Ulweso
JF-Expert Member
- May 24, 2016
- 23,106
- 28,062
Hapo umenena, bora arudi akaanze na moja aachane naye sahizi anavipesa vinampa kiburi, yeye akapambane na maisha yake, wengi wanakimbiwa na wanasimama wenyewe, kuvumilia huko mwisho wake nikusubilia kifo tu mwingine kachomwa mkuki na kufa .my dear pole sana, huwa siwaelewi wamama wanaowambiaga watoto wao wakike wavumilie mateso kwa wanaume? kwani HUYO mama ako anaishi wapi na anakula nini? kwanini asikwambie urudi nyumbani mhangaike wote kuliko kukwambia uvumilie mateso ya namna hiyo JAMANI? Nnachoweza kukushauri kwanza hebu achana na huyo mwanaume nimeona kuna watu wamekushauri eti urudi SIELEWI WANATAKA URUDI KUFANYA NINI KWA MTU WA NAMNA HIYO, ukasubirie ukimwi au ili uweze kupata sababu ya kujiua vzr? bcz am sure ukisema uendelee kuishi nae iko siku kweli atakupa sababu ya utajitoa uhai, anza kabisa kumfuta kwenye mawazo, isitoshe hata ndoa hamjafunga eti kisa mtoto, huyo sio mtu wa kusema ufunge nae ndoa hakuna guarantee ukimzalia akakuoa atabadilika awe mume mwema, mwanaume mshenzi na malaya ni mshenzi tu, sema huyo wako kapata sababu kisa hujamzalia kwahiyo anatumia kama fimbo ya kukuchapia lakini hiyo ni tabia yake hata uzae na muingie kanisani mfunge hiyo ndoa he wont change. Kama ni swala la mtaji ili upate pa kuanzia am sure humu tunaweza changishana ukapata hela ya kuanza biashara hata kama ni kupika maandazi na chapati lakini hutaweza kukosa mtaji, just say the word.. Kingine kwa hali nnavyoiona kama mtoto bado yuko shule ya msingi na umempelekea shule za kulipia, nakushauri ni heri umrudishe shule za bure za serikali, hata sisi mbona tumesoma hizo hizo natulifanya tu vzr tukafika mpaka vyuoni, jikune unapifikia mamy. Mwisho piga goti mlilie sana Mungu akupe amani na akufungulie njia
Sent using Jamii Forums mobile app