Naomba msaada mume wangu amekamatwa na polisi nyumbani saa nane usiku kwa tuhuma za kununua simu ya wizi. Vituo vyote wanadai hayupo na tusimtafute

Mkushi Mbishi

JF-Expert Member
Sep 30, 2018
318
513
Kaka naomba unisaidie kunielezea matatizo yangu kwenye ule mtandao wenu wa jamii forums ulionisaodia kipindi kile, wakati huu nahitaji msaada sana

Haya ni maneno ya binti ambaye anaitwa Rahma Shaabani Kiwangala, mwenye mtoto mdogo wa takriban mwaka mmoja mkazi wa Manzese mburahati, mtaa wa kwa jongo Kata ya makurumla ambaye saa nane usiku akiwa na mume wake nyumbani walifuatwa na mjumbe wa mtaa anayeitwa Zuhura Ngwenje namba zake ni 0715328582 (yupo tayari kutoa ushirikiano) akiwa ameambatana na maaskari wawili WA kituo kikubwa cha polisi CHANIKA MWISHO ambao majina Yao ni Mussa Ally na Bonifas Gablier ambao walimkamata mume WA binti huyu anayeitwa OMAR MWELEA HUSSEIN kwa kosa la kununua simu ya wizi.

Polisi hao wawili walimchukua mpaka kituo kikuu cha polisi CHANIKA MWISHO, asubuhi ndugu wa mtuhumiwa walikuja kumuangalia ndugu Yao na kufuatilia kesi yake wakaambiwa kesi IPO kwenye upelelezi na hawakupewa ruhusa ya kumuona ndugu yao, kuanzia siku hiyo kila wakija kufuatilia wakawa wanazungushwa bila kuruhusiwa kumuona ndugu Yao,na wakati mwingine wakawa wanakuja na mjumbe wao aliyefanikisha kukamatwa kwake lakini jibu la mwisho wakajibiwa kwamba HAKUNA KESI KAMA HIYO KITUONI HAPO NA WASIENDE TENA KUFUATILIA HAPO.

Binafsi nimempgia mjumbe na amekiri kutokea kwa tukio hilo na amesikitika sana kwa sheria kupindishwa na ndugu hao kutopata haki ya kusikilizwa,kujua wapi alipo ndugu Yao na amesema ameenda kwa mkuu kulifikisha swala hilo na amewakuta maaskari hao wapo kituoni hapo na akawatambua kuwa ndio walewale walikuja kumkamata Bwana Omary lakini bado hakupewa ushirikiano wowote.

Tukio hili limetokea usiku WA tarehe 18 mwez WA pili jumamosi kuamkia jumapili saa nane usiku.mpaka Leo umetimia mwezi mmoja bila ndugu kujua lolote na wameambiwa Hakuna kesi Kama hiyo WASIENDE kufuatilia kituoni HAPO.

Tunaomba serikali ya Jamhuri ya Tanzania iwasaidie ndugu hawa kujua ukweli unaofichwa ni upi katika hili, ili iwasaidie familia hii kujua alipo ndugu Yao?

Mke wake na ndugu kwa ujumla wanasema wanahitaj tu kujua hata Kama polisi hawa wamemuuwa ndugu Yao basi waonyeshwe mwili wakazike ama wajue tu kuwa ameuwawa wazike nguo zake.

Inauma sana kwa kweli imagine ni ndugu yako ndio amefanyiwa hivyo,ndugu zangu tumsaidie huyu Bwana asiyejulikaana alipopelekwa,familia yake na mke wake kwa ujumla angalau wafaham alipopelekwa na polisi hawa

Tukumbuke Tanzania ni ya kwetu sote na sote tuna haki sawa.

Mama wasaidie wanao, kwani waliopewa mamlaka ya kusaidia ndio wamepata maguvu ya kukandamiza wenzao
 
Hayo maelezo. Kuna vitu binti anaficha.

Polisi sio wajinga hawakurupuki.

Mpaka polisi wakufate nyumbani usiku wa manane maana yake wameshakujua tabia zako. Mnunuzi wa kawaida angepigiwa simu tu afike kituoni. Ndio angekamatwa..ila wa kufatwa usiku wa manane ujue ni mtu wa matukio.

Kununua simu ya wizi sio sababu kuu

Mimi nilivyoona mkazi wa mburahati na mambo ya simu ya wizi. Akili yangu inaniambia mumewe ni mwizi mtu wa matukio. Kuna maeneo dar es salaam yamejaa watu wa matukio ndio wanaishi. Mojawapo ni kigogo mburahati, tandika kwa kindande, yombo taa nyekundu, chanika. Hayo maeneo yamejaa vibaka na majambazi

Nahisi Huyo mumewe ni mwizi na polisi huwa hawawacheleweshi wezi.
 
Hayo maelezo. Kuna vitu binti anaficha. Polisi sio wajinga hawakurupuki.

Kununua simu ya wizi sio sababu kuu

Mimi nilivyoona mkazi wa mburahati na mambo ya simu ya wizi. Alili yangu inaniambia mumewe ni mwizi mtu wa matukio.

Huyo mumewe ni mwizi na polisi huwa hawawacheleweshi wezi. Ajiandae kufata mwili
Mkuu mke wake hajui kitu Bali tukio halisi liko Ivo na wao ndio wanautaka huo mwili Kama familia wakazike Kama binadam wengine wanavyozikwa kwani mambo ya kuuwawa si jambo geni.tuwaelekeze wakaufate wapi?
 
Nenda kwa OCD, na kwa RPC.

Au neñdeni kwa BASHITE.

Mkishindwa mtafuteni WAKILI akafungue kesi mahakamani dhidi ya hao majambazi wenye sare za kipolisi.

Lakini kwa BASHITE ndio kiboko zaidi. BASHITE ni zaidi ya MUHIMILI.

Maaskari wote wanatetemeka mbele ya BASHITE mpaka wanajikojolea. He carries the true POWER.
 
Hayo maelezo. Kuna vitu binti anaficha.

Polisi sio wajinga hawakurupuki.

Mpaka polisi wakufate nyumbani usiku wa manane maana yake wameshakujua tabia zako. Mnunuzi wa kawaida angepigiwa simu tu afike kituoni. Ndio angekamatwa..ila wa kufatwa usiku wa manane ujue ni mtu wa matukio.

Kununua simu ya wizi sio sababu kuu

Mimi nilivyoona mkazi wa mburahati na mambo ya simu ya wizi. Akili yangu inaniambia mumewe ni mwizi mtu wa matukio.

Huyo mumewe ni mwizi na polisi huwa hawawacheleweshi wezi. Ajiandae kufata mwili
Acha ujinga

Kwani yule dogo wa mtwara alieuliwa na polisi alikuwa na matukio gani?
 
Huwa inatokea sana temeke huko kubeba wezi wa sim usiku, huyo kama kesi yake ni hiyo tu bas mtampata ila mtapigwa hela
Ni mwez sasa umefika na hajulikani alipo na Askari hawatoi
Nenda kwa OCD, na kwa RPC.

Au neñdeni kwa BASHITE...
Acha niwashauri hatua inayofuata ianzie kwa OCD ama RPC,au Bashite ndio cheo gani mkuu na ofisi yake iko wapi mbona jina geni wapo DSM hawa watu wenye matatizo.tuwasaidie kwa kweli
 
hIZI SIMU ZINASHIDA SANAA
WENGINE UNAKUTA WAMEUAAA

OLE WAKUKUTE NASIMU YA MAREHEMU

CHUNGUZAA KAMA ALIEIBIWA YUKO HAI

KAMA NDIO PONA YAKE KAMA KAFAA NDUGU NAPITATU
Sawa sasa si waweke wazi ama sheria inasemaje?! Au kuna sheria za Siri wanamalizia wao wenyewe hukohuko kimyakimya ,wakumbuke na hawa wanaowatendea ni binadam na wanakutana nao kila siku katika maisha hayahaya ya chini ya jua.

Inauma kwa kweli imagine ni ndugu yako ndio amefanyiwa hivyo unajisikiaje nafsini!?
 
Hayo maelezo. Kuna vitu binti anaficha.

Polisi sio wajinga hawakurupuki.

Mpaka polisi wakufate nyumbani usiku wa manane maana yake wameshakujua tabia zako. Mnunuzi wa kawaida angepigiwa simu tu afike kituoni. Ndio angekamatwa..ila wa kufatwa usiku wa manane ujue ni mtu wa matukio.

Kununua simu ya wizi sio sababu kuu

Mimi nilivyoona mkazi wa mburahati na mambo ya simu ya wizi. Akili yangu inaniambia mumewe ni mwizi mtu wa matukio.

Huyo mumewe ni mwizi na polisi huwa hawawacheleweshi wezi. Ajiandae kufata mwili
Wewe ni mjinga na JUHA.
 
Back
Top Bottom