaaa hapa tumepigwa changa mitambo ishanunuliwa jamaa keshachukua chake taratibu tu zinakamilishwa kalakabaho!!!!!
 
Kwa nini wasitoe tender tu na Dowans wa-compete kama yeyote yule? Why do sole source? Utajuaje kama hakuna yeyote anayeweza kutuletea generator within kipindi fulani bila kutangaza??
 
Tusianze kunyosheana vidole na kuitana wasaliti,nafikiri ni wakati wa kutafakari hasara itakayopatikana kwenye uchumi wa nchi incase tukiamua kuacha kununua hiyo mitambo ya Dowans.Nakumbuka wakati wa crisis ya umeme mwaka 2006,biashara nyingi za wajasirimali ziliathirika na wengine walifisika kabisa kutokana na madeni ambayo walikopa kwenye micro-credit institutions.
Vilevile nafahamu hasira za watu,kutokana na vitendo vya serikali kutochukua hatua madhubuti dhidi ya wahusika wa Richmond/Dowans mpaka tumefikishwa hapa tulipo.In real fact serikali imendeshwa mno kwa mwendo wa kusuasua mpaka hapo maadui zetu wamejipanga vizuri na kutuweka kwenye malumbano haya.Ukweli ni kwamba ndani ya baraza la mawaziri sasa hivi kuna camp zinavutana sana angalia Vitambulisho,ATCL na sasa Richmond/Dowans.Shime watz nafikiri ni wakati wa kujitambua na kuweka priorities zetu sawasawa bila ya kusubiri huruma ya viongozi wetu.
Namuunga mkono massanja.
 
Back
Top Bottom