1. Mkuu joka, Heshima mbele, ningekuelewa kama unamfahamu huyo dada wa Malecela, lakini ukweli ni kwamba humfahamu, wala uwezo wake kipesa, lakini una hukumu tayari kuwa amepata wapi hizo pesa, wewe huoni kuwa hayo ni matusi kwa mwana-mama ambaye wala humfahamu wala hujawahi kumsikia, wala kumuona? Je hizi ndio mila zetu za ki-Tanzania kuwahukumu wananchi bila sababu just because kaka yake ni Malecela? That is exactly what you are doing, ningekuelewa ungeuliza info kuhusu huyu dada wa Malecela, tena kwa ustaarabu kama ulivyouliza swali la kwanza, lakini huwezi kutafuta info kwa kutoa hukumu kwanza kwa mama ambaye wala humjui, Mkuu huna hata aibu unauliza "Where did she get the money?" are you serious au unatania? Mimi nikushawishi wewe mtu nisiye kufahamu wala sijawahi kukuona for what? Ili unipe nini? Sasa na wewe unataka kunishawishi niamini kwamba katika ukoo au familia ya Malecela, ni yeye tu mwenye uwezo? Wewe unawafahamu wote? Huyo mama unajua kama ana watoto au hana? Wana uwezo au hawana? Halafu eka moja ya shamaba kwa eneo lilipo hilo shamba, Mkoka unafikiri inaweza kuwa inauzwa shillingi ngapi za bongo? Hivi hata unajua hako kakijiji Mkoka bongo kako sehemu gani? I mean mkuu Joka kweli among all the brain kwenye hii forum ninakuheshimu siku zote kuwa ni one of them unaweza kuuliza maswali ya kitoto na daharau kwa watu usiowajua kiasi hiki? Kwa hiyo kwa mantiki yako mkuu, member yoyote wa familia ya Malecela, akiwa na hela au uwezo ni dhambi, maana ni za wizi Malecela ameiba serikalini? is that so? Mkuu Malecela, ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto 11, na ukweli ni kwamba wenziwe walikuwa na mali hata kabla Malecela, hajaingia kwenye siasa, na ndio waliomsomesha shule na ndio waliompa hata nyumba yake ya kwanza pale kata ya Kikuyu, Dodoma mjini alipotoka shule India, na leo wamebaki yeye na dada zake wawili tu, kwa hiyo mali zote zilizoachwa na ndugu zake wengine na hasa za mashamba, ziliangukia mikononi mwake yeye mwenye uwezo, mkuu wangu kuna kaka yake mkubwa, aliyekuwa akiishi Chalinze, Dodoma, aliyefariki miaka mitatu iliyopita, aliacha mashamba, karibu eka 300 ambayo Malecela ameshindwa mpaka leo hata kuyagusa maana it is too much kwake, sasa wewe unashangaa hayo ya Mkoka, ambako value ya ardhi sidhani kama inaweza hata kufikia dola moja per eka? Mkuu Baba wa Malecela, alikuwa mtengeneza mvua, which made him the richest man in Dodoma then, na mpaka ku-draw the attention ya wazungu wa kwanza, waliomrubuni mpaka kutoka dini yake ya Upagani, na kuwa Mu-Anglikana wa kwanza bongo, na hatimaye kuileta dini hiyo Dodoma, kwanza na hatimaye bongo nzima, sasa by the time anakufa unafikiri alikuwa ameacha mali kiasi gani as far as mashamba na mifugo? Huyo Dada yake unayesema hawezi kuwa na hela, amekuwa akimiliki Hospitali yake binafsi Urambo, Tabora ambapo hasa alikuwa akijishughulisha na kina mama kujifungua watoto, na hizi ni enzi za kuanzia 50s, 60S, 70s, mpaka mwishoni mwa 80s, sasa hiyo miaka yote alikuwa akilifanyia kazi ya charity, au alikuwa akitengenza pesa? Halafu aliyekuambia kuwa Dodoma ni sehemu ngumu kiasi kuwa mwananchi hawezi kuwa na shamba kubwa ni nani mkuu? Mkuu Dodoma kuna ardhi njema ya kustawisha mahindi, mtama, uwele, Tende, Zabibu, na Mbegu za mafuta ya Alizeti, na ndio hasa kilimo anachokifanya Malecela sasa kwenye mashamba yake, kwa mbinu za kisasa, na aliyeanza ni huyo dada yake ambaye siku zote amekuwa akilima kwa kutumia matrekta, wakuu hata Dodoma tu nako mnahitaji kusimuliwa kama vile ni majuu? Yaani kupanda basi tu asubuhi ukafika saa tisa ukajifunza jiografia ya kule nayo inahitaji hela za kigeni au kuja kuelimishwa hapa JF? 2. Mkuu joka, this is sad mkuu what is in the expose hapa ni uwezo mdogo wa baadhi ya wananchi wa Tanzania, katika kufikiri, maana inaonekana kuwa tuna mawazo kuwa ndugu wa kiongozi hawezi kuwa na mali zake binafsi, akiwa nazo basi ni za ndugu yake ambaye ni kiongozi alizoiba serikalini, and that mkuu is very pathetic thinking, tena ya u-Azimio La Arusha, yaani Malecela, ataiba hela za nchi halafu ataenda kuzi-invest kwenye ardhi ambayo huwezi kumuuzia binadamu yoyote mwingine akanunua hata kwa bei uliyonunulia, licha ya bei ya faida kutokana na kuitunza ardhi hiyo, unasema hiyo ndio expose ya kuwa viongozi wetu wanaojidai ni masikini? you maust be joking mkuu, kweli haya maneno unaweza kumushawishi mwananchi mwenye akili timamu akakuelewa? Look at this, mashamba yote Mwalimu aliyowagawia viongozi wa juu kule Chamwino, waliyalima tu Mwalimu alipokuwa kwenye madaraka, alipoondoka tu wakayatelekeza, yaani leo hata wewe unaweza ukaenda ukayalima maana sasa ni mapori tu kama yalivyokuwa mwanzoni, sasa akitokea mtu wa kuyalima yakapendeza then kutatokea kina wewe Joka, kuwa ooh hii ni mali za viongozi waliowapa ndugu zao? Does this make a sense at all mkuu? 3. Mkuu joka, labda kuna mtu ameiba pasword yako, no way this is you ninayemfahamu, mkuu wizi na rushwa serikalini ilianza toka Mwalimu, akiwa madarakani, yeye binafsi Mwalimu, alimuondoa waziri wake wa kwanza wa sheria, chief Mwakwaiya kwa ajili ya rushwa, hiyo ilikuwa in the 60s, kwa hiyo Mkapa sio kiongozi wa kwanza kama unavyosema hapo. Mwalimu, aliandika kitabu kikubwa sana akimtukana Malecela, kwamba ndiye tatizo la Taifa letu kwa sababu haulindi Muungano, yaani sisi wabongo umasikini wetu unatokana na Malecela kutoulinda muungano, na katika hicho kitabu kuna mahali Mwalimu, anamuambia Malecela, aache uongozi akalime mashamba yake, siku ile kwenye mkutano wake na waandishi wa habari Kilimanjaro Hotel, alizungumzia tena kwa kirefu kuhusu mashamba ya Malecela, lakini never even once Mwalimu aliwahi kusema mashamba hayo ya Malecela, ni ya hela za wizi alizoiba serikalini, lakini Mwalimu alisema mwaka 1995 kuwa Malecela,anazo billions of money alizopewa na wa-Iran kutafuta urais, ukweli ni kwamba mpaka leo hizo hela hatujaziona, lakini recently tumesikia kuna waliopewa hela toka Iran za uchaguzi, hivi ni mwananchi gani ambaye hakuziona zikitumika? Sasa Malecela, aliamua kuziweka wapi ambako mpaka leo hatujawahi kuziona? Kama ni mauza uza ya Mkapa, yametolewa kwa kina magazeti yetu to this day ameshindwa kukanusha wala kukubali, sasa kama ya Malecela yapo kwa nini hayo magazeti yasiseme, yanasema mpaka habari za rais wa sasa yatashindwa kumsema Malecela na mali zake? Mkuu uwezo au priviledge ya kuandika hapa JF isitufanye tukaamini kuwa tunaweza kuwachafua tu hata viongozi wasiohusika na uchafu, licha ya wananchi wa kawaida, uzuri wa bongo siku hizi mambo ni hadharani kama mwendo wa Msondo ngoma ya wa-Tanzania, na mkulu wangu marehemu TX-moshi, hakuna siri tena mambo yote huwekwa hadharani tu, kwa hiyo mkuu samahani sana kama nimekugusa kule kwenye ishu ya Rupia, Lakini mwendo utaendelea kuwa mdundo tu kwa viongozi wachafu waliotuibia mali zetu za taifa, na wale wasafi hawana sababu ya kuogopa maana tunawajua wote na tutawatetea, lakini wale wezi wote kila mmoja atabeba mzigo wake, Isipokuwa tu mkuu wangu joka, umenishitua sana hizi nywepesi nywepesi, ambazo ni dalili za kutokuwepo hoja za msingi against Malecela, sasa ikibidi hata dada yake, ili mradi tu tumpate na hatia kama za Mkapa, masikini ya Mungu, ndio taifa letu hili na sisi ndio wananchi wenyewe!