Mungu nisamehe kwa nilichotaka kufanya

Mungu nisamehe kwa nilichotaka kufanya

dada ONDOKA!
kama kufa ukafie mbele na mwanao!
Huyo hapati mtoto leo wala mtondogoo!
Hivyo hayo mateso na kukufanya ujiskie mnyonge hakutaisha leo wala keshokutwa!
Ndipo anapopata urijali akikutesa!
Hataacha mpk ahakikishe amekufikisha anapopataka!
Ndo mana anaamua kukunyan'ganya pesa zote anajua ukiwa nazo hatafanikiwa kukunynyasa hivo!
Ndo mana anakujibu wazi silali nyumbani, naleta mwanamke hapa ili NATAFUTA MTOTO!
anajua ndilo ENEO UNALOTAKA MUUNGANISHE FAMILIA, yani anahakikisha ujifeel responsible yeye kutokuwa na mtoto!
Shogare , utasanda!
ONDOKA!
akiona huondoki ataanza KUKUPIGA NA KUKUJERUHI!, kama bado hajaanza ntashangaa sana!
RUN FOR YOUR LIFE!
 
pole sana mamii, wanaume ndo walivyo ila mtangulize Mungu katika kila jambo najua unapitia wakati mgumu hata mimi mchumba alinipa stress kisa kutaka mtoto hapo anasema ukipata mimba tunafunga harusi, hospital wanasema hatuna tatizo jamani niliumia sana lakini nilijipa faraja watoto wanatoka kwa Mungu, Niliamua kuondoka na kuanza maisha upya Mungu akanifuta machozi akanipa mume tunaishi kwa upendo na ametubariki mtoto, Yule kijana bado hajaoa na hajapata mtoto ,,Hamida inawezekana huyo kaka siyo mume wako kubali kuanza upya wewe na mtoto wako na Mungu atakupigania kama analeta wanawake hadi ndani na kuna ukimwi mamii jipende wewe na mwanao.🥰🥰🥰🥰🥰
 
Kila nafisi ni huru, kwanini uruhusu nafisi ya mtu ikuendeshe maishani,yule ana maisha yake na ww una part yako,weka malengo yako ,usiyumbishwa na mtu unaekutana nae njiani katika safari ya maisha yako ,move on
Nikesikitika sana uliootaka kumpa sumu mwanao,jamani kila mtu anahaki ya kuishi haijalishi umemleta ww duniani
Njoo inbox nibadilishane mawazo ya kisaikolojia dada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana dada yangu kwa hio hali unayo pitia
Kwa sisi tunaosoma hapa tunaweza kuona ni kawaida, lakini ukweli changamoto yako ni kubwa sana.lakini bado haijawa kubwa kuliko uwezo wako ndio maana mpaka muda huu upo na uzima wewe na mwanao.
Kwa hio maadamu leo upo na kesho utakuwepo pia.
Ukumbuke pia furaha ama huzuni ya leo ilitengejezwa jana hivyo kadhalika furaha na huzuni ya kesho inatengenezwa leo.
Kwa hio leo upo usiangalie machungu ya leo yaliotengenezwa jana bali angalia furaha ya kesho inayotengenezwa leo.
Pole sana lakini pia hongera sana kwani hii changamoto unayopitia ni njia moja wapo ya kuinuka kwa kiasi ambacho haukuwahi kutarajia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati tunazani tunapitia magumu katika maisha na kukata tamaa.lakini tungekuwa na uwezo wa kuona wanayopitia watu wengine yetu sio kitu....Nimejifunza hakuna kukata tamaa kwa hili life haijalishi unapitia kitu gani wakati uliopo kwani kwenye kila jambo kuna njia ya kushinda na jambo zuri na la faraja lipo hapo mbeleni...Tupeane moyo na tuzidi kuhope kwa mazuri yajayo wakuu.
 
Pole sana mkuu, huyo mtoto wako ndiye Malaika wako mlinzi, anakuepusha na roho za kishetani, endelea kumuombea maana kupitia yeye utaona na kupata nguvu mpya na sababu ya kuendelea kuishi itatamalaki. Mwenyezi Mungu hajawahi kumuacha aliyetubu kwa dhati.
 
Binafsi kifo cha Mpauko kimenipa funzo sana. Nimepitia nyuzi zote na comment Mungu naomba tu unisamehe kwa mawazo niliyokua nayo.

Binafsi nilizaa 2014 mume akafariki ghafla kwa ajali nikabaki na mtoto. Nilihangaika sana sababu sikuwa na pakushika.

Mama yangu alikuwa Mtendaji alistaafu 2015, bahati nzuri akanipa mtaji milioni 1.5 nikafungua duka la dawa. Mungu akanisaidia nikawa naenda vizuri na maisha, 2016 nikapata mchumba aliyekuwa tempo TANESCO. Mshahara ulikuwa haukidhi na maisha ya kwao yalikuwa duni sana hivyo yeye ndio alikuwa tegemezi.

Kidogo mimi biashara haikunitupa hivyo akikwama nilikuwa namsaidia. Mungu akamsaidia Januari 2018 akapata ajira ya Uengineer mkoa mwingine. Turifurahi sababu tulimuomba sana Mungu.

Baada ya mwaka akanitolea mahari nikahamia anapoishi. Duka nikaweka mtu akaniiibia nikabaki ikabidi nilifunge. Jamaa akanifungulia duka lingine huku tulipohamia. Jamaa mshahara ukawa mzuri hakosi milioni 4 kwa mwezi pamoja na overtime, marupurupu kibao.

Akabadilika akawa hanishirikishi tena, hatupangi pamoja kama zamani tukipata kidogo tunapanga pamoja.

Changamoto ikawa uzazi ukagoma tangu 2018 mwenzangu ana hamu sana ya mtoto. Last year nikapata ujauzito Juni 26 ukatoka. Nimehangaika hospitali, dawa za kienyeji, tiba lishe, bila mafanikio.

Jamaa kaanzisha mahusiano na mfanya kazi wake mpaka kumleta ndani. Nikimuuliza anadai anatafuta mtoto.

Duka nililofungua jamaa hela zote anachukua.
Mtoto wangu shule mwaka huu kasimama. Nikimpigia mama anadai vumilia sasa utaenda wapi ushapoteza kila kitu?

Inafikia hatua unaona dunia imekutenga, huna thamani tena hasa inapofikia usiku jamaa analala nje ukimpigia anadai anatafuta mtoto.

Nilikata tamaa nikaamua nimpe sumu mtoto wangu na mimi ninywe ili haya maumivu yapotee. Juzi nimechukua mtoto tukaja guest house ili tufe wote. Kila nikitaka nimpe anywe anakuja na story nzuri tunacheka naogopa jamani.

Nisamehe Mungu wangu natubu mimi mbele zako. Eee Mungu baada ya kusoma kifo cha mpauko nisamehe mimi. Acha nipambane tu bado Mungu una makusudi na maisha yangu. Sasa hivi saa 11 sijafumba macho hata tone moja.

Jamani tupeane tu moyo haya maisha hatujui tunapitia yapi. Wewe unaweza kuwa na furaha usifikiri ni wote. Mtu akiomba ushauri humu tufarijiane tu wengine JF inatupa faraja sana.

Mbarikiwe
Pole sana dear kwa mapito unayopitia, naamini ipo njia ya kutokea kwa kila pito. Mungu akasikie kilio chako na akupatie watoto wa kike na wakiume.
 
Pole sana new hamida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku kuu ya mwaka mpya , mama mjamzito kanywa sumu na kumnywesha mwanae wa miaka Minne , , , Bahati nzuri wasamaria wakawaona maana Walinywea barabarani ... Mama kapona na mtoto pia , , , Juzi kajifungua Twins , , , Mmoja kafa ... Chanzo cha kunywa sumu ni mwanaume( mateso kutoka kwa mume) Chonde chonde wanaume tuwe na huruma na hawa viumbe wana akili ndogo na Hisia zao mnazijua ....
Tujitahidi kuepuka ukatili kwa hawa viumbe...nfo mama zetu , walezi wetu na kwa watoto wetu pia

Nawapenda wanawake wote
 
Huyu ni kind ya wanaume ambao ni controller. Hataki.kuwa responsible na muda wote ana laumu mtu mwingine kwa makosa yake mwenyewe.

Sasa huyu mwanaume anaweza kumdhuru asipokuwa makini. So.long as mwanaume amezini na kamkuta live inatosha kumpa sababu ya yeye kuondoka akalee mwanae mbele ya safari. Anaumizwa kisaikolojia atafanikiwa kumuonyesha kuwa yeye hana thaman ni mjinga hana.analoweza kufanya kosha huyu binti atajichukia. Aondoke ila kwa hesabu kali kusudi asiweze kumdhuru.
dada ONDOKA!
kama kufa ukafie mbele na mwanao!
Huyo hapati mtoto leo wala mtondogoo!
Hivyo hayo mateso na kukufanya ujiskie mnyonge hakutaisha leo wala keshokutwa!
Ndipo anapopata urijali akikutesa!
Hataacha mpk ahakikishe amekufikisha anapopataka!
Ndo mana anaamua kukunyan'ganya pesa zote anajua ukiwa nazo hatafanikiwa kukunynyasa hivo!
Ndo mana anakujibu wazi silali nyumbani, naleta mwanamke hapa ili NATAFUTA MTOTO!
anajua ndilo ENEO UNALOTAKA MUUNGANISHE FAMILIA, yani anahakikisha ujifeel responsible yeye kutokuwa na mtoto!
Shogare , utasanda!
ONDOKA!
akiona huondoki ataanza KUKUPIGA NA KUKUJERUHI!, kama bado hajaanza ntashangaa sana!
RUN FOR YOUR LIFE!
ambao.
 
Back
Top Bottom