Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,618
Wanabodi,
Hizi kelele za wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kuhusu hii IGA ya DPW na Bandari zetu, sio za kuzipuuzia!. Katiba hii mbovu tuliyonayo!, Sheria zetu mbovu tuliyonayo, mikataba mibovu ya kimataifa tunayoingia, mwisho wa siku tunajikuta tumepigwa!, tunafunguliwa mashitaka, tunashindwa, tunapigwa tozo za mabilioni ya fedha!, ambazo ni lazima tulipe.

Haya yote ni matokeo ya kazi ya wanasheria wabovu na baadhi yao vilaza!. Leo nimeianza siku kwa bad news kutoka Marekani, Tanzania tumeshindwa kesi, tunadaiwa tozo ya dola za Marekani zaidi ya Millioni 100!, na lazima tulipe!.

Soma taarifa hii hapa chini
1689682884428.png

  1. Kama Tanzania tulipitisha sheria kuwa kwenye uwekezaji hakuna mashauri yoyote ya nje ya nchi!. Mashauri yote ni hapa nchini kutumia sheria za Tanzania!, sasa haya mashauri yanaendelea vipi kupelekwa nje?.
  2. Hii maana yake ni ama tuna sheria mbovu, ama tuna wanasheria wabovu wanaotunga sheria mbovu, zinazotupa mikataba mibovu, na mwisho wa siku tunaishia kupigwa na kutozwa matozo ya ajabu ajabu!.
  3. Huku kila siku kushindwa kesi za kimataifa na kupigwa tozo nako ni ama tuna sheria mbovu za mikataba mibovu ama kama sheria ni nzuri, then tuna wanasheria wabovu wasio na uwezo wa kushauri the right thing to do!, hivyo serikali yetu inavunja mikataba kitutusa na mwisho wa siku tunaishia kuumizwa kwa kushindwa kesi na kupigwa tozo!.
  4. Kabla ya kuvunja mkataba wowote, serikali yetu inaomba ushauri wa kisheria kufanya kitu kinachoitwa mitigation, wanasheria hawa huishauri vibaya serikali yetu, mwisho wa siku, tunaishia kuumizwa!.
  5. Issues ya Richmond, Dowans, tukaunda tume, ikatoa matokeo kwa mbwembe kuwa Richmond ni kampuni hewa hata tukivunja mkataba, hatutashitakiwa popote!.
  6. Tukamfanya Edward Lowassa ni mbuzi wa kafara, tukavunja mkataba!.
  7. Tukashitakiwa tukashindwa, tukapigwa tozo!. Waliotushauri tuvunje mkataba wakajiapiza "over my dead body!, hatulipi". Tulilipa kisiri siri every cent!. Hawa wanasheria walifanywa nini?
  8. Mitambo ya Richmond ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule na tukawalipa!.
  9. Chuma JPM, alipoingia tukavunja mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, tukapigwa tozo, Chuma JPM, akagoma hatulipi!
  10. Mama kaingia, tumelipa fasta fasta, kimya kimya!. Wanasheria waliotufikisha hapa walifanywa nini?!.
  11. Tulipotunga sheria mbovu, watu humu tulishauri Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?, leo baada ya kutuletea hii IGA mbovu, watu tumeeleza matatizo yake kibao!.
  12. Wanasheria hawa hawa, Bunge letu hili hili wanaipitisha hivyo hivyo ilivyo, wanaiambia serikali yetu hii IGA ni nzuri, safi na haina matatizo yoyote!.
  13. Wanasheria hawa wanao tufikisha hapa, tukiwaita ni wanasheria wabovu au vilaza, itakuwa ni kuwaonea?.
  14. Tanzania tutaendelea kufanywa shamba la bibi na kichwa cha Mwendawazimu na wanasheria wabovu na vilaza wa aina hii hadi lini?!.
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
 

Attachments

  • 02687624_230718_101239 arbitration.pdf
    330.4 KB · Views: 7
Kwenye mikataba mikubwa naona tungeajiri makampuni ya nje ili watusaidie kuliko kiweka vilaza wanasaini kwa maslahi yao

Sijawahi kuona mikataba inasainiwa haraka hivi kama kwetu

Na kuwa na Rais mwenye mamlaka ya kukubali bila ushauri nalo mkaliangalie la sivyo tutakuwa wajinga wa kudaiwa mpaka mwisho

Tusimlaumu mzungu kwa ujinga wetu ingawa mleta Mada hakulaumu hao bali sisi wenyewe
 
Bwana Mayala: haya yooooote unaweza kuyasema kwa neno moja: RULE OF LAW, i mean maneno matatu.

Sheria ya zamani ilikuwa na RETENTION LICENSE, yaani wakati unachimbachimba kutafuta dhahabu ulipewa miaka 5, unachukua RETENTION LICENSE kwa miaka mingine mitano ujaribu tena. Usipopata ndiyo basi. Huyu alikuwa na haki zote, kafanya kama ilivyotakiwa na sheria, kaja mtu mmoja akamnyanganya eneo lake, just like that. Huo si uzalendo, ni uvunjifu wa sheria tu.

Inawezekana huyo ndiyo alikuwa na maslahi yake binafsi, aulizwe - hii haihotaji tumehuru. Rais yuko Magogoni machimbo tako Makongolosi Chunya, atajuaje? Ni huo ushauri mbovu, si katiba mpya. Nakumbuka wote mlishangilia hiyo sheria isiyo sheria ilipopitishwa uweje sasa mnatupa crocodile tears?

Kuna wazalendu uchwara hawajui kama na wenzao nao ni wazalendo kwa nchi zao. Bomba la Mafuta linatoka Uganda ni maliasili yao watataka watumie sheria za Uganda.

Bomba linapita Katoma na Ng'wakitolyo hadi Chumbageni Tanga hiyo ni Nji yetu turataka tutumie sheria yetu. Nani ashinde? Nani ashindwe? Ndiyo maana wapuuzi kina Shivji Marxist na Slaa Msaliti wanagangania tutumie Jaji wa Kisutu wakati Mwarabu naye HELA zake ni mali ya Mfalme wake.

Katika hali hii tunatumia Geneva Convention inayotaka muende kwenye Nchi ya tatu lakini hawa wapumbavu hawataki kusikiliza. Mimi nakushauri soma Ilani ya CUF ilisemaje kuhusu bandari na ya CHADEMA halafu linganisha na ta CCM.

Mwaka 2020 ni ilani ya CCM ndiyo iliyoshinda, waachwe waitekeleze. Wananchi tusiyumbishwe na Wasaliti na mafisadi katika maisha yao.
 
Wanabodi,
Hizi kelele za wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kuhusu hii IGA ya DPW na Bandari zetu, sio za kuzipuuzia!. Katiba hii mbovu tuliyonayo!, Sheria zetu mbovu tuliyonayo, mikataba mibovu ya kimataifa tunayoingia, mwisho wa siku tunajikuta tumepigwa!, tunafunguliwa mashitaka, tunashindwa, tunapigwa tozo za mabilioni ya fedha!, ambazo ni lazima tulipe.
Kaka Paskali,
viongozi wetu ni kama mamba. Hawasikii hadi damu itokee masikioni..!!!
 
Hebu tazama kitu, kama wakati wa JPM licha ya kupigwa hizo faini lakini aligona kulipa, amekuja huyu Samia, akalipa, Samia huyu huyu aliyetuletea hili balaa kubwa zaidi la DPW, hivi hapa inahitajika darubini gani kuijua nia ovu ya huyu mwanamke anayetuongoza sasa?

Anaonesha dhahiri, hii mikataba mibovu anaingia makusudi, huku akijua madhara yote, then akitokea jasiri wa kuvunja hiyo mikataba, wajinga wanalalamika kwanini mnaivunja tutalipishwa faini, kwani ikiwa inatekelezwa kama taifa tunapata nini cha maana mpaka tuogope hizo faini?

Nasisitiza, wacha tulipishwe hizo faini, kuliko kuendelea kuonekana wajinga na wazungu na waarabu, wanaotumia upumbavu wa viongozi wetu kusaini mikataba ya hovyo inayolinyonya taifa miaka yote.

Wacha tuwaoneshe kwa vitendo wapo watanganyika wanaojielewa, wasiopenda ujinga wa 10%, hata kama watatuumiza kwenye fidia, lakini heshima yetu kama taifa tunailinda.
 
Ni kwamba
1. Hizo hela wanalipwa watanzania kupitia migongo ya makampuni ya nje. Rost arm
2. Watz wasio na huruma na nchi au wenye uraia pacha wanatengeneza mikataba hiyi kisha wanaipeleka kwa makampuni ya nje ili watukamue. Rost arm
3. Huwezi ingia mikataba kama DPworld ukiwa na akili timamu. Rist arm

Wazalendo tuungane kutafuta uhuru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom