Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 55,024
- 59,684
Pole sana dada. Na bora hujamuua huyo Malaika atakuja kuwa mtu mkubwa sana na atakusaidia huko mbeleni. Wewe pambana tu
Asante nduguKwanza kabisa, sifa na utukufu zimwendee Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema. Kwa maana amesema na wewe rohoni na kukufanya upate tumaini jipya katika maisha, hakika ilikuwa ni ushindi mkubwa huko mbinguni kwani shetani aligaragazwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Maisha yana changamoto nyingi na mara nyingi sisi wanadamu tunapopatwa na changamoto nzito tunahisi hakuna maisha tena wala hakuna faida ya kuishi. Kukata tamaa ni janja ya shetani ambayo haipaswi kupewa nafasi hata kidogo katika maisha yetu.
Mfano rahisi ni huu, ni lini jua lilizama na likaacha kuchomoza siku iliyofuata? jibu ni hakuna. Basi hivyo ndivyo tunapaswa kuwa na tumaini kwamba kwa namna yoyote kila gumu lina mwisho wake na ukimtumaini Mungu lazima tu utashinda.
Duuh...! Pole sana sana.Binafsi kifo cha Mpauko kimenipa funzo sana. Nimepitia nyuzi zote na comment Mungu naomba tu unisamehe kwa mawazo niliyokua nayo.
Binafsi nilizaa 2014 mume akafariki ghafla kwa ajali nikabaki na mtoto. Nilihangaika sana sababu sikuwa na pakushika.
Mama yangu alikuwa Mtendaji alistaafu 2015, bahati nzuri akanipa mtaji milioni 1.5 nikafungua duka la dawa. Mungu akanisaidia nikawa naenda vizuri na maisha, 2016 nikapata mchumba aliyekuwa tempo TANESCO. Mshahara ulikuwa haukidhi na maisha ya kwao yalikuwa duni sana hivyo yeye ndio alikuwa tegemezi.
Kidogo mimi biashara haikunitupa hivyo akikwama nilikuwa namsaidia. Mungu akamsaidia Januari 2018 akapata ajira ya Uengineer mkoa mwingine. Turifurahi sababu tulimuomba sana Mungu.
Baada ya mwaka akanitolea mahari nikahamia anapoishi. Duka nikaweka mtu akaniiibia nikabaki ikabidi nilifunge. Jamaa akanifungulia duka lingine huku tulipohamia. Jamaa mshahara ukawa mzuri hakosi milioni 4 kwa mwezi pamoja na overtime, marupurupu kibao.
Akabadilika akawa hanishirikishi tena, hatupangi pamoja kama zamani tukipata kidogo tunapanga pamoja.
Changamoto ikawa uzazi ukagoma tangu 2018 mwenzangu ana hamu sana ya mtoto. Last year nikapata ujauzito Juni 26 ukatoka. Nimehangaika hospitali, dawa za kienyeji, tiba lishe, bila mafanikio.
Jamaa kaanzisha mahusiano na mfanya kazi wake mpaka kumleta ndani. Nikimuuliza anadai anatafuta mtoto.
Duka nililofungua jamaa hela zote anachukua.
Mtoto wangu shule mwaka huu kasimama. Nikimpigia mama anadai vumilia sasa utaenda wapi ushapoteza kila kitu?
Inafikia hatua unaona dunia imekutenga, huna thamani tena hasa inapofikia usiku jamaa analala nje ukimpigia anadai anatafuta mtoto.
Nilikata tamaa nikaamua nimpe sumu mtoto wangu na mimi ninywe ili haya maumivu yapotee. Juzi nimechukua mtoto tukaja guest house ili tufe wote. Kila nikitaka nimpe anywe anakuja na story nzuri tunacheka naogopa jamani.
Nisamehe Mungu wangu natubu mimi mbele zako. Eee Mungu baada ya kusoma kifo cha mpauko nisamehe mimi. Acha nipambane tu bado Mungu una makusudi na maisha yangu. Sasa hivi saa 11 sijafumba macho hata tone moja.
Jamani tupeane tu moyo haya maisha hatujui tunapitia yapi. Wewe unaweza kuwa na furaha usifikiri ni wote. Mtu akiomba ushauri humu tufarijiane tu wengine JF inatupa faraja sana.
Mbarikiwe
Mwana umevuta fegi za wapi...mwenzio anamatatizo wewe unawaza vitu vya ajabu
M/mungu aendelee kukubarikiNaomba pitia kwenye kwenye uzi zote zinazohusu shida ambayo naona ya kweli humu JF nnimetoa mchango wa pesa. Nikisema kutoa namananisha chief.
Sent using Jamii Forums mobile app
Acha tu unaweza kuta mtu anachangia humu kwa bashasha lakini nyuma huku moto unawaka tunavumilia tu!maisha ya wanadam yamejawa mapito magum sana, unaweza hisi pekee unapitia magum bt hapana wapo wengi wanapitia magum zaidi yako hivo tuweni wavumilivu sana