Mungu nisamehe kwa nilichotaka kufanya

Mungu nisamehe kwa nilichotaka kufanya

Moja ya matatizo makubwa kwa sisi binadamu ni kulikuza tatzo kwa akili zako na kujifikiria wewe pekee. Hakuna tatzo lisilokua na njia ya kulitatua. Wadada kila mara nasema na leo narudia mwanaume hatulii mpaka atulizwe,ukiona yte hayo ujue umeshindwa kumtuliza mwanaume.
Kuna muda ambao ktk maisha unakubali kurud nyuma na kuanza upya..mwanaume akikuletea vitimbi usijibishane nae,mpe tabasam,mpe upendo,mpe mapenz akihitaj,mpe bashasha,akija na demu kaza roho hata kama inakuuma,muulize niwapishe mlale au mtalala chumba cha wagen? Muulize niwaandalie chakula gani kitakachowapendeza kabla hajamlala?
Najua inauma sana lakin amin nakuambia hakuna silaha kubwa kwa mwanaume akikuudhi kama kumpa tabasam anaekuudhi.

Mwisho ww ndo utakua mshindi.,usikumbuke vituko vyake,vihifadh moyon,lazima atageuka na kurud kwako maana anajua mlipotoka. Nafs itamsuta na atajiona mjinga,mwsho mshindi utabaki wewe. Heb chukulia mwanamke anavyoumia akiandaa chakula halaf mumeo anagoma kula?? Pole sana najua unaumia sana lakin nakuhakikishia mshindi mpk sasa ni wewe ila hujajua tu silaha moja ya kua chini kwa muda huu. Tchao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo wanawake huwa hamjui kwamba Mwanaume huwa hasahau manyanyaso na maneneo ya kashfa na kejeli ulizokuwa unatoa wakati hana kitu.
Ulivyokuwa unamsimanga Wewe mwanaume gani, Mimi nakulisha.Sioni faida ya kuolewa huku ukimfananisha na ex wako

Sent using Jamii Forums mobile app
haya umeyasema wewe mkuu
 
Binafsi kifo cha Mpauko kimenipa funzo sana. Nimepitia nyuzi zote na comment Mungu naomba tu unisamehe kwa mawazo niliyokua nayo.

Binafsi nilizaa 2014 mume akafariki ghafla kwa ajali nikabaki na mtoto. Nilihangaika sana sababu sikuwa na pakushika.

Mama yangu alikuwa Mtendaji alistaafu 2015, bahati nzuri akanipa mtaji milioni 1.5 nikafungua duka la dawa. Mungu akanisaidia nikawa naenda vizuri na maisha, 2016 nikapata mchumba aliyekuwa tempo TANESCO. Mshahara ulikuwa haukidhi na maisha ya kwao yalikuwa duni sana hivyo yeye ndio alikuwa tegemezi.

Kidogo mimi biashara haikunitupa hivyo akikwama nilikuwa namsaidia. Mungu akamsaidia Januari 2018 akapata ajira ya Uengineer mkoa mwingine. Turifurahi sababu tulimuomba sana Mungu.

Baada ya mwaka akanitolea mahari nikahamia anapoishi. Duka nikaweka mtu akaniiibia nikabaki ikabidi nilifunge. Jamaa akanifungulia duka lingine huku tulipohamia. Jamaa mshahara ukawa mzuri hakosi milioni 4 kwa mwezi pamoja na overtime, marupurupu kibao.

Akabadilika akawa hanishirikishi tena, hatupangi pamoja kama zamani tukipata kidogo tunapanga pamoja.

Changamoto ikawa uzazi ukagoma tangu 2018 mwenzangu ana hamu sana ya mtoto. Last year nikapata ujauzito Juni 26 ukatoka. Nimehangaika hospitali, dawa za kienyeji, tiba lishe, bila mafanikio.

Jamaa kaanzisha mahusiano na mfanya kazi wake mpaka kumleta ndani. Nikimuuliza anadai anatafuta mtoto.

Duka nililofungua jamaa hela zote anachukua.
Mtoto wangu shule mwaka huu kasimama. Nikimpigia mama anadai vumilia sasa utaenda wapi ushapoteza kila kitu?

Inafikia hatua unaona dunia imekutenga, huna thamani tena hasa inapofikia usiku jamaa analala nje ukimpigia anadai anatafuta mtoto.

Nilikata tamaa nikaamua nimpe sumu mtoto wangu na mimi ninywe ili haya maumivu yapotee. Juzi nimechukua mtoto tukaja guest house ili tufe wote. Kila nikitaka nimpe anywe anakuja na story nzuri tunacheka naogopa jamani.

Nisamehe Mungu wangu natubu mimi mbele zako. Eee Mungu baada ya kusoma kifo cha mpauko nisamehe mimi. Acha nipambane tu bado Mungu una makusudi na maisha yangu. Sasa hivi saa 11 sijafumba macho hata tone moja.

Jamani tupeane tu moyo haya maisha hatujui tunapitia yapi. Wewe unaweza kuwa na furaha usifikiri ni wote. Mtu akiomba ushauri humu tufarijiane tu wengine JF inatupa faraja sana.

Mbarikiwe
Usichukie mabaya yajapo maisha mwako bali mshukuru Mungu kwa maana anajua kwa nini yamekuja kwako na jinsi gani yataondoka.Mungu hajafunga mahesabu nawe mjue sana Mungu ili uwe na amani kwani anajua mwisho tangu mwanzo.
 
Yeye ana uhakika gani na uwezo wake wa uzazi?
Yalimkuta mpwa (binti). Aliolewa na kijana mzuri na siha njema. Wote tulimpokea kama mkwe na kushirikiana naye katika masuala ya kijamii.
Katika kuendelea na maisha yao, mume alianza kubadilika tabia. Ukali na matusi kwa mkewe ulizidi. Kipigo kikawa sehemu ya maisha ya binti yetu. Lakini hakuwahi kusema kwetu kama wazazi badala yake taarifa tulizipata kwa majirani zao.
Binti akiulizwa alikataa hakuna tatizo, alisema maisha yao ni ya kawaida. Hatukuwa na namna ya kuingilia. Sababu ya mateso hayo ilikuwa ni kutozaa mtoto.
Baadaye binti aliamua kutoroka kwa mume na kuelekea kusikojulikana. Familia pande zote tulikaa kutafuta namna ya kumpata lakini haikuwezekana.
Mungu yu mwema. Siku ya siku alirejea mwenyewe akiwa mjamzito kama miezi 6 hivi. Tulimpokea na kufanya mawasiliano na upande wa pili. Uamuzi ukawa watengane na mahari irejeshwe.
Yule kijana hadi leo amekwishaoa na kuacha mara tatu na kati ya hao wanawake hakuna aliyepata ujauzito.
Huenda na mumeo anashida ila hajijui.
Mungu akuongezee ujasiri na ni mwiko kukata tamaa maishani.
 
Moja ya matatizo makubwa kwa sisi binadamu ni kulikuza tatzo kwa akili zako na kujifikiria wewe pekee. Hakuna tatzo lisilokua na njia ya kulitatua. Wadada kila mara nasema na leo narudia mwanaume hatulii mpaka atulizwe,ukiona yte hayo ujue umeshindwa kumtuliza mwanaume.
Kuna muda ambao ktk maisha unakubali kurud nyuma na kuanza upya..mwanaume akikuletea vitimbi usijibishane nae,mpe tabasam,mpe upendo,mpe mapenz akihitaj,mpe bashasha,akija na demu kaza roho hata kama inakuuma,muulize niwapishe mlale au mtalala chumba cha wagen? Muulize niwaandalie chakula gani kitakachowapendeza kabla hajamlala?
Najua inauma sana lakin amin nakuambia hakuna silaha kubwa kwa mwanaume akikuudhi kama kumpa tabasam anaekuudhi.

Mwisho ww ndo utakua mshindi.,usikumbuke vituko vyake,vihifadh moyon,lazima atageuka na kurud kwako maana anajua mlipotoka. Nafs itamsuta na atajiona mjinga,mwsho mshindi utabaki wewe. Heb chukulia mwanamke anavyoumia akiandaa chakula halaf mumeo anagoma kula?? Pole sana najua unaumia sana lakin nakuhakikishia mshindi mpk sasa ni wewe ila hujajua tu silaha moja ya kua chini kwa muda huu. Tchao

Sent using Jamii Forums mobile app
Sorry umewah kuwa mwanamke ama ww ni mwanamke?
Umajua kuwa binadamu tumetofautiana degree of tolerance? Ndio utampisha chumba utampikia utamfulia kwasabb inreturns unataka nini? Upendo? Usiokuwepo? Unataka nini kubaki kwenye ndoa isiyo kuwa na heshima?
Biblia.inasema hivi ndoa na iheshimiwe.na watu wote na malazi yawe safi. Hapo kuna heshima kwenye hiyo ndoa?
Tena ikasema ndoa haiwez kuvunjika isipokuwa kwa habari.ya uzinzi. Sasa huyu umemkuta live analeta nyumban bado unaona usamehe na kutoa tabasamu la kinafiki? Uendelee kumkosea Mungu?

Heb ifike.mahali wanaume na wanawak3 waheshimu hii taasis ya ndoa. Na ukiona huwez ondoka usije kufa kwa kubywa sumu.wala.presha
 
Huyo mtoto yupo darasa la ngapi? Nipe jina la shule number ya simu ya mwalimu mkuu na kiasi cha ada nitamlipia aende shule. Pls usituulie future generation.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu kama nyinyi ndo 2nawahitaji jf.
Hongera kwa moyo wa kipekee.
Naamini hamida ataiona faraja sasa.ubarikiwe sana
 
Moja ya matatizo makubwa kwa sisi binadamu ni kulikuza tatzo kwa akili zako na kujifikiria wewe pekee. Hakuna tatzo lisilokua na njia ya kulitatua. Wadada kila mara nasema na leo narudia mwanaume hatulii mpaka atulizwe,ukiona yte hayo ujue umeshindwa kumtuliza mwanaume.
Kuna muda ambao ktk maisha unakubali kurud nyuma na kuanza upya..mwanaume akikuletea vitimbi usijibishane nae,mpe tabasam,mpe upendo,mpe mapenz akihitaj,mpe bashasha,akija na demu kaza roho hata kama inakuuma,muulize niwapishe mlale au mtalala chumba cha wagen? Muulize niwaandalie chakula gani kitakachowapendeza kabla hajamlala?
Najua inauma sana lakin amin nakuambia hakuna silaha kubwa kwa mwanaume akikuudhi kama kumpa tabasam anaekuudhi.

Mwisho ww ndo utakua mshindi.,usikumbuke vituko vyake,vihifadh moyon,lazima atageuka na kurud kwako maana anajua mlipotoka. Nafs itamsuta na atajiona mjinga,mwsho mshindi utabaki wewe. Heb chukulia mwanamke anavyoumia akiandaa chakula halaf mumeo anagoma kula?? Pole sana najua unaumia sana lakin nakuhakikishia mshindi mpk sasa ni wewe ila hujajua tu silaha moja ya kua chini kwa muda huu. Tchao

Sent using Jamii Forums mobile app
Abeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
new Hamida, pole sana my dear kwa hilo jaribu. achana na mawazo ya kujiua mrudie Mungu sali sana kwa imani yako. maana shetani asije kukujaribu baadae ukaingiwa na hayo mawazo. na unaweza jikuta umepoteza mtoto wewe umebaki, utakuwa na majuto mabaya sana maishani mwako. kaa na marafiki pmj na ndugu acha kuwaza negative na kumfikiria uyo mwanaume. simama jikung'ute mavumbi inuka tena. sbb una akili ya biashara muombe mama angalau akuwezeshe kidogo kamtaji uanze upya hata maandazi hata genge biashara ndogondogo itakayokukeep buzy na kukuingizia kipato angalau. na pia ikiwezekana rudi nyumbani kwa wazazi waambie tu huwezi tena kuishi na yule mwanaume naamini wazazi watakupokea tu. pole sana Hamida, wanasema nyakati za furaha hazidumu na za huzuni pia hazidumu. maisha haya ni siri sana yaani usione watu wanatembea, acha kabisa mawazo ya kujiua. kuna anayepata hili akakosa kile, usijiue my dear kwa ajili ya mwanaume chonde. hivi unajua ukifa unaenda wapi? unahisi unaenda kupunguza matatizo? what if km ndo unaenda kukutana na matatizo zaidi? huna uhakika na unapoenda my dear acha kabisa. MUNGU AKUPE NGUVU ZA KUSIMAMA NA KUSHINDA. NAKUOMBEA
 
Mpauko ni kijana alikua memba hapa jamvini. Bahati mbaua amejiiua kwasababu ya kukosa fedha na msaada wa kimaisha. Aikue na partial hearing imparement. Apiwah kuomba msaada hapa.jamvini lkn baadhi ya watu walimdhihaki . Sasa amejinyonga kabisa manake kaona maisha ni machungu sana. Mungu atusamehe kwa kukosa utu
Haya jamani naona kimya, ngoja nikafanye kazi za watu. Badae

Sent using Jamii Forums mobile app
nijaana
 
Chimbuko Letu Ni Baba Na Mama Mmoja Tupendane Tuoneane Huruma

Tupeane Hope Haya Maisha Yanasiri Nzito Sana Usione Mtu Anaposti Nyuzi Flan Ukahisi Ndio Maisha Yake Sometimes

Anajaribu Kujiliwaza Angalau Kufikiria Positive kama Wengine
Tusaidiane Nakuombeana Sana sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamida naomba nikutie moyo.nilishakuwa kwenye mahusiano na mwanaume kwa mda mrefu mno. Miaka 4+ ila sikubahatika kupata hata mimba ya bahati mbaya na yule mwanaume ,
Mwanaume akaanza ujeuri .ikumbukwe kwamba ni girlfriend tu sio mke hata pete alikuwa hajanivisha,
Akaanza vituko...oooo mara ukitaka nikakutambulishe kwetu ujilipie nauli...ohoo mara mbona hunizalii mtoto uzae kwanza ndo nikuoee..
Na nlikuwa nampenda kufa,kumwacha siwezi,nalia tu.mimba sipati.
Baadae nikachoka😭😭 nikasema hata kama nampenda vipi ntamove on...

Kweli nilifanikiwa kuachana nae.baada ya kuachana nae nikawa na mahusiano mengine baada ya miezi minne nikapata ujauzito.na ndoa nikapata,na mtoto wa kiume nikapata..
Nikasema
HUENDA MUNGU ALIKUWA HATAKI NIZAE NA YULE MWANAUME KWA SABABU ZAKE YEYE.NIKAMSHUKURU

..yeye yupo hana hata mtoto wa kusingiziwa.
So mungu anakuepusha kuzaa na huyo mwanaume wako.huenda mungu anakuepusha na jambo baya.
Relax dear...
Mpende mwanao pambana kwa ajili yake fanya chochote ilimradi mwanao ale.na usiogope watu watakuonaje.kwani unafnya kwa ajlili ya malaika wako mpendwa...
Msalimie mtoto..
❤
 
Nakumbuka uzi wako uliopokuwa unahama na duka lilivyofirisiwa, nikushauri kitu kaa na huyu mume kwa akili calculate miezi yote uliyofungua hilo duka ambalo anachukua hela yote, jilipe mshahara tafuta laini za uwakala fungua hapo pembeni weka mfanyakazi ili utunze mwanao
 
Nmeskitika eti mtu anataka kujinyonga kwa sabb ya mwanaume..hivi wanawake mnajua kua ninyi ni wasaidiz wa wanaume tu na sio wategemez? Kama hili mnalijua hamna sababu ya kukata tamaa.
Kuna wanawake wamekua wajasili sana kpambana na Familia..
Kijijn kwetu mwaka 1983..kulikua na Mzee mmoja alikua na watoto 10..yy alikua mtu wa Pombe sana..nakumbuka alikua na ng'ombe kama 4 hivi...yule Mzee sikuwahi kumwona anahangaika na watoto..ispokua mkewe..mama alipika komoni watoto wavae na waende shule. Nakumbuka Mzee yule siku moja alifika home kwake alikuta ng'ombe hawajapelekw malishoni alipga mkewe na watoto 2 mmoja alikua agemate wangu..
Kaka wa mama yule walikuja kumchukua lakn alikataaa akasema siwez kuondoka nikawaacha watoto hapa..alipambana sana..mpaka mda huu naandika hapa..watoto wale wamekua na uchumi mkubwa sana..wamemjengea mama yao nyumba nzr sana..naweza Sema pale kjjn mama yule ndy mwenye uchumi...
Nataka niseme mwanamke hodar ni yule a napambana na watoto wake mpaka mwisho Bila kujali hali aliyonayo!! Watoto ni zawad yenu Mungu amewapa wanaume wasiwafanye muvunjike moyo!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi kifo cha Mpauko kimenipa funzo sana. Nimepitia nyuzi zote na comment Mungu naomba tu unisamehe kwa mawazo niliyokua nayo.

Binafsi nilizaa 2014 mume akafariki ghafla kwa ajali nikabaki na mtoto. Nilihangaika sana sababu sikuwa na pakushika.

Mama yangu alikuwa Mtendaji alistaafu 2015, bahati nzuri akanipa mtaji milioni 1.5 nikafungua duka la dawa. Mungu akanisaidia nikawa naenda vizuri na maisha, 2016 nikapata mchumba aliyekuwa tempo TANESCO. Mshahara ulikuwa haukidhi na maisha ya kwao yalikuwa duni sana hivyo yeye ndio alikuwa tegemezi.

Kidogo mimi biashara haikunitupa hivyo akikwama nilikuwa namsaidia. Mungu akamsaidia Januari 2018 akapata ajira ya Uengineer mkoa mwingine. Turifurahi sababu tulimuomba sana Mungu.

Baada ya mwaka akanitolea mahari nikahamia anapoishi. Duka nikaweka mtu akaniiibia nikabaki ikabidi nilifunge. Jamaa akanifungulia duka lingine huku tulipohamia. Jamaa mshahara ukawa mzuri hakosi milioni 4 kwa mwezi pamoja na overtime, marupurupu kibao.

Akabadilika akawa hanishirikishi tena, hatupangi pamoja kama zamani tukipata kidogo tunapanga pamoja.

Changamoto ikawa uzazi ukagoma tangu 2018 mwenzangu ana hamu sana ya mtoto. Last year nikapata ujauzito Juni 26 ukatoka. Nimehangaika hospitali, dawa za kienyeji, tiba lishe, bila mafanikio.

Jamaa kaanzisha mahusiano na mfanya kazi wake mpaka kumleta ndani. Nikimuuliza anadai anatafuta mtoto.

Duka nililofungua jamaa hela zote anachukua.
Mtoto wangu shule mwaka huu kasimama. Nikimpigia mama anadai vumilia sasa utaenda wapi ushapoteza kila kitu?

Inafikia hatua unaona dunia imekutenga, huna thamani tena hasa inapofikia usiku jamaa analala nje ukimpigia anadai anatafuta mtoto.

Nilikata tamaa nikaamua nimpe sumu mtoto wangu na mimi ninywe ili haya maumivu yapotee. Juzi nimechukua mtoto tukaja guest house ili tufe wote. Kila nikitaka nimpe anywe anakuja na story nzuri tunacheka naogopa jamani.

Nisamehe Mungu wangu natubu mimi mbele zako. Eee Mungu baada ya kusoma kifo cha mpauko nisamehe mimi. Acha nipambane tu bado Mungu una makusudi na maisha yangu. Sasa hivi saa 11 sijafumba macho hata tone moja.

Jamani tupeane tu moyo haya maisha hatujui tunapitia yapi. Wewe unaweza kuwa na furaha usifikiri ni wote. Mtu akiomba ushauri humu tufarijiane tu wengine JF inatupa faraja sana.

Mbarikiwe
Pole sana.. kama uliamini Mungu kipindi mmeo hana kazi ukaomba kwa bidii na akapata kazi, basi imani hiyo hiyo ikuwezeshe kuomba tena ili Mungu yule yule uliyemuamini kipindi kile akutoe kwenye hilo janga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole Sana kwa hayo unayopitia. Nshawahi kutana na dada mmoja alinisimulia mengi yafananayo na yako. Mme wake alikuja kuondoka nyumbani na kumuacha akiwa na mtoto mwingine tumboni, mama yake aliyekuwa akimtegemea naye akafariki. Alifikia hatua ya kunywa sumu ila ikashindikana. Saizi maisha yake yameendelea focus yake kubwa ni maisha yake na wanae na ana furaha sana sasa.
 
Huyo mme wako alipata kazi engineer kampuni gani? Kama ni tanesco ni uongo mkuu na hii inasababisha maelezo yote uliyotoa kupoteza uhalali.
 
Back
Top Bottom