Msanii Nay wa Mitego ahojiwa na Polisi na kufunguliwa kesi ya Uchochezi

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,211
42,072
Msanii Nay wa Mitego anahojiwa na jeshi la polisi Dar es Salaam kutokana na wimbo wake “AMKENI”

Bado najiuliza ni nani anamshauri Rais kutumia hii style kukabiliana na wote ambao hawamsifii?
Rais ni kweli umechangua njia hii? Kweli njia nii utaiweza? Utakamata na kuhoji wa ngapi?

Rais mbona kuna mambo mengi ya kushughulika nayo kama ukosefu wa Umeme,mafuta na Dolla?

----
Msanii Emmanuel Elibariki maarufu ‘Nay wa Mitego’ ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa kwa tuhuma za kufanya uchochezi kupitia wimbo wake wa ‘Amkeni’.

Akiambatana na wakili wake Jebra Kambone, Ney wa Mitego amesema ameachiwa kwa dhamana baada ya mahojiano yaliyochukua takribani saa tatu na kukamilisha masharti aliyopewa.

Ney wa Mitego alifika katika Kituo cha Polisi Central, Dar es Salaam baada ya kuitwa kwa ajili ya mahojiano.

Hata hivyo Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema halihusiki na kuitwa kwake polisi licha ya kwamba wamemuita mara kadhaa kufika katika ofisi hizo lakini hakuitikia wito huo.

“Tumetoa wito mara mbili kwa ajili ya maadili ya kawaida tu lakini kwa bahati mbaya sana hakuwahi kutokea, na jana tumeandika wito mwingine tukimtaka aje Ijumaa saa 4 asubuhi hajatujibu, sijui kama atakuja ama hatokuja.

Mambo ya polisi nafikiri hayo ni masuala ya kijinai, sisi tunahusiana na masuala ya Sanaa tu wala hatuna jukumu la kwenda kumshitaki,” amesema Mwanasheria wa BASATA, Christopher Kamugisha.

Chanzo: Swahili Times
 
Msanii Ney wa Mitego anahojiwa na jeshi la polisi Dar es salaam kutokana na wimbo wake “AMKENI”

Bado najiuliza ni nani ana mshauri Rais kutumia hii style kukabiliana na wote ambao hawamsifii?
Rais ni kweli umechangua njia hii?
Kweli njia nii utaiweza? Utakamata na kuhoji wa ngapi?

Rais mbona kuna mambo mengi ya kushughulika nayo kama ukosefu wa Umeme,mafuta na Dolla?
Serikali ni dude kuuuubwa

inaweza ikashughulikia Umeme na mafuta na huku ikishusha Wenge la wenye vihele hele bila ya muingiliano
 
Msanii wa Hiphop nchini Tanzania , Ney wa Mitego , amefunguliwa kesi ya Uchochezi , kutokana na Wimbo wake Mkali unaoitwa 'AMKENI' .

Awali kulikuwa na taarifa kwamba Msanii huyo ameitwa Polisi kituo cha kati , DSM kwa ajili ya Mahojiano

Bado haijafahamika Masharti ya dhamana aliyopewa wala siku atakayopelekwa Mahakamani .

Screenshot_2023-09-06-16-12-30-1.png
 
Msanii wa Hiphop nchini Tanzania , Ney wa Mitego , amefunguliwa kesi ya Uchochezi , kutokana na Wimbo wake Mkali unaoitwa 'AMKENI' .

Awali kulikuwa na taarifa kwamba Msanii huyo ameitwa Polisi kituo cha kati , DSM kwa ajili ya Mahojiano

View attachment 2741029
Wakiambiwa ukweli wanakuwa wakali. Hongera sana Ney utayavuka tu wewe ni sauti ya watanzania. Watanzania wana imani na wewe.
 
Back
Top Bottom