Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

Wakija kusema hao ni alliance waliunda vyote hivyo ( annunaki ) basi waambie kama ni wao sisi tumeamua kuwaita Mungu kwa sababu wametuumba , hatuna uwezo juu yao na ndo Mungu ni taofauti ya majina tu.
Inamaana hata wewe hujui unacho kiabudu na huna uhakika nacho
 
MUNGU ni suala la kiimani na huwezi thibitisha suala la kiimani nje ya imani. Tunaamini MUNGU yupo sababu hakuna mbadala wa concept isiyo na shaka ya uwepo wa ulimwengu. Hii imani ni zao la kutokewepo kwa facts zisizo na shaka za sababu za uwepo wetu na vyote tuvionavyo. Ukisema tuachane na imani ya uwepo wa MUNGU njoo na hitimisho la yote tuliyoyakuta duniani.

Siku tukipata jibu kuwa ss ni nn na ulimwengu ni nn basi hiyo imani itafutika. Kwa sasa yoyote apingaye uwepo wa MUNGU bila ushahidi timilifu wa kutokuwepo kwake ni mfuasi wa adui wa MUNGU aitwaye shetani, ibilisi. Hii kutaka kubatilisha uwepo wa MUNGU kwa njia ya kushindwa kuthibitisha uwepo wake nje ya imani haipo sawa sababu imani ya uwepo wake ni matokeo ya uwepo wetu pasipo kuwa na ushahidi usio na shaka wa sababu za uwepo. Hii sababu ya uwepo wetu tusiyoweza kuithibitisha ndiyo iliyozaa imani ya uwepo wa MUNGU.
Kwaiyo ibilisi na Mungu Ni washindani?
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Sawa mkuu nimekuelewa.

Hivyo kwa mujibu wako ni kwamba;
Hakuna Mungu, na ulimwengu huu pamoja na vyote vilivyomo, tuvijuavyo na tusivyovijua- haijulikani vimekuaje vile vilivyo. Utafiti zaidi unahitajika.
Nimekupata vizuri sana.




Lakini Mkuu kama hujui vitu hivyo vilikujaje lakini waumini dini wanadai wanajua na wanaeleza kila leo juu ya uwepo wake na kueleza kwanini vipo mahali hapa vilipo, na nani alivileta.

Swali ni kuwa kwanini kwako inakuwa ngumu kukubali madai yao ilhali wewe mwenyewe hauna majibu?
Aisee we jamaa unachekesha kwaiyo unataka aamini hekaya zisizo na ushahidi
 
Nimejaribu kupitia comments za watu katika hii thread, Nilichogundua Ni kwamba Kama ambavyo binadamu tulivyo tofauti kimuonekano basi pia tupo tofauti sana kifikra.
Nirudi kwenye mada kwanza kuthibitisha kuwa Kuna mungu au hayupo ni lazima tukubaliane juu ya maana ya Mungu, Kisha ndio tuthibitishe uwepo wake au kutokuwepo.
Pili tuelewe ni ngumu kutenganisha dhana ya uwepo wa mungu na dini yaani uyahudi,uislamu na ukristo.
Nianze na maana ya mungu(N.b kwa jinsi ninavyofahamu Mimi)
Mungu kutoka katika Mwenyezimungu yaani mwenye- enzi -mungu.
Mwenye-mmiliki wa
Enzi- ya kale au mwanzo
Mungu- muweza wa kila Jambo/ anayepaswa kuabudiwa
Hivyo unaposema Mwenyezimungu maana yake -wa mwanzo mwenye kupaswa kuabudiwa au wa mwanzo muweza wa kila Jambo.
Sasa turudi juu ya uwepo wake na kutokuwepo.
Hapa tuelewe kuwa wengi wanao support uwepo wa mungu ni watu wenye dini yaani waislamu,wakristo na wayahudi ndio maana mwanzo nikasema ni ngumu kutenganisha mungu na dini.
Kwa uzoefu wangu wengi wanaopinga uwepo wa mungu (Atheists) wanatumia hoja za kiakili na logic pamoja na ushahidi wa kisayansi kuthibitisha kuwa hakuna mungu na hapo ndipo tatizo limapoanzia, kivipi? ..kuwa makini point inayofuata.
Unapotaka kuthibitisha kuwa hakuna mungu kwa kutumia let say milango ya fahamu yaani macho, pua, masikio n.k hii tunasema ni sayansi kwa maana nyingine ni vipimo vya kupimia vitu vyenye asili ya maada (matters) na mungu sio maada Hivyo kutaka kumpima mungu kupitia vipimo vya kupimia maada ni kosa kwa maana wale Wanaosema mungu hayupo kwa sababu haonekani , hashikiki huwezi kumnusa hoja yao inakosa nguvu automatic kwani wametumia vipimo ambavyo sio sahihi kumpimia mungu yaani ni sawasawa na uchukue mizani ya kupimia uzito alafu unataka kujua kimo cha ndoo hutapata kimo utapata uzito lakini haimanishi hiyo ndoo haina kimo inayo na ukitaka Kupata kimo chake tumia tape measure na sio mizani.
Hoja Ni nyingi Sana ambazo Atheists wanazitumia na Mimi apo nimetoa hoja moja tu na nimeikosoa hoja hio ..mwenye hoja nyingine aweke hapo alafu tuchambue kila hoja
N.b msimamo wangu mungu yupo na linathibitika kiakili, kisayansi na kiimani..​
Umejuaje Kama Mungu sio maada? Ulitumia kipimo gani kuthibitisha uwepo wa Mungu
 
Ukitaka kuthibitisha uwepo wa MUNGU KWA kutumia milango ya fahamu basi haitakupa majibu kwa Sababu yenye ya udhaifu mkubwa
 
Nakusikitikia sana
Sijakuuliza kama unanisikitikia au hunisikitikii.

Nimekuuliza hivi.

"Unahakikishaje hilo ulilosema ni kweli na si hadithi tu unazojiaminisha bila kuwa kweli?".

Hujajibu uliloulizwa.

Ulilojibu hujaulizwa.
 
Sijakuuliza kama unanisikitikia au hunisikitikii.

Nimekuuliza hivi.

"Unahakikishaje hilo ulilosema ni kweli na si hadithi tu unazojiaminisha bila kuwa kweli?".

Hujajibu uliloulizwa.

Ulilojibu hujaulizwa.
Nathibitisha kulingana na jinsi nilivyoumbwa? Kwa njia ya ajabu sana, kiwanda gani duniani kinatengeneza damu? Huoni huo ni mfumo wa ajabu?
 
Nathibitisha kulingana na jinsi nilivyoumbwa? Kwa njia ya ajabu sana, kiwanda gani duniani kinatengeneza damu? Huoni huo ni mfumo wa ajabu?
Logical non sequitur plus argument from ignorance.

Dunia kutokuwa na kiwanda cha kutengeneza damu, ikiwa hilo ni kweli, ni uthibitisho kwamba hakuna kiwanda cha damu duniani.

Hilo halithibitishi Mungu yupo.

Unaunganisha mambo mawili ambayo hayana muungano.

Inawezekana dunia ikawa haina kiwanda cha damu na Mungu akawa hayupo, hakuna contradiction hapo.

Ni sawa na mimi nikuambie nyumba yako haina jokofu, hivyo weee lazima ni shabiki wa Arsenal!

Yani mambo hayana uhusiano wowote, unayaunganusha kwa nguvu tu.
 
Hakuna jina alaf hicho kitu kisiwepo. Sema Mungu sio huyo Mkuu basi Mungu ni nini?
 
Inawezekana dunia ikawa haina kiwanda cha damu na Mungu akawa hayupo, hakuna contradiction hapo
Nani anatengeneza damu? Huoni kama muumba ana sifa za kipekee? Na hakuna anaeweza kuwa sawa na yeye?
 
Nani anatengeneza damu? Huoni kama muumba ana sifa za kipekee? Na hakuna anaeweza kuwa sawa na yeye?
Unafahamu damu ni nini?

Kwa nini swali la kutengeneza damu liwe swali la "nani"?

Unaelewa "anthropic bias" ni nini?

Unaweza kuthibitisha muumba yupo?

Unaweza kuthibitisha Mungu anatengeneza damu?
 
wakija kudhibitisha ni kutaka kujengea watu imani flani tu bila udhibitisho unaoingia akilin , hyo imani ya kuamn Mungu hayupo haina tofauti na iman ya din flan tu, waulize ni nguvu gani ilipangilia mifumo mbalimbali kiustadi bila kuathiri viumbe hai , wanasema wanaamni sayansi waulize sayansi inaweza simama bila kutegemea rawmaterial iliyokuwepo tu bila ufundi kutoka kwa binadamu? waulize ni nguvu gani na intelligence ipi inayofanya kazi ndani sperm kuunda kiumbe kilicho na mifumo na mipangilio maalumu ? ni kitu gan kiliweka sukari ndan ya muwa na kwa dhumuni lipi je ilitokea tu bila nguvu na inteligence yoyote?
Swali kabambe hili.Atheists njooni mlijibu
 
Back
Top Bottom