Nakubaliana kwa kiasi kikubwa na hoja za Muhingo, japo nami najiuliza kutokana na historia yake amapata guts gani za kutamka kwamba mwenyekiti wake wa chama na katibu wake ni 'wamekufa'ni hatua kubwa kwa kada kutamka hayo! ama ana uchungu wa kukosa 'ukuu wa wilaya' alioahidiwa!ama amejirudi baada ya maumivu mengi aliyowasababishia wengine! Inashangaza pia kama alikuwa anawajua waliokuwa wakimtumia kijana wetu mpambanaji kama chambo cha mapambano dhidi ya madawa ya kulevya na kuamua kukaa kimya!Yawezekana na yeye ni muuaji pia! Tuache hayo!
Kifo cha kijana wetu kinatuachia maswali mengi yasiyokuwa na majibu! Mimi ni mmoja wa watu ambao nilikuwa nafuatilia hali ya amina,kujaribu kutafuta suluhu toka mapema, bila mafanikio!Nakumbuka mara ya mwisho kuzungumza na simu na amina ilikuwa na usiku ambao hakutokea kuzungumza na wanahabari. Lengo likiwa ni kufahamu kulikoni hasa ukuzingatia nilimshauri tokea mapema mara baada ya majira kutoa habari juu ya talaka yake kukaa kimya, nikijua kwamba akiongea tu waandishi watakuwa wamepata kwa kutokea! Mazungimzo yetu yalinipa picha kwamba kijana wetu hakuwa vizuri! kwa ufupi alikuwa haeleweki anaongea nini kabisa! Kitu alichonijibu ambayo ilikuwa ni kauli yake ya mwisho kwani baada ya hapo simu yake ikawa haipatikani tena ni kwamba 'amewasiliana na ubalozi wa marekani, na ubalozi husika umemwambia kwamba watarusha live toka kwao kile ambacho ilikuwa akakieleze maelezo'Nilishtuka! Siku mbili baadae baada ya kutokumpata kabisa kwenye simu nilifunga safari mpaka kwao, lengo likiwa ni kumjulia hali na kutaka kusaidia..hatukuruhusiwa kuingia ndani,tukaambiwa amina hayupo- nilijua nadanganywa,nikawa sina jinsi! Ikanilazimu nitafute namba ya mdogo wake , nikawa namshauri wampeleke hospitali! Nakumbuka nilikuwa namwambia mara kwa mara mkicheza amina atakufa!Ilifikia hatua nikawatafutia daktari wa mambo ya depression na psycholigy!hawakuhangaika nae kabisa, walikuwa busy na waganga wakiamini kabisa binti yao amelogwa! Kibaya zaidi wale mabinti wadogo hawakuwa na sauti kwao! Mpakanjia alikuwa na sauti!
Amina amekuja kupelekwa hospitali akiwa kwenye koma, mwili wake ukiwa umebadilika rangi kabisa!Nilifanikiwa kuongea na Mhe. mmoja ambaye yasemekana alikuwa mshauri wake wa karibu, aliniambia alipotea kitanda na kumpita amina! alikuwa mweusi Tii! sio rangi yake, kumbe cell zinazorutubusha ngozi ya bindamu zilikuwa zimeshakufa! Kwa kweli inasikitisha sana!
Jambo ambalo nakuwa nimejiuliza kwa kipindi kirefu!Hali ya Amina ilikuwa inajulikana fika na serikali, kwa nini wazazi wake hawakulazimishwa wampeleke hospitali? Tunajua kabisa Mzee Chifupa ni kada wa chama, chama kingetoa amri lazima angetii, kwa nini chama kiliamua kukaa kimya? Je waliamua kumtoa kafara sababu tu watu aliokuwa akiwazungumzia ndio wanaoongoza kwa kukichangia chama katika kampeni za uchaguzi? au kwa kuwa na baadhi yao wao wanauza? Ni mara ngapi tumekuwa tukishuudia viongozi wenye mafua wakienda tibiwa nje ya nchi? Yaani Amina walikuwa hawajui? Na hawa wabunge wa CCM na manaibu mawaziri(UVCCM) ambao walipeleka umbea kwa mpakanjia (baadhi yao ilikuwa inasemekana walikuwa na uhusiano na amina)kulikopelekea msongo wa mawazo hata kufa kwa amina wamechukuliwa hatua gani?
mimi daima huamini malipo ni hapa hapa duniani! Najua mtanikebehi!anayeua kwa upanga , naye atakufa kwa upanga!
Amina ametangulia, sote tutamfuata!
Muhingo, 2010 endelea kuwa mtakatifu, utakatifu ambao umeanza kuuonyesha kwa Amina!