KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 86
Mwanakijiji,
Mzee wangu umezungumza mengi sana kuhusu Lowassa na hakuna mtu alochoka kusoma malalamiko yako. Sii peke yako hapa JF kila siku tunarusha madongo na kukemeana tunapotaka kutoka ktk msitari.. huo ndio uhuru wa maoni, hata siku moja tusije fikiria uhuru wa maoni una include matusi toka kwa kiongozi mwingine wa chama.
Jamani Mitkila sio Machinga, huyu ni Mchungaji tena mgombea urais lakini lugha anayotumia hakika imetoka nje ya uhuru huo.
Pili, Upande mwingine wa shilingi hiyo hiyo, JK pia amekuwa mtu wa kuvutwa sana bila kujaribu kufanya utafiti wa swala hili kupitia wanasheria wetu kwanza. Tatizo lolote linalohusu Waislaam linaweza tatuliwa kama vile tunavyoweza kutatua matatizo ya wanawake kwa kumleta mtaalam wa mabo yao kama shahidi wa upande wowote ule uwe wamashtaka ma mshtakiwa. Wendawazimu huitwa Psychiatrist na pengine hata maswala ya alama na DNA wapo wataalam wake. Kinachotakiwa ni kuongezwa kipengele kimoja tu kinachohusu swala husika kama kweli lipo maanake nashindwa kabisa kufikiria kitu ambacho kinahitaji korti ya kadhi hasa Tanzania.
Nimezaliwa ktk Uislaam lakini wazee wetu walikuwa na wake kibao wengine wametumia mila zetu kuoa na sio Uislaam ( wakiwa na wake zaidi ya wanne), wamezaa nje ya ndoa, wazinifu na wanapiga maji (pombe) kama hakuna kesho.
Hesabu ya waislaam wanao yafanya haya ni kubwa sana na nadiriki kusema labda asilimia 70 hawafuati sheria za dini hii ktk maisha yao ya kila siku pamoja na kwamba wengi huenda misikitini kusali.
Hivyo basi mimi mwenyewe pamoja na kuwa muislaam siwezi kukubali kuhukumiwa ktk korti hizi hata siku moja kwani mengi yaliyojengwa ktk sheria hizi yanahusu Uislaam kwa ujumla na pia mazingira tofauti kabisa. Kuna vitendo ambavyo Shia wanavipa uhalali wakati havikubaliki ktk Sunni na vise verse, mfano ndoa za safar tutatoa hukumu kwa kufuata sheria ipi.
Jibu la yote haya ni kwamba mahakama hizi hazitufai hata kidogo ila tunaweza kumtumia Mtaalam wa sheria hizi kama atahitajika...Na sidhani kama kuna nafasi hiyo.
WELL SAID ! SINA LA ZIADA HAPA !