Mtikila akamatwa na polisi kwa kumkashifu Rais

Mtikila amepatia sana kumwita huyu Kikwete muhuni na gaidi,na ndio jina analostahili...kuachia mabilioni ya BOT yanapotea huku wewe tumekuchagua usimamie nchi kuna uhuni zaidi ya huo,angalia mikataba ya kuuza nchi ambayo tumeipitia yote hapa kama Buzwagi na Richmond...hivi mnajua kwa vitu hivyo vitatu tuu tumepoteza pesa kiasi gani? ameshindwa hata kusimamia idara za serikali kama TRA ambazo zinaendeleza uhuni kwa wananchi? ni muhuni tuu na gaidi wa mali ya umma na hana maana kabisa sijui mnapulizia nini hapa wakati mnajifanya mna hasira za mikataba waliyotuingiza hawa wahuni...unafiki unafiki mpaka kiama na msahau maendeleo kaqma hamuoni huyu jamaa ni muhuni tena tapeli.
 
Nafikiri kwa ufupi Mwanakijiji anamaanisha kwamba ili vyama hivyo husika viweze kuungana si lazima vifanane kiitikadi na kifalsafa top bottom na ndio maana akatumia neno "msingi"kwasababu msingi ndio unaodefine lengo,na malengo ya falsafa na itikadi za DP yanaweza yakawa na utofauti mkubwa na vyama hivyo vilivyoungana.Ni wazi kwmba ili muweze kuungana ni lazima muwe na mambo mengi mnayokubaliana kuliko yale msiyokubaliana.Na pia ni kweli mtikila ana wivu mbaya,wivu ni nature ya ubinadamu lakini ukiwa ni wivu mbaya then haijalishi kuwa mwenzako anasema nini ama anafanya nini!hautakubaliana na wenzako kama hauna maslahi binafsi kuhusiana na mafanikio hayo,huo ndio wivu mbaya!
 
Big Up Mtikila.....kila Mtu Ana Style Yake Ya Mapambano....ya Mtikila Ni Mahakamani...kaza Buti.
 
Mkuu graph ya umaarufu wa Mtikila ishafika peak, kwenye uchumi kuna "law of diminishing return" hiyo ndio ina apply kwa mtikila kilichopo sasa umaarufu wake utakuwa una increase at decreasing rate, atakuwa anafanya kosa kubwa kama anadhani kwa mtindo huu atapata umaarufu.

NI KWELI USEMAYO ILA TOPIC INAWEZA IKAWA TOO HOT KUIGNORE THE FACT KWAMBA JINA LAKE LITAKUWA LIKIANDAMANA NA MTAFARUKU WOWOTE UTAKAOSABABISHWA NA HIZO ISSUE ALIZOZIIBUA ZA WAISLAMU,SERIKALI,NA MAHAKAMA YA KADHI.KAMA MALUMBANO YA MAHAKAMA YA KADHI KATI YA WAISLAMU NA WAKRISTO YATAENDELEA KUWEPO THEN NI RAHISI SANA KUONA JINA LA MTIKILA LIKIAMBATANA NA HABARI HIZO MARA KWA MARA!
 
Hudhani, huna uhakika. Je Mtikila yuko juu ya sheria ( au pia hudhani / huna uhakika)

"SIDHANI NA SINA UHAKIKA KAMA PUNDAMILIA NI MWEUPE MWENYE MABAKA MEUSII AMA NI MWEUSI MWENYE MABAKA MEUPE!"
ACHILIA MBALI MALUMBANO MAANA YANGU HALISI NI VERY OBVIOUS;NILIPOSEMA SINA UHAKIKA AMA NADHANI NILIMAANISHA KUWA NI MAHAKAMA PEKEE "KWA KUTAFSIRI SHERIA ZILIZOWEKWA"YENYE UWEZO WA KUAMUA KAMA AMEVUNJA SHERIA AMA LA,SIWEZI KUWA 100%SURE KWAMBA HAJAVUNJA SHERIA KWASABABU SIJAUONA USHAHIDI UTAKAOTUMIWA NA WAENDESHA MASHTAKA,ILA BASED ON WHAT WE ALL KNOW THA ALIONGEA MBOVU BADO SIDHANI NA SINA UHAKIKA KWA ASILIMIA 100% KWAMBA NI VIELELEZO TOSHA VYA KUMSWEKA NDANI MAISHA YAKE YOTE.HUNA HABARI KWAMBA KESI KAMA HIYO YA UCHOCHEZI ILIYOFUNGULIWA DHIDHI YA MREMA NA TUNDU LISU IKO HATARINI KUFUTWA?
 
Kama nilivyoikwisha sema huko nyuma hili swala la kadhi linatakiwa kujibiwa kwa hoja peke yake na sio Imani za watu ktk dini. Nina hakika wale wote wanaopinga ombi hili la waislaam hawakuwa na sababu za msingi ila ni maneno ya watu kama Mtikila ambayo hauna mantiki hata kidogo. Hakuna sheria iliyokwisha kuwa imposed on us ila imeombwa na swala hili linatazamwa.

Sheria yoyote nchini hutumika kulingana na mazingira ya wananchi wake na sio imani za dini zao, unless dini hiyo ndio imejenga msingi wa taifa hilo. Waislaam wanataka korti hizi bila kufiikiria mazingira yetu na hasa ukweli kuwa tamaduni zetu zinatumika zaidi kuliko hata dini zetu ktk maswala mengi ya kijamii. Na mfano mkubwa niliotoa ni huo wa ndoa zetu kutochagua dini ya mtu, watoto kuzaliwa nje ya ndoa yote haya yanapingana na mafundisho ya dini ya kiislaam. Nina hakika waislaam hawawezi kabisa kuepuka gonjwa hili na hadi hapo watakapo mafundisho kama hayo then tunaweza kufikiria sheria hii kwani itawahusu waumini hao, leo hii hawapo kwa hiyo sheria ita fail na upotezaji wa fedha na gharama za kuwalipa hawa mahakimu. Ni costs zaidi kutoka kwa wananchi walipa kodi..

Kwa hiyo serikali itakapo kubali kuundwa kwa korti ya kadhi ni kukaribisha matatizo mengine ya kijamii kwani hawakutaka kuangalia mila, Tamaduni na mazingira yanayotufanya sisi tuitwe WATANZANIA kwani sio Ukristu wala Uislaam uliojenga jina TANZANIA. Hizi ndizo sababu na sio Ujinga wa mtu kama Mtikila ambaye anadai kuwa ni mwanana siasa. No wonder tunazidi kuibiwa kwani hatuna viongozi wanaofahamu ku- raise motisha wa wananchi ila kutugawa makundi makundi.

Tutaheshimu mafundisho ya dini zote isipokuwa pale yanapohatarisha usalama wa Taifa letu iwe Mtikila ama hizo korti za kadhi.

Sielewi kwa nini swla hili limechukua mkondo huu mbaya wenye kila chuki na matusi ambayo hapa JF wenyewe kwa kauli zenu mumeweza kusema kuwa mwafrika wa kike alikosea aliposema kuhusu hulka ya JK. Tena kwa support kubwa mliweza kusema huyu binti amekosea na wala msije fikiria hiyo haki yake ya maoni. Huyu ni rais tu tena amechaguliwa kwa kura zenu hawezi kushika nafasi ya UUngu wala kukaribia utume wa Mungu lakini mpo tayari kumpa protection lakini sio waislaam. Leo kuna watu hapa wanaona Mtikila anayo haki ya kuzungumzia dini nyingine isomhusu kabisa ktk imani yake ama maisha yake ya kila siku.

Sometimes huwa nashindwa kabisa kuelewa jinsi watu hapa wanavyoweza kufikiri hasa inapofikia upande wa pili wa shilingi.

Nitarudia kuwakumbusha msemo wangu mmoja toka bcstimes....

Kila shilingi ina sura mbili, moja ni upande wa kichwa (head) ambao kamwe hauoneshi thamani ya fedha hiyo ila sura na viashirio vya Utawala husika. Ni upande wa pili (tail) pekee unaokupa thamani ya fedha hiyo lakini juu ya kusoma maandishi huwezi kujua thamani hiyo bila kuitumia fedha hiyo. Mfano One pound inasomeka kama 1 lakini inathamani ktk matumizi kuliko Dollar moja ama shilingi ya madafu (Tanzania)..

Hivyo basi kila unaposoma hoja ya mtu jaribuni sana kutazama vipengele hivi na mara nyingi utakuwa bingwa wa kukata issue ama kuelewa kilichowekwa mezani.
- Ahsanteni.
 
Kama nilivyoikwisha sema huko nyuma hili swala la kadhi linatakiwa kujibiwa kwa hoja peke yake na sio Imani za watu ktk dini. Nina hakika wale wote wanaopinga ombi hili la waislaam hawakuwa na sababu za msingi ila ni maneno ya watu kama Mtikila ambayo hauna mantiki hata kidogo. Hakuna sheria iliyokwisha kuwa imposed on us ila imeombwa na swala hili linatazamwa.


Mzee Mkandara, umenitangulia kidogo. Kuanzia kesho nina mfululizo wa makala mbili kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi. Makala hizo kimsingi zinajibu hoja za Mashehe Kadhaa ambao walizijenga kwenye kipindi cha Jenerali on Monday, wiki iliyopita. Katika makala yangu ninaonesha mambo kadhaa.

a. Kwanza hoja zinazotolewa hadi hivi sasa za kwanini Mahakama ya Kadhi ianzishwe nyingi kati ya hizo hazina msingi na ni rahisi kuonesha jinsi gani zina makosa. Na ninachambua hoja kubwa sita.

b. Pili naonesha ni hoja gani zinastahili kutolewa na kujengwa na ambazo kimsingi zinakubalika.

c. Tatu, ninaonesha ni jinsi gani Mahakama ya Kadhi ni haki ya Waislamu na inaweza kuanzishwa TAnzania na mambo matatu yakawa bado yanazingatiwa yaani, 1. inaridhisha matakwa ya waislamu, 2. Haivunji sheria au Katiba yoyote, 3. Haitishii kwa namna yoyote Wakristu au watu wasio waislamu, au waislamu wasiotaka kuwa chini ya uwezo (under its jurisdiction).

Binafsi sidhani kama kuna sababu yoyote ya msingi kwanini Mahakama ya Kadhi isianzishwe TAnzania na katika makala yangu ambayo niliimaliza kabla ya Mtikila kukamatwa niliandika hivi kuhusu Mtikila.

Nijinukuu "kesi iliyofunguliwa na Mch. Mtikila kuhusu kupinga uanzishwaji wa mahakama hiyo ni suala la kwake kama raia wa nchi hii. Isichukuliwe hata kidogo kuwa Mtikila anawakilisha Wakristu wa Tanzania katika kesi hii. Hivyo basi kauli zake zenye kuumiza hisia za Waislamu zichukuliwe kama ni kauli zake na zisichukuliwe kama ni maneno ya Wakristu dhidi ya ndugu zao waislamu. Na kama ilivyokawaida ya viongozi wetu wa Kikristu hakuna aliyetokea hadharani na kupinga kauli za Mtikila kuwa haziwakilishi mawazo au misimamo ya makanisa nchini. Ingekuwa jambo la kupendeza kusikia TEC, CCT, na Muungano wa Makanisa mengine kutoa kauli zao kupinga madai ya Mtikila kuwa kuanzishwa mahakama ya kadhi kutachochea Ugaidi na kuleta vurugu."

Nimekwepa kuandika mengi kwa sasa hadi makala hizo mbili zitoke Tanzania kwenye gazeti la "Kulikoni". Natumaini by the end of the day nitaweza kuweka sehemu ya kwanza hapa.
 
Jamani Tukubaliane Kitu Kimoja;once Upon A Time Afrika Haikuwa Na Uislamu Wala Ukristo,mwarabu Na Mzungu Ndio Walituletea Hizo Tamaduni Zao Na Badala Ya Kutuletea Maendeleo Zimetugawanya,kutupiganisha Na Kutuletea Umasikini Uliokithiri.licha Ya Kwamba Sina Noma Na Mwanakiji Na Mkandara Kujadili Hiyo Hoja,jambo La Muhimu Tujiulize Ni Kwamba Kwanini Tusiweke Utaifa Na Uafrika Wetu Mbele Wakati Wa Kufanya Mambo Ya Kimaendeleo Kwa Nchi Yetu?ni Wazi Kwamba Elimu Ndio Suluhishi Kwa Watu Wote Bila Kujali Dini Zao?kama Wote Mna Elimu Then There's Someting In Common,kama Hakuna Something In Common Then Gap Ya Utengano Inakuwa Kubwa Zaidi!badala Ya Kuongeza Utengano Kati Ya Waislamu Na Wakristo Ni Vema Kutafuta Kitu Ambacho Kitawaleta Karibu Zaidi Na Kushirikiana Katika Ujenzi Wa Taifa Letu!kama Tunataka Tuwe Na Taifa Moja Lisilojali Dini,kwanini Tuanze Kufikiria Namna Ya Kuwahumia Wananchi Wa Nchi Moja Tofauti Kisheria Just Because Ni Dini Tofauti?kwanini Tusichukuliane Kama Ndugu Ndani Ya Taifa Moja Bila Kujali Vurugu Kati Ya Mzungu Na Mwarabu?je Tunayofanya Yanalinufaisha Taifa Letu Na Wananchi Wake Au Ni Taratibu Za Kuwaplease Waarabu Na Wazungu Kwa Kujidai Tunazijua Sana Culture Zao?ni Very Obvious Kwamba Tulishaingia Kwenye Huo Mtego Long Time Ago,lakini Tujitahidi Na Kufanya Mambo Ambayo Yatauunganisha Zaidi Badala Ya Kutuletea Matengano!
 
Mtikila is a normal citizen like JK and other people. He have a right to criticize president or any non profit organization group, however his criticizing can stay as opinion as long as he does not brake the law.

Let me go back on Kadhi issue, i discussed this issue bofore. We both knows that rule of law is important cornerstone in any nation. We also knows that Judiciary system is a sensitive part of any nation that seek rights and justice to his people. Kadhi system has no problem what so ever, but the problem come on the country like Tanzania which has too much diversity.

I know kadhi system will only work on Muslim people, but who will fund the organization? It's my believes that no tax payer cent will go on this organization, because its benefit certain people and not the whole nation.

Second, i want to challenge those who support the Kadhi system in Tanzania. How will system work in such a diversity nation? Will it work for those people who put on their will that my mirathi should split-ted under sheria law? Or every muslim will be forced to participate on such a system? I believe Tanzania has many muslim who does not practice, will they qualify to be judge under kadhi system?
Who will run the kadhi system? Tanzania judiciary system? Who will assign which case belong to kadhi and which belong to rule of law court?

There are many misleading and false idea that people are throwing to the public concern kadhi court, i believe on kadhi system however Tanzania is a wrong place to implement this due to nature of the country.

For those who argue that it doesn't brake Tanzania constitution, can you guys prove it? I'm a muslim that practice all aspect of Islam, but i believe in Tanzania Kadhi system will be challange due to the nature of the country. Can someone explain how will it be established in Tanzania?
 
Barua kwa Lowassa yamletea matatizo Mtikila




na Ratifa Baranyikwa



BARUA yenye maneno makali ambayo Mchungaji Christopher Mtikila alimwandikia Waziri Mkuu, Edward Lowassa, ndiyo chanzo cha mwanasiasa huyo kutiwa mbaroni na kuhojiwa na Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Tangu Ijumaa iliyopita, Mtikila amekamatwa na kuhojiwa mara mbili, na hivi sasa anasubiri kufikishwa mahakamani wakati wowote, habari za uhakika zinaeleza.

Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imesema kuwa wanaangalia kwa undani maelezo yaliyotolewa na Mtikila, pamoja na maneno yaliyomo kwenye barua yake, na iwapo itathibitika kuwa ni vya uchochezi, mwanasiasa huyo, ambaye pia ni kiongozi wa kidini, atafikishwa mahakamani mara moja.

Kwa mujibu wa Polisi, kuna uwezekano mkubwa Mtikila akafikishwa mahakamani akikabiliwa na kesi ya uchochezi.

Moja kati ya kauli ambazo zinamtia matatani Mtikila zilizomo katika barua hiyo (Tanzania Daima ina nakala yake), inamshutumu Lowassa kwa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete kuisilimisha Tanzania kwa mbinu na mipango ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi nchini.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Alfred Tibaigana, alisema kuwa Mtikila bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi na kwamba iwapo upelelezi unaoendelea utabaini kuwa ana kosa, atafikishwa mahakamani mara moja.

"Amekamatwa kwa tuhuma za uchochezi kupitia barua hiyo aliyoisambaza kwenye vyombo vya habari mwishoni mwa wiki iliyopita… atawekwa chini ya ulinzi mpaka uchunguzi utakapokamilika na ikibainika ana kosa atafikishwa mahakamani," alisema Tibaigana.

Barua hiyo, ambayo Mchungaji Mtikila ameisaini kama mwangalizi wa kanisa, mbali na kusambazwa kwenye vyombo vya habari, pia inaonyesha kuwa nakala nyingine zimesambazwa kwa viongozi wa makanisa yote nchini na mitandao ya Kikristo.

Katika barua hiyo ya Novemba 1 mwaka huu, Mtikila anamshutumu vikali Lowassa kwa usaliti wake wa kumsaidia Rais Kikwete kuileta Mahakama ya Kadhi, ilhali (Lowassa) akijua kwamba kikatiba ni mwiko kwa kiongozi yeyote wa taifa hili kujihusisha na masuala ya kidini.

"Kikatiba ni mwiko kabisa uongozi wa taifa hili ambalo ni secular kujihusisha na dini fulani, ambapo dini inabaki kuwa ni uhusiano wa mtu binafsi na Mungu wake, hivyo kwamba jukumu la Serikali ni kulinda tu haki ya msingi ya uhuru wa kuabudu (ibara ya 19 na 20(1) ya Katiba ya Jamhuri.

"(Ulifanya hivyo) huku ukijua kwamba katiba inakupiga marufuku wewe na mamlaka yoyote ya nchi hii kutunga sheria au kuweka taratibu na kanuni yoyote yenye ubaguzi au upendeleo wa aina yoyote ile kwa dhahiri au kwa taathira yake," inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Mtikila, ambaye ni kiongozi wa Kanisa la Full Salvation, pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP).

Kupitia barua hiyo, Mchungaji Mtikila anamshutumu Waziri Mkuu kuwa wakati akiwa kwenye ziara mkoani Mbeya Oktoba 20 mwaka huu, alitumia madaraka yake mwenyewe kuelezea suala hilo aliposema kuwa wameipa mamlaka tume ya kurekebisha sheria chini ya Wizara ya Katiba na Sheria, kuandaa utaratibu wa kubadili katiba ili kuanzisha Mahakama ya Kadhi kwa kutumia Bunge la Jamhuri ya Muungano, wakati akifahamu kuwa kuna kesi mahakamani kuhusiana na suala hilo.

"Na wewe ndiye uliyewezesha kuzungumzwa bungeni suala hili la kigaidi, na kuridhia azima hii ya hatari ifanyiwe kazi na Wizara ya Sheria," inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Mtikila pia amesisitiza katika barua hiyo kuwa lengo la Mahakama ya Kadhi ni kuuangamiza Ukristo nchini, na kuwaua watu wasiokubali Uislamu na pia kuwaua Waislamu watakaoiacha dini hiyo na kujiunga na imani nyingine.

Oktoba 18 mwaka huu, Mchungaji Mtikila alifungua kesi Mahakama Kuu, iliyopewa namba 80 ya mwaka 2007, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akipinga mchakato wa urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara, akidai kuwa kufanya hivyo ni kuvunja katiba ya nchi kwa sababu Mahakama ya Kadhi ni chombo cha Jihad na ugaidi.

Akirejea katika kesi yake hiyo, Mtikila alimwambia Lowassa: "Umeusaliti Ukristo kiasi kwamba ulipojua kwamba kesi ipo mahakamani wewe ulitangaza kule Mbeya kuendelea na Jihad kwa kutumia Tume ya Kurekebisha Sheria ili hatimaye mtumie Bunge la nchi kuupa ugaidi nguvu ya sheria nchini, umefanya kosa hili wakati ukijua kuwa ni mwiko kabisa kwa serikali au Bunge kushughulikia jambo lolote ambalo liko katika Mahakama Kuu."

Source:http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/11/5/habari4.php

Du kumbe isu ni na EL?
 
Duh maneno makali na ya hatari, kuna tatizo kubwa hapa. Nimesema kule mwanzo kwamba Mtikila hakujaliwa kuzungumza kwa hekima. Hata kama ni kupinga jambo, maneno haya hayafai kabisa.

Kwa ufahamu wangu kama mkristo, mahakama za kadhi huwa hazitumiki kuua ukristo, wanazitumia waislamu kwa mambo yao yanayowahusu. Kama nchi nzima ni waislamu watupu basi si ajabu hiyo ikawa kama ndio sheria ya nchi hiyo, kwa hiyo serikali yao ikigharamia mahkama hizo ni muafaka kabisa. Lakini kama kuna mchanganyiko, basi mahakama ya kadhi wanabaki nayo waislamu (na kwa uzoefu wangu, sio wote, bado waislamu wengine wanaweza kuamua kutumia mahakama za kawaida kwa kesi hizohizo ambazo wenzao wanapeleka kwa kadhi). Ndio maana mie nadhani kwamba mahakama kama hii haihitaji mabadiliko ya katiba, ni suala la kuianzisha tu na kuiwekea uhusiano na sheria zilizopo za nchi hii, ingawa sidhani kwamba inapaswa kugharamiwa na serikali.

Labda kama Mtikila kuna anayojua kuhusu uislamu na mahakama hizo ambayo miye siyajui, lakini kwa msimamo wake huo nina mashaka kama hana tatizo jingine binafsi, yaani it sounds paranoid!
 
Mtikila ashitakiwa kwa madai ya kutoa maneno ya uchochezi
Na Tausi Ally (Mwananchi)

MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka mawili ya kutoa maneno ya uchochezi, yenye nia ya dharau na kuisababishia Jamhuri ya Tanzania mtafaruku.


Mchungaji Mtikila alifikishwa katika mahakama hiyo jana majira ya saa 7:30 mchana akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari polisi.


Mara baada tu ya kufikishwa katika mahakama hiyo, aliwasalimia waumini wake waliokuwa wakimsubiri kwa shauku huku wakilalamikia kukamatwa kwake. Mtikila aliwambia waumini wake kuwa �Amani ya Bwana Idumu�.


Baada ya kupewa salamu hiyo na kuitikia, waumini hao walionyesha mabango yaliondikwa �Je! ni lazima mahakama ya kiislamu iingizwe kwenye katiba�.


Bango lingine lilisomekana, �Hii siyo haki mtu akisema ukweli akamatwe, hatutaki mahakama ya Kadhi kupita Bungeni viongozi msilazimishe,� wakati bango lingine liliandikwa kuwa �kwa mujibu wa katiba Je? serikali yetu ina dini,� na baada ya waumini hao kuona askari wenye silaha walificha mabango yao na kutawanyika.


Baada ya waumini hao kutawanyika, Mtikila alipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka mawawili yanayomkabili.


Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Euphimia Mingi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Charles Kenyela, alidai kuwa Oktoba 31, mwaka huu, katika nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), zilizopo Ilala alitamka kuwa rais Jakaya Kikwete ni gaidi.


Kenyela alidai pia kuwa Novemba Mosi, mwaka huu, Mtikila alichapisha na kusambaza machapisho ya uchochezi yaliyoelekezwa kwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na kwamba nakala nyingine kwa viongozi mbalimbali wa makanisa nchini na kwa vyombo vya habari.


Aliendelea kudai kuwa machapisho hayo yaliandikwa, �Usaliti wako wa kumsadia Rais Kikwete kuisilimisha nchi kuwa mahakama ya Kadhi�.


Mengine yalidai kuwa �Mpendwa Lowassa wewe na Kikwete na mtandao wenu hamna kabisa sifa ya kuongoza nchi� na kwamba ufisadi na ushirikina unanuka kabisa kuiongoza nchi hii na mungu hapendi ufisadi wenu mnaoufanya katika nchi hii�.


Baada ya Kenyela kumaliza kusoma hati hiyo ya mashtaka, Mtikila alikana kutoa maneno hayo ya uchochezi.


Kenyela alidai kuwa upande wa mashtaka hauna pingamizi la dhamana na kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Aliiomba mahakama itoe masharti ya dhamana yanaoendana na uzito wa shitaka hilo kwa madai kuwa kosa analotuhumiwa kulitenda Mtikila linahatarisha usalama wa nchi na linaweza kuleta mgawanyo wa kidini.


Wakili Mpale Mpoki anayemtetea Mtikila, aliiomba mahakama itoe dhamana kwa mteja wake kulingana na taratibu za kisheria.


Hakimu Mingi alimuachia huru mshtakiwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja anayeaminika ambaye alisaini bondi ya Sh1milioni.


Pia alimtaka Mtikila asitoke nje ya jiji la Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama na kuiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 3, mwaka huu itakapotajwa tena.
 
sijawahi kuona kesi bogus na isiyo na merit kama hii...nina uhakika hata kikwete huko anasema what the https://jamii.app/JFUserGuide na hawa waendesha mashitaka!
 
sijawahi kuona kesi bogus na isiyo na merit kama hii...nina uhakika hata kikwete huko anasema what the https://jamii.app/JFUserGuide na hawa waendesha mashitaka!

Koba,
Umesema kweli kabisa, na sijui watakamata na kushitaki wangapi? tusubili makubwa yaja kabla ya tarehe 15 mwezi huu. Hii kadhi itazua mambo!
 
Tatizo la serikali yetu ni kwamba tume create environment ya kuabudu VIONGOZI wetu na kwa muda mrefu tumekuwa tukiwaogopa sana na vile vile kufikiria kwamba wao ni miungu wadogo. Na pale walipokosea hatukutakiwa kusema chochote, kwa sababu athari yake ni kubwa mno. Kutokana na hali hii, na utamaduni huu wengi wetu tumetokea kuwa wanyonge na "kuwashangaa" wale wenye UJASIRI wa kujitokeza na kuwakosoa viongozi wetu (Siongelei kutoa kashfa kwa viongozi). Na viongozi wetu nao kutokana na dhana hii ya kutokuwa challenged na UMMA wamejenga mawazo kwamba, wao ni wateule na wana haki ya kutumia chochote hata nguvu za dola kuonyesha mfano kwa yeyote yule atakayejitokeza kukosoa, ama kutofautiana nao kifikra ama kuuliza maswali mazito yanayotokana na sera mbovu. Lakini wamesahau kwamba mambo hubadilika kadri muda unavyokwenda. Uoga wa kukemea maovu, waliokuwa nao wananchi unaanza kuondoka taratibu taratibu na wananchi wanaanza kuwa outspoken.
Tukirudi katika swala la Rev. Mtikila...nafikiri ni waste of resources za jeshi la Polisi kumfungulia mashtaka. 10 years from now if not sooner..I predict tutakuwa na katiba itakayoipa UHURU WA SPEECH THUMBS UP. This means tutaweza ku make fun ya Rais wetu na mawaziri wake (bila kujali chama/vyama wanavyotokea)kwenye media outlets kama wafanyavyo akina Jay Leno na John Stewart na wengineo wengi. Hiyo siku itakuwa true democracy...lakini in the mean time tu enjoy JF kwani hii forum inaleta mapinduzi.
 
Mwanakijiji,
Mzee wangu umezungumza mengi sana kuhusu Lowassa na hakuna mtu alochoka kusoma malalamiko yako. Sii peke yako hapa JF kila siku tunarusha madongo na kukemeana tunapotaka kutoka ktk msitari.. huo ndio uhuru wa maoni, hata siku moja tusije fikiria uhuru wa maoni una include matusi toka kwa kiongozi mwingine wa chama.
Jamani Mitkila sio Machinga, huyu ni Mchungaji tena mgombea urais lakini lugha anayotumia hakika imetoka nje ya uhuru huo.
Pili, Upande mwingine wa shilingi hiyo hiyo, JK pia amekuwa mtu wa kuvutwa sana bila kujaribu kufanya utafiti wa swala hili kupitia wanasheria wetu kwanza. Tatizo lolote linalohusu Waislaam linaweza tatuliwa kama vile tunavyoweza kutatua matatizo ya wanawake kwa kumleta mtaalam wa mabo yao kama shahidi wa upande wowote ule uwe wamashtaka ma mshtakiwa. Wendawazimu huitwa Psychiatrist na pengine hata maswala ya alama na DNA wapo wataalam wake. Kinachotakiwa ni kuongezwa kipengele kimoja tu kinachohusu swala husika kama kweli lipo maanake nashindwa kabisa kufikiria kitu ambacho kinahitaji korti ya kadhi hasa Tanzania.
Nimezaliwa ktk Uislaam lakini wazee wetu walikuwa na wake kibao wengine wametumia mila zetu kuoa na sio Uislaam ( wakiwa na wake zaidi ya wanne), wamezaa nje ya ndoa, wazinifu na wanapiga maji (pombe) kama hakuna kesho.
Hesabu ya waislaam wanao yafanya haya ni kubwa sana na nadiriki kusema labda asilimia 70 hawafuati sheria za dini hii ktk maisha yao ya kila siku pamoja na kwamba wengi huenda misikitini kusali.
Hivyo basi mimi mwenyewe pamoja na kuwa muislaam siwezi kukubali kuhukumiwa ktk korti hizi hata siku moja kwani mengi yaliyojengwa ktk sheria hizi yanahusu Uislaam kwa ujumla na pia mazingira tofauti kabisa. Kuna vitendo ambavyo Shia wanavipa uhalali wakati havikubaliki ktk Sunni na vise verse, mfano ndoa za safar tutatoa hukumu kwa kufuata sheria ipi.
Jibu la yote haya ni kwamba mahakama hizi hazitufai hata kidogo ila tunaweza kumtumia Mtaalam wa sheria hizi kama atahitajika...Na sidhani kama kuna nafasi hiyo.
 
Pamoja na kuwa mpigania haki inabidi uwe makini kutovunja sheria waziwazi. Huwezi kutukana mtu yoyote hadharani na excuse iwe ni uchungu wa nchi yako! Busara ni muhimu kwa mpigania haki yoyote na uukitumia jazba na ubabe you play into the hands of your enemies... unawapa risasi za kutumi kukutungua kirahisi.
Mtikila inabidi akuwe!
 
Pamoja na kuwa mpigania haki inabidi uwe makini kutovunja sheria waziwazi. Huwezi kutukana mtu yoyote hadharani na excuse iwe ni uchungu wa nchi yako! Busara ni muhimu kwa mpigania haki yoyote na uukitumia jazba na ubabe you play into the hands of your enemies... unawapa risasi za kutumi kukutungua kirahisi.
Mtikila inabidi akuwe!

YOU MAYBE RIGHT!LAKINI ELEWA KUNA TOFAUTI KATI YA SHUTUMA NA MATUSI!SIO LAZIMA KWAMBA MTU AKIITWA GAIDI AMETUKANWA!NI SHUTUMA!
 
Mwanakijiji,
Mzee wangu umezungumza mengi sana kuhusu Lowassa na hakuna mtu alochoka kusoma malalamiko yako. Sii peke yako hapa JF kila siku tunarusha madongo na kukemeana tunapotaka kutoka ktk msitari.. huo ndio uhuru wa maoni, hata siku moja tusije fikiria uhuru wa maoni una include matusi toka kwa kiongozi mwingine wa chama.
Jamani Mitkila sio Machinga, huyu ni Mchungaji tena mgombea urais lakini lugha anayotumia hakika imetoka nje ya uhuru huo.
Pili, Upande mwingine wa shilingi hiyo hiyo, JK pia amekuwa mtu wa kuvutwa sana bila kujaribu kufanya utafiti wa swala hili kupitia wanasheria wetu kwanza. Tatizo lolote linalohusu Waislaam linaweza tatuliwa kama vile tunavyoweza kutatua matatizo ya wanawake kwa kumleta mtaalam wa mabo yao kama shahidi wa upande wowote ule uwe wamashtaka ma mshtakiwa. Wendawazimu huitwa Psychiatrist na pengine hata maswala ya alama na DNA wapo wataalam wake. Kinachotakiwa ni kuongezwa kipengele kimoja tu kinachohusu swala husika kama kweli lipo maanake nashindwa kabisa kufikiria kitu ambacho kinahitaji korti ya kadhi hasa Tanzania.
Nimezaliwa ktk Uislaam lakini wazee wetu walikuwa na wake kibao wengine wametumia mila zetu kuoa na sio Uislaam ( wakiwa na wake zaidi ya wanne), wamezaa nje ya ndoa, wazinifu na wanapiga maji (pombe) kama hakuna kesho.
Hesabu ya waislaam wanao yafanya haya ni kubwa sana na nadiriki kusema labda asilimia 70 hawafuati sheria za dini hii ktk maisha yao ya kila siku pamoja na kwamba wengi huenda misikitini kusali.
Hivyo basi mimi mwenyewe pamoja na kuwa muislaam siwezi kukubali kuhukumiwa ktk korti hizi hata siku moja kwani mengi yaliyojengwa ktk sheria hizi yanahusu Uislaam kwa ujumla na pia mazingira tofauti kabisa. Kuna vitendo ambavyo Shia wanavipa uhalali wakati havikubaliki ktk Sunni na vise verse, mfano ndoa za safar tutatoa hukumu kwa kufuata sheria ipi.
Jibu la yote haya ni kwamba mahakama hizi hazitufai hata kidogo ila tunaweza kumtumia Mtaalam wa sheria hizi kama atahitajika...Na sidhani kama kuna nafasi hiyo.

WAZI WAZI!
 
Back
Top Bottom