Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,598
Hapa simuelewi huyu Ngereja. Alisema hivyo ili kuonyesha kuwa kununua mitambo ya DOWANS ni jambo sahihi au?
Pia nimeshangaa sana kusikia Zito anaunga mkono jambo hili (soma Nipashe ya leo). Nadhani tunahitaji majibu zaidi toka kwa Zito ili tuweze kumuelewa vizuri. Kama Richmond/DOWANS ilisababisha serikali yote kuvunjika lakini leo tunataka kununua mitambo yao, basi kuna haja ya Bunge kufuta azimio lake, kuiomba radhi serikali kwa kuikosea adabu na hasa EL na mawaziri wengine walioachia ngazi. Baada ya hapo tuamue kuwalipa fidia wote walioguswa na huo uamuzi mbovu wa bunge ndo tukanunue hiyo mitambo. Kama ni mimi, ningekubali tukae gizani hata miaka 2 kuliko kuingia kwenye dili na kampuni ambayo ina utata.