Mungu nisamehe kwa nilichotaka kufanya

Mungu nisamehe kwa nilichotaka kufanya

Huyo mme wako alipata kazi engineer kampuni gani? Kama ni tanesco ni uongo mkuu na hii inasababisha maelezo yote uliyotoa kupoteza uhalali.
Uongo kwanini?
Nakuhusia usiingie kwenye mtego wa YEHODAYA ukahukumu mtu mwisho yakakutokea puani.
 
Hamida naomba nikutie moyo.nilishakuwa kwenye mahusiano na mwanaume kwa mda mrefu mno. Miaka 4+ ila sikubahatika kupata hata mimba ya bahati mbaya na yule mwanaume ,
Mwanaume akaanza ujeuri .ikumbukwe kwamba ni girlfriend tu sio mke hata pete alikuwa hajanivisha,
Akaanza vituko...oooo mara ukitaka nikakutambulishe kwetu ujilipie nauli...ohoo mara mbona hunizalii mtoto uzae kwanza ndo nikuoee..
Na nlikuwa nampenda kufa,kumwacha siwezi,nalia tu.mimba sipati.
Baadae nikachoka[emoji24][emoji24] nikasema hata kama nampenda vipi ntamove on...

Kweli nilifanikiwa kuachana nae.baada ya kuachana nae nikawa na mahusiano mengine baada ya miezi minne nikapata ujauzito.na ndoa nikapata,na mtoto wa kiume nikapata..
Nikasema
HUENDA MUNGU ALIKUWA HATAKI NIZAE NA YULE MWANAUME KWA SABABU ZAKE YEYE.NIKAMSHUKURU

..yeye yupo hana hata mtoto wa kusingiziwa.
So mungu anakuepusha kuzaa na huyo mwanaume wako.huenda mungu anakuepusha na jambo baya.
Relax dear...
Mpende mwanao pambana kwa ajili yake fanya chochote ilimradi mwanao ale.na usiogope watu watakuonaje.kwani unafnya kwa ajlili ya malaika wako mpendwa...
Msalimie mtoto..
[emoji173]
@melanny nje ya mada hivi una undugu na sanchi?[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dunia mapito new hamida

jipe moyo,vuka mabonde,panda milima..tembea tambarare yote ni mapito

Pambana, just kipuuzee hicho kijamaa; usijidhuru

Kwani ameondoka na roho yako.?

*na nextime ikatokea tena pepo la kutaka kuji suicides missions...(tambua mtoto hahusiki) usim kill,utahesabika muuaji; jidedishe mwenyewe

mtoto atalelewa na Jamhuri.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni tanesco nimeshasema ni uongo hakuna kitu kama hicho cha mshahara
Nimejumuisha mshahara, overtime pamoja na safari
Safar kila akitoka analipwa laki 1 kwa siku na hajawahi kumaliza mwezi kazini akikaa Sana wiki 1... Sasa hv navyoongea yupo mwanza
Kama unabisha uliza
Wiki 2 au 3 zilizopita alikua dodoma kwenye kikao na wazili pia uliza ....Safar tu kwa mwez sio chini ya mil 1,. Over time Kuna muda inafika kiwango Cha mshahara nahapo m4 nikiwango Cha chini
 
Nimejumuisha mshahara, overtime pamoja na safari
Safar kila akitoka analipwa laki 1 kwa siku na hajawahi kumaliza mwezi kazini akikaa Sana wiki 1... Sasa hv navyoongea yupo mwanza
Kama unabisha uliza
Wiki 2 au 3 zilizopita alikua dodoma kwenye kikao na wazili pia uliza ....Safar tu kwa mwez sio chini ya mil 1,. Over time Kuna muda inafika kiwango Cha mshahara nahapo m4 nikiwango Cha chini
Hahahaa, yaani wewe ni muongo au mumeo anakudanganya sana. Mwambie akwambie ukweli.
 
Pole sana dada
Lakini usidhulumu maisha ya mwanao
Bado naye hajajaribu bahati yake...
 
Binafsi kifo cha Mpauko kimenipa funzo sana. Nimepitia nyuzi zote na comment Mungu naomba tu unisamehe kwa mawazo niliyokua nayo.

Binafsi nilizaa 2014 mume akafariki ghafla kwa ajali nikabaki na mtoto. Nilihangaika sana sababu sikuwa na pakushika.

Mama yangu alikuwa Mtendaji alistaafu 2015, bahati nzuri akanipa mtaji milioni 1.5 nikafungua duka la dawa. Mungu akanisaidia nikawa naenda vizuri na maisha, 2016 nikapata mchumba aliyekuwa tempo TANESCO. Mshahara ulikuwa haukidhi na maisha ya kwao yalikuwa duni sana hivyo yeye ndio alikuwa tegemezi.

Kidogo mimi biashara haikunitupa hivyo akikwama nilikuwa namsaidia. Mungu akamsaidia Januari 2018 akapata ajira ya Uengineer mkoa mwingine. Turifurahi sababu tulimuomba sana Mungu.

Baada ya mwaka akanitolea mahari nikahamia anapoishi. Duka nikaweka mtu akaniiibia nikabaki ikabidi nilifunge. Jamaa akanifungulia duka lingine huku tulipohamia. Jamaa mshahara ukawa mzuri hakosi milioni 4 kwa mwezi pamoja na overtime, marupurupu kibao.

Akabadilika akawa hanishirikishi tena, hatupangi pamoja kama zamani tukipata kidogo tunapanga pamoja.

Changamoto ikawa uzazi ukagoma tangu 2018 mwenzangu ana hamu sana ya mtoto. Last year nikapata ujauzito Juni 26 ukatoka. Nimehangaika hospitali, dawa za kienyeji, tiba lishe, bila mafanikio.

Jamaa kaanzisha mahusiano na mfanya kazi wake mpaka kumleta ndani. Nikimuuliza anadai anatafuta mtoto.

Duka nililofungua jamaa hela zote anachukua.
Mtoto wangu shule mwaka huu kasimama. Nikimpigia mama anadai vumilia sasa utaenda wapi ushapoteza kila kitu?

Inafikia hatua unaona dunia imekutenga, huna thamani tena hasa inapofikia usiku jamaa analala nje ukimpigia anadai anatafuta mtoto.

Nilikata tamaa nikaamua nimpe sumu mtoto wangu na mimi ninywe ili haya maumivu yapotee. Juzi nimechukua mtoto tukaja guest house ili tufe wote. Kila nikitaka nimpe anywe anakuja na story nzuri tunacheka naogopa jamani.

Nisamehe Mungu wangu natubu mimi mbele zako. Eee Mungu baada ya kusoma kifo cha mpauko nisamehe mimi. Acha nipambane tu bado Mungu una makusudi na maisha yangu. Sasa hivi saa 11 sijafumba macho hata tone moja.

Jamani tupeane tu moyo haya maisha hatujui tunapitia yapi. Wewe unaweza kuwa na furaha usifikiri ni wote. Mtu akiomba ushauri humu tufarijiane tu wengine JF inatupa faraja sana.

Mbarikiwe
Pole sana Dada..kila kitu kitapita
 
Ngoja nikushauri kilevi

1 Tafuta mchepuko smart ukuliwaze

2 Anzisha maisha yako ondoka kwa huyo fala mshamba

Nasema hiviiiii maamuzi magumu huokoa jahazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole sana best jaribu kuhudhuria sehemu za ibada upate ushauri na maombi pia vilevile jua kuwa Mungu ana kusudi nawe hivyo usikate tamaa na haya maisha ambayo ni ya muda na wala usijikatishe ukajiua Mungu anaweza sana mshirikishe na mtwike fadhaa zaoko naye atakutokea ondoa hiyo dhana ya kutaka kujiua ukiona hali hiyo inakujia hebu toka nje na anza kutembea uku ukiomba Mungu atakutokea
 
Pole sana dear,wakati wa Mungu ndio wakati sahihi,usikate tamaa wakati wako wakufurahi upo karibu,usiwaze kujiua tena.
 
Back
Top Bottom