Yaani inauma kwa kweli, mi wangu alinifundisha ile siku nakaa kwenye steringi na kupiga stata gari inaanza mdogomdogo alianza kunigombeza oooh umeanza mbio,mara utagonga!!mpaka nikachanganyikiwa nikamrudishia funguo na kujiapiza sitaki tena kufundishwa nae. Najiandaa kwenda driving school.Nijinunulie kigari changu.Wanaume ni wabinafsi sana!!
Siyo bure ana matatizo inawezekana kapewa masharti ya biashara na magari yake.Kabisa!! Jamaa aliugua alikuwa anapanda bodaboda, mke ndo wakumuhudumia kila kitu, gari imepaki tu!ndugu wakamuuliza kisa cha kutokumfundisha gari mkewe kabaki kimya, alivyopona asb ye anaondoka na gari mke anapanda 55.Inauma sana sana.
habari wana Mmu
Niko kwenye ndoa miaka 10 sasa,tumejiajiri tuna kaofisi ketu mjini,tunafanya kazi pamoja na mume wangu.
mume wangu ana gari 3,kwa kawaida yeye huwahi ofisini mapema kufungua,mm nafanya mawili matatu kwanza ili kuiacha nyumba sawa.
wakati nakwenda kibaruani humfahamisha mume wangu ambaye hunitumia usafiri wa bodaboda.Hata wakati wa kurejea home nachukua bodaboda na yy anakuja na gari yake full kiyoyozi.
Nikiomba anifundishe gari huwa hanijibu lolote(anapotezea) na ataanzisha mada nyingineeee. Maswala mengine ya nyumbani yako vizuri tatizo ni hapo tu kwenye usafiri.
Akienda na gari moja mawili yanapark hapo nyumbani yakipigwa jua na vumbi,na daily anachange analotaka.
nimechoka kutembea na bodaboda,potelea mbali,nimeamua kupiga zangu kwa mguu wakati magari yako home.
gari hizi amenunua tukiwa pamoja kwenye ndoa,wakati tunaoana hatukuwa hata na baiskeli.
Aaaghrrrrr,,,,,,,acha tu nisuse,inatia hasira sana na inanyongesha pia.
Mie alinifundisha kwa ukali hivyo hivyo nikavumilia tu wanasema mtumikie kafiri upate mradi wako sasa ni mwaka wa 7 nipo barabarani bila mgogoro nae na siku akininyima yake nakamua yangu hakuna kutishana dunia ya leo
nunua lako aiseehabari wana Mmu