Kwanini Mzee Malecela alijulikana ghafla kama “Jumanne”?

Heshima mbele, mambo mengine mnapoyasikia muwe na wenyewe mjaribu kuyafuatilia kama yana ukweli, Malecela sio mtu wa anasa hata siku moja, na besides uamuzi wa nyumba ya ofisa yoyote uablozini hutolewa na balozi, sasa kama alikuwa na kinyongo na hiyo nyumba si angekataa tu kusiani mkataba wa kuilipia na huyo ofisa asingeafnya kitu chochote, halafu hebu njoo bongo uone nyumba anayokaaa Malecela, Sea View halafu uende nyumba za mawaziri wakuu wastaaafu wengine uone kama hayo maneno yako yanaweza kuwa ni kweli, na kwa taarfia yako tu ni kwamba ameombwa sana apewe nyumba nzuri zaidi lakini amekuwa akikataaa, haya mkuu ni majungu, nijuavyo ni kuwa Malecela akiwa London, ndiye balozi pekee aliyekuwa akiwafanyia sherehe wananchi kuliko balozi yoyote yule aliyewahi kuwa balozi pale.

Wa-Tanzania tuache majungu, maana haya hayalisaidii taifa kwa lolote.

Asante Mkuu,

Kama nilivyosema kwenye post ya awali, ni mambo ambayo niliyasikia. Kwa hiyo yanaweza kuwa yalikuwa ni mepesi mepesi tu.
Asante, kwa mealezo yako anyway.
 
1.

Mkuu Engineer,

Heshima mbele mkuu, Muungwana ni mpitiaji wa kawaida sana hapa forum, na besides yaliyotokea Dodoma majuzi ni dalili tosha kuwa anazo habari zote za yanayoendelea, kitendo cha kumnyima umakamu Luwassa, sio kidogo mkuu wangu ni kikubwa kuliko wengi hapa tunavyokiona, kuwanyima almost Mtandao wengi nafasi za cc, na NEC, watu kama Kamalla kukosa ujumbe haikuwa mchezo ndugu yangu, urais sio mchezo, Muungwana ameulilia kwa muda mrefu hatimaye akaupata, sasa alihitaji muda kidogo wa excitement na sasa umekwisha ninaamini ndio kwanza anaanza kazi, sasa ninaaamini pole pole he is starting to get it, lakini ninakubaliana na wewe kuwa baadhi ya yaliyofanyika toka aingie urais yanakatisha tamaa especially kwa wale tunaomfahamu kwa karibu, lakini kosa ni kurudia kosa, sio kufanya kosa na anaelekea kulielewa hilo, na unajua kuwa majuzi alitamka kuhusu internent, hivi unafikiri alikuwa akimaanisha internent ipi hiyo zaidi ya hii? Kwa hiyo mkuu, please saa za usiku mkuu hupita hapa na pia hata ukimtumia SMS huwa anajibu kwenye ile namba yake ya zamani!


2.

Kutokana na uchunguzi wangu binafsi, G55 chini ya kiongozi wao Kasaka, hawakuwa na nia ya walichokuwa wakikipigania, bali walikuwa na another ishu kutokana na the fact kwamba hawakudai hoja zao Warioba akiwa Waziri Mkuu, wakaksubiri Malecela ndio wakaanza, walikuwa wakisaidiwa na Mwalimu, ambaye alikuwa very smart kwenye hili, ingawa ukweli upo kuwa Kasaka alikuwa akishinda Msasani kupewa hoja saa za usiku. Pia kulikuwa na another factor kwenye hilo kundi yaani Salmin, ambaye aliamini kuwa under serikali tatu ingekuwa rahisi kwake kuwa rais wa Muungano, ambao alikuwa akiutaka sana na Mwalimu, alijua hili lakini akammezea, na Malecela pia aligundua baadaye kuwa rafiki yake wa karibu Salmin, naye kwa mbali alikuwemo kwenye lile kundi, ila ninaamini kuwa na yeye Malecela, alimlipa kwenye Salmin kutaka term ya tatu, maana ni Malecela ndiye aliyeiua hiyo na hata kumpa urais Karume, badala ya Bilali pia ilikuwa another revenge ya Malecela kwa Salmin rafiki yake, ndio maana tunasema siasa ni mchezo mchafu sana,

Kuhusu kuanzishwa kwa serikali tatu, ile ilikuwa ni kanyabwoya tu ambayo ingepelekea kuvunjwa kabisa kwa Muungano, ukweli ni kwamba uamuzi wa mwisho ulikuwa wa Mwinyi na Diria, ambao pia hawakuwa wakweli mbele ya Malecela kwenye hili, ukweli forces zote zilizokuwa kwenye hiii play zilikuwa na egemeo isipokuwa Malecela tu ambaye in the end, aliishia ku-pay the price huku wahusika wengine wote wakikingiana vifua, na kumgeuka ile ishu kama ingeachiwa kweli, basi Muungano ungekuwa umekwisha by now, kwa maoni yangu!

Binafsi siungi mkono kuvunjwa kwa Muungano, isipokuwa ningependa kuona unakuwa more defined kisheria ili ulalie zaidi kwenye mahusiano ya kiulinzi na usalama tu, na kupunuguza siasa na uchumi, na pia kuondolewa kwa cheo cha Makamu wa rais ambacho ukweli kilianzishwa na Mwalimu, ili kumbana Malecela asipate nafasi yoyote tena kubwa kiserikali kwa hiyo akaanzisha cheo hicho eti kwa ajili tu ya wa-Pemba, so far CCM hatujapata kura hata moja huko, ni hasara tu kwa taifa rais za ZNZ anatosha kuwa veep!

FieldMarshal ES;Darsa limekaa uzuri lakini umenifanya sasa niipende siasa ;Nadhani uko radhi kutujenga vijana ktk siasa. Niko tayari kuianza safari hii ya kisiasa chini ya uangalizi wako.
 
Mkuu,Naomba unipe maelezo ambayo yananipa Utata,Umeeleza mambo mengi kuhusu Mzee wetu Samwel Malecela,naona hili pia itakuwa vyema kama utalitolea maelezo,"Nakumbuka Mke wa Kwanza wa Mzee Malecela,kipindi kirefu cha Ugonjwa wake aliuguziwa Kigoma nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa,Wakati huo Mkuu wa Mkoa alikuwa Mzee Crysant Majiyatanga Mzindakaya,Kipindi hicho Mzee Malecela alikuwa Waziri Mkuu,naomba maelezo yako kuna Uhusiano gani kati ya Malecela na Mzindakaya?".Kwa sababu kwa urafiki wa kawaida isingekuwa rahisi Mzindakaya kubeba jukumu hilo,nakumbuka Marehemu Mama Malecela (RIP) alikuwa Mnyakyusa,na Mzee Mzindakaya ni Mfipa.

Si rahisi kwa mtu wa kawaida kutoa huduma hiyo nzito,au ilikuwa ni yale mambo ya Kujiweka karibu na mkuu?Swali sio zuri sana lakini naomba maelezo yake,kwani kama ni kumjadili Malecela tumesikia mengi hapa na ni vyema na hili litolewe maelezo.Heshima mbele Mkuu!!!!
 
Ingawa swali ni out of the legacy, lakini still, ukweli ni kwamba mke wa Malecela, alikuwa akiumwa ugonjwa ambao wataalamu wake wa medicine kutoka Japan, walishauri kuwa alipaswa kuishi mji wenye hali ya hewa inyofanana na ya huko Japan, ambako alienda kutibiwa mara ya mwisho,

katika bongo, scientifically ikakubalika kuwa only Kigoma ndio kuna hali ya hewa ambayo ni almost kama ya Japan, sijui ni vigezo gani vililitumika kuamua, kwa hiyo Mzindakaya, ambaye amekuwa rafiki wa karibu sana na familia ya Malecela, to the point kuwa sasa wao ni ndugu kabisa, maana hakuna shughuli yoyote muhimu ya ukoo huo isiyomjumuisha Mzindakaya, alijitolea kumsaidia rafiki yake, maana hata asingemsaidia ilikuwa akaishi hapo hapo Ikulu ndogo alipokuwa akiishi Mzindakaya, kama RC, kwenye nyumba ya wageni ndani ya compound hiyo, ambayo kwa kweli ni safi sana na imetengenezwa sana.

Kwa hiyo mkuu, haikuwa kujikomba wala anything, isipokuwa hao wakuu wawili wana uraifiki wa karibu wa muda mrefu ambao umegeuka kuwa undugu, na huyu mama kama mke wa the then sitting Waziri Mkuu, even now kama mke wa ex-PM, angeweza kuishi hapo Ikulu ndogo anyways, regardless nani ni sitting RC, hata asingekuwa Mzindakaya.

Baadaye mama huyo, alihamishiwa Nairobi, ambako Rais Daniel Arap Moi, alimsaidia sana sana mpaka alipoitwa kurudi kwa Muumba wake, Moi alikuwa ni mgeni wa karibu kila siku kwenye jengo alilowekwa mama huyo, na hata alitoa ndege yake kurudisha mwili wa marehemu. Sasa dhana ya kujikomba kwa Mzindakaya inakosa nguvu hapa maana Moi alikuwa akijikomba nini kwa Malecela?

I hope mkuu wangu Mwanzage, , nimesaidia angalau kidogo kama sio sana.
 
Field marshal nimeanza kukuogopa,wewe unaonekana unajua mengi sana sio rahisi vitu unavyoeleza hapa kwa mtu wa kawaida kujua...unaonekana uko deep sana na wakulu wa nchi au na wewe ni mmojawapo,who are you?
 
Field Marshall es,
Unajua mzee wangu huwa unaeleza mengi mazito na wakati mwingi hunifungua akili na kunijenga zaidi ktk kuelewa siasa za Bongo.
Kitu kimoja nachofahamu kwa uhakika ni kwamba Mdanganyika siku zote huwa nawe ktk Ushindi lakini unaposhindwa utabakia peke yako!..kama vile baharia aliyerudi akianza kupigwa jua, wapambe wote hupotea.
Hili ndio tatizo alokuwa nalo Mzee Malecela pamoja na kwamba nia yake ilikuwa nzuri - He paid big time!
 
Bubu Msemahovyo,
..bahati nzuri nimevisoma vitabu[uongozi wetu..., utenzi wa tanzania] vya Mwalimu vinavyohusiana na hoja ya Tanganyika.

..hoja hujadiliwa bungeni kwa ruhusa ya SPIKA wa Bunge, siyo Waziri Mkuu. kwa hiyo Malecela hakuwa na say hapo.

..Mwalimu alialikwa Bungeni kujaribu kuwashawishi G-55 kuachana na hoja yao lakini alishindwa na Wabunge wale wakaendelea na hoja yao. Sasa kwanini anamlaumu Malecela?
..Serikali na CCM na Mwalimu walishindwa hoja. Demokrasia ilifuata mkondo na Bunge likaazimia kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.

..Kulikuwa hakuna njia ya kuiua hoja ile zaidi ya kutumia VITISHO na UDIKTETA. Mzee Mwinyi aliwachosha Watanganyika.

..Mwalimu alitumia ujanja wa kusema CCM wapige kura ya maoni kuona kama wanabadili sera yao ya serikali 2. Baadaye ikarangazwa ati wana CCM wamekataa.

..Mwisho wa hoja ya Tanganyika ni Bunge kuazimia kuendelea na serikali 2 kwa lengo la kuwa na serikali 1. Je serikali moja ni sera ya CCM?

How dare you say Mwalimu alishindwa kuwashawishi hao wabunge? Mwalimu alikuwa hashindwi kwa hoja bana....
 
Kitu kimoja nachofahamu kwa uhakika ni kwamba Mdanganyika siku zote huwa nawe ktk Ushindi lakini unaposhindwa utabakia peke yako!

Hiyo ni very interesting lakini ndiyo ukweli huo. Wadanganyika wanapenda kuwa sehemu ya mafanikio lakini sio sehemu ya mapambano (struggle)!
 
Mzee ES,
Natanguliza samahani hapa tunamkoma nyani...naomba maelezo.

Nimesoma kwamba Mzee Malecela ana shamba la ekari 300. amelipataje shamba hilo? Waziri Mkuu mwenzake, Sumaye, alijipatia shamba la eka 7 tukasema ni rushwa. Je, Malecela ametumia ujanja gani kupata hizo eka 300?
 
Mzee ES,
Natanguliza samahani hapa tunamkoma nyani...naomba maelezo.

Nimesoma kwamba Mzee Malecela ana shamba la ekari 300. amelipataje shamba hilo? Waziri Mkuu mwenzake, Sumaye, alijipatia shamba la eka 7 tukasema ni rushwa. Je, Malecela ametumia ujanja gani kupata hizo eka 300?

jamani watanzania ..watanzania ujamaa umetuharibu ..tunaona wivu watu kuwa na mashamba wakati wenyewe kulima hatutaki..nani ametaka shamba akanyimwa...??...by the way ..what is three hundred acres????..tanzania inayo robo tatu ya ardhi[inayofaa kwa kilimo] na haitumiki-yaani haina watumiaji..sasa mtu kuwa na viheka 300 mnaona ishu??!!!...hata ile ya sumaye tangu mwanzo niliona ni propaganda tu..

mzee kama malecela hata angekuwa na heka 3,000..singeshangaa na wala isingezuia mtu hapa kupata shamba..wana jf kwa taarifa kuna vijiji vingi tu vinatafuta watu wa kuwagawia mashamba na hawaendi...wanagawa kuanzia heka 50 kwa mtu mmoja...ukitaka unajiandikisha tu na hata pesa hulipi..mradi uwahakikishia kuwa utalima..go and get yours!!!!
 
Nimesoma kwamba Mzee Malecela ana shamba la ekari 300. amelipataje shamba hilo? Waziri Mkuu mwenzake, Sumaye, alijipatia shamba la eka 7 tukasema ni rushwa. Je, Malecela ametumia ujanja gani kupata hizo eka 300?

Mkuu joka,

Heshima mbele, Malecela ana mashamba katika vijiji vya Mkoka, Mvumi, na Chamwino Mkoani Dodoma, karibu na Ikulu ndogo, ambako ana ng'ombe pia wa kufuga na mbuzi wengi sana.

1. Shamba la Mkoka, originally, lilikuwa ni la dada yake anyeitwa Mdala Pelestachi Malecela, ambaye katika umri wake wa sasa wa miaka 93, hawezi tena kulihudumia shamba hilo la eka karibu 400, kwa hiyo kwa sasa huishi Dodoma nyumbani kwa kaka yake, na shamba hilo alimkabidhi kaka yake Malecela, na ndio anayeliendeleza mpaka leo.

2. Shamba la Zabibu lililoko Mvumi, lina eka karibu 300 hili ni urithi wa ukoo wa Malecela, ambao unamiliki sehemu kubwa sana ya ardhi katika eneo hilo ambalo ndio mwanzo wa familia hiyo ya Malecela, hili ni shamba la Malecela na dada zake waliobaki wawili, ambalo waliachiwa na marehemu mama yao, kwa kuwa mwenye uwezo ni Malecela, ndio maana anaonekana kama mmiliki wake.

3. Shamba la Chamwino, hili ni mali binafsi ya Malecela, ambayo alipewa wakati Mwalimu, alipoamua kuweka Ikulu pale, the matter of fact viongozi karibu wote wa enzi zile za Mwalimu, wana eka zao hapo Chamwino, ambako originally, lilikuwa ni pori tu limejikalia, Mwalimu akaamua kuwagawia viongozi wote vipande vya kulima ili kuisaidia eneo hilo, na hili shamba si kubwa sana, isipokuwa lina mifugo mingi sana ambayo Malecela, aliachiwa na marehemu kaka yake aliyekuwa akiitwa Kefa Malecela, ambaye alikuwa ni Mkunga mashuhuri sana katika mkoa huo mzima na ya jirani na Dodoma, yeye alikuwa akitahiri vijana wa kiume wa kigogo kulingana na mila na maadili ya Kigogo, na alikuwa aki-charge either Ng'ombe, mbuzi au kondoo kwa kila mtoto aliyemtahiri, matokeo yake ni kwamba by time anafariki alikuwa na mifugo isiyohesabika ambayo Malecela aliirithi kutoka kwake, yote ipo hapo kwenye shamba lake la Chamwino.

Now nafikiri you can see clear, tofauti ya mashamba ya Malecela, na yale ya Sumaye, kule Mvomero, ambayo yalikuwa ni ya kijiji cha ujamaa cha Mvomero, hata kabla mkuuu hajawa Waziri mkuu, sasa kama Mtikila anasema kweli ni kwamba Sumaye, aliyapora kutoka kwa kijiji hicho akitumia u-PM wake, hiyo ndio tofauti yake mkuu.

Again I hope ninaendelea kuwasaidia wakuu kumuelewa vizuri Malecela, na legacy yake, kama kuna mengine yanayohusiana na Legacy tu, sina noma wakuu maana tuliahidi siku zote kuwa viongozi waadilifu wa Tanzania tunawafahamu, na mafisadi pia!

Halafu futhermore, Mzee huyu akishavuna mazo yake huuza nusu tu na mengine yote hugawa bure kwa wananchi mabli mbali, pale nyumbani kwake Kilimani anytime ukienda pale utayakuta magunia na mafuta ya Alizeti ambayo hutokana na mbegu zinazolimwa kwenye shamba lake la Mkoka, yakigawiwa kwa mtu yoyote mwenye kuhitaji, in fact mpaka viongozi pia huchukua hapo, kwa hiyo sio kwamba mzee hulima kwa njaaa.
 
Wewe inavyoelekea unamjua sana huyu Malecela...lazima utakuwa kinfolk wake kujua hayo yote unayoyajua...
 
Mkuu wangu Nyani,

Heshima mbele, Legacy mkuu, kwenye hii forum hakuna kinfolk wa mtu yoyote, ni kukata ishus tu maana kama wote ninaowatetea hapa ni kinfolk wangu basi nitakuwa na wengi sana, mpaka kina Carol wa kule UK, Freeman, Mramba, Zitto, Dr. slaa,

Anyways, tuendelee kukata ishus mkuu, kumkoma nyani hapa tena kwa roho mbaya mkuu! Hatumjui mtu hapa ni matendo yao tu kwa taifa ndio tatizo letu!
 
Labda ni mbunge mpya wa kurithishwa 2010! You never know with these things.

I know hoja zikiisha then mkuu MMJ alishatumabia what to expect next, yaani viroja!
 
Mzee ES,

tafadhali bwana. hivi unataka kutushawishi ati dada yake Malecela alikuwa na uwezo wa kumiliki shamba la eka 400? tena eneo gumu kwa kilimo kama dodoma? please. where did she get all the money?

hii habari ina-expose viongozi wa Tanzania ambao wanajidai maskini lakini wana mali wameficha. wanatudanganya watanzania tuukumbatie umaskini lakini wao wanakwapua mali huku na kule.

member wengine hapa ni vijana wanafikiri haya mauzauza yameanza na Mkapa. Toka enzi za Baba wa Taifa kulikuwa kuna madudu yanafanyika.
 
1.
tafadhali bwana. hivi unataka kutushawishi ati dada yake Malecela alikuwa na uwezo wa kumiliki shamba la eka 400? tena eneo gumu kwa kilimo kama dodoma? please. where did she get all the money?

Mkuu joka,

Heshima mbele, ningekuelewa kama unamfahamu huyo dada wa Malecela, lakini ukweli ni kwamba humfahamu, wala uwezo wake kipesa, lakini una hukumu tayari kuwa amepata wapi hizo pesa, wewe huoni kuwa hayo ni matusi kwa mwana-mama ambaye wala humfahamu wala hujawahi kumsikia, wala kumuona? Je hizi ndio mila zetu za ki-Tanzania kuwahukumu wananchi bila sababu just because kaka yake ni Malecela? That is exactly what you are doing, ningekuelewa ungeuliza info kuhusu huyu dada wa Malecela, tena kwa ustaarabu kama ulivyouliza swali la kwanza, lakini huwezi kutafuta info kwa kutoa hukumu kwanza kwa mama ambaye wala humjui,

Mkuu huna hata aibu unauliza "Where did she get the money?" are you serious au unatania? Mimi nikushawishi wewe mtu nisiye kufahamu wala sijawahi kukuona for what? Ili unipe nini? Sasa na wewe unataka kunishawishi niamini kwamba katika ukoo au familia ya Malecela, ni yeye tu mwenye uwezo? Wewe unawafahamu wote? Huyo mama unajua kama ana watoto au hana? Wana uwezo au hawana? Halafu eka moja ya shamaba kwa eneo lilipo hilo shamba, Mkoka unafikiri inaweza kuwa inauzwa shillingi ngapi za bongo? Hivi hata unajua hako kakijiji Mkoka bongo kako sehemu gani?

I mean mkuu Joka kweli among all the brain kwenye hii forum ninakuheshimu siku zote kuwa ni one of them unaweza kuuliza maswali ya kitoto na daharau kwa watu usiowajua kiasi hiki? Kwa hiyo kwa mantiki yako mkuu, member yoyote wa familia ya Malecela, akiwa na hela au uwezo ni dhambi, maana ni za wizi Malecela ameiba serikalini? is that so?

Mkuu Malecela, ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto 11, na ukweli ni kwamba wenziwe walikuwa na mali hata kabla Malecela, hajaingia kwenye siasa, na ndio waliomsomesha shule na ndio waliompa hata nyumba yake ya kwanza pale kata ya Kikuyu, Dodoma mjini alipotoka shule India, na leo wamebaki yeye na dada zake wawili tu, kwa hiyo mali zote zilizoachwa na ndugu zake wengine na hasa za mashamba, ziliangukia mikononi mwake yeye mwenye uwezo, mkuu wangu kuna kaka yake mkubwa, aliyekuwa akiishi Chalinze, Dodoma, aliyefariki miaka mitatu iliyopita, aliacha mashamba, karibu eka 300 ambayo Malecela ameshindwa mpaka leo hata kuyagusa maana it is too much kwake, sasa wewe unashangaa hayo ya Mkoka, ambako value ya ardhi sidhani kama inaweza hata kufikia dola moja per eka?

Mkuu Baba wa Malecela, alikuwa mtengeneza mvua, which made him the richest man in Dodoma then, na mpaka ku-draw the attention ya wazungu wa kwanza, waliomrubuni mpaka kutoka dini yake ya Upagani, na kuwa Mu-Anglikana wa kwanza bongo, na hatimaye kuileta dini hiyo Dodoma, kwanza na hatimaye bongo nzima, sasa by the time anakufa unafikiri alikuwa ameacha mali kiasi gani as far as mashamba na mifugo?

Huyo Dada yake unayesema hawezi kuwa na hela, amekuwa akimiliki Hospitali yake binafsi Urambo, Tabora ambapo hasa alikuwa akijishughulisha na kina mama kujifungua watoto, na hizi ni enzi za kuanzia 50s, 60S, 70s, mpaka mwishoni mwa 80s, sasa hiyo miaka yote alikuwa akilifanyia kazi ya charity, au alikuwa akitengenza pesa?

Halafu aliyekuambia kuwa Dodoma ni sehemu ngumu kiasi kuwa mwananchi hawezi kuwa na shamba kubwa ni nani mkuu? Mkuu Dodoma kuna ardhi njema ya kustawisha mahindi, mtama, uwele, Tende, Zabibu, na Mbegu za mafuta ya Alizeti, na ndio hasa kilimo anachokifanya Malecela sasa kwenye mashamba yake, kwa mbinu za kisasa, na aliyeanza ni huyo dada yake ambaye siku zote amekuwa akilima kwa kutumia matrekta, wakuu hata Dodoma tu nako mnahitaji kusimuliwa kama vile ni majuu? Yaani kupanda basi tu asubuhi ukafika saa tisa ukajifunza jiografia ya kule nayo inahitaji hela za kigeni au kuja kuelimishwa hapa JF?

2.
hii habari ina-expose viongozi wa Tanzania ambao wanajidai maskini lakini wana mali wameficha. wanatudanganya watanzania tuukumbatie umaskini lakini wao wanakwapua mali huku na kule.

Mkuu joka, this is sad mkuu what is in the expose hapa ni uwezo mdogo wa baadhi ya wananchi wa Tanzania, katika kufikiri, maana inaonekana kuwa tuna mawazo kuwa ndugu wa kiongozi hawezi kuwa na mali zake binafsi, akiwa nazo basi ni za ndugu yake ambaye ni kiongozi alizoiba serikalini, and that mkuu is very pathetic thinking, tena ya u-Azimio La Arusha, yaani Malecela, ataiba hela za nchi halafu ataenda kuzi-invest kwenye ardhi ambayo huwezi kumuuzia binadamu yoyote mwingine akanunua hata kwa bei uliyonunulia, licha ya bei ya faida kutokana na kuitunza ardhi hiyo, unasema hiyo ndio expose ya kuwa viongozi wetu wanaojidai ni masikini? you maust be joking mkuu, kweli haya maneno unaweza kumushawishi mwananchi mwenye akili timamu akakuelewa?

Look at this, mashamba yote Mwalimu aliyowagawia viongozi wa juu kule Chamwino, waliyalima tu Mwalimu alipokuwa kwenye madaraka, alipoondoka tu wakayatelekeza, yaani leo hata wewe unaweza ukaenda ukayalima maana sasa ni mapori tu kama yalivyokuwa mwanzoni, sasa akitokea mtu wa kuyalima yakapendeza then kutatokea kina wewe Joka, kuwa ooh hii ni mali za viongozi waliowapa ndugu zao? Does this make a sense at all mkuu?

3.
member wengine hapa ni vijana wanaziikiri haya mauzauza yameanza na Mkapa. Toka enzi za Baba wa Taifa kulikuwa kuna madudu yanafanyika.

Mkuu joka, labda kuna mtu ameiba pasword yako, no way this is you ninayemfahamu, mkuu wizi na rushwa serikalini ilianza toka Mwalimu, akiwa madarakani, yeye binafsi Mwalimu, alimuondoa waziri wake wa kwanza wa sheria, chief Mwakwaiya kwa ajili ya rushwa, hiyo ilikuwa in the 60s, kwa hiyo Mkapa sio kiongozi wa kwanza kama unavyosema hapo.

Mwalimu, aliandika kitabu kikubwa sana akimtukana Malecela, kwamba ndiye tatizo la Taifa letu kwa sababu haulindi Muungano, yaani sisi wabongo umasikini wetu unatokana na Malecela kutoulinda muungano, na katika hicho kitabu kuna mahali Mwalimu, anamuambia Malecela, aache uongozi akalime mashamba yake, siku ile kwenye mkutano wake na waandishi wa habari Kilimanjaro Hotel, alizungumzia tena kwa kirefu kuhusu mashamba ya Malecela, lakini never even once Mwalimu aliwahi kusema mashamba hayo ya Malecela, ni ya hela za wizi alizoiba serikalini, lakini Mwalimu alisema mwaka 1995 kuwa Malecela,anazo billions of money alizopewa na wa-Iran kutafuta urais, ukweli ni kwamba mpaka leo hizo hela hatujaziona, lakini recently tumesikia kuna waliopewa hela toka Iran za uchaguzi, hivi ni mwananchi gani ambaye hakuziona zikitumika? Sasa Malecela, aliamua kuziweka wapi ambako mpaka leo hatujawahi kuziona?

Kama ni mauza uza ya Mkapa, yametolewa kwa kina magazeti yetu to this day ameshindwa kukanusha wala kukubali, sasa kama ya Malecela yapo kwa nini hayo magazeti yasiseme, yanasema mpaka habari za rais wa sasa yatashindwa kumsema Malecela na mali zake? Mkuu uwezo au priviledge ya kuandika hapa JF isitufanye tukaamini kuwa tunaweza kuwachafua tu hata viongozi wasiohusika na uchafu, licha ya wananchi wa kawaida, uzuri wa bongo siku hizi mambo ni hadharani kama mwendo wa Msondo ngoma ya wa-Tanzania, na mkulu wangu marehemu TX-moshi, hakuna siri tena mambo yote huwekwa hadharani tu, kwa hiyo mkuu samahani sana kama nimekugusa kule kwenye ishu ya Rupia,

Lakini mwendo utaendelea kuwa mdundo tu kwa viongozi wachafu waliotuibia mali zetu za taifa, na wale wasafi hawana sababu ya kuogopa maana tunawajua wote na tutawatetea, lakini wale wezi wote kila mmoja atabeba mzigo wake,

Isipokuwa tu mkuu wangu joka, umenishitua sana hizi nywepesi nywepesi, ambazo ni dalili za kutokuwepo hoja za msingi against Malecela, sasa ikibidi hata dada yake, ili mradi tu tumpate na hatia kama za Mkapa, masikini ya Mungu, ndio taifa letu hili na sisi ndio wananchi wenyewe!
 
Back
Top Bottom