Pole sana dada yangu . Kwanza nikupongeze kwa kushikilia kiapo cha ndoa hapo umethibitisha upendo wako kwake si katika nyakati za vyuku na mazagazaga ya kila namna kwenye freji, yaan hata katika pito hilo bado unampenda na kuwajibika maana ndoa ni kusaidiana .
Pia kuhusu kutopata ajira tangu 2011 hiyo isikuvunje moyo kabisa hata mm binafsi bado sijapata ajira na nimemaliza chuo 2011 na nina professional kozi za IT zenyewe si hiz za vicollege vyetu ILA bado nina imani ipo siku mambo yatakuwa sawa tena mwezi huu huu.
NINI UFANYE KATIKA PITO HILO .
1. Kwanza Mtangulizeni sana Mungu katika mambo yenu na kuweni na imani kuwa ni Mungu tu awezae kuwatoa katika jaribu hilo.
2. usioneshe au kumuonesha kuwa unaumia na hiyo hali yake bali wewe fanyika faraja kwake kwani wewe ndio mtu wa karibu sana kwake baada ya MUNGU.
3. Kuhusu kilimo ninacho washauri jaribuni kufuata kanuni za kilimo kitaalam zaid hapa angalieni mbegu mnazotumia , mbolea, na aina ya udongo mlipandia hayo mazao.
4. Kubwa zaidi ongea na Mumeo kama anaweza kufundisha hata shule binafsi za sekondari basi afanye hivyo naamini atapata tu . ( LA KUZINGATIA ASIDEMAND MSHAHARA MKUBWA SANA ILA UWE MZURI KWA KUENDANA NA HALI HALISI.)
Na pia kama anaweza aombee kujitolea kufanya kazi kwenye ofisi hata hizi za serikali au watu binafsi. ( MWAMININI MUNGU ATAFUNGUA MILANGO NA KAZI ATAPATA MZURI NA YA MAANA.)
NB: USIKATE TAMAA NA MUMEO NI WAKO HUYU NA HILO NI PITO LA MUDA MDOGO SANAAAA KUMBUKA KILA SIKU MUNGU YUPO ONTIME.
MUNGU AWAONEKANIE NDANI YA MWEZI HUU MUMEO APATE KAZI NZURI SANA. KAMA UNAAMINI SEMA " AMENI "