Muhingo Rweyemamu on Amina's Death

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Alituma kwa Wana Tumaini University Yahoo Group

Salaam wana Tumaini na wapenzi wa ukweli kote mliko. Tangu Amina alipofariki usiku wa juzi, mimi binafsi kama Mhariri wa gazeti la Rai, nimepokea simu na ujumbe mwingi wa simu. Nimepokea emails nyingi tu. Nimewasikia waheshimiwa, vijana kwa wazee wakiomboleza kifo chake.

Wengine kama tunavyojua wanajaribu kwa kila wanavyoweza kutaka kubashiri kwa nini Amina kafariki katika umri huu mfupi. Mimi ninajiuliza tumejifunza nini kutokana na kifo cha mwanamapinduzi huyu? Jawabu ninalolipata, ni kwamba sisi ni wanafiki.

Wakati fulani, nilikuwa kuandika makala ya ukurasa mzima katika Rai nikisema: "WANAOMPENDA AMINA, WATAMLINDA." Kwanza wana Tumaini nataka niwaeleze kwamba Amina alikuwa rafiki yangu na mshauri wake. Siku alipopata matatizo ya kuanzisha urafiki na mume wa mtu mwaka 1999 wakati huo akiwa Tambaza kidato cha tano, mimi na aliposongwa na mashutumu na majaribu mengi, mimi na mwandishi mwenzangu, Absalom Kibanda, ndiye tulimpa ushauri wa kuwaambia walimu wake.

Tulimshauri akubali na awaeleze kuwa yule mwanaume alimuingia kwa gia ya kutaka kumuoa. Akasema yeye kama Mwislam, hakuwa na kipingamizi. Amina alitoa sababu hizo shuleni, wakazikataa. Akaenda shule ya private ya Makongo. Wakati tunamshauri, alikuwa akifanya kazi ya utangazaji pale Clouds FM. Ofisi yake ilikuwa ghorofa ya tano
ya jengo la Kitega Uchumi na mimi ofisi yangu ilikuwa ghorofa ya sita. Kwa hiyo tulikuwa karibu sana yeye na mwimbaji maarufu Lady Jaydee. Kipindi hicho, alionekana kijana anayeimudu fani yake katika umri mdogo. Absalom Kibanda alimfanyia interview na kuchapishwa kwenye jarida la Wiki Hii ambalo baadaye ndiyo liligeuka jina na kuitwa Mwananchi. Wakati huo nilikuwa Mhariri Mtendaji.

Katika siku za hivi karibuni, watu wenye malengo mengi, wamekuwa wakimtumia Amina. Wakati wa vita ya biashara ya dawa za kulevya hakuwa peke yake.

Kuna kundi kubwa la wafanyabiashara mashuhuri lilikuwa nyuma yake. Kwa sababu yeye ni jasiri, walimpatia orodha ndefu sana aipeleke kwenye mamlaka zinazohusika. Siku moja Rais Kikwete alitueleza kuwa kama angeamua kuishughulikia orodha hiyo, hakuna watu wangeshikana uchawi. Anasema kwamba baadaye, iligundulika kwamba majina mengi kwenye orodha hiyo, yaliwekwa si kwa sababu ni wafanyabiashara ya dawa za kulevya. Hakufafanua zaidi lakini wengi tulijua kwamba ni vita za kibishara zinazotembea katika nchi zote zilizoamua kuukumbatia ubepari.

Kasi ya Amina ilinitisha, kama mhariri na kama rafiki yake. Nilimwita tukazungumza naye. Akaniambia kwamba hiyo ndiyo njia aliyoamua kupandia kisiasa. Niliamua kukubaliana naye lakini nikamwambia achukue tahadhari. Nilimwambia kwamba Morocco ni nchi ya kwanza kulima bangi duniani. Shamba kubwa la bangi mjini Rabat liko upande wa kulia wa njia inayokwenda uwanja wa ndege wa nchi hiyo. Bangi imepigwa marufuku nchini Morocco lakini hakuna kiongozi yeyote wa kisiasa anayekubali kuzungumzia shamba hilo la bangi wakati wakienda uwanja wa ndege kuwachukua wageni wao au hata wakisafiri.

Nilimuonya kama ni ajenda yake, aende nayo taratibu, kama siyo yake, awaachie wenye nayo. Hakukubali wala kukanusha kwamba kuna watu wanataka kupandia mgongoni mwake.

Niliamua kuandika makala ya kuwaonya wale wanaomtumia (kwa sababu nilikuwa na habari zao kamili). Amina akapunguza kuwa public, akaamua kuifanya kazi hiyo kisayansi kwa kushirikiana na polisi chini kwa chini kama alivyosema Tibaigana.

Sasa likafuata hili suala la ndoa yake na wanasiasa walioingilia kati. Hilo jambo lilikuja kwa kasi sana . Yeye wakati huo alikuwa na ambition ya kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM. Akaenda kumwomba mwenyekiti wa sasa amuunge mkono. Kwa bahati mbaya kwake Amina, Mwenyekiti huyo akakataa kwa kumwambia point blank kwamba hatamuunga mkono. Kwa bahati mbaya tena, mwenyekiti huyo alikuwa rafiki mkubwa wa mume wake. Mume wake tayari alikuwa akimhisi kufanya mapenzi na Zitto Kabwe. Amina akachanganya mambo, akadhani Mwenyekiti wa UVCCM, ndiye amemchongea kwa mume wake. Ikafuata talaka. Amina akaahidi kwenda kwenye vyombo vya habari pale Maelezo kuanika yote. Yaani kutoa dukuduku lake. Kwa bahati mbaya, wakati vyombo vyote vya kitaifa na kimataifa vikimsubiri pale, baba yake ndiye akatokea. Kwa hiyo Amina akabaki na fundo lake. (wale walioko Tumaini chuoni wanaochukua shahada ya Councelling au walimu wao wanaweza kutueleza hapa).

Kilichotokea ni depression. kwa walimu wetu wa councelling nadhani watakubaliana nami kwamba depression can disrupt, disable, and kill. In terms of human suffering, the consequences of untreated depression are beyond measure. They include loss of self-esteem, family and career disruption, chronic disability and, in many cases, death. Suicide, is the outcome of depression. Kwa wale wanaojua siku za mwisho za Amina, watakubaliana nami kwamba kilichomuua ni depression.

Wataalam wanatueleza kwamba depression inaweza kuua sawa na ugonjwa wa moyo au magonjwa mengine. Kwa mfano Dr. Joseph Gallo, wa Chuo Kikuu cha Pennsylvania katika jarida la kitabibu nchini Marekani linalojulikana kama Geriatric Psychiatry, anasema kuna uwezekano kwamba depression inaingilia mfumo wa moyo pamoja na kushambulia immunity system ya mwili. Hivi ndivyo anavyosema:

"How depression increases death rates is not clear," said Dr. Joseph Gallo.
"Possibly depression makes people less likely to take care of themselves, or acts directly on the immune system in ways we do not completely understand."

Kosa kubwa alilolifanya baba yake Amina, ni kumzuia kwenda kuzungumza na waandishi wa habari. Kwa yeyote anayejua mambo haya, atakubaliana nami kwamba Amina alianza kufa siku aliyozuiliwa kukutana na waandishi wa habari. Kwa sababu tangu siku hiyo, alianza kuwa recluse. Alianza kukataa kukutana na watu na tunaambiwa alifungiwa ndani, akaanza kujinyoa nywele, na wakati mwingine kuwasahau hata marafiki zake.

Kwa nini nasema sisi ni wanafiki? Nasema hivyo kwa sababu kulikuwa na uwezekano wa kuokoa maisha yake. Jamii haijajiandaa kuwasaidia vijana kutimiza malengo yao na kuvivuka vikwazo vya kimaisha. Amina amekuwa akipambana na mambo mengi ya maisha. Najua hivi kwa sababu ingalau najishughulisha na matatizo ya vijana. Wakati magazeti ya Shigongo yamemwandama kumchafulia jina, jamii ilikaa kimya. Amina akawa analia wakati akiwa chumba cha habari cha Clouds, watu wanasema shangingi huyo.

Leo ni wale wale wanaomsifu na kumwagia sifa. Napenda kumaliza kwa kusema
Amina hajafa. Waliokufa ni sisi tunaodhani tuko hai. Sisi wanafiki wa kupeleka maua kwenye majeneza wakati tungeweza kutoa maua hayo kukamilisha azma yake ya masha. Aliyekufa ni mwenyekiti wa CCM na Katibu Mkuu wake waliokataa kusuluhisha mgogoro wake wakidai ni wa kifamilia. Aliyekufa ni Spika wa Bunge aliyesema mambo ya Zitto na Amina hayalihusu bunge lakini sasa wanatoa ndege ya serikali kwenda kwenye mazishi. Aliyekufa ni mtuhumiwa Zitto Kabwe ambaye pamoja na kuendelea kukataa hadharani, alikuwa akiendelea kuwasiliana naye kwenye simu. Aliyekufa ni Shigongo na magazeti yake ambayo hata baada ya kufariki, waliendelea kuandama maiti yake kwa kutumia vyombo vyake vya habari. Amina hajafa na ndiyo sababu amepumzika siku ya kupiga vita dawa za kulevya; njia aliyoichagua kumjenga kisiasa.

muhingo
 
Masikini Amina,

Yaani hata huyu kuwadi wa manyang'au anajidai alikuwa rafiki yake?

Yaani hawachelewi hata siku kutoa makucha yao?
 
huyu si ndo yule mwandishi ambae anapoamua kuwasagia baadhi ya watu hubadili jina? si huyu aliepakaza uongo kwa Dr salim? nnaomba mnijuilishe
 
Ni huyu huyu kuwadi wa kila nyang'au wa nchi yetu ambaye wakati wa kampeni alikuwa akitamba kwa kila mtu kuwa atakuwa mkuu wa wilaya akidhani JK mlugaluga kama yeye.

Na ni huyu huyu aliyezunguka katika vyombo vya habari kuwasaliti wanafunzi wa mlimani mwaka 2004 wakati walipokuwa wakipinga ile sheria ya mikopo. Sheria ambayo hadi leo inazua kizaazaa kwa wasio na chao. Yote hayo ilikuwa kutetea maslahi yake akiwa kama mwanafunzi katika vyuo binafsi ambapo ilikuwa ni juhudi za Zitto na wenzake kulobby serikali ili nao waingizwe katika mpango huo wa mikopo ya serikali.
 
Hii ni coincidence, au mchongoma alinukuu hapa kabla hajapost juzi!!?? Read between lines; lakini hizi posting zinashabihiana.
Hivi humu katika wachangiaji wa JF hakuna madaktari wa binadamu humu? Kuna hali inayoitwa Depression, sijui tafsiri yake kwa kiswahili, hali inayomfanya muathirika kuvuruga mfumo mzima wa kemikali katika mwili wake hivyo kusababisha kupanda kwa Msukumo wa damu (BP), ambayo nayo inasababisha kupanda na kushuka bila mpangilio kwa kiwango cha sukari mwilini!... Depression inasababishwa haswa iwapo muathirika hakupata nafasi ya kutatua msongamano wa mawazo yalokuwa yanamkabili!

Kwa mtizamo wangu naona machungu ya kuvunjika ndoa yake na kunyimwa nafasi ya kujitetea/kujielezea ndiyo chanzo kikuu cha Depression, (kama hiyo ndiyo hali iliyomsibu). Hali hiyo ikimpata mtu mwenye roho ndogo na kutopata msaada wa kitaalamu kwa wakati muafaka, kila gonjwa lilokuwemo na lisokuwemo litafumka, na ndiyo maana wengine huishia kujitundika kitanzi kama sio kunywa dawa ya panya!

Katika nchi zinazokubali dubwana hili "Depression", wamefikia hatua hata ya kuwa na trained psychologists, psychitrists, na Counsellors, wenye mafunzo maalum kuwasaidia watu wenye matatizo hayo!
 
Kuna kazi kwenye kifo hiki.Ni vizuri wananchi wafahamu kila kitu na kiwe wazi kwa kila mmoja.
 
naona HII IMEBACKFIRE!
540ehj5-1.jpg
 
jamani wana jf,lazima kuwa makini sana na kila neno la baadhi ya maandishi ya watu ambao mnafahamu,someni kwa makini mtakuja gundua kuwa lengo kuu la makala hayo ni moja tu nalo ni kumchomoa mtu katika lawama za jamii ili aweze kuonekana kwamba hafahi ndani ya jamii na ndicho alichofanya huyo mwandishi,ni nni ujanja tu tu lakini lengo ni kuonekana mtu anayeshukiwa hausiki na katika hilo mtashuhudia mambo mengi sana ebu na tusubiri shigongo naye lazima atatumika kama patriot ya kuokoa upande ambao kwa sasa unalaumiwa
 
Bigman... hawa watetezi wa Amina sasa hizi, I'll square with them one of these days..!

Walikuwa wapi siku ile Amina kanyamazishwa kama mtoto mdogo?
Walikuwa wapi siku Amina ameanza kuweweseka na kubwabwaja?
Walikuwa wapi taarifa za kuwa Amina ni mgonjwa?
Walikuwa wapi wakati tunaambiwa kuwa ameenda Iringa na baba yake kurudisha fomu wakati Babu wa Marehemu amesema kuwa mara ya mwisho Amina kwenda huko kwao ni April akiwa na mumewe? Mbona hawajauliza habari hizo zilitoka wapi?
Walikuwa wapi hawa watetezi wakati Amina anapelekwa kwa waganga wa kienyeji na kupoteza muda mwingi kunyimwa matibabu ya kisayansi?
Walikuwa wapi pale ambapo serikali ilishindwa kabisa kuingilia kati maisha ya Mbunge wake na kuwataka wale wanaomzuia kumuachilia (haijalishi walikuwa ni wazazi au mume). Katiba yetu inapotoa haki ya kupata na kutoa maoni haisemi wazazi wana uwezo wa kuingilia haki hiyo!

Leo watu wanaibuka ati "wanamtetea Amina". Eti wanadai sisi ndio tuliokufa... hapana ni sisi tulio hai ndio tumefumba macho na kutokupiga kelele zetu kwa pamoja na kulazimisha Amina apatiwe kile anachostahili kama mwanadamu na kama raia.. ni sisi ambao mikono ya kutushtaki itaelekezwa kwetu, ni sisi ambao hatuna budi kuinamisha vichwa vyetu kwa haya kwa kushindwa kumtetea alipokuwa hai!!!

Kwa wengi, ilikuwa ni kama igizo la kigiriki ambalo mwisho wake is always ni tragedy!!
 
Mzee Mwanakijiji,

Usiwanyoshee vidole wenzako. Walau huyu jamaa Muhingo amekuwa rafiki na mtetezi wa Amina toka yuko High School wakati Amina sio almaarufu. Wewe umeanza kwa "mtetezi wake" toka alivyofungiwa ndani na babake na kukatazwa kuongea - wiki kadhaa zilizopita, umeanza kumshikia bango toka ameanza kuwa "news item". Kwa maana hiyo, wewe mnafki mkubwa kuliko mtu kama Muhingo.
 
Huyu Muhingo Rweyemamu ni mwandishi wa hadithi za similizi na mtunzi wa ngonjera.
Kayafupisha maisha ya marehemu kama kwamba ni maisha ya inzi asojua pa kutua.
Leo anadiriki kusimama na kutoa lawama kwa baba mzazi wake marehemu kwa sababu dhana yake imelenga depression.
Sasa sisi tunakwambia kuwa Amina hakuwa na depression kabisa kwani talaka za namna hii kesha zipata toka kwa mumewe wala sii mara moja. kwa hiyo tupe sababu nyingine ambayo inaweza kusababisha depression ikiwa marehemu alikuwa ktk nafasi nzuri na kubwa zaidi ktk uhai wake.
Na imekuwaje swala la kuchukua form za kugombea uenyekiti wa CCM vijana hukumpa ushauri?...bali unasimulia tu kwamba marehemu alifikiri mumewe alitoa talaka kwa ushauri wa mwenyekiti wa UVCCM....Ni wakati gani marehemu aliweza kusema hivyo?

Na mwisho ikiwa kweli ulikuwa mshauri wa marehemu alipoanza uhusiano wake na Mkapanjia, nashindwa kuelewa:[
1. Ulikuwa wapi alipokuwa na matatizo ya kuvunjika ndoa hiyo.
2. Ulikuwa wapi ktk ushauri alipochukua form za kugombea UVCCM na hata kukataliwa na mwenyekiti UVCCM kumuunga mkono hali wengi tunafahamu uhusiano wako na mwenyekiti huyo?..Wewe umejua vipi kuwa mwenyekiti huyu alikataa kumuunga mkono marehemu..urafiki pia na mwenyekiti au sio?
3. na iweje marehemu bila baraka za mwenyekiti wake azushiwe tena kutembea nje ya ndoa wakati marehemu alipochukua form za kugombea kinyume cha matakwa ya mwenyekiti wake....
Acha Unafiki, unafiki unao wewe mwenyewe kwa kuonyesha huruma ambazo zimetanda sumu mbaya ya kulipaka tope jina la marehemu na familia yake. Ikiwa kweli wewe mkweli na sio mnafiki basi kubali kuwepo na uchunguzi wa kitaalam ktk mwili wa marehemu. Hayo ya daktari fulani toka Penn States hayana msaada wowote ikiwa ushahidi wa karibu ni maiti iliyolala Iringa.
 
My dear mugongo..it counts most when people need you the most...! Wakati watu wako kwenye matatizo na shida.. na hasa pale ambapo haki zao zinanyimwa au kubanwa kitakachokumbukwa siyo maneno ya adui zetu bali ukimya wa rafiki zetu. Na zaidi ya yote kitachothaminiwa ni ukarimu wa wageni. Kuna wale wanaomtetea kwa vile wanamjua na wengine tunamtetea kwa vila hatumjui... rafiki anahaki ya kutetea na kusimama upande wako.. lakini usiyemjua anapokutetea.. ndio maana mtu alisema ni lipi lililo rahisi, kufa kwa ajili ya ndugu yako au kufa kwa ajili ya mtu usiyemjua?
 
My dear mugongo..it counts most when people need you the most...! Wakati watu wako kwenye matatizo na shida.. na hasa pale ambapo haki zao zinanyimwa au kubanwa kitakachokumbukwa siyo maneno ya adui zetu bali ukimya wa rafiki zetu. Na zaidi ya yote kitachothaminiwa ni ukarimu wa wageni. Kuna wale wanaomtetea kwa vile wanamjua na wengine tunamtetea kwa vila hatumjui... rafiki anahaki ya kutetea na kusimama upande wako.. lakini usiyemjua anapokutetea.. ndio maana mtu alisema ni lipi lililo rahisi, kufa kwa ajili ya ndugu yako au kufa kwa ajili ya mtu usiyemjua?

Hapa the order of things matters. Amina amekuwa na misukosuko tangu amevunja ungo...Muhingo, as collaborated by Kibanda, anasema wamekuwa marafiki na mshauri wake toka miaka ya 1990, na ndio waliomsaidia kupangua noma za kufukuzwa shule, n.k. Ndiye aliyempa siri yake ya kuamua kuichukuwa agenda ya madawa ya kulevya, n.k.

Wewe, as far as I have followed your coverage, umeanza kuona Amina ni mtu wa kutunzwa na kutetewa pale alipofungiwa na babake (immediately kabla ya hapo, skandali ya Zitto ilipo-break, wewe ulikuwa upande wa Zitto).

This is just fine. What is wrong ni kuwashutumu wenzako walikuwa wapi, kisa wewe ulienda photshop ukatengeneza fulana za Free Amina Now. Wenzako hawa wanakwambia walikuwa naye toka miaka ya tisini wakati akiwa na misukosuko mingine...wewe unasema "wanajifanya watetezi wa Amina". Wewe unataka ku-monopolise huu "utetezi" peke yako?
 
Mugongo Mugongo,
Tafajali njomba tafajaliiiii... rudisha chipudu hichooo!

Choo mjomba kuandika vitu kama hivi wakati sisi tunakupa heshima hapa, nakuomba sana usitake kutumiwa kama mtumwa wa mawazo. Wewe mtu mzima na mchango wako muhimu sana hapa. Humjui marehemu zaidi ya kusimuliwa ama ushabiki wako na maisha yake marehemu hayakuhusu wala kumhusu mtu.
Huyo mnafiki wako anatumiwa kuondoa dosari zote za kesi hii. Amina hakupewa majina na watu anaodai Rweyemamu....hata ushauri anaodai kumpa marehemu haukufanya kazi na pengine ndio ulo mfukuzisha shule.

Rweyemamu kamjua marehemu kupitia kwa Mkapanjia, tunafahamu vijana wa mjini na tunafahamu pia urafiki wake na mwenyekiti wa UVCCM kwa hiyo msilete za kuleta hapa!...

Kifupi mnavyozidi kujitetea ndio mnadhihirisha kuhusika kwenu ktk swala hili.
 
Mkandara

Wewe si ndiye ulileta habari hapa JF kwamba JK kaenda kumuona Amina hospitali mchana wa siku aliyokufa? Kumbe JK siku hiyo na iliyopita alikuwa Tanga. Au siye wewe? Ni kama vile unanunua kitabu, uko excited, baada ya kurasa ya nane unaona an obvious factual error. You are deflated, and you put the book down.

Iweje leo nikuamini unaposema Rweyemamu kamjua Amina kupitia Mpakanjia. Does it matter kama kamjua hivyo anyway.
 
Mugongo once again you are wrong.. nainaonekana ni jinsi hukuangalia nilichoanza kuandika wakati sakata hili lilipoanza. Sijawahi kuwa upande wa Zitto au upande wa Amina! Nenda ukasome ni kitu gani nilichokuta nakitetea. Hata kwenye suala zima la Amina sikuwa namtetea kama Amina... au nilipokuwa natetea Zitto asilazimishwe kusema kama hataki kusema sikuwa na mtetea Zitto kama Zitto (ingawa baadhi ya watu humu hawakuelewa).

Kama utachukua muda kusoma.. utaona nilikuwa natetea nini hasa na ni kitu gani sikuwa natetea...
 
Mugongo Mugongo,
Prove me wrong!.... kuwa JK hakwenda mtembelea marehemu akiwa hai ktk siku nilosema. Tanga kuna umbali gani au mwenyekiti UVCCM ndio kakupa hili pia?... muulize huyo mwandishi wako alimjua vipi marehemu!
Yes it matters soma tena maelezo yake ukizingatia kwamba Mkapanjia ndiye kiungo cha urafiki anaodai yeye.
 
....guyz inatosha sasa. Hakuna anayeweza kuwa na uchungu na Amina zaidi ya Mama na Baba yake. Wenyewe wameamua kulimaliza suala hili. Naamini basi ni vizuri na sisi tukaishia hapa.
 
JokaKuu... wakati mwingine mama na baba ndio wahusika katika vifo vya watoto wao.. sasa tuwaachie tu kwa vile watu wanamwaga machozi? Ina maana kuanzia leo kwa vile wazazi watasema "ni mapenzi ya Mungu" basi polisi wasifanye kazi zao au watu wasitake uchunguzi?
 
Jokakuu,
nadhani hapo nyuma watu wengi tumeacha kabisa kuzungumzia maisha ya marehemu. Mada ilikuwa buriani na kweli wengi walianza kutazama nje ya marehemu mwenyewe.
Binafsi sioni ubaya kuzungumzia hoja zinazohuziana na kifo chake bila kuyaweka maisha ya marehemu ktk banda la kumchambua.
Huyu Mugongo Mugongo katokea na hizi habari za Tumaini, kuanza kusema marehemu alikuwa hivi ama vile kabla hata hajavunja ungo....damn!..maneno kibao ili mradi kuonyesha kuwa marehemu na familia yake ndio wa kulaumiwa.
Mimi nataka kumwambia tu kwamba tupo watu tunaofahamu vizuri maisha ya Mumewe, marafiki zake na upuuzi wote wanaotaka kutumia dhidi ya marehemu na familia yake ili kufumba maovu ya marafiki zao.
Huyu mwenyekiti mwenyewe kaombewa ruksa ya kwenda toa Pole na watu wa juu laa sivyo asingekanyaga kabisa msibani!... msitufanye hamnazo tunapata data kama mnavyozipata.
 
Back
Top Bottom