JumaKilumbi
JF-Expert Member
- Sep 7, 2022
- 432
- 507
- Thread starter
- #161
Safi umenielewa vizuri sana.Nimejaribu kupitia comments za watu katika hii thread, Nilichogundua Ni kwamba Kama ambavyo binadamu tulivyo tofauti kimuonekano basi pia tupo tofauti sana kifikra.
Nirudi kwenye mada kwanza kuthibitisha kuwa Kuna mungu au hayupo ni lazima tukubaliane juu ya maana ya Mungu, Kisha ndio tuthibitishe uwepo wake au kutokuwepo.
Pili tuelewe ni ngumu kutenganisha dhana ya uwepo wa mungu na dini yaani uyahudi,uislamu na ukristo.
Nianze na maana ya mungu(N.b kwa jinsi ninavyofahamu Mimi)
Mungu kutoka katika Mwenyezimungu yaani mwenye- enzi -mungu.
Mwenye-mmiliki wa
Enzi- ya kale au mwanzo
Mungu- muweza wa kila Jambo/ anayepaswa kuabudiwa
Hivyo unaposema Mwenyezimungu maana yake -wa mwanzo mwenye kupaswa kuabudiwa au wa mwanzo muweza wa kila Jambo.
Sasa turudi juu ya uwepo wake na kutokuwepo.
Hapa tuelewe kuwa wengi wanao support uwepo wa mungu ni watu wenye dini yaani waislamu,wakristo na wayahudi ndio maana mwanzo nikasema ni ngumu kutenganisha mungu na dini.
Kwa uzoefu wangu wengi wanaopinga uwepo wa mungu (Atheists) wanatumia hoja za kiakili na logic pamoja na ushahidi wa kisayansi kuthibitisha kuwa hakuna mungu na hapo ndipo tatizo limapoanzia, kivipi? ..kuwa makini point inayofuata.
Unapotaka kuthibitisha kuwa hakuna mungu kwa kutumia let say milango ya fahamu yaani macho, pua, masikio n.k hii tunasema ni sayansi kwa maana nyingine ni vipimo vya kupimia vitu vyenye asili ya maada (matters) na mungu sio maada Hivyo kutaka kumpima mungu kupitia vipimo vya kupimia maada ni kosa kwa maana wale Wanaosema mungu hayupo kwa sababu haonekani , hashikiki huwezi kumnusa hoja yao inakosa nguvu automatic kwani wametumia vipimo ambavyo sio sahihi kumpimia mungu yaani ni sawasawa na uchukue mizani ya kupimia uzito alafu unataka kujua kimo cha ndoo hutapata kimo utapata uzito lakini haimanishi hiyo ndoo haina kimo inayo na ukitaka Kupata kimo chake tumia tape measure na sio mizani.
Hoja Ni nyingi Sana ambazo Atheists wanazitumia na Mimi apo nimetoa hoja moja tu na nimeikosoa hoja hio ..mwenye hoja nyingine aweke hapo alafu tuchambue kila hoja
N.b msimamo wangu mungu yupo na linathibitika kiakili, kisayansi na kiimani..
Natafuta Ajira angepita hapa aelewe naye.

