Mume ana gari tatu, natembea kwa miguu

Mume ana gari tatu, natembea kwa miguu

Umeshajua kuendesha gari au bado unatumia TZ 11 na boda boda kwa sana?

habari wana Mmu

Niko kwenye ndoa miaka 10 sasa,tumejiajiri tuna kaofisi ketu mjini,tunafanya kazi pamoja na mume wangu.

mume wangu ana gari 3,kwa kawaida yeye huwahi ofisini mapema kufungua,mm nafanya mawili matatu kwanza ili kuiacha nyumba sawa.

wakati nakwenda kibaruani humfahamisha mume wangu ambaye hunitumia usafiri wa bodaboda.Hata wakati wa kurejea home nachukua bodaboda na yy anakuja na gari yake full kiyoyozi.

Nikiomba anifundishe gari huwa hanijibu lolote(anapotezea) na ataanzisha mada nyingineeee. Maswala mengine ya nyumbani yako vizuri tatizo ni hapo tu kwenye usafiri.
Akienda na gari moja mawili yanapark hapo nyumbani yakipigwa jua na vumbi,na daily anachange analotaka.

nimechoka kutembea na bodaboda,potelea mbali,nimeamua kupiga zangu kwa mguu wakati magari yako home.
gari hizi amenunua tukiwa pamoja kwenye ndoa,wakati tunaoana hatukuwa hata na baiskeli.

Aaaghrrrrr,,,,,,,acha tu nisuse,inatia hasira sana na inanyongesha pia.
 
Huyo amechukua imano ya kishirikina mganga wake ndo alivyomuagiza wala hamna lolote zaid ya hilo
 
Hii post inaonekana ni ya 2014,vipi mpaka leo bado tu anakubania hayo magari?
 
keshakusoma kakuona mjinga mjinga anaogopa akikupa gari ndo huo ujinga wako utazidi...zinatokeaga hizo kwhy jichunguze udhaifu wako labda mtu wa misifasifa mtaani na mashoga wa kipuuzi wengi au mtu wa kubweteka hv...tuondoe wanaume bahili km wapare hp nazungumzia mwanaume mwenywe akili timam au muoga ww utampa hasara....ni ngumu ujue
 
Tafuta la kwako. Hii biashara ya kujifanyaga mnapenda saana, nguvu zako zote zinaishia kumfurahisha yeye tu, unakosa hata ka vits yeye anatumia magari 3 bila kukujali naishangaaga sana. Sidhani kama toka mwanzo hukuwa umemsoma mumeo kwa ubinafsi alionao. Nawe jikaze kike fight upate vyako looool
 
are you this WEAK??

juzi niliona comment yako unasema wanaharakati wa haki sawa ni mitandaoni tu huko duniani hamna kitu nikataka kukushushia m paragraph nikaone nisichafue hali ya hewa.

ni wewe ulisema kwenye thread flani kuwa wanaume wengi wana michepuko na huwezi kuacha mume kwa sababu ya mchepuko kwasababu utakuwa umewapa ushindi.

sasa mshindi unapanda boda boda, wake wenza wanabadilishiwa magari!!!

me navyopenda umalkia I don't see this happening to me.

umesema ni kampuni yenu lakini magari ni yake. HOW? Those are YOUR cars. Hivi hata alikushirikisha wakati ananunua kuuliza unapenda gari gani??

Is this man your father or your man??

I just hope uliendaga driving school, siku ukaibuka kazini na gari na akafurahi
 
Pole sana dada. Nenda driving school ujifunze uanze kuendesha mwenyewe. Na ukianza kwenda nalo ofisini tafuta dereva uende nae siku mbili tatu akuzoeshe barabara na maarifa machache. Lakini pia uwe makini ukianza kuendesha maana hapo ukigonga gari atakujia juu sana kwa jinsi anavyoonekana kwa maelezo yako. Jambo lingine asikufundishe mumeo, tafuta dereva kwa sababu naonaga kiyu fulani hivi kama hiki: akikufundisha ndugu wa karibu ambae ni mmiliki wa gari mara nyingi wanakuwaga wakaliiiii anaona kama unagonga gari lake na anakuwa hakuamini kitu ambacho kitakuletea woga tu.
Kila la kheri.
 
je akijua hilo gari na akapewa anao uwezo wa kulihudumia kuweka mafuta au ndo mafuta mume ahahangaike tena kumuwekea?
Ww nawe unauliza maswali gan,kwan mumewe anatoa wap hela ya kuweka mafuta,think big bhana
 
Nimeisoma na kuielewa...ila ninachotaka kukuambia ni kwamba hiyo ofisi ya huko mjini...ni initiatives na mwanaume...na ndio maana wamefika hapo walipo...suala la yeye kwenda huko ofisini ni kusaidiana tu mfano anakaa na kuuza duka pamoja labda huku wanapiga stori...kutokumkuta hata baiskeli hana sio kigezo cha yeye kupewa gari....amablo hata akipewa huenda hata kulihudumia hatoweza...! tatizo lenu wanawake ni wabishi sana na mnapenda sana kushabikia ili ionekane ananyanyaswa..something which is not true...kwanza kitembea Kwa mguu si ndio vizuri apunguze na kitambi.
Bado ww ni mgumu kuelewa,ww ni mwenyeji wa wap mkuu
 
Back
Top Bottom