Mwachieni Gire, nunueni mitambo ya Dowans! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwachieni Gire, nunueni mitambo ya Dowans!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 27, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Well, kuna wakati inabidi tuseme tu kuliko kuzungushana kwenye huu utando wa buibui wa ufisadi. TUmekuwa kama kumbikumbi, na kama vipepeo tumenaswa na wao wanatuchezea tu.. kama paka aliyeshiba anavyomchezea chezea panya aliyechoka kukimbia!

  Sasa naomba tulimalize hili la Richmond/Dowans:
  a.) Bw. Gire aachiliwe kwani tayari tunanyajua kampuni yake ilikuwa feki na kama maelezo ya jana yana dalili yote "upepelezi bado unaendelea". Sasa huu upepelezi wa miaka mitatu nadhani unatosha, na kwa vile hakuna ushahidi (msiniulize kwanini walimfungulia kesi kama hawakuwa wamekamilisha upepelezi au walikuwa wanakaribia kuukamilisha).

  b.) Mitambo ya Dowans hatimaye tutainunua kwa vile tunapaswa kuinunua kwani kutoinunua haiingii akilini wakati "ipo tu pale"! Mitambo hii haiendi kwa mtu yeyote binafsi na matatizo ya umeme yanayokuja mwezi wa nne itakuwa ni ushahidi kuwa ni "bora" tuinunue tu!. So why not buy them!?

  Sasa tumefikia kamati mbili za Bunge, Wizara, na wengine tunaanza kurushiana utadhani Taifa zima linacheza "Ready". Mara mpira huku, mara kule, huku mafisadi wanakwepa katikati wakiendelea kujaza chupa yao mchanga wa utajiri wa nchi yetu!, so why not just buy them, wapeni hizo fedha (kwani zipo nyingi tu). Tulimalize?

  c.) Kwa vile hakuna mtu mwingine atakayepelekwa makahamani kwani muda unapita na mwisho mambo ya statutes of limitations inaweza kuingia kwenye baadhi ya mashtaka, kwanini tusiamue tu kusema "screw it" wameshajiuzulu watu (wakapewa mafao yao) na Richmond haipo tena.. so tulifunge tu.
  Kimsingi, hatuwezi kulimaliza hili la Richmond na Dowans isipokuwa kwa kufuta hii kesi moja, kununua mitambo ya Dowans, kuwalipa kina Rostam na washiriki wake, halafu tumaliize yaishe. Hatuwezi kama taifa kuendelea kupiga kambi kwenye hili bonde la kashfa miaka nenda rudi. Hili la Dowans tulimalize, tujue limekwisha kuliko kuzunguka zunguka utadhani watoto wanaocheza "ukuti ukuti!"

  Then, tutaangalia haya mengine, haya mambo ya kuzugana kwa kweli wakati mwingine inabidi tukubali tu yaishe!
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Of all the months mwezi wa nne kuwe na shida ya umeme? Gimme a break!
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...Mama, i know you know that it's a mere preemptive strike. tunashida ya umeme hata kwenye mvua za vuli... don't we?
   
 4. M

  Mama JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo kama tuna shida ya umeme kwenye mvua za vuli lazima tuwe na shida ya umeme kwenye mvua za masika?

  Kama tuna shida ya umeme, iwekwe kwamba hiyo mitambo inunuliwe kwa sababu tuna shida ya umeme. Sio inunuliwe kwa sababu kuna shida ya umeme mwezi wa nne, ni uongo period!
   
 5. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...huo ulikuwa mfano Mama.

  ...Mama, hoja ya msingi aliyotoa bado iko hapo hapo. Kila mmoja wetu ana aina yake ya uandishi. Nina amini kuwa wengi watakao soma hiyo hoja hapo juu wataelewa alichotaka kumaanisha kwenye hicho kipengele unachokiita ni cha uongo.

  ....Pale unapopika mboga yenye limao kama mojawapo ya kiungo na mgeni wako kukutana na mbegu moja akiwa anatafuna; hasusii bakuri lote, bali atachukua tahadhari wakati akiwa anatafuna matonge yafuatiayo. Maana mpikaji hahitaji kumtafunia huyo mgeni.
   
 6. M

  Mama JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Steve hii tabia ya kuweka limao na viungo kwenye habari, inapotosha ukweli, inapotosha jamii. Tukubali kujifunza kuwa precise. Wote tunakosea, lakini ni vyema kujifunza na kuwork hard kupunguza makosa madogo madogo. If you always aim higher, your failure will be success.

  Halafu Watanzania, tuko very vulnerable na kulambishwa sukari ya kuchemsha na kuambiwa ni asali. Tunakubali tu kwa vile ni tamu!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nani amekuambia shida yote ya umeme wa Tanzania inahusiana na Mvua!!?
   
 8. M

  Mama JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Huyo aliekuambia kwamba mwezi wa nne kutakuwa na shida ya umeme!
   
  Last edited: Feb 27, 2009
 9. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mama, hapa umesema uongo au umesema ukweli?
   
 10. M

  Mama JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Hapo sijasema uongo wala ukweli.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  na maoni yangu pia sitakiwa kuyatoa ninavyoyatoa; maoni nayo imekuwa habari! haya mama nielekeze jinsi ya kutoa maoni nisikukwaze!
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  wewe basi ni mshirika wa uongo!!
   
 13. M

  Mama JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Maoni yanakuwa habari unapoyaweka hapa. Yako wazi kujadiliwa. Rejea JF motto.

  Jinsi gani utoe maoni ili usinikwaze: usiweke speculations kwa mfano kusema kutakuwa na shida ya umeme mwezi wa nne bila kueleza kinagaubaga kwa nini unadhani (kwa maoni yako) mwezi wa nne kutakuwa na shida ya umeme.
   
  Last edited: Feb 27, 2009
 14. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ninakubaliana na yote hayo uliyoyasema Mama. Mimi nilichoelewa alipotolea "mfano", maana naami kuwa huo ulikuwa mfano (kunradhi kama siyo), kuhusiana na mwezi wa nne, alikuwa anataka kuvuta hisia za kipindi kile Mtera na Ruvu (chini na juu) zote zilikauka kwa kisingizio cha mvua... halafu mwezi wa nne (au wa tatu) ulipokuja, mvua kubwa ikanyesha na kujaza mabwawa yote matatu, ilihali kilichosemwa mwanzo kilikuwa kuwa misimu miwili ya mvua ilihitajika kuweza kujaza mabwawa yale.

  Halafu baada ya hapo tu, pamoja na mabwawa kujazwa huku tukiwa tumeletewa Richmond, bado migao ya umeme iliendelea... na mpaka hivi sasa bado inaendelea. Mimi sipendi mambo ya siasa, lakini kawaida nakuwa namwelewa Mkjj mapema saa nyingine hata kabla hajamalizia sentensi zake kwa sababu ya yale ninayoyasoma kuhusiana na mazingira yetu ya nyumbani kisiasa na uchumi. Sasa pale anapoleta satire zake kwenye maandishi au pale anapotaka kuchochea kitu fulani hivi ili watu wakiongelee, ana dhumuni lake. Sisi kama ma-critics tujue pahali pa kumshupalia kwenye uandishi wake. Tukikumbuka kuwa kila mmoja ana aina yake ya uandishi na aina ya u-critic tuliyonayo inapojirudia rudia, haina tofauti na aina ya uandishi aliokuwa nao yeye. Ndo maana nikamaanisha kuwa ukimhoji mwenye kukutengea bakuri la mboga hachelewi kukuambia kuwa kajipikie yako isiyotumia limao au yenye kutumia chujio kali.

  Ahsante.

  SteveD.
   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nilishaandika zamani sana kuwa "Wahindi na Waarabu/Wairan waachiwe na au tumallizane wenyewe au tusameheane wenyewe. Kuonea Ngozi nyeupe wakati SERIKALI ni sisi, huu ni upuuzi wa ajabu.
  Tusubiri tu siku akaja KICHAA. Kuanzia Mzee anayetakiwa apumzike kwa amani na hadi wanaopigia debe kuwa Mzee apumzike kwa amani, itabidi wajengewe vyumba Keko. Kama Malawi nao wamempandisha Rais wao, Zambia walifanya hivyo, hii ni habari ambayo siku moja Tanzania itafika. Heri wajifunza sheria za wacheza kamali yaani "Lazima ujuwe muda wa kukimbia meza ya kamali". Kama hujui, basi utaishia pabaya!!!!
   
 16. M

  Mama JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0


  Mwanakijiji hajasema kwamba huo ni mfano. Na wewe unazua. Unaona sasa Steve, hili ni tatizo sugu la wengi wetu.

  Yaani kwa vile wewe una uwezo wa kumwelewa Mwanakijiji kabla hata hajamalizia sentensi yake, basi umeassume kwamba members 8500 wa JF wanamwelewa kama wewe unavyomwelewa.

  Tujifunze jamani kuwa katika mawasiliano every word counts, kama hatujakuzwa hivyo, tujifunze basi.


   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Feb 27, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Priceless! Lol
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  nitatumia maneno ninavyoweza, jinsi ninavyoweza, namna ninavyoweza na katika kufanya hivyo nakusudia kukukwaza..
   
 19. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ....sawa Mama, hayo ni maoni yako.

  ....Mama, inakuwa habari kwa wananchi wote wa Tanzania, wana JF au akina nani?
  ....Na yanapobadilika na kuwa habari, je habari hiyo ni sawa na ya DailyNews, Nipashe, CNN au TBC1?


  Mama, kwa heshima kubwa nimesema "mimi ninachoelewa".... Sasa ukisema nimezua, je kuelewa kwangu kwa kitu fulani ni sawa na "kuzua?"

  Pia nimesema "saa nyingine", sijasema kijumlajumla kama jinsi ulivyoweka hiyo sentensi juu.

  Ahsante.

  SteveD.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kuna msemo wa kumpigia mbuzi gitaa.. sielewi mantiki yake lakini wakati mwingine nauelewa.
   
Loading...