Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

$¥€)@"Dunde ni?,,,, MBA!
Eti nini?,,,,MBA!
Dunia kapasuka MBA!"
%@&£


Pole dadangu,
Kumbuka yetu ni advise ila uamuzi ni wako, wako peke yako.

Unapoamua kufanya uamuzi kwa swala nzito kama hili usifikirie itakavyokuchukulia jamii. Jiangalie WEWE mwenyewe na MUNGU wako.

1. Unaweza kumsamehe na kuishi mume mzinifu?
2. Unaweza kumwamini tena?
3. Unaweza kumsamehe dada msaliti?
4. Mtoto akizaliwa, matumizi atatoa nani? Mumeo?
5. Utakuwa na uhakika gani kwamba mumeo hataendelea na uhusiano na dadako now that bond imekuwa thick?

NB. When you find yourself at the edge of a cliff, let yourself go. God will provide wings for you to fly.
 
Pole sana, ingawa unamapungufu yako lakini kwa hili la mumeo kuzaa na mdogo wako halivumiliki especially kama n mdogo wa tumbo moja
Kama siwatumbo moja ningekushaur umvumilie, ila kwa hili siwez shaur hivo
Sorry ningependa kutoa ushaur wakukutia nguvu, ila its too much
 
Kiukweli hapo bila kumung 'unya maneno hakuna ndoa tena maana aliyepewa ujauzito ni mdogo wako wa damu kabisa!!
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
Siyo wewe utakaeoneka vibaya mbele ya jamii bali ni mumeo na mdogo wako,usiondoke kwako endelea kuishi na majukumu ya kulea mimba ya mdogo wako na mtoto muachie mumeo,kaa kimya na songa mbele,mumeo atakuja kukulilia tu umsamehe na hatakaa akarudia tena,wakati mwingine kupambana na shetani anaweza kukuumiza tu.
 
Pole Sana dada Leah think twice kwa action utakayochukua bt make sure upo happy kwa decision utakayochukua.usifanye maamuzi kuwafurahisha wazazi au ndugu yoyote hayo Ni maisha yako.msamehe mumeo na mdogo Wako kwa maana hakuna mkalimifu na hujui siku wala saa ya kurud kwa muumba Wako usikubali kubeba mizigo ya usinzi wao kwa kutowasamehe.in short dada hapo ndoa hakuna huna nae mtoto usikubali laana ya kuzaa na mwanaume mmoja wewe na mdogo Wako WA damu.hama mkoa Anza new life
 
Pole Sana dada Leah think twice kwa action utakayochukua bt make sure upo happy kwa decision utakayochukua.usifanye maamuzi kuwafurahisha wazazi au ndugu yoyote hayo Ni maisha yako.msamehe mumeo na mdogo Wako kwa maana hakuna mkalimifu na hujui siku wala saa ya kurud kwa muumba Wako usikubali kubeba mizigo ya usinzi wao kwa kutowasamehe.in short dada hapo ndoa hakuna huna nae mtoto usikubali laana ya kuzaa na mwanaume mmoja wewe na mdogo Wako WA damu.hama mkoa Anza new life
Huu ushauli hatauelewa ndugu! Umemwambia asamehe lakini pia umemwambia asibebe laana,ahame mkoa aondoke,ashike lipi labda ulomaanisha?
 
Vumilia, samehe, sahau na jifunze wapi ulikosea, hakuna mwanadamu mkamilifu. Baki ishi na mumeo
 
Asante heaven sent umeugusa moyo wangu mpaka nimejikuta nalia, to be honest siwezi endelea na hii ndoa, sioni future serious na huyu mtu.
Oops pole sweetheart, ila ukijisikia kulia please lia tu utakavyoweza. Machozi yanasaidia sana kupunguza maumivu na uchungu. Mwisho wa siku Jitahidi uwasamehe wote (kusamehe sio lazima urudiane na mumeo), usije zuia baraka zako bure. Mungu akupitishe salama katika pito lako hili
 
Back
Top Bottom