Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Kwakuwa hamjazaa mtoto naye naona ni vema kumwachia mdogo wako mume naamini utapata mume wa kuendana na wewe utaishi bila amani katika hiyo ndoa sepa tu mwambie mungu yatosha akupe mume mwingine.
 
Leah simulizi yako ni nzuri sana na umeandika kwa ufasaha sana, mimi nakushauri chukua uamuzi wakuwasamehe wote wawili, mdogo wako na mme pia rejea usalama wa ndoa ni pande zote mbili kwenu wana ndoa na wazazi wa pande zote kwa kuwa wao waliridhia kusameheana chukua maneno hayo ya hekima kutoka kwa wazazi.

nafahamu watu waote tumeumbwa na hasira ukiambatana na wivu pia lakini Mungu ametupa nguvu ya kusahau kama binadamu, hivyo basi na wewe huna budi kurejerea huruma ya moyo ambayo itakufanya kuimarisha ndoa yako zaidi lakini pia wazazi watakulaumu wewe kwa uamuzi wako wa kuishi ndani ya ndoa bila kuzaa, wanaume na wazazi wanapenda sana kuona mtoto anapatikana baada ya ndoa.Fanya marekebisho ya ndoa kwa kuchukua uamuzi wa kubeba mimba ili mmeo aondoe fikra za kuzaa nje inawezekana kabisa mmeo hajakwambia ukweli wake moyoni lakini hili la mtoto lazima limekuwa limemsukuma kumpa mimba mdogo wako.

mtoto atakaezaliwa pia ni mwanao, kwa sababu kiuno kilichozaa mtoto huyo ni kizazi cha ukoo wako.

NDOA HAIFUNGWI MARA MBILI, ni AGANO LA MILELE usitegemee kuja kuolewa na mme mwingine kwa kibali kingine cha wazazi wako na Mungu pia HAPANA HAKIPO TENA!!!! Amua moja kuwasamehe wakosaji uwe na AMANI moyoni mwako na mbele za Mungu hatia itatoweka kabisaaaa dada!!
 
Kaa na mumeo kwa Mara nyingine tena muongee na akuombe msamaha naamini kama utamsamehe kwa mara nyingine tena huyo mumeo kwa aibu aliopata atakuwa mume mwema mbele zako
Sidhani kama naweza kumwamini tena, na kama ujuavyo huwezi kuishi na mtu usiyemwamini
 
Nasalute kwamba leo kichwa changu kimegota na kukosa la kukushauri.....yataka moyovwa ziada hapa.maana umepondeka na kuumia kuanzia kichwani hadi moyoni....pole
Asante[emoji24]
 
  • Thanks
Reactions: nao
Ndoa ni makubaliano ya watu wawili, lakini zitokeapo changamoto tunafanya kuwa tena si makubaliano ya watu wawili bali ya jamii.
Naamini ukweli wa nini kimetokea, jinsi mlivyoishi, jinsi mlivyokubaliana kutopata mtoto , na jinsi hisia zenu zilivyo juu ya kila mmoja wenu, hivi vyote wewe na mumeo mnavijua!
Na hii haihitaji ushauri hapa hii inahitaji kusimama binafsi kutetea unachoamini!
Tunaweza shauri hapa na usifanye kama tulivyo shauri, lakini ngoja tusiache kushauri ukasema niliwaomba mshauri tukasema uende mwenyewe. Binafsi nashauri Simamia unachoamini kitakupa faraja na amani, changamoto zipo na usiangalie mwingine anakuonaje as long as huvunji sheria ya Mungu na ya Wanadamu. Nakutakia kila la Kheri na Amini siku zote Ubongo wako unaweza tafuta majibu mazuri kadri unavyouongoza.
Nashukuru
 
Habari bibie Leah

I feel sorry for you kwa kile kilichotokea.
Ninafikiri ukikubali kuendelea na huyo mmeo hakutakuwa na ndoa tena, hata kwenye Biblia inaruhusiwa kumwacha mwana ndoa kwa uasherati.

Bahati mbaya sana jipu limeota pabaya, I am very sure Mdogo wako hataolewa na huyo the so called mmeo, umetumia hekima kubwa sana kushirikisha Pande zote mbili.

You've got to think about uamzi wako huo, labda nikwambie kitu kimoja, achana na mume wako, samehe na sahau, ila wakiamua waoane na waoane, asipomuoa usimchukie Mdogo wako, na natakiwa kuwa karibu sana na Mdogo wako ndiye mwenye wakati mgumu kuzidi hata wew na anaweza chukua maamzi ya ajabu sana, msamehe Mdogo wako hata kama kakukosea pakubwa.
Asante sana
 
"Eti tulia utapewa mume mwingine"nani kasema?mwanamke mume wako ni mmoja tu ukiachana nae usitegemee kupata mume huyo atakua mume wa watu,samehe endelea na maisha siku zenyew za kuishi zishakua chache.
 
Nakubaliana Na wewe kuchapiwa Na vitu vingine ingekua mimba kapewa binti mwingine uko mtaani ningemwambia avumilie tu lakini mdogo mtu chaaa hii ngumu.
Dada nao,Huku kwetu simiyu ni tusi kubwa sana alichokifanya mumeo lakini pia ukisoma fasihi ya mapenzi inakuambia kuwa mapenzi hayakanywi yakikanywa yanazidi kwahiyo kubali kataa mdogo wako na mumeo kamwe hawataacha japo mara mojamoja kwa kuiba hata kama umewasamehe na ukizingatia wametiana bila mpira utamu hautosahaurika huo pengine hata sasa wako pamoja waliko.

Mwambie mungu yatosha ukupe mume mwingine wala usijali mpaka natamani nikuone nikupe ushauri ana kwa ana,kwa maisha ya leo ukiwa na kazi na elimu yako wala usiwaze kama tabia yako ni njema siyo nyeusi kama mkaa tulia utapata mume mzuri na mwema kabisa huyo ni shetani kimbia utapata adhabu kubwa zaidi siku za usoni toka mapema.
 
Mnaoshauri aachane na mumewe kuna mambo mawili kama si matatu:

1. Mumewe being desperate atamuoa huyo mdogo mtu (in which im not sure kama bado hajafanya hivyo) kawafukuza kwake na hajui walipokwenda. Mdogo mtu hana kazi, lazima atamtegemea shemeji mtu. Mume mtu ni mfanyabiashara, vi shilingi vya hapa na pale havimpigi chenga. In her life, she (leah) will never get away with this itakuja kuonekana ni mke alishindwa kumzalia mtoto and mume ended up eloping with her sister. Itakuuma zaidi kuliko kuachana na mumeo

2. Mtoto atakayezaliwa bado atakuwa anakupa uchungu, unless kama utakuwa na control juu ya ukuaji wake na aku acknowledge kama "mama mkubwa" point ambayo ukiachana na huyu mumeo hii heshima haitakuwepo tuu. A second thing you will not get away with it.

3. Undugu una heshima, utakapomrudisha mumeo nyumbani, utaset clear boundaries na ndugu yako kwamba una maamuzi juu ya ndoa yako kama mke wa ndoa,nafasi ambayo yeye hatakuwa nayo.

So uchaguzi bado ni wako, ila kwa upumbavu wangu naona madhara yakuachana ni ya muda mrefu na kidonda chake kitakuuma zaidi kuliko hilo lililotokea.
 
Pole sana! Maamuzi uliyochukua ni sahihi kwa asilimia 100% hongera sana kwa kutokuwa mkurupukaji.. naamini kuanzisha upya sio ujinga, usijali jamii itakuchukulia vipi maumivu yako haiwahusu hiyo jamii .. keep calm and move on.
 
Dah pole Leah 2 hakika nayaona maumivu moyoni mwako Mungu akutie nguvu zaidi ktk maamuzi utakayo, uamuzi wowote utakao chukua Mimi nakubaliana na wewe maana am speechless hili zito kama ugaidi vile.
Asante nao..nikweli nimeumia na kulia bila mfariji bjt nadhan imetosha kulia.
 
Pole sana Leah naomba niseme kwamba nimeliangalia hili kiundani na kuona root cause (kisababishi ) cha tatizo lililojitokeza ni pale wewe uliposema kwamba usibebe mimba kwa kisingizio cha wewe kuwa masomoni. So hapo ujue nawe ulikosea maana ndiyo kwanza mlikuwa mmetoka kufunga ndoa aidha ulitakiwa kuahirisha masomo uje kuendelea kama ungebeba ujauzito na kujifungua. Ombi langu kwako kwa vile wote mmekosea umsamehe mmeo arudi nyumbani na mdogo wako aondoke hapo. Kumbuka hata akijifungua anabakia kuwa mdogo wako tu you cannot denie this fact.Hebu lifanyie kazi hili
 
"Eti tulia utapewa mume mwingine"nani kasema?mwanamke mume wako ni mmoja tu ukiachana nae usitegemee kupata mume huyo atakua mume wa watu,samehe endelea na maisha siku zenyew za kuishi zishakua chache.
Acha kupotosha watu tupo kwenye dunia hii tunaishi wote na mifano hai tunayo watu wamesepa bado wakapata waume wema kabisa tena kama hukukosea mungu yu pamoja nawe tu,unaona kabisa anaishi ya shetani mwenzako unamwambia asubili kasubiri wewe uje uone moto wake siku za usoni.
 
Dada nao,Huku kwetu simiyu ni tusi kubwa sana alichokifanya mumeo lakini pia ukisoma fasihi ya mapenzi inakuambia kuwa mapenzi hayakanywi yakikanywa yanazidi kwahiyo kubali kataa mdogo wako na mumeo kamwe hawataacha japo mara mojamoja kwa kuiba hata kama umewasamehe na ukizingatia wametiana bila mpira utamu hautosahaurika huo pengine hata sasa wako pamoja waliko.

Mwambie mungu yatosha ukupe mume mwingine wala usijali mpaka natamani nikuone nikupe ushauri ana kwa ana,kwa maisha ya leo ukiwa na kazi na elimu yako wala usiwaze kama tabia yako ni njema siyo nyeusi kama mkaa tulia utapata mume mzuri na mwema kabisa huyo ni shetani kimbia utapata adhabu kubwa zaidi siku za usoni toka mapema.
My kaka hata kwetu uku kahama ni tuzi ndo maana nilikua namshangaa huyu mchaga anasema kwao ni kawaida.hata huyu mwenye hii inshu ambaye ni Leah nimeona bora akasonga mbele aibu kwa pande zote za familia amwache tu huyu bwana.
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
uko sahihi,isitoshe hamjazaa bado so ni heri uwaache u move on na maisha yako but msamehe mdogo wako kwa ujinga wake maan nyie ni ndugu still you need each other
 
Nina miaka 4 kwenye ndoa, ninaomba kwanza nikushaurii, kwanza, ndoa inayo pendeza ni ile yenye watoto au mtto ndani ya nyumba ni si masstarz ndani ya nyumba, kitendo cha kusbubiri umalize shule ndo uzae ulikosea sana, nikujuze, mfano mimi nilipotaka kuoa, nje ya kuwa na hamu ya ndoa, nilikuwa na hamu sana ya kuitwa baba, kama mke wangu niliyemuuoa angeniambia mpaka amalize shule ndo azae, hakika ningezaa na mdogo wake, nje ya ndoa)

Pili, dada, hiyo dhambi ni ya mmeo, yeye kam amekuomba msamaha, msamehe, haraka sanaaa, maana ndani ya mafundisho ya ndoa kama kweli ulifunga ndoa yeneye mafundisho hilo si jambo la kuomba ndoa ivunjwe, sjui wewe ni dhehbu gani,ila kwa wakatoliki ili halipo kabsa, mmeo yeye anatakiwa kutubu mbere ya Mungu wake na hatasamehewe.

Tatu, umejiuliza kwa nini mmeo amegegeda mdogo wako,wakati naisi we bado mbiich kbsa hata mtt mmoja hujaazaaa? kuna kitu hapo, Masstz plus owning the house can be the source, sjui kama kweli yeye anafanya biashara na wewe unasoma mastaz sjui anakiwango gani cha elimu, ila naona famiily hisyo na amani na hasa km wewe ulifunga ndoa na mtu ambaye hana kiwango km chako cha elimu alafu unamletea habari zanimalize mastaz ndo tuzae.

Nne dada point hii naomba uisome kimnya kimnya, mbona nasikia hata moja ya watu maharufu nchini na kiongozi mkubwa tu, nae amezaa na mdogo wa mkewe, tena watto wawili sio mmoja wakati mkewe bado analipa?wewe sikiza muhite mmeo, kumbuka Mungu ikupa mme mmoja mkiwa hai, akifa yeye utampata mwingine wa lkuzeeka nae km Mungu atamchukua mapema, tena nikwambie hukutakiwa ili jambo kulireta umu ndani.

ushauri, ameni ilo eneo, mwambie mdogo wako arudi kijijini, akizaa alete mtt, na wewe huyo utamlea vizuri hivi pata picha wewe ukimaliza mastaz na huszae, wakati uo mmeo kazaaa na mdogo wako si utalea damu yako?tuliza mawazo, mrudie mmeo.
 
Back
Top Bottom