Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 1,211
- 230
Hakuna anayemuhukumu Mtikila Bali kwa upande wangu na wengine wanaomuona Rev. Mtikila amevunja sheria ni kutokana na sheria za nchi tulizonazo ni kwamba amekiuka, tena hasa ukizingatia kwamba yeye ni mmoja wa watu ambao amekuwa msitari mbele kutafuta Haki kupitia sheria na katiba ya nchi. Kutoa kauli za Uchochezi ni kosa Tanzania na kutumia lugha ya Matusi Ni Kosa, Sasa kama haya ameyafanya ,kisheria amekosa.Sasa mimi si Mhukumu kwasababu hiyo si kazi yangu Lakini kama yaliyoripotiwa hapa ni kweli ameyafanya anaangukia kwenye kundi la uvunjaji wa sheria kwa kutenda kosa na huo ndiyo ukweli. Kwa kuyadiscuss haya hakunifanyi niwe nimemuhukumu bali nimeelezea sheria inasema nini juu ya hilo.swala la kupatikana na hatia au laah hilo tunawaachia wenye wajibu wao.Inabidi utulie upitie tena maandishi ya wachangiaji wenye maoni tofauti hapa. Hakuna anayemtete au kumkandamizi Mtikila hapa. Hapo kinachogomba ni uhalali na haki ya mtu kutoa hisia zake pamoja na kupinga mtu kuhukumiwa nje ya mahakama kama baadhi yenu mnavyofanya hapa. Nyie mnatia Mtikila hatiani kama nani? Tunapinga vilevile hii tabia ya kumsweka ndani badala kumfikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Ni hilo, kwamba alitukkana matusi na kama amevunja sheria, ni mahakama ndiyo yenye uwezo wa kuamua, sisi hapa hatuwezi!
Mwisho ni swala zima la uvumilivu. Tunachosema ni kwamba huwezi kukuza demokrasia bila uvumilivu. Sasa demokrasia inahitaji uvumilivu pamoja na wananchi kama Mtikila. Bila uvumilivu hakuna demokrasia. Sasa wewe ukiambiwa ni gaidi na wakati unajua sio gaidi, tatizo liko wapi? Au mtu akikwambia wewe ni mwanamke wakati wewe inajulikana kuwa ni mwanamume ndio kusema utageuka kuwa mwanamke? Ingekuwa ni hivyo akina Bush na Blair wangeshafunga watu wangapi katika utawala wao? Leo hii mchana nilikuwa naangalia katuni inayomwigiza Gordon Brown, ni ya ajabu na ya kudhalilisha mno, tena kwenye BBC. Lakini Gordon anaendelea na uPM wake bila kutetereka wala kunyooshea watu vidole achalia mbali kusweka watu ndani. Sasa sisi mtu kusema wewe ni gaidi imekuwa nongwa? Ndio kusema urais wako unapungua thamani? Nani mwenye wajibu hapo, Mtikila kuthibitisha kauli yake au huyu aliyeambiwa ni gaidi kuthibitisha kwamba yeye sio gaidi? It take two to tangle!