Mungu nisamehe kwa nilichotaka kufanya

Mungu nisamehe kwa nilichotaka kufanya

Binafsi kifo cha Mpauko kimenipa funzo sana. Nimepitia nyuzi zote na comment Mungu naomba tu unisamehe kwa mawazo niliyokua nayo.

Binafsi nilizaa 2014 mume akafariki ghafla kwa ajali nikabaki na mtoto. Nilihangaika sana sababu sikuwa na pakushika.

Mama yangu alikuwa Mtendaji alistaafu 2015, bahati nzuri akanipa mtaji milioni 1.5 nikafungua duka la dawa. Mungu akanisaidia nikawa naenda vizuri na maisha, 2016 nikapata mchumba aliyekuwa tempo TANESCO. Mshahara ulikuwa haukidhi na maisha ya kwao yalikuwa duni sana hivyo yeye ndio alikuwa tegemezi.

Kidogo mimi biashara haikunitupa hivyo akikwama nilikuwa namsaidia. Mungu akamsaidia Januari 2018 akapata ajira ya Uengineer mkoa mwingine. Turifurahi sababu tulimuomba sana Mungu.

Baada ya mwaka akanitolea mahari nikahamia anapoishi. Duka nikaweka mtu akaniiibia nikabaki ikabidi nilifunge. Jamaa akanifungulia duka lingine huku tulipohamia. Jamaa mshahara ukawa mzuri hakosi milioni 4 kwa mwezi pamoja na overtime, marupurupu kibao.

Akabadilika akawa hanishirikishi tena, hatupangi pamoja kama zamani tukipata kidogo tunapanga pamoja.

Changamoto ikawa uzazi ukagoma tangu 2018 mwenzangu ana hamu sana ya mtoto. Last year nikapata ujauzito Juni 26 ukatoka. Nimehangaika hospitali, dawa za kienyeji, tiba lishe, bila mafanikio.

Jamaa kaanzisha mahusiano na mfanya kazi wake mpaka kumleta ndani. Nikimuuliza anadai anatafuta mtoto.

Duka nililofungua jamaa hela zote anachukua.
Mtoto wangu shule mwaka huu kasimama. Nikimpigia mama anadai vumilia sasa utaenda wapi ushapoteza kila kitu?

Inafikia hatua unaona dunia imekutenga, huna thamani tena hasa inapofikia usiku jamaa analala nje ukimpigia anadai anatafuta mtoto.

Nilikata tamaa nikaamua nimpe sumu mtoto wangu na mimi ninywe ili haya maumivu yapotee. Juzi nimechukua mtoto tukaja guest house ili tufe wote. Kila nikitaka nimpe anywe anakuja na story nzuri tunacheka naogopa jamani.

Nisamehe Mungu wangu natubu mimi mbele zako. Eee Mungu baada ya kusoma kifo cha mpauko nisamehe mimi. Acha nipambane tu bado Mungu una makusudi na maisha yangu. Sasa hivi saa 11 sijafumba macho hata tone moja.

Jamani tupeane tu moyo haya maisha hatujui tunapitia yapi. Wewe unaweza kuwa na furaha usifikiri ni wote. Mtu akiomba ushauri humu tufarijiane tu wengine JF inatupa faraja sana.

Mbarikiwe
Pole sana Hamida, mpaka umefikia hatua ya kwenda guest na mwanao ili umuue nawe ujiue na ikashindikana basi jua ya kwamba ulilotaka kulifanya ni chukizo kubwa mbele za Mungu maana bado ana mpango na maisha yako hapa duniani.
Changamoto zipo na zipo kwaajili yetu na ni sisi wa kuzitatua. Usife moyo hayo ni mapito tu, ipo siku Mungu atasikia kilio chako na kukufungulia tumbo lako na furaha itarudi palepale kama mwanzoni
 
Huyo mtoto yupo darasa la ngapi? Nipe jina la shule number ya simu ya mwalimu mkuu na kiasi cha ada nitamlipia aende shule. Pls usituulie future generation.

Sent using Jamii Forums mobile app
Daah wewe ndio wa kwanza kutoa comment yenye mchango wa fedha. Lakini nasisitiza uwe na nia ya kweli usije ukawa unamchezea kama Yule jamaa aliyechezea mpauko. Mungu akuzidishie .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba pitia kwenye kwenye uzi zote zinazohusu shida ambayo naona ya kweli humu JF nnimetoa mchango wa pesa. Nikisema kutoa namananisha chief.
Daah wewe ndio wa kwanza kutoa comment yenye mchango wa fedha. Lakini nasisitiza uwe na nia ya kweli usije ukawa unamchezea kama Yule jamaa aliyechezea mpauko. Mungu akuzidishie .

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mpauko ndio nani ? Maana siku hizi siingii huku jf kivile. Yani hapa kama bahati tu kuingia naona uzi wa huyu dada.
Daah wewe ndio wa kwanza kutoa comment yenye mchango wa fedha. Lakini nasisitiza uwe na nia ya kweli usije ukawa unamchezea kama Yule jamaa aliyechezea mpauko. Mungu akuzidishie .

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni sehemu ya maisha tu,kuna watu wana maisha magumu na wanateseka kuliko wewe,mshukuru MUNGU KWA KILA JAMBO,kuna watu wakikusimulia matatizo yao,matatizo yako utayaona kama CHIPSI MAYAI,ili mradi unapumua songa mbele maana asilimia 80 ya maisha ni mahangaiko na asilimia 20 ni chembechembe za raha.......Pambana
 
Sasa new hamida ukishakunywa sumu na kujiuwa sisi rafiki zako utatuachaje Kwa mfano? Usijifikirie wewe tu, fikiria na sisi tutavyoteseka kukuwaza na kulilia, na mama yako je utamuachaje? Amka mamii nenda kapambane.
 
Binafsi kifo cha Mpauko kimenipa funzo sana. Nimepitia nyuzi zote na comment Mungu naomba tu unisamehe kwa mawazo niliyokua nayo.

Binafsi nilizaa 2014 mume akafariki ghafla kwa ajali nikabaki na mtoto. Nilihangaika sana sababu sikuwa na pakushika.

Mama yangu alikuwa Mtendaji alistaafu 2015, bahati nzuri akanipa mtaji milioni 1.5 nikafungua duka la dawa. Mungu akanisaidia nikawa naenda vizuri na maisha, 2016 nikapata mchumba aliyekuwa tempo TANESCO. Mshahara ulikuwa haukidhi na maisha ya kwao yalikuwa duni sana hivyo yeye ndio alikuwa tegemezi.

Kidogo mimi biashara haikunitupa hivyo akikwama nilikuwa namsaidia. Mungu akamsaidia Januari 2018 akapata ajira ya Uengineer mkoa mwingine. Turifurahi sababu tulimuomba sana Mungu.

Baada ya mwaka akanitolea mahari nikahamia anapoishi. Duka nikaweka mtu akaniiibia nikabaki ikabidi nilifunge. Jamaa akanifungulia duka lingine huku tulipohamia. Jamaa mshahara ukawa mzuri hakosi milioni 4 kwa mwezi pamoja na overtime, marupurupu kibao.

Akabadilika akawa hanishirikishi tena, hatupangi pamoja kama zamani tukipata kidogo tunapanga pamoja.

Changamoto ikawa uzazi ukagoma tangu 2018 mwenzangu ana hamu sana ya mtoto. Last year nikapata ujauzito Juni 26 ukatoka. Nimehangaika hospitali, dawa za kienyeji, tiba lishe, bila mafanikio.

Jamaa kaanzisha mahusiano na mfanya kazi wake mpaka kumleta ndani. Nikimuuliza anadai anatafuta mtoto.

Duka nililofungua jamaa hela zote anachukua.
Mtoto wangu shule mwaka huu kasimama. Nikimpigia mama anadai vumilia sasa utaenda wapi ushapoteza kila kitu?

Inafikia hatua unaona dunia imekutenga, huna thamani tena hasa inapofikia usiku jamaa analala nje ukimpigia anadai anatafuta mtoto.

Nilikata tamaa nikaamua nimpe sumu mtoto wangu na mimi ninywe ili haya maumivu yapotee. Juzi nimechukua mtoto tukaja guest house ili tufe wote. Kila nikitaka nimpe anywe anakuja na story nzuri tunacheka naogopa jamani.

Nisamehe Mungu wangu natubu mimi mbele zako. Eee Mungu baada ya kusoma kifo cha mpauko nisamehe mimi. Acha nipambane tu bado Mungu una makusudi na maisha yangu. Sasa hivi saa 11 sijafumba macho hata tone moja.

Jamani tupeane tu moyo haya maisha hatujui tunapitia yapi. Wewe unaweza kuwa na furaha usifikiri ni wote. Mtu akiomba ushauri humu tufarijiane tu wengine JF inatupa faraja sana.

Mbarikiwe
Dooh pole sana ndg kikubwa ni utimamu wa afya haya mengine yapo na huja kwa wakati wa Mungu

$ There's clear light at the end of the Tannel $
 
Back
Top Bottom