Hujanielewa vizuri.
Labbda niandike kwa point form.
1. Mazungumzo mengi ya hapa ni very basic na hayagusi aspects nyingi za falsafa ya kuwepo, kutokuwepo Mungu.
2. Kwa kuanzia (msisitizo ni kwa kuanzia) mazungumzo mengi yanatokana na Mungu aliyeandikwa misahafuni, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kama alivyoandikwa kwenye Torati, Biblia, Quran na vitabu vingine.
3.Umenisoma vibaya kwamba napinga Mungu huyu na nataka Mungu fulani, mimi sitaki Mungu yeyote, mimi nataka logical consistency, si kwenye hoja ya Mungu tu, kwenye hoja yoyote. Maana yake ni kwamba, mtu akija na kuniambia Mungu yupo ila ni mshenzi anapenda kutesa watu, hoja yake kuhusu kuwapo Mungu huyo itakuwa na mashiko na logical consistency kubwa kwa kuangalia dunia hii ilivyo, kuliko Mungu aliyeandikwa kwenye misahafu hiyo niliyoitaja hapo juu. Bado nitakuwa na maswali mengi sana kuhusu huyo Mungu, pamoja na imekuwaje Mungu akawa mshenzi na mtesi wa viumbe wake, lakini hiyo dhana itakuwa na logical consistency kubwa zaidi ya hii ya Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, halafu anaumba ulimwengu ambao unawezekana kuwa na mabaya mengi.
4. Kuhusu dhana ya chanzo cha yote, hiyo dhana yenyewe tu inatokana na umasikini wa mawazo unaotupata sisi kama watu. Kimsingi unaongelea causality.Dhana ya kwamba kuna chanzo, kinaleta matokeo. Matokeo hayawezi kuja bila chanzo kuanza. Dhana hii ni potofu, tumeona katika quantum physics kwamba inawezekana kukawa na mzunguko wa chanzo na matokeo kwa namna ambayo hatuwezi kusema chanzo kimeleta matokeo au matokeo yameleta chanzo. Kwa hivyo, kwa mujibu wa Quantum Physics, causality is not fundamentally linear. Tunahitaji kujifunza kuelewa zaidi, si kurukia kutaja Mungu. Kwa sababu hata ukiambiwa kwamba kuna chanzo, na chanzo ni quantum probability, utasema quantum probability ndiyo Mungu? What if there is something weirder than quantum probability that we still don't know and that has no resemblance to any of our current notions of God?
Untangling how the human perception of cause-and-effect might arise from quantum physics may help us understand the limits and potential of AI.
plus.maths.org