Mwachieni Gire, nunueni mitambo ya Dowans!

Nilishaandika zamani sana kuwa "Wahindi na Waarabu/Wairan waachiwe na au tumallizane wenyewe au tusameheane wenyewe. Kuonea Ngozi nyeupe wakati SERIKALI ni sisi, huu ni upuuzi wa ajabu.
Tusubiri tu siku akaja KICHAA. Kuanzia Mzee anayetakiwa apumzike kwa amani na hadi wanaopigia debe kuwa Mzee apumzike kwa amani, itabidi wajengewe vyumba Keko. Kama Malawi nao wamempandisha Rais wao, Zambia walifanya hivyo, hii ni habari ambayo siku moja Tanzania itafika. Heri wajifunza sheria za wacheza kamali yaani "Lazima ujuwe muda wa kukimbia meza ya kamali". Kama hujui, basi utaishia pabaya!!!!

maneno mazito..
 
nitatumia maneno ninavyoweza, jinsi ninavyoweza, namna ninavyoweza na katika kufanya hivyo nakusudia kukukwaza..

Mwanakijiji, sisi ni Observers tu lakini katika coments ambazo umewahi kuvurunda hii ni namba wani! Kwanza unamshambulia huyu "mama" kwa topic ulioanzisha wewe. Wewe umesema "umeme utakuwa wa shida April"; she commented, so give the reasons why will be such a shortage!

Halafu huyu "Gire and the GROUP"; wana kesi ya kujibu (kama mahakama na sheria zetu zingekuwa strong). They brought an old "turnkey" project at a hiked USD 170 million dollar cost while the machines/equipments cost only USD 22 million; you know when these equipments where made? And for your information do you know the cost of efurbishment? Then when they were brought here were not fit for the purpose; they couldn't use natural gas as fuel; they had to be modified. How much the tax payers money have been squandered!

You better tell us how much do you think the government should buy from Dowans? There are many sources for such cheap stuff, you need one? I can send it to your private message and you can help your government.

Your writing is easy than the real issue is, these guys should be punished in a severe way possible, and pay the costs!
 
Mwanakijiji hajasema kwamba huo ni mfano. Na wewe unazua. Unaona sasa Steve, hili ni tatizo sugu la wengi wetu.

Yaani kwa vile wewe una uwezo wa kumwelewa Mwanakijiji kabla hata hajamalizia sentensi yake, basi umeassume kwamba members 8500 wa JF wanamwelewa kama wewe unavyomwelewa.

Tujifunze jamani kuwa katika mawasiliano every word counts, kama hatujakuzwa hivyo, tujifunze basi.

...na akina nani.........unaona sasa na wewe una tatizo........yaani kushindwa kwako kumuelewa Steve ndio inakupa kibali cha ku-generalise........duuh
 
...na akina nani.........unaona sasa na wewe una tatizo........yaani kushindwa kwako kumuelewa Steve ndio inakupa kibali cha ku-generalise........duuh

Hehehehe...na wewe naona umempata kibonde wako...eheheheheee

Vipi sasa Dk. Masau?
 
No...ni ubishani usio na msingi au usio na kichwa wala miguu!!

........yote sawa tu........wee warudishie ila mada ya Dr. Masau kiaina........na kiongozi wao ataibuka.......shauri zako.........BTW tomorrow isn't here yet...........only "true substances of life" will be served tomorrow
 
Oh yeah...kesho itabidi watu wa-dish out the true substance of life...Lol...mazee hebu acha kunichekesha
 
Mwanakijiji, sisi ni Observers tu lakini katika coments ambazo umewahi kuvurunda hii ni namba wani! Kwanza unamshambulia huyu "mama" kwa topic ulioanzisha wewe. Wewe umesema "umeme utakuwa wa shida April"; she commented, so give the reasons why will be such a shortage!

IO, nimetoa maoni yangu. Kama kuna kitu ambacho mtu hajakielewa au anataka nifafanue unauliza tu. Inashangaza hukuzingatia jibu lake kwangu ambalo ni hili:

Of all the months mwezi wa nne kuwe na shida ya umeme? Gimme a break!

Fuatilia majibu yake hadi nilipofikia kusema kwa vile ni mtu anayekwazwa na maneno yangu, basi dhamira yangu nitaendelea kuandika niwezevyo, kwa namna yangu na kwa staili yangu, mwenye kukwazika akwazike. Huo ndiyo msimamo. Sina lengo la kufurahisha kila mtu asomaye.

Halafu huyu "Gire and the GROUP"; wana kesi ya kujibu (kama mahakama na sheria zetu zingekuwa strong). They brought an old "turnkey" project at a hiked USD 170 million dollar cost while the machines/equipments cost only USD 22 million; you know when these equipments where made? And for your information do you know the cost of efurbishment? Then when they were brought here were not fit for the purpose; they couldn't use natural gas as fuel; they had to be modified. How much the tax payers money have been squandered!

You better tell us how much do you think the government should buy from Dowans? There are many sources for such cheap stuff, you need one? I can send it to your private message and you can help your government.

Your writing is easy than the real issue is, these guys should be punished in a severe way possible, and pay the costs!

You can never have selective justice. Suala la Richmond ni kubwa mno lakini hakuna nia ya kweli ya kulishughulikia zaidi yakulifanya liendelee miaka nenda rudi. Mwaka huu atashtakiwa mmoja, miezi sita baadaye mwingine n.k Kwangu mimi huku ni kupoteza muda.

Hoja yangu ni kuwa hatuwezi kulizungumzia la Richmond na Dowans miaka nenda rudi. Yote uliyoyasema yanajulikana na wengine tumeyaandika sana huko nyuma. Tatizo serikali haina nia wala sababu ya kuhakikisha suala hili linafikia mwisho the same way hawana mpango wa kumaliza la Rada, JWTZ, Meremeta n.k

Ndiyo maana nimetoa hilo pendekezo la kwanza. Kwangu mimi ni bora hata kesi zote hizi zifutwe tu tuanze upya!! Kama kuibiwa tumeshaibiwa, vinginevyo tunachezeana mazingaombwe hadi qiyama. Tujifunze kumaliza masuala haya ya kitaifa aidha kwa kuyafuta au kuexpedite ile yafikie ukingoni.

that is the message katika ujumbe wangu.
 
"wewe basi ni mshirika wa uongo!!" Mkjj wrote

soma kilichoandikwa; kama yeye anasema aliyemwambia kuwa matatizo yote ya umeme Tanzania yanatokana na mvua ndiye aliyeniambia mimi kuhusu kauli yangu basi mimi nikamwambia kuwa yeye ni mshirika wa uongo kwani mtu huyo huyo ametuongopea wote wawili!!

Duh.. hata hilli nilifafanue!
 
Well, kuna wakati inabidi tuseme tu kuliko kuzungushana kwenye huu utando wa buibui wa ufisadi. TUmekuwa kama kumbikumbi, na kama vipepeo tumenaswa na wao wanatuchezea tu.. kama paka aliyeshiba anavyomchezea chezea panya aliyechoka kukimbia!

Sasa naomba tulimalize hili la Richmond/Dowans:
a.) Bw. Gire aachiliwe kwani tayari tunanyajua kampuni yake ilikuwa feki na kama maelezo ya jana yana dalili yote "upepelezi bado unaendelea". Sasa huu upepelezi wa miaka mitatu nadhani unatosha, na kwa vile hakuna ushahidi (msiniulize kwanini walimfungulia kesi kama hawakuwa wamekamilisha upepelezi au walikuwa wanakaribia kuukamilisha).

b.) Mitambo ya Dowans hatimaye tutainunua kwa vile tunapaswa kuinunua kwani kutoinunua haiingii akilini wakati "ipo tu pale"! Mitambo hii haiendi kwa mtu yeyote binafsi na matatizo ya umeme yanayokuja mwezi wa nne itakuwa ni ushahidi kuwa ni "bora" tuinunue tu!. So why not buy them!?

Sasa tumefikia kamati mbili za Bunge, Wizara, na wengine tunaanza kurushiana utadhani Taifa zima linacheza "Ready". Mara mpira huku, mara kule, huku mafisadi wanakwepa katikati wakiendelea kujaza chupa yao mchanga wa utajiri wa nchi yetu!, so why not just buy them, wapeni hizo fedha (kwani zipo nyingi tu). Tulimalize?

c.) Kwa vile hakuna mtu mwingine atakayepelekwa makahamani kwani muda unapita na mwisho mambo ya statutes of limitations inaweza kuingia kwenye baadhi ya mashtaka, kwanini tusiamue tu kusema "screw it" wameshajiuzulu watu (wakapewa mafao yao) na Richmond haipo tena.. so tulifunge tu.
Kimsingi, hatuwezi kulimaliza hili la Richmond na Dowans isipokuwa kwa kufuta hii kesi moja, kununua mitambo ya Dowans, kuwalipa kina Rostam na washiriki wake, halafu tumaliize yaishe. Hatuwezi kama taifa kuendelea kupiga kambi kwenye hili bonde la kashfa miaka nenda rudi. Hili la Dowans tulimalize, tujue limekwisha kuliko kuzunguka zunguka utadhani watoto wanaocheza "ukuti ukuti!"

Then, tutaangalia haya mengine, haya mambo ya kuzugana kwa kweli wakati mwingine inabidi tukubali tu yaishe!

Mkjj acha uchochezi mbona mwaka ule tulika bila umeme kwa miezi kama miwili na taifa halikuingia hasara yoyote kwa nini tuogope sasa? Hosea wa Takukuru alithibitisha hivyo, waziri mkuu enzi hizo EL alithibitisha pia na hata muungwana JK alituhakikishia hilo............tehe tehe tehe teheee!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kaswali ka kizushi. RA ndiye preszidaaa nini mbona anaonekana kuwa na nguvu kiasi hicho??????????????????
 
...na akina nani.........unaona sasa na wewe una tatizo........yaani kushindwa kwako kumuelewa Steve ndio inakupa kibali cha ku-generalise........duuh

Wewe nae, ndio maana unashindwa kuconstrust sentences. Rudi kwanza shule. Mtoto wa standard 3 can do better kuonyesha kwamba uliruka stage ndio maana unang'ang'ania na wafuasi wako Masau Masau, mara Masha Masha!
 
soma kilichoandikwa; kama yeye anasema aliyemwambia kuwa matatizo yote ya umeme Tanzania yanatokana na mvua ndiye aliyeniambia mimi kuhusu kauli yangu basi mimi nikamwambia kuwa yeye ni mshirika wa uongo kwani mtu huyo huyo ametuongopea wote wawili!!

Duh.. hata hilli nilifafanue!

Wewe kwa uongo, uchochezi na uzushi umekubuhu na wiki hii ndo ilikuwa peak yako ya uongo.

Siko hapa kumshambulia mtu, kuambiwa nongwa! Acha hizoo.
 
a.) Bw. Gire aachiliwe kwani tayari tunanyajua kampuni yake ilikuwa feki na kama maelezo ya jana yana dalili yote "upepelezi bado unaendelea". Sasa huu upepelezi wa miaka mitatu nadhani unatosha, na kwa vile hakuna ushahidi (msiniulize kwanini walimfungulia kesi kama hawakuwa wamekamilisha upepelezi au walikuwa wanakaribia kuukamilisha).

b.) Mitambo ya Dowans hatimaye tutainunua kwa vile tunapaswa kuinunua kwani kutoinunua haiingii akilini wakati "ipo tu pale"! Mitambo hii haiendi kwa mtu yeyote binafsi na matatizo ya umeme yanayokuja mwezi wa nne itakuwa ni ushahidi kuwa ni "bora" tuinunue tu!. So why not buy them!?

Sasa tumefikia kamati mbili za Bunge, Wizara, na wengine tunaanza kurushiana utadhani Taifa zima linacheza "Ready". Mara mpira huku, mara kule, huku mafisadi wanakwepa katikati wakiendelea kujaza chupa yao mchanga wa utajiri wa nchi yetu!, so why not just buy them, wapeni hizo fedha (kwani zipo nyingi tu). Tulimalize?

c.) Kwa vile hakuna mtu mwingine atakayepelekwa makahamani kwani muda unapita na mwisho mambo ya statutes of limitations inaweza kuingia kwenye baadhi ya mashtaka, kwanini tusiamue tu kusema "screw it" wameshajiuzulu watu (wakapewa mafao yao) na Richmond haipo tena.. so tulifunge tu.
mm, sorry. ni ngependa kuandika ifuatavyo kuhusu ulichoandika hapo juu;
a.) Kuhusu kuachiwa gire, hilo tulisilifanye. kama tunajua kampuni yake ilikuwa feki si ndio tumemkuta na kosa la kutudanganya? kwa kudanganya kajipatia hela kutoka kwetu. na lingine kwa kudanganya katutia hasara. sa kwanin tusimhukumu kwa hilo? ndo kusema hawajapata ushahidi kuwa uwezo wa kampuni yake ulikuwa sio kama ulivyodaiwa? au pia ushahidi haujakamilika kwa hilo?

Tukithubutu kumwachia, kesho atarudia tena. au wengine watathubutu kutufanyia kama hivi halafu itabidi tuwaachie kwasababu zitakazopelekea tumwachie gire leo. adhabu tena kali ni muhimu kwa mambo haya na adhabu hutuma ujumbe maridhawa kwa wote. adhabu kali ni kinga maridhawa dhidi ya watu watakao jaribu kutufanya ndivyosivyo baadae.

b.) Kuhusu kununua mitambo ya dowans, sina uhakika niandikeje. teh teh teh. sijui huko ndani tanesco na wizarani kukoje.

Huenda kuinunua ndo ikawa ultimate solution (uamuzi pekee na bora zaidi). na mtego unaweza kuwa tusipoinunua wahusika ambao wana jukumu la kutafuta mbadala wa mitambo ya dowans watakaa kimya mpaka tatizo la umeme lianze kutafuna nchi. Halafu wataibuka wakisema 'mnaona? Tuna tatizo la umeme kwasababu hatukununua mitambo ya dowans?'. Halafu sisi sote tutaanza kuwalaumu waliosababisha mitambo ya dowans isinunuliwe. Kumbe watu wamehonga pa kuhonga tatizo likatokea. Na huenda kuna options zingine bora zaidi zilikuwa zichukuliwe tangia zamani lakin watu walikaa kimya (au kwa uzembe au kwa makusudi). Lakini huenda right now kuna best solutions to the problem lakin watu hawazileti hadharani kwasababu wanataka mitambo ya dowans inunuliwe.

c.) Yeah, sio mtaalamu wa sheria mimi lakini kesi za ufisadi/uhujumu nchi au uchumi ziwe zinaweza kuendelea siku zote labda kama mwenyewe akiamua 'kufa'. Hii ni kwasababu negative impact ya ufisadi kama huu (kama kweli gire katenda kosa) ni kwa watu wengi sana (nchi) na hudumu kwa muda mrefu sana. kwahiyo na kesi pia ziwe zinaweza kuendelea to infinity.. na akipatikana na kosa adhabu yake iwe to infinity... ili next time tomorrow mtu akitaka kuiingiza tanzania mkenge ajifikirie mara mbilimbili.
Otherwise kila siku tutabaki kulia na wezi/ufisadi.... wezi/ufisadi.... wezi/ufisadi.... na hautokaa uishe. na hatutokaa tuanze kushughulikia matatizo mengine katka tz yetu kwa umadhubuti wizi/ufisad utakuwa umetuweka bize
 
Katika mahojiano aliyofanya Waziri wa nishati na madini mheshimiwa sana Ngereja na gazeti la Mwananchi (tolea la leo tarehe 27.02.2009) alipokuwa aking`aka kwa ujasiri kutetea uamuzi wa kununua mitambo mitumba ya Dowans aliamua kusema kwa ujasiri kuwataja mafisadi wengine bila kificho ambao wana tabia ya kukiuka sheria ya manunuzi kwa kununua mitumba na wamekuwa wakiachwa na srikali,bunge na mahakama bila kukemewa.

Mafisadi hao aliowataja bila kumeza maneno ni shirika la Ndege la Tanzania.Amewataja kuwa huwa wananunua ndege mitumba kinyume na sheria ya Manunuzi na hawapingwi.

Hongera mheshimiwa kututajia mafisadi wengine.Je kuna Waziri mwingine jasiri kama Waziri Ngeleja atutajie wengine wanaonunua mitumba kinyume na sheria ya manunuzi?

Mawaziri wengine igeni ujasiri wa Ngereja tunaomba tajaneni.Nadhani sasa vita ya ufisadi inaelekea kuzuri maana na mawaziri wameanza kuiunga mkono.Keep up Ngereja taja wengine.

Bunge mpira huo. ATCL walishanunua ndege mbovu kinyume cha sheria ya manunuzi na wapo wanaendelea kula kuku kwa mrija bila kubughudhiwa na bunge wala yeyote.Ngereja kawaletea mashtaka hayo mnanasemaje wabunge? Mwakyembe mtoto wa Kyela una la kuongea hapo? Au unayo mengi ya kuongelea Richmond tu yale ya ATCL unayakalia kimya?

Nadhani kama kuna wengine wanaowajua mahali popote walionunua vitu vibovu ambavyo ni mitumba kinyume cha sheria ni vizuri kuiga mfano wa Ngereja.Waanikwe na watajwe bila kumeza maneno.
 
Last edited:
mm, sorry. ni ngependa kuandika ifuatavyo kuhusu ulichoandika hapo juu;
a.) Kuhusu kuachiwa gire, hilo tulisilifanye. kama tunajua kampuni yake ilikuwa feki si ndio tumemkuta na kosa la kutudanganya? kwa kudanganya kajipatia hela kutoka kwetu. na lingine kwa kudanganya katutia hasara. sa kwanin tusimhukumu kwa hilo? ndo kusema hawajapata ushahidi kuwa uwezo wa kampuni yake ulikuwa sio kama ulivyodaiwa? au pia ushahidi haujakamilika kwa hilo?

Tukithubutu kumwachia, kesho atarudia tena. au wengine watathubutu kutufanyia kama hivi halafu itabidi tuwaachie kwasababu zitakazopelekea tumwachie gire leo. adhabu tena kali ni muhimu kwa mambo haya na adhabu hutuma ujumbe maridhawa kwa wote. adhabu kali ni kinga maridhawa dhidi ya watu watakao jaribu kutufanya ndivyosivyo baadae.

b.) Kuhusu kununua mitambo ya dowans, sina uhakika niandikeje. teh teh teh. sijui huko ndani tanesco na wizarani kukoje.

Huenda kuinunua ndo ikawa ultimate solution (uamuzi pekee na bora zaidi). na mtego unaweza kuwa tusipoinunua wahusika ambao wana jukumu la kutafuta mbadala wa mitambo ya dowans watakaa kimya mpaka tatizo la umeme lianze kutafuna nchi. Halafu wataibuka wakisema 'mnaona? Tuna tatizo la umeme kwasababu hatukununua mitambo ya dowans?'. Halafu sisi sote tutaanza kuwalaumu waliosababisha mitambo ya dowans isinunuliwe. Kumbe watu wamehonga pa kuhonga tatizo likatokea. Na huenda kuna options zingine bora zaidi zilikuwa zichukuliwe tangia zamani lakin watu walikaa kimya (au kwa uzembe au kwa makusudi). Lakini huenda right now kuna best solutions to the problem lakin watu hawazileti hadharani kwasababu wanataka mitambo ya dowans inunuliwe.

c.) Yeah, sio mtaalamu wa sheria mimi lakini kesi za ufisadi/uhujumu nchi au uchumi ziwe zinaweza kuendelea siku zote labda kama mwenyewe akiamua 'kufa'. Hii ni kwasababu negative impact ya ufisadi kama huu (kama kweli gire katenda kosa) ni kwa watu wengi sana (nchi) na hudumu kwa muda mrefu sana. kwahiyo na kesi pia ziwe zinaweza kuendelea to infinity.. na akipatikana na kosa adhabu yake iwe to infinity... ili next time tomorrow mtu akitaka kuiingiza tanzania mkenge ajifikirie mara mbilimbili.
Otherwise kila siku tutabaki kulia na wezi/ufisadi.... wezi/ufisadi.... wezi/ufisadi.... na hautokaa uishe. na hatutokaa tuanze kushughulikia matatizo mengine katka tz yetu kwa umadhubuti wizi/ufisad utakuwa umetuweka bize

Wandugu mnabishana na MMJ nini? Wakati Serikali inasema hivi......

Kununua mitambo Dowans si ufisadi
Source: Mwananchi
Date::2/27/2009

Na Ramadhan Semtawa

WAKATI Bunge la Jamhuri ya Muungano likiwa limenawa mikono katika mpango wa kununua mitambo ya kufua umeme wa dharura ya kampuni ya Dowans, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ameonyesha msimamo kutetea mpango huo, akisema si wa kifisadi.

Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ilishashauri kuwa serikali isinunue mitambo hiyo kutokana na kuwa imeshatumika, ikieleza kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria ya manunuzi ya umma, lakini serikali imeonekana kupitia mlango mwingine na kuwasilisha mpango huo kwenye kamati nyingine ya bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, ambayo iliomba kamati hizo zikutanishwe ili kutoa uamuzi kuhusu mpango huo.

Hata hivyo, katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah alisema hakuna haja ya kamati kukutana kujadili suala hilo kwa kuwa bunge halina uwezo wa kuilazimisha au kuikataza serikali kufanya manunuzi kama inavyokuwa wakati ikinunua magari yake na vitu vingine.

Kwa sasa mitambo hiyo inashikiliwa na Tanesco, ambalo linadai kuwa itatumika kama fidia iwapo shirika hilo litashinda kwenye kesi ambayo Dowans imefungua dhidi ya Tanesco kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Biashara iliyo Paris, Ufaransa.

Lakini jana, Waziri Ngeleja aliiambia Mwananchi katika mahojiano ofisini kwake kuwa kununua mitambo hiyo hakutakuwa na chembechembe zozote za ufisadi ingawa wengi wanahisi hivyo.

"Nchi haiongozwi kwa hisia," alisema Ngeleja, ambaye alitetea sana mpango wa kununua mitambo hiyo wakati akiongea na waandishi kuhusu uamuzi wa serikali kukubaliana na ushauri wa kamati ya bunge wa kuzuia kununuliwa kwa mitambo hiyo.

"Ni hatari kuacha kujadili mambo muhimu ya nchi yanayozingatia maslahi ya taifa, na badala yake kuendekeza hisia zisizo na mantiki,"alisema.

Ngeleja alisema kitendo cha watu kuhisi kuna kuna ufisadi katika mpango huo wa kununua mitambo hiyo, hakina mantiki, akisema kuwa serikali iko makini na haiwezi kukubali matokeo kama ya Richmond, ambayo ilipewa zabuni ya kufua umeme wa dharura kwa mazingira tata na kusababisha Bunge kuingilia kati na kufanya uchunguzi uliosababisha Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa uwaziri mkuu na baadaye kufuatiwa na mawaziri wawili.

Ngeleja alisema vipo vyombo vya serikali vinavyosimamia sheria na vinafanya kazi kwa umakini na akahoji: "Hivi watu hawaoni vigogo wanavyoburuzwa mahakamani, sasa watu wanafikiri serikali imelala, kwanini tuendeshe nchi kwa hisia."

Alipoulizwa kama kuna msukumo wowote kutoka kwa watu ambao walituhumiwa kuhusika katika mpango wa kuifanikisha Richmond kushinda zabuni ya ufuaji umeme wa dharura, Ngeleja alijibu: "Umeangalia maslahi ya taifa tu."

Ngeleja alisema msukumo wa kutaka kununua sasa mitambo hiyo unatokana na kuangalia ukuaji wa uchumi, ambao mahitaji yake ya umeme yanaongekeza kwa asilimia kati ya 10 hadi 15 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi 2012.

"Utafiti uliofanywa katika Power System Master Plan (mpango wa kuendeleza sekta ya umeme) unaonyesha mahitaji ya umeme yanakua kwa wastani wa asilimia 10 hadi 15 kila mwaka katika kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi 2012," alisema.

Alisema changamoto ni kwamba mipango iliyopo ya kuongeza uzalishaji haitaweza kuziba pengo kati ya uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme na mahitaji ya umeme yanayotarajiwa kati ya mwaka huu na mwaka kesho, baada ya miradi ya dharura kuondolewa.

"Hii inatokana na ukweli kwamba, ni vigumu kubuni mradi unaoweza kukamilika kabla ya mwaka 2009 kuisha," alisisitiza.

Kuhusu bunge kushauri mitambo hiyo ya Dowans isinunuliwe kutokana na kwenda kinyume na sheria ya manunuzi ya umma, Ngeleja alijibu: "Ninachokumbuka, bunge lilijadili na kupitisha azimio kuhusu uhalali wa mkataba wa Richmond.

"Hakuna mtu anayepinga... mkataba wa Richmond ulibainika kuwa tata na serikali ilichukua hatua. Serikali haiwezi kuzembea wala kufumbia macho vitendo vya kifisadi.

"Juni 28, 2008 serikali ilitoa tamko la kusitishwa mkataba huo ifikapo Agosti mosi na kweli ilifanyika... hatua hiyo ilichukuliwa na serikali lakini pia kwa kuzingatia maelekezo ya bunge," alifafanua.

Alipoulizwa sababu za kung'ang'ania kununua mitambo hiyo kinyume na Sheria ya Manunuzi ya Umme ambayo inazuia taasisi za serikali kununua mitumba, Ngeleja alihoji: "Mbona watu wanasema tununue mitambo ya IPTL.

"Ni kweli sheria ya PPRA inatakaza ununuzi wa vitu vilivyotumika, lakini yapo maeneo ambayo kutokana na mazingira halisi ya kisekta si lazima kinachonunuliwa kiwe kipya.

"Angalia, ATC leo hii inaweza kununua au kukodi ndege lakini si lazima iwe mpya. Tuangalie maeneo ya msingi, jambo kubwa ni watalaamu kuthibitisha ubora na uwezo wa kukidhi mahitaji ya nchi. Mitambo ile unaweza kuifunga leo hii katika toroli na kuipeleka mkoa wowote wenye uhaba wa umeme."

Kuhusu gharama za kununua mitambo mipya kulinganisha na gharama za mitambo ya mitumba ya Dowans, Ngeleja alijibu: "Tuliwahi kupata mtaalamu akasema hii ya Dowans ni kati ya dola 58 hadi 60 milioni, wakati mipya ni kati ya dola 120 milioni... mara mbili ya hii."

Alisema uamuzi huo wa kutaka kununua mitambo ya Dowans, hauna msukumo wala mkono wa mafisadi kwani unalenga kuikoa nchi katika tatizo la mgao wa umeme.

"'Sasa hapa, utaona kwamba uamuzi huu hauna msukumo wala mkono wa mafisadi," alisema.

Utata wa mitambo hiyo ya Dowans sasa unaendelea kama sakata la zabuni ya ufuaji umeme wa dharura lilivyoanza. Dowans ilirithi mkataba wa Richmond iliyobainika kuwa haikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme huo wa dharura.

Matokeo ya uchunguzi wa kamati hiyo ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge Harrison Mwakyembe ulisababisha Lowassa kujiuzulu baada ya kutuhumiwa kuingilia mchakato wa zabuni na kushauriwa atumie busara kuamua juu ya ushiriki wake katika suala hilo.

Hali mkataba wa Dowans ukiwa umeshaisha, kampuni hiyo imewasilisha mashtaka Mahakama ya Kimataifa ya Biashara dhidi ya Tanesco, ambayo nayo imeshikilia mitambo ya Dowans ikisema kuwa itatumika kama fidia iwapo shirika hilo la serikali litashinda kesi hiyo.
 
Back
Top Bottom