Mtoto wa miaka 14 ashikiliwa na polisi kwa kubaka na kulawiti watoto 2

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,114
Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linamshikilia Mtoto mwenye umri wa miaka 14 ambaye ni Mkulima na Mkazi wa Kitongoji cha Chiano Kata ya Nalingu, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kwa tuhuma za kubaka na kulawiti Watoto wawili ambao ni ndugu (watoto wa dada yake) ambao alikuwa anaachwa nao nyumbani kama Mlezi pindi dada yake anapokwenda kufanya shughuli zake za kila siku za kujiingizia kipato.

Mama mzazi wa watoto hao ameiambia Ayo TV kwamba; alipomuhoji mdogo wake amekiri kufanya hivyo ambapo amesema mtoto wa kike amembaka hadi akazoea na sasa anamuona kama Mke wake huku mtoto wa kiume akiwa amemuingilia kwa siku tatu na alikuwa anafanya hivyo mama yao anapokuwa mbali na nyumbani huku akiwatishia kuwa wakimwambia mama yao atawapiga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Nicodemus Katembo amesema Mtoto aliyebakwa ni wa kike mwenye umri wa miaka saba na wa kiume wa miaka mitano amelawitiwa ambapo matukio hayo yametokea kuanzia October mosi hadi 15, mwaka huu, katika nyakati tofauti.

“Alimbaka Mtoto wa kike na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri na kisha alimlawiti Mtoto wa kiume na kumsababishia maumivu katika sehemu yake ya haja kubwa.

Mbinu aliyotumia Mtuhumiwa kuwafanyia vitendo hivyo wahanga hao ni pamoja na kuwavamia nyakati za usiku wakiwa wamelalala kisha kuwaingilia mmoja baada ya mwingine, wote wawili wamefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na hali zao zinaendelea vizuri."

RPC Katemboa amesema kiimi cha tukio ni tama za kimwili hivyo ametoa rai kwa wananchi wa Mtwara, kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia pamoja na maadili yanayokinzana na sheria za nchi. Licha ya umri wao kuwa mdogo watoto hao wote watatu hawasomi shule.
 
Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linamshikilia Mtoto mwenye umri wa miaka 14 ambaye ni Mkulima na Mkazi wa Kitongoji cha Chiano Kata ya Nalingu, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kwa tuhuma za kubaka na kulawiti Watoto wawili (pichani) ambao ni Ndugu (Watoto wa Dada yake) ambao alikuwa anaachwa nao nyumbani kama Mlezi pindi Dada yake anapokwenda kufanya shughuli zake za kila siku za kujiingizia kipato.

Mama Mzazi wa Watoto hao ameiambia AyoTV kwamba alipomuhoji Mdogo wake amekiri kufanya hivyo ambapo amesema Mtoto wa kike amembaka hadi akazoea na sasa anamuona kama Mke wake huku Mtoto wa kiume akiwa amemuingilia kwa siku tatu na alikuwa anafanya hivyo Mama yao anapokuwa mbali na nyumbani huku akiwatishia kuwa wakimwambia Mama yao atawapiga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Nicodemus Katembo amesema Mtoto aliyebakwa ni wa kike mwenye umri wa miaka saba na wa kiume wa miaka mitano amelawitiwa ambapo matukio hayo yametokea kuanzia October mosi hadi 15, mwaka huu, katika nyakati tofauti.

“Alimbaka Mtoto wa kike na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri na kisha alimlawiti Mtoto wa kiume na kumsababishia maumivu katika sehemu yake ya haja kubwa, mbinu aliyotumia Mtuhumiwa kuwafanyia vitendo hivyo Wahanga hao ni pamoja na kuwavamia nyakati za usiku wakiwa wamelalala kisha kuwaingilia mmoja baada ya mwingine, wote wawili wamefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na hali zao zinaendelea vizuri"

RPC Katemboa amesema kiini cha tukio ni tamaa za kimwili hivyo ametoa rai kwa Wananchi wa Mtwara, kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia pamoja na maadili yanayo kinzana na sheria za Nchi…… licha ya umri wao kuwa Mdogo Watoto hao wote watatu hawasomi Shule.

Source: MillardAyoUPDATES
 
Hali imekuwa tete jamani, tusiache kusali sana aisee.
Kusali tu?

Bila kuchukua hatua madhubuti?

Tujikite katika malezi...wote baba na mama. Tuwafundishe watoto wetu maadili mema. Tuache kuamini watu hata kama ni ndugu wa karibu namna gani. Familia sasa ni mama, baba na watoto basi. Hakuna mgeni kulala na wanetu hata awe nani. Ni zama za kupambana kwa kutumia kila aina ya silaha (yakiwemo maombi) ili kulinda uzao wetu...
 
Kusali tu?

Bila kuchukua hatua madhubuti?

Tujikite katika malezi...wote baba na mama. Tuwafundishe watoto wetu maadili mema. Tuache kuamini watu hata kama ni ndugu wa karibu namna gani. Familia sasa ni mama, baba na watoto basi. Hakuna mgeni kulala na wanetu hata awe nani. Ni zama za kupambana kwa kutumia kila aina ya silaha (yakiwemo maombi) ili kulinda uzao wetu...
Amen mkuu maana hali inatisha sana☹️
 
Back
Top Bottom