Wakati tunaendela na matanga ya dada yetu Amina nadhani itakuwa busara vilevile kujitayarisha na matanga ya ndugu yetu mugongomugongo.
Nimekuwa nikifuatilia mambo yake humu. Mwanzoni nilidhani ndio wale kina Muhingo walioamua kujipa kazi maalumu ya kutetea wenye nchi na kuwavua nguo wale wote wanao onyesha kuwavua nguo mabosi wao katika ulaji.
Lakini sasa ninakuwa na wasiwasi kuwa huyu jamaa amekumbwa na matatizo ya kisaikolojia. Ukifuatilia mwenendo wa uchangiaji wake humu utagundua kuwa hakuna mahala ambapo ameongelea kingine zaid ya kujaribu kuonyesha jinsi gani wenzake walivyo na mapungufu.
Ukiondoa uwezekano wa kuwa anafanya kazi maalum ya kuzuia ushawishi wa baadhi ya wana forum hapa ambao wanaonekana wana mlengo wa kupingana na maslahi ya wenye nchi naamini kuwa vilevile anasumbuliwa na chuki na wivu mkubwa dhidi ya wengine.
Kwangu mimi ni kuwa huyu jamaa hana raha na maisha yake binafsi na zaidi anajiona valueless hivyo inakuwa vigumu kwake kuona wenzake wanaonyesha dalili za kupata umuhimu ama katika forum hii ama katika jamii ya Tanzania. Na hili analijua ndio maana hata siku moja hajibu maswali wala kurespond counter arguments ambazo wanaforum huzielekeza kwake kama majibu ya michango yake.
Hizi zote ni dalili za depression ambayo hupelekea katika kile ninachokiita vicious circle of self destruction na huko ndiko anakoelekea ndugu yetu mugongomugongo.
Mimi sio daktari wa darasa la muhimbili lakini darasa la mitaani limenifundisha mengi kiasi....
na tujiandae na matanga mengine..
Tanzanianjema
Tanzanianjema,
Matumizi yako ya maneno "matanga ya mugongo mugongo" siyo mazuri. Tumia lugha nyingine tafadhali.
Mugongo Mugongo,
Nimekuomba unithibitishie kuwa JK aliondoka Dar tarehe 25 na kulala huko hadi tarehe 26, iweke hiyo source yako usitake kuzungusha vitu, na kama kweli unavyosema basi naahidi kuiweka source ya habari yangu.
this is not from a "source", I saw it kwa macho yangu)
MugongoMugongo,
Wewe ulimwona Rais akiwasili Tanga June 25 na kulala pale hadi 26?....nipe source nimeuliza na kama huyo G.Baluan alikuwa ktk msafara mpe PM yangu!....mazungumzo yote kati yetu yaweke hapa wazi... Hilo la RTD mtu yeyote anaweza kusema. My source ni kubwa kuliko umri wako - JK kenda Lugalo mara mbili kumtazama AC safari ya kwanza alipolazwa na pili siku ya Jumanne.
Wee sema umeona msafara wa Rais wakirudi tarehe 27 sio vinginevyo.
MugongoMugongo,
Alikwenda kuhani baada ya sherehe za BBC?....na hizo sherehe zilifanyika saa ngapi vile!
Nipe huyo mwandishi kupitia PM au simu na mazungumzo kati yetu unaweza ya record, habari nyingine zote tisa... najua kama alikuwa kwenye msafara huo ndiye namhitaji....bado ni maneno yako mwenyewe toka mdomoni mwako ama magazeti ya Bongo.
Leo hii rasmi natangaza kuomba kadi ya Chadema!...
Mh. Freeman, Zitto, J.J.Mnyika, Mwanasisa naomba tuwasiliane!
Mkandara sina kuficha wala mpango wa kupitia mlango wa nyuma.Nataka kutiwa maji ya ubatizo..
Ila tu kumbukeni Mkandara nina sifa moja!.......BABU UBISHI!
Tupo pamoja 2010!