Mungu nisamehe kwa nilichotaka kufanya

Mungu nisamehe kwa nilichotaka kufanya

Pole sana mama mungu ni mwema atakutoa katika hiyo dhiki be strong hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho
 
Pole sana mpendwa...Mungu wetu wa mbinguni akuinue na kukutendea makuu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sasa kama anakomba hela hapo dukani na wewe ndio muuzaji kwanini usiwe unatenga zakuweka akiba yako mapema?

Alafu unawaza kujiua na mtoto! Hivi unadhani mtoto na yeye anawaza kama wewe au unataka kumuonea tu!?

Anatafuta mtoto mshauri aowe mke mwengine kama muislam,hata kama itakuuma ila baadae utapata utulivu kuliko hicho anachokifanya unalitafuta janga la kiafya kwake na kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaaah mpk nmepata
Binafsi kifo cha Mpauko kimenipa funzo sana. Nimepitia nyuzi zote na comment Mungu naomba tu unisamehe kwa mawazo niliyokua nayo.

Binafsi nilizaa 2014 mume akafariki ghafla kwa ajali nikabaki na mtoto. Nilihangaika sana sababu sikuwa na pakushika.

Mama yangu alikuwa Mtendaji alistaafu 2015, bahati nzuri akanipa mtaji milioni 1.5 nikafungua duka la dawa. Mungu akanisaidia nikawa naenda vizuri na maisha, 2016 nikapata mchumba aliyekuwa tempo TANESCO. Mshahara ulikuwa haukidhi na maisha ya kwao yalikuwa duni sana hivyo yeye ndio alikuwa tegemezi.

Kidogo mimi biashara haikunitupa hivyo akikwama nilikuwa namsaidia. Mungu akamsaidia Januari 2018 akapata ajira ya Uengineer mkoa mwingine. Turifurahi sababu tulimuomba sana Mungu.

Baada ya mwaka akanitolea mahari nikahamia anapoishi. Duka nikaweka mtu akaniiibia nikabaki ikabidi nilifunge. Jamaa akanifungulia duka lingine huku tulipohamia. Jamaa mshahara ukawa mzuri hakosi milioni 4 kwa mwezi pamoja na overtime, marupurupu kibao.

Akabadilika akawa hanishirikishi tena, hatupangi pamoja kama zamani tukipata kidogo tunapanga pamoja.

Changamoto ikawa uzazi ukagoma tangu 2018 mwenzangu ana hamu sana ya mtoto. Last year nikapata ujauzito Juni 26 ukatoka. Nimehangaika hospitali, dawa za kienyeji, tiba lishe, bila mafanikio.

Jamaa kaanzisha mahusiano na mfanya kazi wake mpaka kumleta ndani. Nikimuuliza anadai anatafuta mtoto.

Duka nililofungua jamaa hela zote anachukua.
Mtoto wangu shule mwaka huu kasimama. Nikimpigia mama anadai vumilia sasa utaenda wapi ushapoteza kila kitu?

Inafikia hatua unaona dunia imekutenga, huna thamani tena hasa inapofikia usiku jamaa analala nje ukimpigia anadai anatafuta mtoto.

Nilikata tamaa nikaamua nimpe sumu mtoto wangu na mimi ninywe ili haya maumivu yapotee. Juzi nimechukua mtoto tukaja guest house ili tufe wote. Kila nikitaka nimpe anywe anakuja na story nzuri tunacheka naogopa jamani.

Nisamehe Mungu wangu natubu mimi mbele zako. Eee Mungu baada ya kusoma kifo cha mpauko nisamehe mimi. Acha nipambane tu bado Mungu una makusudi na maisha yangu. Sasa hivi saa 11 sijafumba macho hata tone moja.

Jamani tupeane tu moyo haya maisha hatujui tunapitia yapi. Wewe unaweza kuwa na furaha usifikiri ni wote. Mtu akiomba ushauri humu tufarijiane tu wengine JF inatupa faraja sana.

Mbarikiwe
Goosebumps[emoji80]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ebu ngoja kwanza niku kumbushe kwamba.... Hakuna linalompa haki yeyote anayejiua na kujiua ni sawa na kuua na hivyo ndivyo ilivyo kujiua mwenyewe. Mungu ndiye pekee huamua na kupanga lini/vipi na wapi mwanadamu atapatwa na umauti. Hivyo basi, mtu anapo chukua jukumu hilo mkononi mwako nisa naku kufuru kwa Mungu.
 
Kwanza hongera kwa kumshinda shetani. Nimewahi kupita huko ulipo, kwa mambo ya kijinga kabisa nilitaka kujitoa uhai 2015. Nilikunywa vidonge vingi sana lakini nikapona.

Nikiangalia sasa hivi, lile jambo ambalo nililiona kubwa wala haliathiri maisha yangu kwa namna yoyote ile. So hakuna kubwa linalostahili kujitolea uhai tena na mtoto ndo usimguse kabisa, ana future yake very bright.

Nimesikitika sana kuwa mwanao amesimama shule. Tafadhali fanya ufanyalo mtoto asome. Kama manyanyaso, mateso unayapata tayari, chukua pesa dukani dogo asome. Kikiwaka sawa, ila mtoto asome.

Halafu huyo mume anatafuta mtoto tangu lini? Mbona hapati? Napata hisia yeye ndo mwenye tatizo. Wewe unahangaika nini peke yako na una mtoto? Muende wote huko kwenye tiba!
 
Fanya hivi, usimuulize tena kitu chochote kuhusu mchepuko wake... Relax wewe baki na Mungu tu akikupiga akikutukana usimjibu maana atapata sababu ya kukufukuza.. Amka usiku sali kimyakimya fanya mambo yako huku kila mara kuwa na Mungu! Atajirudi sio muda
 
Pole Dada.
Amini Mungu bado ana Ahadi yako katikati ya mateso,Amepanga kukuondoa hapo matesoni.

Psalms 50:15
Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.

Zaburi 34:19
Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini BWANA humponya nayo yote.
 
Pole mamy, maisha haya jaman nyie acheni tu watu humu tunapitia magumu sema tunajikaza tu na kujipa moyo.

Binafsi namshuhudia Mungu sana.
Usikate tamaa mamy, muamini Mungu sana
 
Back
Top Bottom