Nadhani ni vema mtu ufanye sacrifice bila kulazimishwa wala bila kutegemea kurudishiwa.., yaani sio kwamba sababu yeye aliangalia mpira na mimi, basi ni lazima nimsindikize shopping ya viatu..., Ndio maana nikasema mkiwa marafiki na wapenzi basi mtapenda kufanya kila kitu bila kulazimishana yaani ile company tu inakuwa furaha tosha,
Pia kuna suala la compatibility kama mnazo hobbies hata chache ambazo zipo sawa safari yenu itakuwa nzuri zaidi ingawa hata kama hamna hobbies mnaweza mkajifunza hobbies mpya ambazo zitawafurahisha nyote na zile chache za wewe kupenda kabia, na kuangalia mpira au shopping ya viatu kila mtu anaweza akawa anafanya kwa muda wake na marafiki zake, nyie mnakutana tu kwenye yale ambayo nyote mnayapenda...,