Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,491
- 40,023
- Thread starter
-
- #21
Nilishaandika zamani sana kuwa "Wahindi na Waarabu/Wairan waachiwe na au tumallizane wenyewe au tusameheane wenyewe. Kuonea Ngozi nyeupe wakati SERIKALI ni sisi, huu ni upuuzi wa ajabu.
Tusubiri tu siku akaja KICHAA. Kuanzia Mzee anayetakiwa apumzike kwa amani na hadi wanaopigia debe kuwa Mzee apumzike kwa amani, itabidi wajengewe vyumba Keko. Kama Malawi nao wamempandisha Rais wao, Zambia walifanya hivyo, hii ni habari ambayo siku moja Tanzania itafika. Heri wajifunza sheria za wacheza kamali yaani "Lazima ujuwe muda wa kukimbia meza ya kamali". Kama hujui, basi utaishia pabaya!!!!
nitatumia maneno ninavyoweza, jinsi ninavyoweza, namna ninavyoweza na katika kufanya hivyo nakusudia kukukwaza..
Kwanza unamshambulia huyu "mama" kwa topic ulioanzisha wewe.
Eti nani anamshambulia nani? Au mimi ninasoma vitu tofauti na vilivyoandikwa hapa?
"wewe basi ni mshirika wa uongo!!" Mkjj wrote
Mwanakijiji hajasema kwamba huo ni mfano. Na wewe unazua. Unaona sasa Steve, hili ni tatizo sugu la wengi wetu.
Yaani kwa vile wewe una uwezo wa kumwelewa Mwanakijiji kabla hata hajamalizia sentensi yake, basi umeassume kwamba members 8500 wa JF wanamwelewa kama wewe unavyomwelewa.
Tujifunze jamani kuwa katika mawasiliano every word counts, kama hatujakuzwa hivyo, tujifunze basi.
...na akina nani.........unaona sasa na wewe una tatizo........yaani kushindwa kwako kumuelewa Steve ndio inakupa kibali cha ku-generalise........duuh
Priceless! Lol
Internet connection: $ 20
Desktop Computer: $ 700
Ubishani usioisha: PRICELESS
No...ni ubishani usio na msingi au usio na kichwa wala miguu!!
........yote sawa tu........wee warudishie ila mada ya Dr. Masau kiaina........na kiongozi wao ataibuka.......shauri zako.........BTW tomorrow isn't here yet...........only "true substances of life" will be served tomorrow
Mwanakijiji, sisi ni Observers tu lakini katika coments ambazo umewahi kuvurunda hii ni namba wani! Kwanza unamshambulia huyu "mama" kwa topic ulioanzisha wewe. Wewe umesema "umeme utakuwa wa shida April"; she commented, so give the reasons why will be such a shortage!
Of all the months mwezi wa nne kuwe na shida ya umeme? Gimme a break!
Halafu huyu "Gire and the GROUP"; wana kesi ya kujibu (kama mahakama na sheria zetu zingekuwa strong). They brought an old "turnkey" project at a hiked USD 170 million dollar cost while the machines/equipments cost only USD 22 million; you know when these equipments where made? And for your information do you know the cost of efurbishment? Then when they were brought here were not fit for the purpose; they couldn't use natural gas as fuel; they had to be modified. How much the tax payers money have been squandered!
You better tell us how much do you think the government should buy from Dowans? There are many sources for such cheap stuff, you need one? I can send it to your private message and you can help your government.
Your writing is easy than the real issue is, these guys should be punished in a severe way possible, and pay the costs!
"wewe basi ni mshirika wa uongo!!" Mkjj wrote
Well, kuna wakati inabidi tuseme tu kuliko kuzungushana kwenye huu utando wa buibui wa ufisadi. TUmekuwa kama kumbikumbi, na kama vipepeo tumenaswa na wao wanatuchezea tu.. kama paka aliyeshiba anavyomchezea chezea panya aliyechoka kukimbia!
Sasa naomba tulimalize hili la Richmond/Dowans:a.) Bw. Gire aachiliwe kwani tayari tunanyajua kampuni yake ilikuwa feki na kama maelezo ya jana yana dalili yote "upepelezi bado unaendelea". Sasa huu upepelezi wa miaka mitatu nadhani unatosha, na kwa vile hakuna ushahidi (msiniulize kwanini walimfungulia kesi kama hawakuwa wamekamilisha upepelezi au walikuwa wanakaribia kuukamilisha).Kimsingi, hatuwezi kulimaliza hili la Richmond na Dowans isipokuwa kwa kufuta hii kesi moja, kununua mitambo ya Dowans, kuwalipa kina Rostam na washiriki wake, halafu tumaliize yaishe. Hatuwezi kama taifa kuendelea kupiga kambi kwenye hili bonde la kashfa miaka nenda rudi. Hili la Dowans tulimalize, tujue limekwisha kuliko kuzunguka zunguka utadhani watoto wanaocheza "ukuti ukuti!"
b.) Mitambo ya Dowans hatimaye tutainunua kwa vile tunapaswa kuinunua kwani kutoinunua haiingii akilini wakati "ipo tu pale"! Mitambo hii haiendi kwa mtu yeyote binafsi na matatizo ya umeme yanayokuja mwezi wa nne itakuwa ni ushahidi kuwa ni "bora" tuinunue tu!. So why not buy them!?
Sasa tumefikia kamati mbili za Bunge, Wizara, na wengine tunaanza kurushiana utadhani Taifa zima linacheza "Ready". Mara mpira huku, mara kule, huku mafisadi wanakwepa katikati wakiendelea kujaza chupa yao mchanga wa utajiri wa nchi yetu!, so why not just buy them, wapeni hizo fedha (kwani zipo nyingi tu). Tulimalize?
c.) Kwa vile hakuna mtu mwingine atakayepelekwa makahamani kwani muda unapita na mwisho mambo ya statutes of limitations inaweza kuingia kwenye baadhi ya mashtaka, kwanini tusiamue tu kusema "screw it" wameshajiuzulu watu (wakapewa mafao yao) na Richmond haipo tena.. so tulifunge tu.
Then, tutaangalia haya mengine, haya mambo ya kuzugana kwa kweli wakati mwingine inabidi tukubali tu yaishe!
...na akina nani.........unaona sasa na wewe una tatizo........yaani kushindwa kwako kumuelewa Steve ndio inakupa kibali cha ku-generalise........duuh
soma kilichoandikwa; kama yeye anasema aliyemwambia kuwa matatizo yote ya umeme Tanzania yanatokana na mvua ndiye aliyeniambia mimi kuhusu kauli yangu basi mimi nikamwambia kuwa yeye ni mshirika wa uongo kwani mtu huyo huyo ametuongopea wote wawili!!
Duh.. hata hilli nilifafanue!
Of all the months mwezi wa nne kuwe na shida ya umeme? Gimme a break!
mm, sorry. ni ngependa kuandika ifuatavyo kuhusu ulichoandika hapo juu;a.) Bw. Gire aachiliwe kwani tayari tunanyajua kampuni yake ilikuwa feki na kama maelezo ya jana yana dalili yote "upepelezi bado unaendelea". Sasa huu upepelezi wa miaka mitatu nadhani unatosha, na kwa vile hakuna ushahidi (msiniulize kwanini walimfungulia kesi kama hawakuwa wamekamilisha upepelezi au walikuwa wanakaribia kuukamilisha).
b.) Mitambo ya Dowans hatimaye tutainunua kwa vile tunapaswa kuinunua kwani kutoinunua haiingii akilini wakati "ipo tu pale"! Mitambo hii haiendi kwa mtu yeyote binafsi na matatizo ya umeme yanayokuja mwezi wa nne itakuwa ni ushahidi kuwa ni "bora" tuinunue tu!. So why not buy them!?
Sasa tumefikia kamati mbili za Bunge, Wizara, na wengine tunaanza kurushiana utadhani Taifa zima linacheza "Ready". Mara mpira huku, mara kule, huku mafisadi wanakwepa katikati wakiendelea kujaza chupa yao mchanga wa utajiri wa nchi yetu!, so why not just buy them, wapeni hizo fedha (kwani zipo nyingi tu). Tulimalize?
c.) Kwa vile hakuna mtu mwingine atakayepelekwa makahamani kwani muda unapita na mwisho mambo ya statutes of limitations inaweza kuingia kwenye baadhi ya mashtaka, kwanini tusiamue tu kusema "screw it" wameshajiuzulu watu (wakapewa mafao yao) na Richmond haipo tena.. so tulifunge tu.
mm, sorry. ni ngependa kuandika ifuatavyo kuhusu ulichoandika hapo juu;a.) Kuhusu kuachiwa gire, hilo tulisilifanye. kama tunajua kampuni yake ilikuwa feki si ndio tumemkuta na kosa la kutudanganya? kwa kudanganya kajipatia hela kutoka kwetu. na lingine kwa kudanganya katutia hasara. sa kwanin tusimhukumu kwa hilo? ndo kusema hawajapata ushahidi kuwa uwezo wa kampuni yake ulikuwa sio kama ulivyodaiwa? au pia ushahidi haujakamilika kwa hilo?Otherwise kila siku tutabaki kulia na wezi/ufisadi.... wezi/ufisadi.... wezi/ufisadi.... na hautokaa uishe. na hatutokaa tuanze kushughulikia matatizo mengine katka tz yetu kwa umadhubuti wizi/ufisad utakuwa umetuweka bize
Tukithubutu kumwachia, kesho atarudia tena. au wengine watathubutu kutufanyia kama hivi halafu itabidi tuwaachie kwasababu zitakazopelekea tumwachie gire leo. adhabu tena kali ni muhimu kwa mambo haya na adhabu hutuma ujumbe maridhawa kwa wote. adhabu kali ni kinga maridhawa dhidi ya watu watakao jaribu kutufanya ndivyosivyo baadae.
b.) Kuhusu kununua mitambo ya dowans, sina uhakika niandikeje. teh teh teh. sijui huko ndani tanesco na wizarani kukoje.
Huenda kuinunua ndo ikawa ultimate solution (uamuzi pekee na bora zaidi). na mtego unaweza kuwa tusipoinunua wahusika ambao wana jukumu la kutafuta mbadala wa mitambo ya dowans watakaa kimya mpaka tatizo la umeme lianze kutafuna nchi. Halafu wataibuka wakisema 'mnaona? Tuna tatizo la umeme kwasababu hatukununua mitambo ya dowans?'. Halafu sisi sote tutaanza kuwalaumu waliosababisha mitambo ya dowans isinunuliwe. Kumbe watu wamehonga pa kuhonga tatizo likatokea. Na huenda kuna options zingine bora zaidi zilikuwa zichukuliwe tangia zamani lakin watu walikaa kimya (au kwa uzembe au kwa makusudi). Lakini huenda right now kuna best solutions to the problem lakin watu hawazileti hadharani kwasababu wanataka mitambo ya dowans inunuliwe.
c.) Yeah, sio mtaalamu wa sheria mimi lakini kesi za ufisadi/uhujumu nchi au uchumi ziwe zinaweza kuendelea siku zote labda kama mwenyewe akiamua 'kufa'. Hii ni kwasababu negative impact ya ufisadi kama huu (kama kweli gire katenda kosa) ni kwa watu wengi sana (nchi) na hudumu kwa muda mrefu sana. kwahiyo na kesi pia ziwe zinaweza kuendelea to infinity.. na akipatikana na kosa adhabu yake iwe to infinity... ili next time tomorrow mtu akitaka kuiingiza tanzania mkenge ajifikirie mara mbilimbili.