Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

uliyeyushwa ni mwili wala sio roho pia acid imepatikana tu kwenye mazingira
Nitajie kitu kimoja ambacho hakipatikani kwenye mazingira halafu kinahusiana na mwili wa Mwanadamu?

Mazingira ni nini?

Je? Mwanadamu sio sehemu ya hayo mazingira?

Hakuna kitu kinachoitwa roho ni dhahania tu kama zilivyo dhahania nyingine
 
Unazunguka palepale.

Hili dai la "alivyoumba" unathibitishaje kuwa ni la kweli?

Unathibitisha vipi hivyo vitu unavyoviita vya asili vimeumbwa na Mungu kweli na kwamba dhana hiyo si hadithi tu uliyorithishwa na watu na wewe ukaikubali bila uthibitisho?
Kwa akili yako vitu vyote vimetokeza vyenyewe?
 
Sijawahi kujadiliana na watu watupu kama nyinyi. Badala ya kujibu hona unakimbia kwa kuandika tuhuma. Hii mbini mtaiacha lini ?

Mimi nakupa kazi Moja tu leta hizo fact unazo dai alizitowa Galileo Kisha ujibu maswali nitakayo kuulizia kutokana na hizo unazo dai kuwa ni facts.

Akili ya kawaida tu inakataa ya kuzunguka kwa Dunia.

Kisha uniwekee hapa jaribio la Kisayansi la kweli linakothibitisha ya kuwa Dunia inazunguka.

Unatakiwa ujibu maswali niliyo uliza.
Akili ya kawaida inakubali kwamba mtume alienda mbingu ya saba kwa kutumia farasi anayepaa?
 
Kwa akili yako vitu vyote vimetokeza vyenyewe?
Kwa nini unafikiri jibu ni lazima liwe ama vitu vimeumbwa na Mungu, au vimetokea vyenyewe?

Umejiridhisha vipi kwamba majibu yapo humo tu?

Unaujua vipi mchakato wa cause and effect kwa anthropic bias inayokupa vantage point ambayo haikuoneshi vitu vya msingi?

Unajua kwamba dhana nzima ya "hiki kinaleta kile" ina makosa sana?

Vitu vyote ni vipi?

Unaelewa kwamba, kama "vitu vyote" vimetokea vyenyewe, au kama havijatokea vyenyewe, majibu yote yaanaonesha Mungu hahitajiki?

Kujibu swali lako.

Kama vimetokea vyenyewe, Mungu muumba vyote hahitajiki.

Kama havijatokea vyenyewe, na kila kilichopo kinahitaji muumba, hata Mungu mwenyewe naye atahitaji muumba na hivyo Mungu muumba vyote atakuwa hayupo.

Unaelewa kwamba jibu lolote nitakalokupa kwenye swali hilo halitatuonesha kwamba Mungu yupo au hata anahitajika kuwepo?

Unaelewa majibu yote hayo yanaonesha Mungu huyo hayupo?
 
Nitajie kitu kimoja ambacho hakipatikani kwenye mazingira halafu kinahusiana na mwili wa Mwanadamu?

Mazingira ni nini?

Je? Mwanadamu sio sehemu ya hayo mazingira?

Hakuna kitu kinachoitwa roho ni dhahania tu kama zilivyo dhahania nyingine

Ndugu waweza kunifafanulia nini maana ya Mwili wa Mwanaadamu Kama ulivyo sema? Nikiwa na maana ya Mwili wa Mwanaadamu ni nini maana yake na Mwanaadamu ni nini maana yake?
Umesema Mwili wa, ina maana Mwili si Mwanaadamu. Kwa maana hiyo Mwili ni Mwili na Mwanaadamu ni Mwanaadamu NIFAFANULIE MAANA YAKE
 
Haya mabaya na uovu duniani nani anasababisha yatokee? Na wewe unaposema Mungu yupo umejuaje kama yupo kweli? thibitisha! Huyo Mungu unamjua au ni akili yako tu inahisi hivyo? Akili yako wewe inahisi tu kwamba kuna Mungu ila huna uthibitisho kama unao ulete.Usiseme eti kwa vile hujui nani aliumba dunia,Jua, nyota,mwezi,bahari,maziwa,mito,milima ndio udhani Mungu yupo? Una uhakika na uthibitisho wa yeye aliumba hivi vitu au unahisi tu? Kama una hisi tu hivyo..Basi na Atheist tuna hisi Mungu hayupo... maana wote mimi na wewe tunahisi tu! Ila hatuna uthibitisho......kama unao uthibitisho wa kuwepo Mungu ulete,, Usiseme unahisi tu au ni imani tu leta uthibitisho...
Ndugu kwani Atheist ina sema vipi uwepo wa Dunia hii na vyote vilivyopo juu yake?
 
hapo tuko pamoja hilo jina ni wajanja flani tu walikaa wakatunga ,ila halina uhalisa wowote na wangeweza kuita jina lolote ambalo wangeamua,na pia hilo jina Mungu nadhani linatumia afrika mashariki tu ila kila jamii ina jina lake kwalo.ingawa kutungwa jina hilo la uongo haiondoi ukweli kwamba kuna nguvu ipo ambayo ndio chanzo cha haya magimba yote ya asili tunayoayaona na nadhani kuna mengine hatuyaoni,hatujui jina la hiyo nguvu lakini haiondoi ukweli kwamba ipo
Ndugu je waweza kunambia hiyo nguvu sababu yake ni nini? Yaani hiyo nguvu iliyo na inayo endelea kusababisha mpaka wasema magimba mengine hayaonekani je Nguvu hiyo sababu yake ni nini? Kipi kina sababisha nguvu hiyo iwepo mpaka utambuzi ukakuijia yakua ni nguvu tu pekee. Tufafanulie ndugu
 
Ndugu kwani Atheist ina sema vipi uwepo wa Dunia hii na vyote vilivyopo juu yake?
Dunia na vyote vilivyomo ndani yake vimesababishwa na nguvu fulani.... lakini hiyo nguvu haijulikani wala haithibitishiki kwa kielelezo chochote kile ni wajanja tu walikaa waka amua kuita hiyo nguvu kwa jina "Mungu"....Mungu ni jina sio nguvu..na hii nguvu ime pachikwa majina mbalimbali kadiri ya imani za watu
 
Mungu yupo kwa sababu ya existance ya solar system and universe ,pili existance ya life(Living organism).
 
"Existance" ndiyo nini?

EXISTANCE.jpg

EXISTENCE.jpg
 
Dunia na vyote vilivyomo ndani yake vimesababishwa na nguvu fulani.... lakini hiyo nguvu haijulikani wala haithibitishiki kwa kielelezo chochote kile ni wajanja tu walikaa waka amua kuita hiyo nguvu kwa jina "Mungu"....Mungu ni jina sio nguvu..na hii nguvu ime pachikwa majina mbalimbali kadiri ya imani za watu
Mkuu Vipi hiyo nguvu iliyo sababisha Dunia na vyote vilivyomo ilitokea katika Mpangilio gani yani je ya muonekano? Je ya sauti? Je yakuto onekana na sauti yake? Je ya kuonekana pamoja na sauti yake? NIFAFA NULIE NIELEWE
 
Kwanini viumbe vimetokea Ke na Me? Hiyo Nguvu ndio iliyosababisha? How about Hamophrodite? Nguvu kwao kwanini haiku_apply?
 
Mungu anakuangalia tu akibinya pumzi dk 5 tu naamini kabisa utaamka unasema
Bwana Yesu asifiwe jioni hii ya leo
 
Mkuu Vipi hiyo nguvu iliyo sababisha Dunia na vyote vilivyomo ilitokea katika Mpangilio gani yani je ya muonekano? Je ya sauti? Je yakuto onekana na sauti yake? Je ya kuonekana pamoja na sauti yake? NIFAFA NULIE NIELEWE
Kwa ufafanuzi zaidi rejea comments za Kiranga katika huu Uzi ame elezea
 
Kwa nini unafikiri jibu ni lazima liwe ama vitu vimeumbwa na Mungu, au vimetokea vyenyewe?

Umejiridhisha vipi kwamba majibu yapo humo tu?

Unaujua vipi mchakato wa cause and effect kwa anthropic bias inayokupa vantage point ambayo haikuoneshi vitu vya msingi?

Unajua kwamba dhana nzima ya "hiki kinaleta kile" ina makosa sana?

Vitu vyote ni vipi?

Unaelewa kwamba, kama "vitu vyote" vimetokea vyenyewe, au kama havijatokea vyenyewe, majibu yote yaanaonesha Mungu hahitajiki?

Soma hapa

Kujibu swali lako.

Kama vimetokea vyenyewe, Mungu muumba vyote hahitajiki.

Kama havijatokea vyenyewe, na kila kilichopo kinahitaji muumba, hata Mungu mwenyewe naye atahitaji muumba na hivyo Mungu muumba vyote atakuwa hayupo.

Unaelewa kwamba jibu lolote nitakalokupa kwenye swali hilo halitatuonesha kwamba Mungu yupo au hata anahitajika kuwepo?

Unaelewa majibu yote hayo yanaonesha Mungu huyo hayupo?
Yeye ndiye mwanzo wa yote. Ndio maana ni wa pekee
 
ene
Ndugu je waweza kunambia hiyo nguvu sababu yake ni nini? Yaani hiyo nguvu iliyo na inayo endelea kusababisha mpaka wasema magimba mengine hayaonekani je Nguvu hiyo sababu yake ni nini? Kipi kina sababisha nguvu hiyo iwepo mpaka utambuzi ukakuijia yakua ni nguvu tu pekee. Tufafanulie ndugu
energy can not be created not destroyed but it can change from one state to another
 
Back
Top Bottom