Mtu kama Liberata Mulamula ambaye amekuzidi kila kitu kuanzia Elimu ,umri , uzoefu na Exposure , halafu utegemee aje kukusifu kama Chawa haiwezekani !

Mtu kama Liberata Mulamula ambaye amekuzidi kila kitu kuanzia Elimu ,umri , uzoefu na Exposure , halafu utegemee aje kukusifu kama Chawa haiwezekani !

Dah,Nakumbuka Kabudi alipopigwa chini na kupewa huyu Mama hiyo wizara mapambio yalikuwa mengi humu!!!
 
Maadili ya Mtanzania ni kufichua UFISADI wa Mama sio other way around.
 
Miaka mingi iliyopita nilikuwa nimeanza kufanya kazi katika moja ya mabenki makubwa ya Wall Street, New York City.

Katika kujitambulisha, nikasema kuwa mimi ni mzaliwa wa Tanzania.

Kuna mkurugenzi mmoja alivyosikia hivyo tu, akaniuliza kama namjua mtu mmoja anaitwa Liberata Mulamula. Nilikuwa simjui. Akawa anamsifia sana. Hapo ndipo nilipopata kujua hilo jina.

Baadaye nikajua alikuwa anafanya kazi Wizara ya Mambo ya Nje, akaja kuwa balozi na waziri.

Ila Mulamula Wamarekani walimkubali sana katika kazi zake. Alijua kuishi nao.

Sasa sijui kumetokea nini huko nyumbani, kwanza kuna uthibitisho kuwa jiwe lililorushwa gizani karushiwa yeye?

Maana siku hizi tunakwenda kwa uongozi wa mipasho ni vigumu hata kujua nani kakusudiwa.
Mkuu umefanya kazi wall street??
 
Mtu kama Liberata Mulamula ambaye amekuzidi kila kitu kuanzia Elimu ,umri , uzoefu na Exposure , halafu utegemee aje kukusifu kama Chawa haiwezekani .

Utalalamika Sana na nakuona upo katika Panic Mode .

MTU unajua kabisa ametumia zaidi ya nusu ya maisha yake kufanya siasa za kutumia akili na ni-mwanadiplomasia wa kimataifa , eti Leo hii unamleta Tanzania akae na Chawa awe anasifu na kuabudu , hiyo haiwezekani.

Utalalamika Sana safari hii Ila huo ndo ukweli.
Ndiyo upumbavu wa CCM
 
Ina maana lijitu linalopigwa vijembe na maza ni li Liberata Mulamula? Ndiyo lipuliza kipenga (li whistle blower) lizalendo lililovujisha mafaili ya ufisadi kule kwa dada wa taifa ama? 😏

Kama li Liberata Mulamula lipo hapa nchini basi likae chonjo aisee maana linaweza kuokotwa msituni likiwa limepigwa nyang'anyang'a!
 
Kuna siku Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Marehemu Dr. Mahiga alikuwa kaja New York City, kwenye mambo yao ya vikao vya Umoja wa Mataifa nafikiri.

Sasa katikati ya safari yake hiyo, akawa kasikia naibu waziri wake katumbuliwa na jiwe.

Yani Waziri yupo katikati ya vikao vya Umoja wa Mataifa New York City, huku nyumbani rais kamtumbua Naibu Waziri, halafu Waziri anapata habari mitandaoni kama watu wengine. Ilikuwa katikati ya safari New York. Ikabidi Waziri amuombe dereva apaki gari pembeni ya barabara kidogo maana habari ilikuwa kubwa sana.

Yani kuanzia pale Waziri hata ku concentrate kwenye vikao ikawa akili nusu iko nyumbani akifikiria wizara inaendaje.Inaonekana waziri alistuka sana.

Kama unavyosema, uongozi wa Tanzania inawezekana ukionekana hujamsifia sana rais tu ijawa kosa la kukuondoa ofisini.
Ila Kiranga we ni muhaya? Samahani lakini, nauliza tu usinichambe jamani
 
Ila Kiranga we ni muhaya? Samahani lakini, nauliza tu usinichambe jamani
Sina tabia ya kuendekeza hoja za ukabila.

Wewe kama masikini mjinga hata nikipiga chafya kwa reflex action utaona napiga chafya kwa kujivuna.

Hata nikikutajia kabila na ukoo wangu utasema najivuna.
 
Nikuulize swali moja tu ndugu yangu: "Sote twajua Fr Kitima ameshambuliwa na kuumizwa vibaya na wasiojulikana. Mfariji na Amiri Jeshi Mkuu anasema kuwa Fr Kitima kajitakia mwenyewe". How do you feel to be proud na Rais wa namna hiyo???

Alidhani nchi itatulizwa kwa mabunduki pamoja na rushwa ya vyeo na fedha. Nchi huwa na utulivu pale raia wake wanapokuwa na furaha hasa wanapoona Utu na Haki ikitendeka kwenye nchi yao.

Hayo unayoyasema yangekuwa na maana endapo tu Rais alikuwa akitenda mema kwa raia wake, jambo lilowapelekea Mataifa mengine wakasirike. Hapo tungeungana pamoja kumtetea.
Kwani nchi haijatulia hii?
 
Huo uzalendo mnaotaka awe nao ni upi?Kufichua uovu ni kukosa uzalendo tuachane na hiyo mbn hajasema chochote anasema uzalendo?Bora tu angeipotezea hii issue
 
Mbona kama tone ni mwenyewe kabisa Libe!. Kama ndiye, why analalamika bila kusema alichokuwa anashea na wazungu wake hadi mama akamtumbua. Uzalendo ni muhimu kuliko machuki haya yasiyo na maana. Hata kama humpendi Rais wa nchi, yeye ni alama yetu kwa sasa, anastahili heshima kwa nafasi yake

We kilaza sana
 
Mkuu,

Tanzania tumekosea step hapa kati tu.

Huko nyuma Nyerere akisema dunia nzima inasikiliza. Nyerere alikuwa anabishana na Ronald Reagan kama marais sawa.

In fact si Nyerere tu, Salim Ahmed Salim ilikuwa bado kidogo awe Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Wamarekani wakamuwekea zengwe la Veto.

Uchina mpaka kesho ukiwatajia Salim Ahmed Salim wanamuheshimu sana.Alifanya kazi kubwa sana kurudisha kiti cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa cha China kwenda China mainland kutoka Taiwan.

Yani mpaka hawa kina Dr. Mahiga walikuwa wanaheshimika sana nje.

Tumejiachia hapa kati tu.
Nakumbuka nime wahi kusoma Ile barua ya vitisho aliyo tumiwa, he was a true version ya kiongozi mwenye malengo na maono.
 
Back
Top Bottom