Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

1. Wewe unamakosa elimu uliyokuwa nayo ya degree ilikuwa inatosha kuzaa na baadaye kuendelea kusoma hiyo masters kutokana na wewe kusoma ulishindwa kutimiza wajibu wako japo wewe umedai ulitimiza, kwangu mimi naona hukutimiza sababu kuzaa na penyewe ni wajibu.
2. Cha kufanya mdogo wako atoe hiyo mimba ili kukulindia heshima yenu na ukoo wenu.
3. Zaa haraka sana na mme wako mwaka huu usiishe bila kushika mimba...!!
4. Fikiria hata wewe kweli miaka minne wenye ndoa bila mtoto..???? naungana na wanaume wezangu wanaowalalamikia wanawake waliosoma...!!

ANGALIZO:- Elimu zinatudanganya sana na kusahau maisha yetu ya kawaida kabisa na kwenye maelezo yako umesema wakupishe kwenye nyumba kwa sababu ni yako. hilo nalo nitatizo pia inaonekana unalingia elimu na mali yako. badilika hilo ni tatizo pia...
 
My kaka hata kwetu uku kahama ni tuzi ndo maana nilikua namshangaa huyu mchaga anasema kwao ni kawaida.hata huyu mwenye hii inshu ambaye ni Leah nimeona bora akasonga mbele aibu kwa pande zote za familia amwache tu huyu bwana.

Sikusema ni kawaida, usiniquote vibaya, nilisema huwa inatokea na watu wanaendelea na maisha. Uko masters (perhaps she is in her late 20's au early 30's) eti unaachana na mumeo halafu ungojee Mungu akupe mwanaume Mwingine. "Mungu huyo aliesema kifo kiwatenganishe??" Msimuingize kwenye dimbwi la upweke. Akae a solve mambo ya nyumbani mwake, ndo kuwa mwanamke huko bana.... Ndoa sio mteremko aisee.
 
ukiendelea na mumeo mtoto akizaliwa atamuitaje mumeo?...baba au mjomba?

na nyie mkipata watoto watamuitaje huyo mtoto mwingine?...binamu au mdogo wao?

nawaza tu jinsi papuchi ilivyo na nguvu ya kubadilisha hata majina ya familia
 
Acha kupotosha watu tupo kwenye dunia hii tunaishi wote na mifano hai tunayo watu wamesepa bado wakapata waume wema kabisa tena kama hukukosea mungu yu pamoja nawe tu,unaona kabisa anaishi ya shetani mwenzako unamwambia asubili kasubiri wewe uje uone moto wake siku za usoni.
Teh teh teh shetan wapi wanawake wanamambo ya hovyohovyo sana ukiachana na alichoandika kiuhalisia ukifuatilia 100% utakuta yeye ndo tatizo,wanaume ndoa tunaziheshimu sana,by the way mzee umenitusi kuniambia nikasubri mm nitake radhi.
 
Soma vzr maana ya ndoa,na ukisoma vzr utamfuata mumeo
 
Asante nao..nikweli nimeumia na kulia bila mfariji bjt nadhan imetosha kulia.
Leah nimehisi kutokwa Na machozi kwa hii kitu,mme akicheat nakiruka njia uko tunapatwa Na maumivu yakutosha si zaidi na mdogo mtu??? Ooh Mungu akawe mfariji wako aisee ktk hiki kipindi cha mpito.
 
Uwiii....tuite tu Neema za Mungu mana kwa akili zetu hatuezi. What I see is bora ata angekua mtu bak nimgekwambia smahee...hiv huyo ni mdogo kweli. She must be insane. If i was that young sisy after knowing i dd a mistake I'd better abort. By the way pole sana dear Leah. Mrudie Mungu, kwanza muombe akupe roho ya kuwasamehe wote na akupe njia yenye kujenga
 
  • Thanks
Reactions: nao
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
Wewe ni mwanamke.....
Mie hicho kifua sina aisee Kitendo cha kusikia Tu wanalumbana ningesha kata mtu shingo
 
Leah nimehisi kutokwa Na machozi kwa hii kitu,mme akicheat nakiruka njia uko tunapatwa Na maumivu yakutosha si zaidi na mdogo mtu??? Ooh Mungu akawe mfariji wako aisee ktk hiki kipindi cha mpito.
Asante sana nao..kinachoniuma zaidi yeye anaona ni jambo la kawaida sana yaani hasumbuki..tangu nimegundua sijawahi kusikia neno nisamehe kutoka kwake zaidi ya kisema yaishe
 
Uwiii....tuite tu Neema za Mungu mana kwa akili zetu hatuezi. What I see is bora ata angekua mtu bak nimgekwambia smahee...hiv huyo ni mdogo kweli. She must be insane. If i was that young sisy after knowing i dd a mistake I'd better abort. By the way pole sana dear Leah. Mrudie Mungu, kwanza muombe akupe roho ya kuwasamehe wote na akupe njia yenye kujenga
Asante but I'm on a very hard way.
 
Mashemeji kupiga wadogo za wake zao siku hizi mmh.....
Wenye wadogo zenu wa kike kueni makini, weka mbali na mume. Pole sana leah uamuzi wako upo sahihi
Nashukuru Evelyn Salt
 
Muache my dearest huyu anatbubutu kulala na mdogo wako hakuheshimu.. Hakuta kuwa na Amani Kabisa samehe sahau time is a good healer...
 
Pagumu hapo. Pole. Kuna maswali ya kujiuliza..Je, wakiishi pamoja uko tayari kumuita huyo mumeo shemeji? Mumeo alijuta na kuomba msamaha kwa dhati? Hapo kuna tatizo kubwa sana kwenye mahusiano wewe na mdogo wako. Chuki yako haitakwisha kwake akiendelea kuishi na Mumeo na ndo aibu itaendelea milele.
Ushauri mumeo akijirudi itakua nafuu na mdogo wako angeondoka angeolewa baadae na mtu mwingine ungepata nafuu kidogo ya chuki. Kwa sasa hata ukija pata mtu mwingine baadae wa kukuoa akisikia hii story anaweza kubadili mawazo.
Ukiweza kapatane na mumeo.
No hapana
 
Dada Leah, pole sana, nimeona huzuni yako ni kubwa, tena ni kubwa. Napenda kukushauri kitu. Iwapo utaishi na mmeo nakuhakikishia hutapata amani maishani mwako....tafuta maisha mengine mwanangu.

Hutaishi kwa amani kwa sababu hizi.....

1. Mdogo wako ataendelea kuishi, mtoto aliyemzaa nae ataishi na utakuwa unawaona, hii itaendelea kukupa kumbukumbu na kutompenda mmeo ikiwa utaendelea na ndoa yako

2. Mmeo atakuwa mzazi mwenzie na mmeo, haitakuondoa wasiwasi kamwe kama mahusiano yao yalikoma, hata kama ataolewa kwingine

3. Mdogo wako hataweza kufika nyumbani kwako kwa uhuru, ni bora mkutane nae ukiwa huna huyo mme au mkutane kwa wazazi wenu kuliko yeye kukutembelea nyumbani kwako ukiwa unaishi na mmeo

4. Mmeo atahitaji kumhudumia mtoto wake, hii itakuwa inakupa flasback (those negative ones) na itaendelea kukuumiza

5. Kama haya yote unaweza ukayamudu, yasikuvuruge katika kipindi chenu cha ndoa, basi endelea na ndoa yako.
 
Back
Top Bottom