Tumepuuza namna ya Ki'Magufuli ya kuendesha nchi yetu matokeo yake tumeharibikiwa kila pahala!

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,939
4,122
Kuifanya akili igome kukumbuka tulikokuwa tumefika kama nchi, tukasahau masuala ya shida ya umeme, huko kunaitwa ni unyanyasaji wa mfumo ubongo, na anayekataa tusikumbuke ni aidha yeye ndo mchawi wa hii nchi

Na nataka niwaambie wote mliokuwa mkimdhihaki Magufuli, sasa mnaumbuka vibaya sana, kwani wengi wetu wenye akiba ya maneno, tulijua nia zenu na hata mwisho wenu kwamba, itakuwa ni fedheha kubwa sana

Mlimfosi na kumkandia maneno magumu na ya kejeli eti, mfumo wa nidhani ya uoga kazini kwa wafanyakazi wa umma ni wa kishamba, mkaahidi mtatengeneza mfumo mzuri ambao mfanya kazi atajikuta akiogopa tu mwenyewe, wenye upeo tuliona kabisa mnaenda kutengeneza wafanyakazi wazembe na wasio na nidhamu pahala popote hasa kwenye eneo la kuhudumia wananchi na mambo ya fedha (ufisadi) rushwa n.k

Mlisema, Magufuli ni mtu ambaye anajua kutumia tu kwenye eneo la mitambo ya Tanesco hajali na haifanyi ukarabati na sasa imechoka sana na itahitaji ukarabati nchi nzima muda wa miezi 3 mpaka 6, hii ni toka 2021 huko na leo ni 2024, kinachonipa hasira sana kwa sasa, hakuna tarifa sahihi ikiwa kuna mitambo iligoma kukarabatiwa na ndiyo maana tupo kwenye mgao ambao umevunja record sasa, ni takribani mwaka sasa unaelekea tukiwa kwenye mgao

Mgao ulioanza kwa rasharasha na sasa unaelekea kwenye kuzima kabisa mitambo na tusiwe na umeme sasa! Hii maana yake ni nini?

SUKARI, jambo hili sasa hata halieleweki ikiwa nchi kweli ni yetu ama kunamahali tumeiuza kwenye eneo hili kuna anayesimamia na ndiyo maana linakwenda tuu na hakuna utaratibu wowote?

Nishati ya Mafuta! Sumatra kipindi cha mwanzoni mwa vita ya Urus na Ukraine, nishati hiyo ilipanda kiasi cha kufika kuuzwa Tsh 3800 kwa lita, ila nauli hazikupanda kihivo

Juzujuzi mafuta yalipanda kufika 4000+ na nauli zipanda juu sana lakini leo mafuta hayo yameshuka hadi 3500 lita na bado nauli hazishuki, hata hivyo, siwalaumu viongozi bali nawalaumu wananchi wenzangu kwenye hili
 
Walaumu hao hao ndugu zako ccm kwa kuweka mifumo mibovu ya kiuongozi. Acha kuwahusisha watu wasiohusika kwenye mambo yenu ya kipuuzi.
 
Back
Top Bottom