Nyuma ya Pazia la kila Biashara kuna mambo mengi ya kujifunza

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,529
Habari za wakati huu;

Nikiwa na umri mchanga kwa sera za kitanzania nilikuwa na kiu kubwa sana ya kumiliki biashara na kuwa mfanya biashara mkubwa.Kipindi hicho internet ilikuwa adimu sana na kompyuta nazo zilikuwa adimu sana.Zilikuwa ni zama Pentium 1 na 2 na internet cafes ambazo zilikuwa zinatumia TimeWatcher.Zilikuwa ni zama za Floppy Disk.

Bahati mbaya shule nilizosoma hazikuwa na somo la kompyuta kabisa ingawa shule moja ilikuwa na chumba cha computer kilichokuwa na computer za msaada kutoka nje ya nchi ambazo zote zilikuwa Mbovu na hakukuwa na mtaalamu wa kuzitengeneza wala mwalimu wa kufundisha kwani zilikuwa zama za Typewriter.Zilikuwa ni enzi ambazo mitandao ya kijamii iliuwa inaitwa myspace na mingine ilikuwa hapa bongo kama darhotwire.Kipindi hicho JF ilikuwa haijwa wazo kicwani kwa Melo na Mushi.

Exposure yangu ya Computer ilikuwa ni katika kuomba kwenda kusafisha Maabara ya Computer ambapo nilikuwa najaribu kuziwasha kuzifungua ili kukagua ndani kuna nini.Real computer nimekutana nayo ilikuwa ni P2 nafikiri ambapo kitu cha kwanza nilijifunza ni kutengeneza html code ya marquee(Scrolling text) hadi leo ninapofundisha watoto wangu kutumia computer huwa naanza ni hio code ya html.Ilikuwa ni miaka mingi ila sio Mingi sana.

Lengo la uzi huu sio kuzungumzi hilo ila nataka ujue ilikuwa ni miaka mingi kiasi.Kipindi hiki ukitaka kusajili kampuni ilibidi uende mpaka Dar es Salaam,hata jina la biashara tu ilibidi uende mpaka Dar es salaam pale kwenye JENGO la ushirika.Nakumbuka sana lile JENGO lilikuwa na LIFT mbovu ambayo wakati wa kupanda na kushuka kulikuwa na mtu amaye ameajiri kwa ajili ya kuendesha LIFT ile na kiti chake so anawahesabu mkiwa wnegi au wanene anawapunguza.Pale BRELA palikuwa panatmbea karatasi tu na ukiwa na mkono mrefu basi kila kitu kinaenda fasta.Kilikuwa ni kipindi ambacho hakukuwa na internet banking na maofisi mengi ya serikali Computer zilikuwa zianfunikwa na shuka ofisi kila kitu ni makaratasi.ilikuwa ni miaka mingi sana.Kilikuwa ni kipindi ambacho matokeo ya sekondari yanatangazwa kwenye magazeti.Kipindi hiki kuna benki chache sana mojawapo ikiitwa sijui meridian nini sijui.

Kama nilivoeleza nilitaka na biashara.SIKUWA na mtaji wala namna ya kupata mtaji na nilikuwa kijana mdogo kwa vigezo vya kitanzania mabapo watoto tunaenda mpaka 40 plus tukiwa bado tunaitwa madogo.Basi nikafunga safari kwenda Dar es Salaam nikasajili Biashara yangu ya kwanza,Ilinichukua mwezi mzima,Nilitalii sana Dar es Salaam,nikafika mpaka Mikadi,nikafika Coco,Nikafika katika viwanja vizuri vya Dar kule Kinondoni na SINZA.Nilitembelea hadi ITV kujua bei za kuweka matangazo ya BIASHARA na RATE CARD nikapewa(Nilikuwa na lengo kubwa kibiashara) ila sikuwa na mtaji.Nilitembelea HOSTEL za Mabibo,nilifika Chuo Kikuu cha Darslam,nilifika mpaka MUHAS,ustawi wa Jamii,Mwalimu Nyerere.Nakumbuka kabisa nilikuja Dar es Salaam na Basi la Scandinavia na kwa kweli ilikuwa ni furaha kutalii JIJI na kufika hadi Msasani Club.

Niliutumia ule mwezi mzima wa kusubiri majibu ya BRELA kufanya utafiti katika JIJI na kulitalii na kwa kweli niliona mengi na kujifunza mengi.Sehemu pekee ambayo sikufika na mpaka leo sijafika zaidi ya kupita njia ni MBURAHATI.Nilikuwa kibiashara zaidi.Nilikuwa na simu Motorola nafikiri,Nilikuwa na Business cards na Barua za utambulisho kampuni yangu mpya ambayo nilikuwa naitambulisha kila mahali na mimi nikiwa kama mkurugenzi wake.

Baada ya kusajili kampuni nilifungua akaunti benki ya kampuni na akaunti benki nyingine ya Binafsi.Kisha nikajiandikia Cheki ya kwanza kutoka akaunti ya kampuni kuja akaunti yangu bianfsi ya Benki nyingine ili nione raha ya CHEKI.Baada ya muamala kusoma kwenye akaunti yangu Mpya basi nilifungua akaunti za Kampuni kwenye Benki nyingi ikiwamo Barclays,Stanbic n.k. Nilikuwa na Vitabu 4 vya Cheki vya benki kwenye makazi yangu.Nilikuwa ni mkurugenzi wa kampuni nikiwa na umri mdogo kwa hesabu za kitanzanzia.Nilifika hadi TRA nikapewa TIN number na makadirio ya kodi.

Najua kuna anayejiuliza nilikuwa napata wapi PESA za kugharamikia hayo yote.UKWELI ni kwamba nilikuwa tayari nimeanza kazi binafsi.NILIKUWA MWALIMU WA TUISHENI.Ndio nilkuwa nafundishi TUISHENI MASOMO YOTE SEKONDARI NA MSINGI,QT NA WANAORUDIA.Nlikuwa najiamini sana hasa baada ya kupata bahati ya kwenda nje ya nchi na kupewa zawaid ya vitabu ambavyo nilikuwa navisoma sana.Wanafuzni walipenda mtindo wangu wa kufundisha Kuanzia saa moja Asubuhi mpaka saa 3 Usiku Jumatata mpaka Jumamosi huku nkiwa nakunywa GLUCOSE kila baada ya Masaa Mawili ili UBONGO Usichoke.Kwa viwango vya elimu ya wakati ule nilikuwa TOFAUTI na wazazi na wanafunzi wali nishangaa.SO PESA ILIKUWEPO KIDOGO na JUKUMU langu kubwa lilikuwa ni kununua KUKU MNAFU na UGALI MCHANA kwa ajili yangu.

Sasa nirudi kwenye MADA inayohusu Mabenki.Kila nilipopata PESA kidogo nilipeleka kwenye Benki zote kulingana na muda kiasi nikawa nimezoeleka kwenye Benki kama Mkurugenzi wa Kampuni,kijana mdogo ambaye kila wiki niliuwa napeleka around 70,000 hadi 300,000 kwenye benki tofauti.Wakanizoea na kunipenda kama mteja wao.Nikawa naalikwa kwenye matukio ya benki na kufahamiana kiasi na mameneja wa benki kama mmoja wa wteja ambaye nilikuwa mfatiliaji mzuri.Nillipenda sana kutumia ATM kiasi kwamba nilikuwa nadeposit hela yangu asubuhi kisha jioni naenda kuitoa hapo kidgo tu ilimradi niende kwenye ATM.Nilihonga mabinti kwa kutumia cheki na kuwafundisha jinsi ya kwenda kuchukua pesa benki kwa kutumia cheki zao.Wengine niliwapa kazi ya kwenda kudeposit pesa zangu kwenye akaunti zangu.Nilikuwa naandika Cheki hadi za miezi sita mbele inaitwa POST dated Cheque.

Katika kipindi chote hiki nilijifunza mambo mengi zaidi kuliko niliyojifunza katika masomo yangu.Nilianzisha project nyingi sana na nikawa natembelea vyuo na taasisi za elimu na ofisi za serikali kutaka wanipe fursa nianzisha services tofauti kama vile elimu kwa nia ya mtandao,maonesho ya biashara,mifumo tofauti ya cerification ya wanataaluma,Vocational education n.k.Kilikuwa ni kipindi ambacho niliambiwa kwamba mimi bado ni kijana mdogo nisome kwanza kisha niingie kwenye hizo shughuli baada ya shule.Kilikuwa ni kipindi cha Practical ya elimu.

NILIFIKA hadi BUNGENI kwa ajili ya kupeleka na maombi ya mabadiliko ya sheria flani flani.Kwa kipindi kile sikujua kuwa nilikuwa nawaza mambo makubwa na wala sikubahatika kuwa na mentor ambaye angenipa moyo na ushauri kwani nilikutana na watu ambao waliamini haiwezekani,siwezi sitaweza.Nilikuwa na mwanasheria wangu(SIKUWAHI kumlipa ila aliniandkia AFFIDAVIT of BIRTH maana sikuwa na cheti cha kuzaliwa) nilikuwa na mhasibu wangu PIA lakini nao walihisi kwamba ni damu tu ilikuwa inachemka.Hawakuweza kunipa mwongozo.

Pamoja na hayo yote nilitambua kwamba katika biashara kila uachokiona kama bidhaa au huduma kamili hupitia mchakato mrefu mpaka kuwa hivyo.Watu huumia moyo na nafsi.Wat hupata hasara na wengine humwaga amchozi katika kufikia malengo yao.Hakunaga mafanikio ambayo hayana changamoto lakini ni lazima mjasiriamali achukue safari yake ya ujasiriamali kama sehemu ya kujifunza na kupata uzoefu kwani uzoefu uanopata utakupa nguvu na ujasiri zaidi.

Changamoto unazopata sasa hivi zinaweza kuja kuwa sehemu ya simulizi zako za ushindi huko mbeleni.
 
Mkuu samahani lakini; nahisi hi story umetunga, sio ya kweli. Kilicho nipelekea kudhani hivyo ni matukio yako yafuatayo:-
1. Bank ya Meridian biyao ulio inukuu ni ya mwanzoni mwa miaka ya 90, ilianzia pale Sukari house na ikafungwa. Hakukua na simu za mkononi
2. Computer zimeanza kutumika kwa baadhi ya taasisi hasa za fedha nadhani katikati ya miaka ya 90, kipindi hiki pia ndio simu za mkononi zilianza kwa mbaali kuwepo, mobitel na Tritel na wewe umesema ulikua unatumia Motolola, fine and very good, now kitendo cha kulitaja basi la Scandinavia ambalo miaka hiyo lilikua ni Iringa Dar na Mbeya Dar nadhani, hiyo mikoa simu za mkononi kwa miaka hiyo hazikuwepo and hence kua simu kwa mikoa hiyo was wastage of money, hapa umetupiga. Hata vocha zilikua zinafatwa ofisini kwao Dar
3. Again kuna hi issue ya wewe kupata mtaji kwamba ulipata kupitia tuition za QT; i am very sorry again here; hivi haka kamfumo ka QT ka miaka 2 kwa O level na mwaka 1 kwa A level na kenyewe sio kameanza mwanzoni mwa miaka ya 2000 kweli? Kipindi hiki computer zilikua bwelele na simu za mkononi ndio zilianza kua nyingi hasa ujio wa Celtel/Zain na sasa Airtel and Vodacom; na hata mfumo wa flobby ni kama ulikua umeanza kupotea, zilianza CD.

Anyway kama story yako ni ya kweli then hongera kwa ubunifu, hongera kwa uvumilivu, story yako inafundisha
 
Mkuu samahani lakini; nahisi hi story umetunga, sio ya kweli. Kilicho nipelekea kudhani hivyo ni matukio yako yafuatayo:-
1. Bank ya Meridian biyao ulio inukuu ni ya mwanzoni mwa miaka ya 90, ilianzia pale Sukari house na ikafungwa. Hakukua na simu za mkononi
2. Computer zimeanza kutumika kwa baadhi ya taasisi hasa za fedha nadhani katikati ya miaka ya 90, kipindi hiki pia ndio simu za mkononi zilianza kwa mbaali kuwepo, mobitel na Tritel na wewe umesema ulikua unatumia Motolola, fine and very good, now kitendo cha kulitaja basi la Scandinavia ambalo miaka hiyo lilikua ni Iringa Dar na Mbeya Dar nadhani, hiyo mikoa simu za mkononi kwa miaka hiyo hazikuwepo.
3. Again kuna hi issue ya wewe kupata mtaji kwamba ulipata kupitia tuition za QT; i am very sorry again here; hivi haka kamfumo ka QT ka miaka 2 kwa O level na mwaka 1 kwa A level na kenyewe sio kameanza mwanzoni mwa miaka ya 2000 kweli? Kipindi hiki computer zilikua bwelele na simu za mkononi ndio zilianza kua nyingi hasa ujio wa Celtel/Zain na sasa Airtel; na hata mfumo wa flobby ni kama ulikua umeanza kupotea, zilianza CD.

Anyway kama story yako ni ya kweli then hongera kwa ubunifu, hongera kwa uvumilivu, story yako inafundisha
Good observation,Meridian ilikuja kuwa chini ya Stanbic Bank,Simu zilianza kuwepo end of 90s mpaka early 2000,kuna mambo nimeweka hapo kwa ajili ya kunogesha lakini kuna either 10% ya ya fiction au 10% ya truth ila ujumbe wa msingi upo humo ndani.
 
Back
Top Bottom