Muhingo Rweyemamu on Amina's Death

Muhingo Rweyemamu on Amina's Death

25/06/2007


jk1xh0.jpg

Afisa kutoka Tume ya kudhibiti Madawa ya Kuevya nchini Bwana Yovin Ivo akimpa Rais Jakaya Kikwete maelezo kuhusu kete ya madawa ya kulevya ambayo ilikuwa imemezwa na mmoja wa watuhumiwa wa kusafirisha mihadarati wakati Rais Kikwete alipotembelea mabanda ya Maonyesho ya vitengo mbalimbali vinavyohusika kudhibiti mihadarati nchini katika viwanja vya Tangamano,mjini Tanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya duniani(photo by Freddy Maro)

Date Picture Taken - 6/25/2007 - 5:45PM
 
jk6ab4.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mkiwa Maige mwenye umri wa miaka 12 ambaye anauguza jeraha baada ya kukatwa mguu kutokana na uvimbe wakati Rais alipotembelea hospitali ya Bombo mjini Tanga muda mfupi baada ya kuhutubia wananchi wa Tanga katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mapambano dhidi ya madawa ya kulevya iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Mkwakwani mkoani Tanga.Mkiwa anasoma darasa la pili.Aliyesimama akiangalia ni mganga mkuu wa hospitali ya Bombo Dr.Margareth Mhando(picha na Freddy Maro)

Date Picture Taken - 6/26/2007 - 1:22PM
 
jk5ea2.jpg


Date Picture Taken - 6/26/2007 - 10:45 AM

jk4lg0.jpg

Date Picture Taken - 6/26/2007 - 11:04 AM

Baadhi ya wanafunzi na vijana kutoka katika shule mbalimbali za manispaa ya Tanga wakiandamana mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakiwa na mabango yanayolaani biashara na matumizi ya madawa ya kulevya wakati wa maaadhimisho ya Siku ya Kimataifa Dhidi ya Biashara na Matumizi ya Madawa ya kulevya iliyoadhimishwa kitaifa katika Uwanja wa Michezo wa Mkwakwani Tanga leo asubuhi(picha na Freddy Maro).
 
jk7mb2.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe la msingi kuashiria kuzindua mradi wa Umeme katika wilaya ya Serengeti,katika sherehe zilizifanyika katika mji wa Mugumu ambao ni makao makuu ya Wiloaya ya Serengeti leo mchana(photo by freddy Maro)

Date Picture Taken - 6/27/2007 12:53 PM
 
jk8ws6.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika simu muda mfupi baada ya kuzindua Mradi wa Optic Fibre ulioenda sambamba na uzinduzi wa mradi wa umeme wilaya ya Serengeti ulifanyika katika mji wa Mugumu leo mchana.Mradi huo utasadidia kuenea kwa mawasiliano ya internet wilaya ya Serengeti na sehemu za jirani. Pembeni ya Rais kushoto ni Waziri wa nishati Nazir Karamagi,Kulia ni Mkurugenzi mkuu tume ya Sayansi na Teknologia Profesa Yadon Kohi(picha na Freddy Maro).

Date Picture Taken - 6/27/2007 - 12:54 PM
 
dsc026333el4.jpg

Rais Jakaya Mrisho kikwete akiweka saini Kitabu cha maombolezo Nyumbani Kwa Wazazi wa Marehemu Amina Chifupa jana jioni. Rais alikwenda nyumbani hapo kifariji familia ya marehemu.

Date Picture Taken - 6/27/2007 8:05 PM


dsc026466mn9.jpg

Rais Jakaya Mrisho kiwete akimfariji Juliana Solomon Mbanga ambaye ni mama yake Marehemu Amina Chifupa wakati Rais alipokwenda kuifariji familia ya marehemu nyumabni kwa Mikocheni jijini Dar es salaam jana jioni(picha na Freddy Maro).

Date Picture Taken - 6/27/2007 8:10 PM
 
jk9qe2.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia zawadi Kijana Segawa David Bright kutoka Uganda zawadi baadaya ya kuibuka mshindi wa kwanza katika shindalo la Nufaika na BBC ambalo lilishirikisha vijana kutoka katika nchi za Kenya Uganda na Tanzania.Pembeni wakiangalia ni mkuu wa iDHAA YA KISWAHLI YA BBC Solomon Mugera na pembeni yake ni Mkuu wa Kitengo cha BBC Africa Mashariki na Kati Jerry Timmins.Makabidhiano hayo yalikuwa ni sehemu ya Hafla ya miaka 50 ya idhaa ya kiswahili iliyofanyika katika Kilimanjaro Hotel Kempinsky, jini Dar es salaam jana jioni(photo na Freddy MARO)

Date Picture Taken - 6/27/2007 - 7:14 PM


SO NOW, THIS IS THE EVIDENCE I HAVE WHICH CAN HELP EVERYBODY TO SEE WHO'S LYING HOWS NOT.


 
jk6ab4.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mkiwa Maige mwenye umri wa miaka 12 ambaye anauguza jeraha baada ya kukatwa mguu kutokana na uvimbe wakati Rais alipotembelea hospitali ya Bombo mjini Tanga muda mfupi baada ya kuhutubia wananchi wa Tanga katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mapambano dhidi ya madawa ya kulevya iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Mkwakwani mkoani Tanga.Mkiwa anasoma darasa la pili.Aliyesimama akiangalia ni mganga mkuu wa hospitali ya Bombo Dr.Margareth Mhando(picha na Freddy Maro)

Date Picture Taken - 6/26/2007 - 1:22PM

Aah! Kumbe kweli!!!! kumbe Rais Kikwete alikwenda hospitali mchana huo wa tarehe 26/June!!! LAKINI hospitali yenyewe ilikuwa Bombo Tanga!!!

Tuendelee na issue nyingine,... hopefully conspiracy theories nazo hazitakuja kufa "kibudu". Enhe, ..."scud" lilitumwa na nani vile?... au ndio inasemekana ni albadiri tu?...
 
Yes, Rais aliwasili Tanga tarehe 25 majira saa tisa, na siku hiyo hiyo akaenda moja kwa moja kwenye mabanda ya maonyesho ya mambo ya madawa ya kulevya, shughuli ambayo pia iliripotiwa na vyombo vya habari, including TVs.

Kesho yake asubuhi (tarehe 26 June - siku ya Jumanne, ambayo unadai ndio alienda kumuona Amina Lugalo) akaenda kupokea maandamano Uwanja wa Mkwakwani - Tanga, na kuhutubia. Kwenye saa saba mchana, akaenda kupata lunch Mkonge Hotel. Later mchana waka-fly to Serengeti, na kufikia Seronera Lodge ambapo alilala hadi kesho yake (June 27), akafungua mradi wa umeme Serengeti, na kuondoka kurudi Dar. Jioni akawa mgeni rasmi shughuli ya BBC, na baada ya hapo straight akaenda kuhani msiba.

Kwahiyo, bwana mkubwa, usitudanganye. Heshima ya Forum mbele.

Fuatilia hiyo alafu fuatilia na picha
 
Could it be Mkandara missed Kikwete's last visit to the late Chifupa by a day? Just wond'ring.
 
Siamini kuwa mnaweza kutumia muda wote huu kubishana kama JK alienda kuhani msibani ama la. Ama ni yupi mkweli kati ya mkandala, mwanakijiji ama mugongomugongo. Wote hawa ukiwauliza ni lini walipata kuongea na kumsikiliza Amina mawazo yake, ndoto zake na hata matatizo yake sidhani kama wanaweza kusema kuwa waliweza hata kwa dakika tano tu za maisha yao.

Ninachokiona hapa ni kuwa mnamsaidia mugongomugongo kuwatoa katika mjadala wenyewe ambao ni maudhui na nia ya tungo ya mpambe(samahani kwa kutumia lugha hii) wa manyang'au mwenzie Muhingo kuhusu kifo cha dada yetu Amina. Mimi siamini(labda hadi hapo nitakapo pata ushahidi) kuwa Amina ameuawa kwa sumu, uchawi ama albadir kama wengi wanavyodhani ama wanavotaka ionekane. Lakini uchafu wa Muhingo ni muhimu kuujadili kwa mapana na zaidi kumjua vizuri huyu jamaa na hatari za wino wake wa damu.

Tanzanianjema
 
Naona Mugongo kaenda kulala sasa...

Kaka inaeleka humjui mugongomugongo bado, yupe macho wazi. Kawaida yake hukwepa arguments na kuishia kutuhumu kila mtu mpambe wa Mbowe ama mwanachadema.....ama akaibuka na players hater nyingine

Tanzanianjema
 
Duh!! Anyways si bora tu mmupigie simu yule Head wa PSU,(jamaa alikuwaga head wa mabodyguard wa Nyerere) jina limenitoka, labda kulikuwa na katrip kasiri kidogo he he.....si unajua mambo ya G 550 Pyuuuuuuuuu!!!
 
Case closed. Nimeitwa majina mengi hapa, lakini as long as ukweli umejidhihirisha, I am in heavens. Wengine wanaona hili suala dogo...lakini sio dogo. Mtu unapoongea with authority hapa JF kwamba "Rais alienda "kumuaga" Amina mchana wa siku aliyofariki pale Lugalo kwa kuwa alijua what is going to happen jioni hiyo", people repeat this assertion mitaani kwasababu wanaiamini JF. Nilitaka tuwekane sawa tu...kwamba kumbe kuongea kwa tone ya authority hakumaanishi mtu anasema ukweli.

Now we can move on to other subjects.
 
Back
Top Bottom