Don Mangi
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,199
- 855
I won't jump into searching a husband instead I will focus on what will make me more respectable.
Oooh a PhD perhaps!!! Goodluck(in Marco's voice)
I won't jump into searching a husband instead I will focus on what will make me more respectable.
Hayo yalikuwa ni makubaliano ya ndoa yao...mwanaume angetaka mtoto asingemshawishi shemeji yake atoe...kosa kubwa ni mwanaume kutembea na shemeji yake...na sio mwanamke kusoma au kukubaliana lini wazae...sasa wewe umeolewa??? kwanza tuanzie hapo. na kama umeolewa baada ya mwezi kuolewa ulimpangia mumeo kuwa unataka kusoma PhD hivyo ufunge uzazi?? mbona kuna watu wanasoma na huku wanazaa?? kama unatabia za kupanga kalenda subiri wadogo zako wapigwe na shemeji yao
Si rahisi watu hawa kuishi pamojaA waache Tu Kubafu na Inavyoelekea huyu mdogo mtu atachwa[emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57] Safi sna
I won't jump into searching a husband instead I will focus on what will make me more respectable.
Wanaume wengine bwana,watu tunatafuta wake wenye heshima ,wao wanawachezea,Du dunia hii bwana kama vipi ni PM tuongee zaidi.
Hayo yalikuwa ni makubaliano ya ndoa yao...mwanaume angetaka mtoto asingemshawishi shemeji yake atoe...kosa kubwa ni mwanaume kutembea na shemeji yake...na sio mwanamke kusoma au kukubaliana lini wazae...
You are a strong woman and definitely you can overcome this. My advice to you is that, as much as you are independent in your decisions, please listen to what your parents have to say so long as your husband accepts and regrets his mistakes. If anything we all make mistakes at one time or the other in our lives. kama wewe ni mkiristo, naamini unajua story ya mwanamke mzinzi aliyetaka kupigwa mawe lakini yesu alifanya kinyume na matarajio ya wengi.Habari za asubuhi wanajamvi,
Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.
Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.
Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.
Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.
Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.
Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.
Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.
Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.
Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.
Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.
Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.
Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..
Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.
Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.
Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.
Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..
Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.
Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.
Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.
Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?
Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.
Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.
Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.
Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.
Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..
Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.
Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,
Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.
Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..
Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.
Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.
Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.
Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..
Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.
Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.
Wameondoka na sijui walipo kwenda.
Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.
Najiuliza heshima yangu iko wapi?
Jamii inanionaje?
Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?
Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.
Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.
Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.
Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
Samahani au wewe ndo mme wake...? Mbona unashadadia sana kuwa mwanamke ndo mwenye makosa? Kiukweli inawezekana mwanamke akawa amechangia kwa kiasi fulani sababu hakuna aliyekamilika ila halikuwa jambo jema mwanaume kumpa mimba shemeji yake....kaka alitaka asome kwanza ndio azae ndoa ya nini?? angesoma hadi akamaliza madarasa yote kisha arudi kwenye ndoa ili akikaa ajue ni kugegedwa na kuzaa, minyodo ya kusoma imemtumbukia nyongo.
Samahani au wewe ndo mme wake...? Mbona unashadadia sana kuwa mwanamke ndo mwenye makosa? Kiukweli inawezekana mwanamke akawa amechangia kwa kiasi fulani sababu hakuna aliyekamilika ila halikuwa jambo jema mwanaume kumpa mimba shemeji yake....
Hahaaaaaa haya banaWala simjui na hanijui, ila ingependeza kama nawe ungesimulia kuwa shemeji ulimuweka blacklist for 6 years umalize research ya malaria ndio mpate watoto, kama ulichana na mtoto akazaliwa hapa unahororoja tu
Dada sikupond lkn naongea tu ndoa inapofungwa kinachofuata n watoto haina kusema nimalize masters au kujenga hao n wazinzi kwa muda wa miez mnne kama mdogo wako alivyokuambia mimba tu ndio imewaumbua labda alikuwa anakula hausigal kabla ya dogo kuja piga chn maisha yaende
Mwenye makosa ni mme wako ambaye kamshawiahi mdogo wako. Mimi naona umechukua maamuzi mazuri nayakistaarabu
Hivi kipi kilicho kibaya zaidi ,kumgegeda mdogo mtu au Mimba aliyo mpa?Samahani au wewe ndo mme wake...? Mbona unashadadia sana kuwa mwanamke ndo mwenye makosa? Kiukweli inawezekana mwanamke akawa amechangia kwa kiasi fulani sababu hakuna aliyekamilika ila halikuwa jambo jema mwanaume kumpa mimba shemeji yake....
Mwanamme au sisi wanaume tukioa kitu cha kwanza tunataka mtoto,leah ulikua hijui? Kama hujui ndio nakufahamisha,hatuhitaji madoido,hata kama utaolewa tena,kitu cha kwanza kazae,watoto wanalinda ndoa,kama huamini basi,ungekua namtoto hata mdogo wako asingeshika mimba,huo ni uzembe wako,jamaa alitakamtoto fasta wewe unataka elimu? Ona sasa